Sunday, May 24, 2015

DUA YA KUANZIA SALA PART 1

Asalaam Aleiykum

Unasikitika Mbona Sala yako dhaifu, unahisi kama husimamishi Sala vizuri, au wakati mwengine unasema bora nisali kabisa nindoshe udhia, Hiyo ndio Sala yako ya kila siku unavopeleka au kwenda kukaribiana na Mollah, sijui hata kama unafika karibu na hiyo Sala, kwanini ikawa hivyo kwa sababu imekua mazoea, kwa sababu huna mapenzi na jambo hilo umeambiwa kusali na wewe unajiburuta kwa kuogopa moto, ndio unakwenda unasimamisha sala.
Ukifika tu kwenye hiyo Sala unanyanyua mikono mbio mbio baada ya sekunde hamsini Sala ishamalizika, pengine hujui ni Sala, pengine hukijui kitendo hichi madhumuni yake, au huyajui maneno ya kutanguliza ukaifanya Sala yako irefuke na wewe uwe mtulivu kwenye hiyo Sala yako.
Sala imewekwa kwa vipindi ili kila mara ukumbuke kurejea Nyumbani kwa Mollah wako, kila mara ubebe huo Mwili wako na kurudi nyumbani ili upate kusema mimi nimepotea kwa kipindi fulani cha masaa, na kila nikipotea huko nendako nafanya makosa yaso idadi basi Mollah wangu Muumba naomba (Maghfira)Msamaha wako.
Vipi Utaanza Sala yako?
Hii ndio Darsa yetu ya leo kuondosha haraka zako na kuifanya Sala yako iwe angalau irefuke kidogo, angalau Malaika wapate kukupokea siku moja moja uwape nafasi ya kuandika maneno yako yanotoka mdomoni asaa kuna siku yatatoka moyoni na siku hiyo ndio utakua umeanza kuipata Sala.
Utaanza Sala yako kwa maneno haya:Ntayaandika kwa lugha ya (Kiswarab)"Allaahumma baaid baynee wa bayna khataayaaya kamaa baa'adta baynal mashriqi walmaghribi, Allaahumma naqqinnee min khataayaaya kamaa yunaqqath thawbul-abyadhu-minad-danasi,Allahum-maghsilnee min khataayaaya,bith-thalji walmaai walbarad".
"Ewe Mollah wangu nitenganishe mimi na madhambi yangu kama ulivotenganisha Mashariki na magharibi","Ewe Mollah wangu nisafishe mimi makosa yangu kama inavosafishwa nguo nyeupe kutolewa madowa", "Ewe Mollah wangu yakoshe Madhanbi yangu kwa Barafu, na Maji, na chembe chembe za theluji".
Hayo ndio yawe maneno yako ya mwanzo katika kuingia kwako kwenye Sala, kwa sababu wewe unahudhuria kwa Mollah wako kila kiungo kimebeba dhanbi, pengine umetizama ya haramu, umeshika yalo haramu, umekanyaga umeua kidudu njiani, kwa hiyo kabla ya kukutana na wewe Mollah wangu basi nakuomba nitenganishe mimi na dhanmbi zote kama ulivoitenganisha mashariki na magharibi, kwa wakati huu nakuja kwako tuwe mbali mbali.
Kwa heshima ya kuja kwako Mollah wangu nakuomba mimi nimebeba mengi yasiri na yaliyo dhahiri, ninayo yajua na nisiyo     yajua basi nakuomba unisafishe nikitoka hapa niwe kama nguo nyeupe inavosafishwa uchafu wake ikawa madowa yote yameondoka, Mollah wangu nakuomba yakoshe Madhanbi yangu nisiwe nakumbuka kumbuka, yakwangue kwa kuyagandisha kwa Barafu, halafu yasafishe kwa maji, ikishe yaondoshe kabisa kwa mtiririko wa theluji yawe mbali na mimi nisiwe narejea rejea kwa kuyakumbuka.
Endelea part 2

