Sunday, May 3, 2015

AJABU YA KIUMBE PART 1

Asalaam Aleiykum

Kiumbe ni Mtu wa kustaajabu katika chungu ya mambo, lakini cha ajabu mno kiumbe huyu huyu anashindwa kabisa kujistaajabia yeye Mwenyewe kwa Ajabu alizonazo, Kazi yangu mimi ni kukumbusha hizo Ajabu na baadhi ya mambo ambayo pengine mja kayasahau.
Ndani ya Ukumbusho huu asaa unaweza kupata kitu cha kushikamana nacho kikawa ndicho ufunguo wako wa mambo makubwa yanayo kusubiri huko mbele, Binaadamu ni kiumbe cha ajabu lakini mwenyewe si mwenye kujijua mpaka apate hekima itokayo kwa Mollah wake.
Amesema Mwenye enzi Mungu katika kitabu chake (Quraan sura ya Dhariyat aya ya 56).
وَمَا خَلَقۡتُ ٱلۡجِنَّ وَٱلۡإِنسَ إِلَّا لِيَعۡبُدُونِ 
Sikuwaumba Majini na Watu(Wanaadamu) ila wapate kuniabudu.
Kwa Uzito wa maneno hayo inapaswa Mwanaadamu Aanguke kwa khofu ya Unyenyekevu, Lakini wapi anasubiri ganda la ndizi ndio limdondoshe lipate kumkumbusha udhaifu alo nao, "Maneno haya kama yataingia kwenye moyo wako yakazama kikweli" basi mazingatio yake yatakupelekea ujiulize swali hivyo madhumuni yangu nini mimi kuwapo hapa Ulimwenguni?.
Utafanya uchunguzi wa Nafsi yako, na ukianza uchunguzi huo ndio utapata mtiririko wa majawabu ya ajabu, yatanza kukushukia kutokea ndani kwenye Roho yako na kukujulisha kama wewe ni (Kiumbe Cha Ajabu). Wanasema Wanasayansi ajabu ya kwanza ya kiumbe ni (alama zake za vidole) hazifanani na yoyote katika Ulimwengu huu tokea mwanzo mpaka mwisho wa Dunia hii, hilo linamfanya Kiumbe kuwa (Unique)lazima aseme Mollah wangu kaniumba mimi sifanani na yoyote.
Mpaka hii leo hawakupatikana wanaadamu wawili wenye kufanana (Finger Prints)zao, Na sio hayo tu yamegundulikana mengine hata viungo vya ndani kila mmoja wetu tafauti na mwengine, Inaonesha Mollah wetu kachukua (special care) katika kumuumba kila mmoja wetu, ndio maana sasa hivi tumegundua kumbe hatufanani ndani wala nje, kwa hiyo tumeanza kutumia mpaka macho kuwa (Pin Number) unanyanyua jicho kuangalia Mlango unafunguka, Naam huyo ndio Mwanaadamu na hiyo ndio tafauti ya viumbe.
Sasa ikiwa hata kucha hatufanani inatakiwa mawazo haya yakikujia siku nyengine umesimama kwenye (Kioo), Usianze kutikisa mabega inabidi ujiulize nani kama mimi?, Unatakiwa useme kumbe Mollah wangu umeniumba mimi (Special) ili Nikuabudu!!, Ajiangalie Mwanaadamu maajabu aliyonayo katika nafsi yake halafu ajiulize hivyo mimi kweli natekeleza dhumuni nilopewa la kuwepo kwangu hapa Ulimwenguni.

No comments:

Post a Comment