Asalaam Aleiykum
Unasikitika Mbona Sala yako dhaifu, unahisi kama husimamishi Sala vizuri, au wakati mwengine unasema bora nisali kabisa nindoshe udhia, Hiyo ndio Sala yako ya kila siku unavopeleka au kwenda kukaribiana na Mollah, sijui hata kama unafika karibu na hiyo Sala, kwanini ikawa hivyo kwa sababu imekua mazoea, kwa sababu huna mapenzi na jambo hilo umeambiwa kusali na wewe unajiburuta kwa kuogopa moto, ndio unakwenda unasimamisha sala.
Ukifika tu kwenye hiyo Sala unanyanyua mikono mbio mbio baada ya sekunde hamsini Sala ishamalizika, pengine hujui ni Sala, pengine hukijui kitendo hichi madhumuni yake, au huyajui maneno ya kutanguliza ukaifanya Sala yako irefuke na wewe uwe mtulivu kwenye hiyo Sala yako.
Sala imewekwa kwa vipindi ili kila mara ukumbuke kurejea Nyumbani kwa Mollah wako, kila mara ubebe huo Mwili wako na kurudi nyumbani ili upate kusema mimi nimepotea kwa kipindi fulani cha masaa, na kila nikipotea huko nendako nafanya makosa yaso idadi basi Mollah wangu Muumba naomba (Maghfira)Msamaha wako.
Vipi Utaanza Sala yako?
Hii ndio Darsa yetu ya leo kuondosha haraka zako na kuifanya Sala yako iwe angalau irefuke kidogo, angalau Malaika wapate kukupokea siku moja moja uwape nafasi ya kuandika maneno yako yanotoka mdomoni asaa kuna siku yatatoka moyoni na siku hiyo ndio utakua umeanza kuipata Sala.
Utaanza Sala yako kwa maneno haya:Ntayaandika kwa lugha ya (Kiswarab)"Allaahumma baaid baynee wa bayna khataayaaya kamaa baa'adta baynal mashriqi walmaghribi, Allaahumma naqqinnee min khataayaaya kamaa yunaqqath thawbul-abyadhu-minad-danasi,Allahum-maghsilnee min khataayaaya,bith-thalji walmaai walbarad".
"Ewe Mollah wangu nitenganishe mimi na madhambi yangu kama ulivotenganisha Mashariki na magharibi","Ewe Mollah wangu nisafishe mimi makosa yangu kama inavosafishwa nguo nyeupe kutolewa madowa", "Ewe Mollah wangu yakoshe Madhanbi yangu kwa Barafu, na Maji, na chembe chembe za theluji".
Hayo ndio yawe maneno yako ya mwanzo katika kuingia kwako kwenye Sala, kwa sababu wewe unahudhuria kwa Mollah wako kila kiungo kimebeba dhanbi, pengine umetizama ya haramu, umeshika yalo haramu, umekanyaga umeua kidudu njiani, kwa hiyo kabla ya kukutana na wewe Mollah wangu basi nakuomba nitenganishe mimi na dhanmbi zote kama ulivoitenganisha mashariki na magharibi, kwa wakati huu nakuja kwako tuwe mbali mbali.
Kwa heshima ya kuja kwako Mollah wangu nakuomba mimi nimebeba mengi yasiri na yaliyo dhahiri, ninayo yajua na nisiyo yajua basi nakuomba unisafishe nikitoka hapa niwe kama nguo nyeupe inavosafishwa uchafu wake ikawa madowa yote yameondoka, Mollah wangu nakuomba yakoshe Madhanbi yangu nisiwe nakumbuka kumbuka, yakwangue kwa kuyagandisha kwa Barafu, halafu yasafishe kwa maji, ikishe yaondoshe kabisa kwa mtiririko wa theluji yawe mbali na mimi nisiwe narejea rejea kwa kuyakumbuka.
Endelea part 2
No comments:
Post a Comment