DUA YA KUANZIA SALA PART 2

Asalaam Aleiykum

Ukishamaliza kusema hivyo unaingia katika maneno ya pili nayo yanatamkwa hivi:
"Subhaanaka Allaahumma wa Bihamdika, Wa Tabaarakasmuka wa ta'aalaa jadduka, wa laa ilaaha ghayruka"
"Utukufu na Shukuran ni wako wewe Mollah wangu""Limetukuka Jina lako  lenye Utukufu"" na hakuna anaestahiki kuabudiwa isipokuwa wewe Mollah wangu".
"Umetukuka Mollah wangu kwa kuumba kila kitu katika Ulimwengu huu nikiwamo na mimi, sina cha kuongeza isipokua Shukurani ya kuniwezesha kuja mbele yako kwa ajili ya kukumbuka wewe Mollah wangu, Limetukuka Jina lako lenye Utukufu ambalo limenifanya mimi kusimama mbele yako na nikatamka hakuna anaestahiki kuabudiwa isipokuwa wewe Mollah wangu".
"Wajjahtu Wajhiya lilladhee fatara-samawati wal-ardhi haneefan wama ana minal mushrikeen, inna salatee wanusukee wamahyaya wamamatee lillahi Rabbil-Aalameen, la shareeka lahu wabidhalika umirtu wa ana minal-muslimeen, Allahumma antal-Maaliku laa illah anta, anta Rabbee waa-ana Aabiduk, Salamtu Nafsee waata'raftu bi-dhanmbi faghfirlee dhunubi Jameean innahu laa yaghfiruu-dhunuba ila anta, Wahidnee li-ahsanil -akhlaq laa yahdee li- ahsaniha ila anta, Wasrif aanne sayyiha laa yasrifu aannee saayyiha illa anta, labbayika wasaadiyk walkhaiyru kulluhu biyadak, washarru laissa ilayyka, Anaa bikka wailayka tabarakta wataa'alaita astakhfiruka wa'atubu ilaika".
"Nimeuelekeza Uso wangu Kwa Yule ambaye aliyevileta Mbingu na Ardhi Na mimi (Najitoa)sio katika wale wenye Kumshirikisha(Mollah)wangu na chochote, Hakika Sala yangu, (Muhanga)wangu, Maisha yangu na kufa kwangu ni kwa ajili ya Mollah wangu, Mollah wa Ulimwengu wote, asiye na mshirika, Na kwa hilo najisalimisha(Kwa kutii)na mimi ni miongoni mwa Waislam, Mollah wangu hakika wewe ni Mfalme wa(Kila kitu)Hakuna apasawe kuabudiwa isipokua wewe, Wewe ni Mollah wangu(Mfalme) na mimi ni Mtumwa wako(Kiumbe)Nimeikosea Roho yangu na nimeyajua makosa yangu, Naomba(Kwa hilo)Nisamehe makosa yangu yote, hakuna awezaye kusamehe makosa isipokua wewe Mollah wangu, niongoze mimi kwenye ubora wa Tabia, kwani hakuna awezaye kuongoza isipokua wewe Mollah wangu, Na nitoe mimi katika Tabia mbaya, kwani hakuna awezaye kunitoa isipokua wewe Mollah wangu, Mollah wangu nimehudhuria Mbele yako, kujibu wito wako,(Wa kukuabudu)na niko tayari kuutumikia wito huu, Mazuri yote yapo kwenye uwezo wako, Na mabaya siyenye kutoka kwako, Na mimi naishi kwa ajili ya uwezo wako na marejeo yangu ni kwako wewe Mollah wangu, Baraka na Utukufu ni wako wewe, Naomba msamaha wako na kwako (Pekee)Mimi natubia (Makosa)yangu..

