Asalaam Aleiykum
Imekujia Habari ya kwamba Mwenye enzi Mungu kakufanyia mambo unaishi kama Mfalme kwenye Ulimwengu huu, Kila kitu chako kakifanya kwa uwezo wake kiwe Rahisi juu yako ili usipate dhiki yoyote, basi hebu zitizame pumzi zako ingekua unazivuta wewe mwenyewe jee ungeshughulika wewe hata kutafuta hiyo mali, ungepata wewe nafasi hata ya kufanya maasi, lakini kwa Ukarimu wake kakufanyia zinaingia na kutoka pasi wewe kushughulika na chochote katika jambo hilo.
Tazama Usingizi wako unakuja bila ya wewe kuutafuta wala kuuomba, na ukimalizika unatoka bila hata ya wewe kua na uamuzi katika jambo hilo, "Ewe Kiumbe cha Ajabu" Angalia chakula chako ukishameza kinasagwa bila ya wewe kuingilia kati, Ukipata maradhi mwili unataka kitu kimoja kutoka kwako (Lala)nitajiponesha mimi mwenyewe, ndio maana ukaona unaambiwa (Mgonjwa kalazwa Hospital) zile dawa ni nyongeza tu za kuusaidia mwili lakini ni wenye kujiponesha wenyewe, Na zaidi ya hilo umewekewa ulinzi wa maradhi yasifike ndani.
"Ewe Kiumbe cha Ajabu" wewe umewekewa mpaka vifaa vya kulindwa macho, pua, masikio japo viko wazi lakini wadudu hawasogei midamu uko hai, na haikufiki dhara yoyote, Na viungo vya ndani vinafanya kazi zake kwa njia ya ajabu kuusafisha, kuutengeneza na kuuweka tayari mwili wako kwa kazi gani? (Hatukumuumba Mwanaadamu ila aniabudu) vinafanya kazi zake viungo hivyo kwa muda ulopangiwa kuishi kwenye Ulimwengu huu, baada ya hayo yote ukapewa uwezo wa kuukalia na kuumiliki mwili huo kwa Amri zako, sasa nyanyuka, , nenda, hamaki, cheka, angusha kilio, yote hayo yanafanya huo mwili wewe hayakugusi.
Wewe yasokugusa ndio unotakiwa baada ya fadhila zote, na neema zote, na ukarimu wote, na rehma zote unatakiwa sasa uubebe huo mwili kila wakati na kuupeleka kwa Mollah wako kwa njia ya mawazo(Kukumbuka) au (Physical) na useme Mollah wangu kwa haya yote mimi najisalimisha mbele yako kwa kunyenyekea, Nakushukuru kwa haya yote ulonifanyia, na mimi nakiri Mollah wangu yakua wewe ndie ulonipa uhai huu kwa ajili moja nayo ni kukuabudu wewe pekee.
Na Kwa hilo Mollah wangu wewe ni mwenye kunijua nimekua bakhili hata kuzifanya Ibada zenyewe, na nimekua mchache wa shukurani wa kutekeleza amri yako hii ya kufanya Ibada, Eti nimebaki na tamaa niipate pepo yako kwa tamaa zangu za jeuri, Mollah wangu mimi ni mwenye kutambua Neema zako zilizo nyingi kwangu mimi, Na mimi naelewa Mollah wangu hata hivi katika uchache wangu wa kukuabudu bado wewe ni Mwenye kunisubiri, kwani wewe ni mwenye kujua mimi sina pa kukimbilia, ni lazima nirejee kwako, nikishikwa na dhiki narejea kwako, nikiumwa wewe wa mwanzo nakukumbuka, na kila nikifanya hivyo nakukuta wewe ni mwenye kusubiri na mapenzi yako ya masamaha, na maajabu yangu yote nilonayo nina hali gani iwapo ntakua sitekelezi Amri zako?.
No comments:
Post a Comment