Asalaam Aleiykum
Tumekwisha kuona au kusoma au kujua vipi (awareness)Fahamu zetu zinavokua zikikutana na jambo la (tupu), vipi akili ina haribika, uharibifu gani unatokea, na sasa tunajua nini kinatokea kama kitu hicho kitafunikwa. Sasa ni wakati wa kulihudhuria Vazi la pili la Ucha Mungu, lile la mwanzo ni Vazi la (Mind)Akili na Utupu, Na hili la Pili ni la (Roho)na Ibada.
Kazi yetu kubwa hapa ni kujua vipi tutalivaa, basi kama aya ilivosema vazi hilo ni bora kwenu na hizo ni (alama)kutoka kwa Mollah wetu ili tupate "kukumbuka". Naendelea kukuonesha tena neno "(kukumbuka)", nakutaka ukumbuke lile vazi la kwanza Nje ni Guo na ndani ni utulivu, Na hili la Pili Nje (Action) ndani Mapenzi, Nini Utulivu? Utulivu ni (Peace)Islam(Surrender), Nini Mapenzi? ni (Bliss).
Kutokana na hayo Mapenzi wewe ndio umeumbwa, kutokana na hayo mapenzi wewe ndio unaishi, kutokana na hayo mapenzi wewe Unaruzukiwa, kutokana na hayo mapenzi Ulimwengu huu unamsabahi Mwenye enzi Mungu, Sasa na wewe unakumbushwa jiunge na Mapenzi hayo ili upate Furaha, upate afya na uipate Pepo ya Mollah wako, Na sharti lenyewe la kujiunga ni lazima uvae hili vazi la Ucha Mungu, unatakiwa bila ya kulazimishwa Umpende Mollah wako, uwapende viumbe wenzako, na utende yalo mema.
Ikiwa utafanya hivo kwa uadilifu kwa upande wake Mwenye enzi Mungu atakupa hayo mambo matatu ambayo yamo katika hiyo Ramadhan, Rehma, Maghfira na Dhamana ya kutoingia motoni.
Vipi tutalivaa Guo hili la Taqwa?
Kumbuka bado tumo kwenye safari yetu ya kutafuta vazi la Taqwa na sasa tunachukua aya hususia iloamrisha kufunga Ramadhan(Baqara 183).
"يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡڪُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِڪُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ "
Enyi Mloamini Mmelazimishwa kufunga(saumu)kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.
Kabla ya kuendelea mbele wacha turudi nyuma tukalihudhurie lile tukio maarufu la mwanzo waloambiwa wazee wetu Bwana Adam na Bibi Hawa walipokatazwa wasile tunda kwenye ule mti, Nini kiliwatokezea walipokwenda kinyume na Amri ya Mwenye enzi Mungu? walipata (Awareness)Fahamu.
Basi Napenda utambue na hivi sasa mnaamrishwa tena msile(Fungeni) Nini Kinapatikana?, Hapa itabidi mnipe nafasi nifafanue japo kwa ufupi ili mpate kunifahamu, Napenda kufahamisha kuwa kuna vitu vitatu vinatokea kwa Mollah wetu navyo ni hivi(From awareness to intelligence from intelligence to love) Na hayo Mapenzi ndio zawadi ya juu Mja kushushiwa kutoka kwa Mollah wako, Nisiseme Mapenzi watu (Wakaanza kuchemsha Supu za Pweza, wengine wakatafuta uji wa kungu manga, na wengine kumtafuta ndege kisiji)sio aina hiyo ya mapenzi, Mapenzi yalokusudiwa hapo yale yanokuja bila sababu, yale unatoa huhitaji malipo, yale ambayo uko radhi kulala na njaa mwenzio apate kula yeye, mapenzi ya mfano wa Mama hatarajii hata kama utampenda kama anavokupenda yeye, yeye anafanya (for the sake of Love)Sasa nini unapata kama utafunga kikweli kweli kwa Imani ya juu kabisa? hapa inabidi ukumbuke tena ulipokula tunda ulipata (Awareness)Fahamu, na sasa kitu cha mwanzo unapata nini?
Endelea part 4
No comments:
Post a Comment