DUA YA KUANZIA SALA PART 3

Asalaam Aleiykum

"Allahumma Rabba Jibril -WaMikail-Wisraafil-Fatira-Sammawati-Wal-ardhi,Aalima-Ghayib washahadah, Anta tahkum bayna Aabadika fiimaa kanoo fiih Yakhtalifuna, Ihdinii limakh-tulifa-fiih minal haqq biidhinika, Innaka tahdii man-tashaau ila siraatin Mustaqqim".
"Ewe Mollah wa Jibril na Mikail na Israfil(Malaika wakubwa) Muumba wa Mbingu na Ardhi, Mjuzi wa vyenye kuonekana na visivyo onekana, Wewe ni Mwenye kuhukumu Baina ya waja wako katika yale walo khitafiliana, Niongoze mimi katika haki ya ile khitilafu kwa uwezo wako, kwa hakika wewe unamuongoza umtakaye katika njia ilonyooka".
"Allahu Akbar Kabeera, Allahu Akbar Kabeera, Allahu Akbar Kabeera, Walhamdu lillahi katheera, Wa Subhaanallahi Bukratan waseela,Audhubillahi Mina-Shaytan, Min Nafkhihi, Wa Naftihi, Wa khamzihi".
"Mollah Mkubwa, Aliye Mkubwa,Mwenye Ukubwa, Shukran zote anasthiki yeye, Utukufu ni wake (Mollah wangu)kuchomoza kwa siku mpaka mwisho wake, Najikinga na shaytan na kuhema kwake, na sauti yake, na mnongonezo wake".
"Allahumma Lakal-Hamdu Anta noor Sammawati wal Ardhi waman fiihina, Walak hamdu anta qayyimu sammawati wal Ardhi waman fii hinna, Walakal Hamdu laka Mulku sammawati wal ardhi waman fii hinna, Walakal Hamdu anta Maliku sammawati wal ardhi walakal hamdu antal Haqq, Wawa'dukal haqq, Wakaulukal haqq, walikaukal haqq, waljannatul haqq, wannarul haqq,Wannabiyyuna haqq, wa Muhammad haqq, walisaa'atu haqq, Allahumma laka a'slamtu, wa'alaika tawakaltu, wabika amantu, wailaika anabtu, wabika khasamtu, wailaika hakamtu, Fakhfirliy maakadamtu, wamaa akhartu, wamasrartu, wamaa a'alantu antal Muqqadimu, waanta Muakhiru, laa illah ilah anta lahiy lailah anta".
"Ewe Mollah wangu  shukuran ni zako wewe, wewe Ni Nuru ya Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo, shukrani ni kwako wewe mwenye kukimiliki kila kitu kwenye Ulimwengu huu, Wewe ni Mwenye Kuimiliki (Kwa uwepo wake)Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo ndani yake, Shukurani zako wewe, Wewe ni (Mfalme)Mollah wa Mbingu na Ardhi na vyote vilivyomo, Wewe ni Mwenye kuitawala Mbingu na Ardhi na vyote vilivyo baina yake, Shukurani zote zinastahiki kwako, Wewe ni Ukweli(Mtupu), Ahadi yako ni ya Ukweli, Maneno yako ni ya Ukweli, uwepo wako ni wa Ukweli, Pepo yako ni ya Ukweli, Moto nao ni wa Ukweli, Mitume ni wa Ukweli, Na (Muhammad)(s.a.w) ni wa Ukweli, Na siku ya Kiyama ni ya Ukweli.
Ewe Allah kwako wewe najitupa(Nimejileta)Na kwako wewe nakutegemea, Nakuamini wewe na kwako narejea kutaka msamaha, Kwa ajili yako (Napigania) Na kwa ajili ya (Utaratibu)wako ndio na hukumu, Nisamahe kwa yale nilofanyia(Nafsi yangu)kuyatanguliza mbele yangu, na yale niloyawacha nyuma yangu, Na yale niliyoyaficha na yale niloyaweka wazi, Wewe ni yule ambaye mwenye kuyatanguliza na wewe ni ambaye Mwenye kuyachelewesha, Wala hakuna Mwenye kupaswa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Wewe Mollah wangu, Wewe ni Mollah wangu, Na hakuna Mwenye kustahiki Kuabudiwa isipokua wewe.
Halafu maliza kusali utuambie Sala yako fupi, na hivi na vile, vipi Sala yako itakua fupi ikiwa kila wakati unaanza na dua hii.Sala yako inakua fupi kwa sababu unakata kona, husomi dua, husomi chochote ukifika unaanza na sura ya (fatiha) ikisha huyo umeporomoka, ukimaliza unasema nisha simamisha Sala, ianze kwa dua na utulivu, fanya marekebisho iwe kila ukiingia kwenye sala unaanza kwa dua, na ukimaliza unamaliza kwa dua, halafu itizame jee sala yako itakua fupi?.

