Asalaam Aleiykum
Kitu hichi Imani ndicho alokitaja Nabii Issa a.s kama utakipata ndani ya moyo wako "Basi unaweza kuwambia Mlima sogea ukasogea" Unaweza kumwambia mtu pona akapona, "unaweza kusema leo hapa Meli haiondoki na haitoondoka" Hiyo ndiyo Imani kama utakua nayo watu wengi watavutika kwako, kwanini nikasema wanavutika kwa sababu pia wanavutika kwa tajiri wa Mali, kwa hiyo na wewe kwako watavutika kwa sababu ya utajiri ulio nao ndani ya nafsi yako, kila mmoja ataona yeye unampenda zaidi kuliko mwenzake, Sasa vipi kinapatikana kitu hichi ikiwa una haja nacho?.
Ndio unakutana na hizo funguo 99 za Imani ili uchague mwenyewe ipi ita (Unlock) moyo wako, funguo gani inafaa ili uitumie, Nilipoandika darsa ya (Uradi wa Dhikr ya kumtaja Mollah) wengi hawakufahamu nini ilikua makusudio yangu, sasa nimeleta hizi funguo 99 ili na wewe upate kuwasha hiyo Taa ilozimika Moyoni. Mimi nina hakika baada ya kuzijaribu funguo hizi 99 lazima iko moja itafungua moyo wako, iko hiyo moja itawasha Taa katika nafsi yako, Na taa ikiwaka baada ya hapo wewe ndio utakua shahid, wewe ndio utajua faida yake lakini kikubwa kinachotakiwa ni hio juhudi na bidii ya kukumbuka hilo jina ambalo litakua ndio ufunguo wako.
Na hiyo Imani ikishajaa Moyoni mwako wewe ushakua tajiri mkubwa kuwapita matajiri wote walokuzunguka, ndio maana utaona "Alexander the Great" alipokua kalala kwenye kitanda na Mauti yashamsogelea akawaambia wasaidizi wake nataka nitakapo kufa mkanitia kwenye jeneza muache mikono yangu inaninginia na kuonekana nje ili halaiki ya watu waione hata "Alexander" na Mali zote na kuiteka kila nchi anaondoka mikono mitupu.
Kaa ukijua hayo ma(Plastic)unayo kusanya, hizo Funiture na makaratasi unayo rundika (Bank) vyote ni vya kupita kwenye Ulimwengu huu havina maana kabisa, Na siku ya kuondoka kwako na wewe utachagua ama utudanganye mikono ifichwe ndani ya jeneza au na wewe utaomba ininginizwe kama "Alexander" chaguo ni lako.
Lakini utakapo pata utajiri huo wa Imani basi mara moja utakuachisha Rushwa, dhuluma, tamaa ya mali, choyo na uchu wa cheo, sasa kitu chenye kukuachisha hayo yote kinakupa nini badili yake?.
Endelea part 3
No comments:
Post a Comment