Sunday, May 17, 2015

UGANGA NA MAOMBEZI (RUQYA) PART 3

Asalaam Aleiykum

Hiyo ni Baadhi ya mifano niloitaja, Basi ikiwa mambo madogo yanafanya kazi namna hiyo, Nini habari yetu sisi unapokutana na yule (Mja)alokua karibu na Mollah wake, Halafu akapewa hayo alopewa katika nguvu za Maombezi ili awasaidie wanaadamu wenzie, Sasa kutana na Muombezi aliyeteuliwa na Mollah wake awe na (Power)au Hijaza hio.
Ama kuhusu kupewa uwezo huo (Quraan sura ya Al-Anaam aya ya 165) Inasema,
وَهُوَ ٱلَّذِى جَعَلَڪُمۡ خَلَـٰٓٮِٕفَ ٱلۡأَرۡضِ وَرَفَعَ بَعۡضَكُمۡ فَوۡقَ بَعۡضٍ۬ دَرَجَـٰتٍ۬ لِّيَبۡلُوَكُمۡ فِى مَآ ءَاتَٮٰكُمۡ‌ۗ إِنَّ رَبَّكَ سَرِيعُ ٱلۡعِقَابِ وَإِنَّهُ ۥ لَغَفُورٌ۬ رَّحِيمُۢ 
"Ni Yeye ambaye aliyekufanyeni washikaji(Warithi)wa mahala pa hao walioondoka katika hii Ardhi, Na amewanyanyua baadhi yenu juu ya wengine daraja kubwa kubwa(Katika kila aina ya mambo)Ili akufanyieni mtihani kwa hayo alokupeni, Hakika Mollah wako ni mwepesi wa kuadhibu, Na hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe na Mwingi wa Kurehemu".
Huyu kapewa utajiri, yule kapewa umasikini, huyu msomi, kila mmoja wetu kapewa daraja yake katika fani tafauti, na kuna wengine wamepewa  fani hii ya uombezi, Na uwezo huu alopewa kapewa pia na ishara zake lakini si rahisi kwa mtu wa kawaida kuzigundua, Na mara nyingi unapelekwa kwake kwa njia za ajabu lakini unashindwa kumjua au kumuuliza, unafika mpaka kunyanyua simu lakini huwezi kuzungumza, kwa sababu huyu si mfanya biashara hajaweka kibao na kusema hapa unaombewa.
Na dalili nyengine hata akikuombea hataki malipo, na hata akichukua hayo malipo ni kwa ajili ya kukusaidia wewe na ubakhili wako, pengine hujatoa sadaka mwaka wa kumi, anakuonea huruma ndio anachukua hizo pesa kukutolea sadaka, mwenyewe hutoi, Jitizame wewe unakwenda kuombewa pengine (Bank) una hamsini Million, lakini kwa yule alokuombea unaacha elfu tano jiulize mwenyewe umekwenda kutafuta kupona au kufanya biashara ya kupona, Kwa hiyo Muombaji wa haki anajua udhaifu wako ndio maana anachukua baadhi ya hizo pesa na kukutolea sadaka, anakutolea zaka, kwani mbele ya muombaji anakuona kama(X-Ray) na Ubakhili wako, anajua pengine maradhi yako yamesababishwa na adabu ya kuwa vile unavopewa huvitoi,  anamuomba Mollah wake "Yaa Rabb" kiumbe chako hiki hakijui kitendacho, au Mshipa wa Ubakhili umemkamata basi msamehe namtolea mimi hii sadaka pasi na mwenyewe kujua, kiumbe chako hiki kimejaa upofu hakijui kinatenda jambo gani, basi sadaka hii na zaka hii kwa ajili ya idhini yako apone (Mja) huyu maradhi yake haya.
Usije ukadhani anatajirika kwa pesa yako, wenye kufanya hivyo pekee ni wafanya biashara. Sasa nini anafanya katika maombezi hayo?
Kwanza kumbuka Mtu huyu kapewa kipaji hicho na Mollah wake, Na yoyote yule alopewa kipaji hichi ana kitu kinaitwa (Sipiritual Eye)Sio kila mtu tu muombezi mpaka uwe na kitu kama hichi ndio unaweza kuwa umepewa (Hijaza)au baraka na Mollah wako ya kujua mambo, au magonjwa na dawa zake, Na kila mmoja wetu anacho kipaji hiki lakini wengine kipo kwenye biashara(Ndio mnasema akigusa jiwe linageuka dhahabu)ana muono mkali wakujua nini atauza na nini atapata hasara.
Sasa huyu alopewa uwezo wa kuponesha ukenda kwake anakuona kama inavokuona (X-Ray) hata wewe mwenyewe kama utapewa mafunzo unaweza kuona viungo vyako vya ndani lakini itachukua muda mrefu kwa wewe kuweza kufanya hivyo, Ukenda kwa mtu kama huyo anaweza kukwambia mpaka ulichokula jana ni kitu gani, Na huyo ndio mwenye uwezo wa kuona hiyo (Etheric Body) yako, Nini anafanya baada ya kuona matatizo yako?, Pengine kaona (Jinni)Linaishi kwenye hiyo (Body)yako, au una matatizo jinsi kadhaa wa kadhaa, ambayo yanatakiwa maombezi yake au unatakiwa uende hospital, yote atakueleza kwa uwazi bila ya kukudanganya, na ikiwa yanahitaji maombezi ya matibabu ya Quraan yeye anajua (Code) zake za hiyo Quraan na akichanganya na (Energy) yake ya maombezi ndipo anakusomea na ikisha kukupa maji au mafuta na kuyapulizia kile alichosoma, kwa kuwa ndani yaani(Deep inside) sote tuko (Inter connect) ndio yanatumika maji kama matibabu ya ndani na mafuta kuwa matibabu ya nje, hiyo ndio (Ruqya) na hayo ndio Maombezi, lakini wale wanobadilisha mchanga kuwa sukari, au kukwambia kalete nazi iloangakua yenyewe, sijui anataka kitambaa cheusi cha kuokota, samaki alokufa kinywa wazi, yote hayo ni (Mambo Jambo)ya kudanganywa na wala hakuna Tabibu yoyote, Mwenye (Energy au Power) inayoweza kuponesha watu kwa makundi ni muongo, msikubali kabisa mambo kama hayo, huyo (Jesus) mwenyewe alikua akiponesha mtu mmoja mmoja, leo wanafanya kuponesha watu kwa makundi wameanza kwenye (Ukiristo) na sasa wameingia kwenye  Uislam wanawauzia  watu dua elfu kumi, hasara ilioje kwa wale wenye kuamini, udanganyifu ulioje na kukubali kudhulumiwa.
Kwa hiyo (Ruqya)ni sehemu ya maombi anayopewa (Mja) ili apate kuwaponesha viumbe wenzie kwa (Idhini) ya Mollah wake, wale walokabiliwa na matatizo ambayo hayana ufumbuzi kwenye dunia hii yenye kuonekana(usiumwe na Malaria ukataka Ruqya), Na jambo hili halijakatazwa wala halina Uharamu wowote katika dini, ila unatakiwa umpate mtu mwenye fani hii ya kukuombea au kukusomea (Ruqya) ili upate nafuu au kupona kabisa.


No comments:

Post a Comment