Sunday, May 17, 2015

UGANGA NA MAOMBEZI (RUQYA) PART 1

Asalaam Aleiykum

Katika maswali nisiyofurahi kuulizwa hakuna kama haya ya (Kiuganga) Watu wananifata na kuniuliza habari za Uganga na Ruqya vipi (Uhalali wake na Uharamu)wake, wanasema nini Maoni yako kuhusu jambo hili, vipi ntakua na maoni katika jambo hilo, mimi nilicho nacho ni kueleza jambo hili, ikisha wewe una hiyari kuchukua au kuniachia mwenyewe maelezo yangu.
Kwanza kabisa unapozungumzia jambo hili la Uganga ujue una kusudio la kitu gani, ukisema neno uganga umekusudia yule anayekupa matibabu, na kwa tafsiri yangu mimi watu hawa wapo wawili lakini wana kazi moja, huyu wa kwanza unamuamini na huyo wa pili unamuogopa. Mganga wa kwanza unaye muamini ni yule unayesikia au kujua kasoma miaka (7) kahitimu mafunzo yake na kuonesha (Certificate)zake ukutani, huyu ukimuona tu unaanza kupona, nafuu inakujia, unajisikia hujambo, Na akiwa mzoefu wa miaka mingi akikupa maji tu inatosha.
Halafu kuna huyu wa pili wa (Kienyeji)yeye hakusoma hana (certificate)lakini anajua dawa za kutibu baadhi ya maradhi ya mwili, na huyu yeye anatumia mbinu za kukufanya (Umuogope) kwa ukweli wawili hawa wote ni (Bussiness)tu. Wafanyabiashara hawa wanajua kuna mambo mawili ukiyaingia yana faida kubwa moja ni chakula na la pili ni maradhi, hupati hasara kabisa katika biashara hii ya chakula na matibabu ya wanaadamu, kwa sababu ni vitu muhimu na wanaadamu wanavihitaji, ndio maana utaona Waganga(Doctors) ni wenye kuweka maslahi yao mwanzo, wewe kufa papatika na maradhi lakini kama huna pesa hupati matibabu, hupewi dawa ya kupunguza maumivu.
Kwa kuwa maradhi yapo ya aina mbili wacha sasa tumtaje Bingwa wa maradhi yasio onekana na yanayo onekana nayo ni haya ya (Sipiritual)mambo ya Kiroho, kwa sababu Mwanaadamu una (body)Mbili, moja ni (Physical body) na ya pili ni (Sipiritual body).
Ili upate kufahamu kwa urahisi wacha nikufafanulie kwa njia ya rahisi, sina shaka ushapata kusikia kitu kama hichi (Body, Mind, and Soul),(Body)yaani Mwili ndio huu (Physical)unayoiona inashambuliwa na maradhi ya (Bacteria) na (Virus) na hivi na vile, halafu kuna hii (Etheric Body) hii inahusiana zaidi na (Mind) hii ndio inashambuliwa na hiyo (Energy) maalum inayotokea kwa Wanaadamu pamoja na Majini.
Endelea part 2



UGANGA NA MAOMBEZI (RUQYA) PART 2

Asalaam Aleiykum

Hapo ndipo wanapofanya kazi Wachawi na Waombezi katika hiyo (Energy). Ama kwenye jambo la Roho(Soul)Yako, kule hana mtu yoyote (Access)Ruhusa iwe Jinn au Mwanaadamu wala Malaika kugusa isipokua kwa Idhini ya Mwenye enzi Mungu.
Darsa yetu ya leo imekita kwenye Fani ya Maombezi, Tumeona yakua Waganga ni (Bussiness)tupu, lakini tuna hamu ya kuwajua hawa Waombezi wana jambo gani muhimu, Lakini kabla ya kuendelea nasikitika kuwa mpaka kwenye Fani hii ya uombezi wameingia watu wanafanya biashara.
Sasa tuingie katika Fani hii ya Maombezi tupate kujibu lile swali la (Ruqya), Kulijibu swali hili itatubidi twende (Deep) tukatizame kwanini ikawa kuombewa?, Na ndani ya kuombewa kuna kitu gani?, Kwanza kabisa napenda ufahamu Wachawi wako wengi sana, kwa sababu ni elimu ya uharibifu, na kila kwenye uharibifu watu wanakua wengi, tizama mfano wa kwenye ngoma na msikitini utalijua hilo, wapi utapata watu wengi?.
Kwa hiyo utajua Wachawi ni wengi sana na Waombezi ni wachache sana, Kwa sababu Uombezi ni Uteule(Selected)wa Mwenyewe Mwenye enzi Mungu, Kwa (Hijaza) Maalum anayopewa (Mja) kutokana na kujikurubisha kwa Mollah wake kwa mapenzi na huruma na unyenyekevu, vikifatiwa na Ibada na Imani ya hali ya juu, akifikia kiwango(Daraja) hiyo kwa Idhini ya Mollah wake anapewa (Energy)Maalum au ita hiyo (Hijaza) ya kuponesha hayo Maradhi ya Siri yanotokezea kwenye hiyo (Etheric Body) inayo milikiwa na (Mind) wasomi wanajua baadhi ya mambo wanaoneshwa, lakini wao husema (Brain) imepeleka (Signal) na hivi na vile, tuwaachie wenyewe wanasayansi.
Sisi tunasafiri na Muombezi huyu Mwenye kutibu maradhi hayo ya Siri na kufukuza viumbe kama majini wanokaa kwenye hiyo (Etheric Body), Unaweza kuniuliza hii (Etheric Body) ni kitu gani?, wacha nikupe mifano labda unaweza kuijua na ukaelewa ni nini kitu hicho, na vipi maombezi yafanyavo kazi yake.
Maombezi yenyewe yanategemea na uwezo wa kinguvu wa Muombaji na hiyo (Energy) yake alonayo, Napenda Uelewe kila kitu ni (Exchange of Energy)basi ikiwa Muombezi huyo ana nguvu za ziada, basi inatosha kukaa karibu au kwenda nyumbani kwake tu unapona maradhi yako ya (Etheric Body) ambayo ndio mengi tulonayo, Na kama nguvu zake za Maombi ni dhaifu itabidi asome na kukutolea sadaka ili upate shufaa itokayo kwa Mollah wako, kumbuka wote hawa wawili wana (Hijaza) lakini mmoja wao ni dhaifu.
Na Mifano ya zifanyavyo kazi zake (Energy) hizi ni kama hivi, kwani haijawahi kutokea kwako wewe ukawa pengine Umekasirika akatokea (Kipenzi) chako ukafurahi hapo hapo?, Hujiulizi wewe kwanini mtu ana nyanyua simu anakwambia maneno tu hulali usiku mzima,maneno yamepita kwenye waya za simu (Physical Body)inataka kulala lakini wapi huwezi kulala, na kitu chenyewe ni maneno tu, hukumbuki kuambiwa kitu ukacheka, na ukaambiwa chengine ukaangua kilio, Jitizame wewe ukenda kwenye mikutano ya siasa unakuaje kwenye ushabiki wako pale unapoambiwa kidumu chama chako, vipi unavoshangiria huwezi kujizuia hata ukiambiwa ndugu yako atauliwa unasema na afe, ushawahi kujitizama ukiingia hospital kwenye wagonjwa mahtuti wewe mwenyewe unakuaje hali yako, hiyo ndio (energy) inayozungumziwa ambayo matatizo mengi yanatokea hapo, na iko ya aina mbili ikichafuka ni (Negetive) na ikitulia (Positive) kwa hiyo maombezi yanofanyika ni katika hiyo (Etheric Body) ambayo inaleta matatizo mpaka kwenye (Physical Body) ndio inabidi Mtu upate Maombi ya (Ruqya).

UGANGA NA MAOMBEZI (RUQYA) PART 3

Asalaam Aleiykum

Hiyo ni Baadhi ya mifano niloitaja, Basi ikiwa mambo madogo yanafanya kazi namna hiyo, Nini habari yetu sisi unapokutana na yule (Mja)alokua karibu na Mollah wake, Halafu akapewa hayo alopewa katika nguvu za Maombezi ili awasaidie wanaadamu wenzie, Sasa kutana na Muombezi aliyeteuliwa na Mollah wake awe na (Power)au Hijaza hio.
Ama kuhusu kupewa uwezo huo (Quraan sura ya Al-Anaam aya ya 165) Inasema,
وَهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَڪُمۡ خَلَـٰٓٮِٕفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٍ۬ دَرَجَـٰتٍ۬ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِى مَآ ءَاتَٮٰكُمۡ‌ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُ ۥ لَغَفُورٌ۬ رَّحِيمُۢ 
"Ni Yeye ambaye aliyekufanyeni washikaji(Warithi)wa mahala pa hao walioondoka katika hii Ardhi, Na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa(Katika kila aina ya mambo)Ili akufanyieni mtihani kwa hayo alokupeni, Hakika Mollah wako ni mwepesi wa kuadhibu, Na hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa Kurehemu".
Huyu kapewa utajiri, yule kapewa umasikini, huyu msomi, kila mmoja wetu kapewa daraja yake katika fani tafauti, na kuna wengine wamepewa  fani hii ya uombezi, Na uwezo huu alopewa kapewa pia na ishara zake lakini si rahisi kwa mtu wa kawaida kuzigundua, Na mara nyingi unapelekwa kwake kwa njia za ajabu lakini unashindwa kumjua au kumuuliza, unafika mpaka kunyanyua simu lakini huwezi kuzungumza, kwa sababu huyu si mfanya biashara hajaweka kibao na kusema hapa unaombewa.
Na dalili nyengine hata akikuombea hataki malipo, na hata akichukua hayo malipo ni kwa ajili ya kukusaidia wewe na ubakhili wako, pengine hujatoa sadaka mwaka wa kumi, anakuonea huruma ndio anachukua hizo pesa kukutolea sadaka, mwenyewe hutoi, Jitizame wewe unakwenda kuombewa pengine (Bank) una hamsini Million, lakini kwa yule alokuombea unaacha elfu tano jiulize mwenyewe umekwenda kutafuta kupona au kufanya biashara ya kupona, Kwa hiyo Muombaji wa haki anajua udhaifu wako ndio maana anachukua baadhi ya hizo pesa na kukutolea sadaka, anakutolea zaka, kwani mbele ya muombaji anakuona kama(X-Ray) na Ubakhili wako, anajua pengine maradhi yako yamesababishwa na adabu ya kuwa vile unavopewa huvitoi,  anamuomba Mollah wake "Yaa Rabb" kiumbe chako hiki hakijui kitendacho, au Mshipa wa Ubakhili umemkamata basi msamehe namtolea mimi hii sadaka pasi na mwenyewe kujua, kiumbe chako hiki kimejaa upofu hakijui kinatenda jambo gani, basi sadaka hii na zaka hii kwa ajili ya idhini yako apone (Mja) huyu maradhi yake haya.
Usije ukadhani anatajirika kwa pesa yako, wenye kufanya hivyo pekee ni wafanya biashara. Sasa nini anafanya katika maombezi hayo?
Kwanza kumbuka Mtu huyu kapewa kipaji hicho na Mollah wake, Na yoyote yule alopewa kipaji hichi ana kitu kinaitwa (Sipiritual Eye)Sio kila mtu tu muombezi mpaka uwe na kitu kama hichi ndio unaweza kuwa umepewa (Hijaza)au baraka na Mollah wako ya kujua mambo, au magonjwa na dawa zake, Na kila mmoja wetu anacho kipaji hiki lakini wengine kipo kwenye biashara(Ndio mnasema akigusa jiwe linageuka dhahabu)ana muono mkali wakujua nini atauza na nini atapata hasara.
Sasa huyu alopewa uwezo wa kuponesha ukenda kwake anakuona kama inavokuona (X-Ray) hata wewe mwenyewe kama utapewa mafunzo unaweza kuona viungo vyako vya ndani lakini itachukua muda mrefu kwa wewe kuweza kufanya hivyo, Ukenda kwa mtu kama huyo anaweza kukwambia mpaka ulichokula jana ni kitu gani, Na huyo ndio mwenye uwezo wa kuona hiyo (Etheric Body) yako, Nini anafanya baada ya kuona matatizo yako?, Pengine kaona (Jinni)Linaishi kwenye hiyo (Body)yako, au una matatizo jinsi kadhaa wa kadhaa, ambayo yanatakiwa maombezi yake au unatakiwa uende hospital, yote atakueleza kwa uwazi bila ya kukudanganya, na ikiwa yanahitaji maombezi ya matibabu ya Quraan yeye anajua (Code) zake za hiyo Quraan na akichanganya na (Energy) yake ya maombezi ndipo anakusomea na ikisha kukupa maji au mafuta na kuyapulizia kile alichosoma, kwa kuwa ndani yaani(Deep inside) sote tuko (Inter connect) ndio yanatumika maji kama matibabu ya ndani na mafuta kuwa matibabu ya nje, hiyo ndio (Ruqya) na hayo ndio Maombezi, lakini wale wanobadilisha mchanga kuwa sukari, au kukwambia kalete nazi iloangakua yenyewe, sijui anataka kitambaa cheusi cha kuokota, samaki alokufa kinywa wazi, yote hayo ni (Mambo Jambo)ya kudanganywa na wala hakuna Tabibu yoyote, Mwenye (Energy au Power) inayoweza kuponesha watu kwa makundi ni muongo, msikubali kabisa mambo kama hayo, huyo (Jesus) mwenyewe alikua akiponesha mtu mmoja mmoja, leo wanafanya kuponesha watu kwa makundi wameanza kwenye (Ukiristo) na sasa wameingia kwenye  Uislam wanawauzia  watu dua elfu kumi, hasara ilioje kwa wale wenye kuamini, udanganyifu ulioje na kukubali kudhulumiwa.
Kwa hiyo (Ruqya)ni sehemu ya maombi anayopewa (Mja) ili apate kuwaponesha viumbe wenzie kwa (Idhini) ya Mollah wake, wale walokabiliwa na matatizo ambayo hayana ufumbuzi kwenye dunia hii yenye kuonekana(usiumwe na Malaria ukataka Ruqya), Na jambo hili halijakatazwa wala halina Uharamu wowote katika dini, ila unatakiwa umpate mtu mwenye fani hii ya kukuombea au kukusomea (Ruqya) ili upate nafuu au kupona kabisa.


Sunday, May 3, 2015

AJABU YA KIUMBE PART 1

Asalaam Aleiykum

Kiumbe ni Mtu wa kustaajabu katika chungu ya mambo, lakini cha ajabu mno kiumbe huyu huyu anashindwa kabisa kujistaajabia yeye Mwenyewe kwa Ajabu alizonazo, Kazi yangu mimi ni kukumbusha hizo Ajabu na baadhi ya mambo ambayo pengine mja kayasahau.
Ndani ya Ukumbusho huu asaa unaweza kupata kitu cha kushikamana nacho kikawa ndicho ufunguo wako wa mambo makubwa yanayo kusubiri huko mbele, Binaadamu ni kiumbe cha ajabu lakini mwenyewe si mwenye kujijua mpaka apate hekima itokayo kwa Mollah wake.
Amesema Mwenye enzi Mungu katika kitabu chake (Quraan sura ya Dhariyat aya ya 56).
وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ 
Sikuwaumba Majini na Watu(Wanaadamu) ila wapate kuniabudu.
Kwa Uzito wa maneno hayo inapaswa Mwanaadamu Aanguke kwa khofu ya Unyenyekevu, Lakini wapi anasubiri ganda la ndizi ndio limdondoshe lipate kumkumbusha udhaifu alo nao, "Maneno haya kama yataingia kwenye moyo wako yakazama kikweli" basi mazingatio yake yatakupelekea ujiulize swali hivyo madhumuni yangu nini mimi kuwapo hapa Ulimwenguni?.
Utafanya uchunguzi wa Nafsi yako, na ukianza uchunguzi huo ndio utapata mtiririko wa majawabu ya ajabu, yatanza kukushukia kutokea ndani kwenye Roho yako na kukujulisha kama wewe ni (Kiumbe Cha Ajabu). Wanasema Wanasayansi ajabu ya kwanza ya kiumbe ni (alama zake za vidole) hazifanani na yoyote katika Ulimwengu huu tokea mwanzo mpaka mwisho wa Dunia hii, hilo linamfanya Kiumbe kuwa (Unique)lazima aseme Mollah wangu kaniumba mimi sifanani na yoyote.
Mpaka hii leo hawakupatikana wanaadamu wawili wenye kufanana (Finger Prints)zao, Na sio hayo tu yamegundulikana mengine hata viungo vya ndani kila mmoja wetu tafauti na mwengine, Inaonesha Mollah wetu kachukua (special care) katika kumuumba kila mmoja wetu, ndio maana sasa hivi tumegundua kumbe hatufanani ndani wala nje, kwa hiyo tumeanza kutumia mpaka macho kuwa (Pin Number) unanyanyua jicho kuangalia Mlango unafunguka, Naam huyo ndio Mwanaadamu na hiyo ndio tafauti ya viumbe.
Sasa ikiwa hata kucha hatufanani inatakiwa mawazo haya yakikujia siku nyengine umesimama kwenye (Kioo), Usianze kutikisa mabega inabidi ujiulize nani kama mimi?, Unatakiwa useme kumbe Mollah wangu umeniumba mimi (Special) ili Nikuabudu!!, Ajiangalie Mwanaadamu maajabu aliyonayo katika nafsi yake halafu ajiulize hivyo mimi kweli natekeleza dhumuni nilopewa la kuwepo kwangu hapa Ulimwenguni.

AJABU YA KIUMBE PART 2

Asalaam Aleiykum

Imekujia Habari ya kwamba Mwenye enzi Mungu kakufanyia mambo unaishi kama Mfalme kwenye Ulimwengu huu, Kila kitu chako kakifanya kwa uwezo wake kiwe Rahisi juu yako ili usipate dhiki yoyote, basi hebu zitizame pumzi zako ingekua unazivuta wewe mwenyewe jee ungeshughulika wewe hata kutafuta hiyo mali, ungepata wewe nafasi hata ya kufanya maasi, lakini kwa Ukarimu wake kakufanyia zinaingia na kutoka pasi wewe kushughulika na chochote katika jambo hilo.
Tazama Usingizi wako unakuja bila ya wewe kuutafuta wala kuuomba, na ukimalizika unatoka bila hata ya wewe kua na uamuzi katika jambo hilo, "Ewe Kiumbe cha Ajabu" Angalia chakula chako ukishameza kinasagwa bila ya wewe kuingilia kati, Ukipata maradhi mwili unataka kitu kimoja kutoka kwako (Lala)nitajiponesha mimi mwenyewe, ndio maana ukaona unaambiwa (Mgonjwa kalazwa Hospital) zile dawa ni nyongeza tu za kuusaidia mwili lakini ni wenye kujiponesha wenyewe, Na zaidi ya hilo umewekewa ulinzi wa maradhi yasifike ndani.
"Ewe Kiumbe cha Ajabu" wewe umewekewa mpaka vifaa vya kulindwa macho, pua, masikio japo viko wazi lakini wadudu hawasogei midamu uko hai, na haikufiki dhara yoyote, Na viungo vya ndani vinafanya kazi zake kwa njia ya ajabu kuusafisha, kuutengeneza na kuuweka tayari mwili wako kwa kazi gani? (Hatukumuumba Mwanaadamu ila aniabudu) vinafanya kazi zake viungo hivyo kwa muda ulopangiwa kuishi kwenye Ulimwengu huu, baada ya hayo yote ukapewa uwezo wa kuukalia na kuumiliki mwili huo kwa Amri zako, sasa nyanyuka, , nenda, hamaki, cheka, angusha kilio, yote hayo yanafanya huo mwili wewe hayakugusi.
Wewe yasokugusa ndio unotakiwa baada ya fadhila zote, na neema zote, na ukarimu wote, na rehma zote unatakiwa sasa uubebe huo mwili kila wakati na kuupeleka kwa Mollah wako kwa njia ya mawazo(Kukumbuka) au (Physical) na useme Mollah wangu kwa haya yote mimi najisalimisha mbele yako kwa kunyenyekea, Nakushukuru kwa haya yote ulonifanyia, na mimi nakiri Mollah wangu yakua wewe ndie ulonipa uhai huu kwa ajili moja nayo ni kukuabudu wewe pekee.
Na Kwa hilo Mollah wangu wewe ni mwenye kunijua nimekua bakhili hata kuzifanya Ibada zenyewe, na nimekua mchache wa shukurani wa kutekeleza amri yako hii ya kufanya Ibada, Eti nimebaki na tamaa niipate pepo yako kwa tamaa zangu za jeuri, Mollah wangu mimi ni mwenye kutambua Neema zako zilizo nyingi kwangu mimi, Na mimi naelewa Mollah wangu hata hivi katika uchache wangu wa kukuabudu bado wewe ni Mwenye kunisubiri, kwani wewe ni mwenye kujua mimi sina pa kukimbilia, ni lazima nirejee kwako, nikishikwa na dhiki narejea kwako, nikiumwa wewe wa mwanzo nakukumbuka, na kila nikifanya hivyo nakukuta wewe ni mwenye kusubiri na mapenzi yako ya masamaha, na maajabu yangu yote nilonayo nina hali gani iwapo ntakua sitekelezi Amri zako?.

AJABU YA KIUMBE PART 3

Asalaam Aleiykum

Naipenda sana Hadith ya Nabii Adam a.s na Bibi Hawa  katika maisha yao ya peponi, hakika yana mazingatio makubwa ikiwa umepewa Hekima kutoka kwa Mollah wako, siku zote nikiwatizama wanyama wananikumbusha (Hadith)hiyo. Nakumbuka Kisa cha Baba yetu Adam, alivokua na Raha Peponi.
Watizame vizuri Wanyama hawana tafauti na sisi isipokua moja tu, tizama furaha walonayo, wanaamka wakiimba na kuita, wanamsabahi Mollah wao kila siku wala si wenye kuasi katika jambo hilo la (Ibada), Wanakula hichi na kile katika ardhi hii wanakwenda huku na kule wala hawana dhiki, Na wakishikwa na maradhi wanamtegemea Mollah wao ndie Mwenye kuwaponesha, hawana wasiwasi wowote, lakini sasa njoo kwa (Kiumbe cha Ajabu) Tafauti yetu na Wanyama ni moja lakini ni kubwa sana, Wanyama wana (Enjoy life) yao wanapata neema hizo na Baraka kutoka kwa Mollah wao wakiwa hawajui nini (Bliss)hawana (Awareness)Fahamu. Mwanaadamu yeye kapewa (Awareness)Fahamu za kuzijua neema na baraka za Mollah wake na hiyo (Bliss)Kwa hiyo Mwanaadamu aki(Enjoy) anazijua raha zake, akifanya Ibada anazijua fadhila zake alizotendewa na Mollah wake, na pia anaelewa yale yote yalowekwa ya kutoa sadaka, kufanya wema na hisani ni matendo ya mtihani wa kutizamwa vipi unaitumia hiyo (Awareness)Fahamu ulonayo.
Ukiwa utafanya jeuri ukatenda kwa makusudi basi juu yako hakuna kusamehewa, sababu unajua ukifanyacho na malipo yake ni yenye uhakika, lakini kwa mnyama yeye hajui na ndio maana na wewe ukifanya hujui unakua katika hali ya unyama, na kwa ajili hiyo unakua huna makosa, lakini ukitenda au kuacha Ibada wakati unajua basi malipo yake anayajua aliyekuumba, Na kama ukifanya alivyoamrisha basi utaanza kupata hicho kitu kinachoitwa (Bliss)hapa hapa duniani, na ukipata kitu hicho ndio utajua maajabu gani yanokusubiri huko akhera, Na ikiwa kakuumba wewe kwa njia ya ajabu, nini malipo yake yanayokusubiri, na malipo ya Mwenye enzi Mungu ni yenye ajabu isiyokatika ikiwa utayapata.
Lakini swali la kujiuliza jee unastahiki kuyapata kutokana na Ibada zako?, au Kwa Radhi zake?. Na kwa hilo inatosha ujiulize jee niyafanyao katika Ibada yanatosha?, jawabu unalo mwenyewe mimi kazi yangu ni kukuuliza kwa hilo nakutakia rehma za fahamu zikushukie.