Tuesday, May 29, 2012

SALA YA TASBIH

Asalaam-Aleiykum Ameagiza Bwana Mtume s.a.w tuipate sala hii ya tasbih ikiwa tutaweza basi tuisali kwa siku mara moja, Au kama hatuwezi basi iwe kila ijumaa na kama haiwezekani basi hata kwa mwezi mara moja, na kama hivo pia ni ugumu basi tufanye mwaka mara moja, na kama hatuwezi kabisa basi angalau katika umri wako uipate mara moja. Imekua Sala hii akiipata muumin basi husamehewa Dhanbi zake zote, kwanini ikawa hivo, kwa sababu hiyo ni sala pekee inoweza angalau kwa mara moja ukapata bahati ya kuipata hicho kitu kinachoitwa sala, kwa sababu ya shuruti za idadi ya hizo tasbih za dhikr zilizomo humo, hupati nafasi ya kufikiri Bank, au kuwaza nyimbo za tarab, au kukumbuka mambo yako ya mipira,Jaribu uipate utaona ladha ya sala hii. Vipi inasaliwa? Utasali Rakaa nne,na kila kwenye Rakaa Utasoma Suratil fatiha(Alhamdu)na sura nyengine yoyote ile uitakayo,utakapomaliza kusoma hali yakua bado umesimama utasema maneno haya(Subbhana-Allah-,Walhammdulillah-wallah-illah-illah-Allah-wallahu-Akbar)mara kumi na tano(15), Ikisha utarukuu utasema mara (10)halafu ukinyanyua kichwa kutoka kwenye rukuu utasoma mara (10),Ikisha utakwenda katika sijda utasoma mara (10)ikisha ukinyanyua kichwa kutoka katika sijda utasoma mara (10)Ikisha utasujudu tena utasoma mara (10)na ukinyanyua kichwa kutoka katika sijda utasoma mara(10)na hivo utakua umepata mara (75)katika kila rakaa na humo ndani yake utakua umepata (Tasbih)(Tahmid)(Takbir)wa (Tahlil)na jumla yake utakuwa umepata hizo dhikr 300 kwa kila neno moja katika hayo manne utapata idadi mara 75.Amekua mwenye kufaulu mwenye kuipata sala hii kwa wingi kama alivosema Mollah wako katika sura ya (Nasr)فَسَبِّحۡ بِحَمۡدِ رَبِّكَ وَٱسۡتَغۡفِرۡهُ‌ۚ إِنَّهُ ۥ ڪَانَ تَوَّابَۢا "Msabih Mollah wako mlezi,na umuombe msamaha,hakika yeye ndiye anaepokea toba" Alipokutana Bwana Mtume s.a.w na Sayyidna Ibrahim Khalil a.s katika mbingu ya saba Nabii Ibrahiim a.s alimwambia Bwana Mtume s.a.w "Nitolee salamu kwa umma wako wape habari waambie peponi kuna udongo mzuri, na maji yake masafi na matuta ya kupanda na mbegu zake ni (Subhanna-Allah)Wal-hamdulillah(Wallaillah-illah-Allah)Wallahu-Akbar. Mwenye-enzi-Mungu atujaalie tupate fadhila zake katika Ibada hii.

Monday, May 28, 2012

UMUHIMU WA KAZI KATIKA DINI

Asalaam-Aleiykum. "Ametukuka Mollah wetu alieumba Ulimwengu huu na sisi wanaadamu ikisha akatuwekea njia tatu za lazima tuzipitie nazo ni Jitihada, Matatizo,na Kipato ili apate kututizama katika Ulimwengu wa akhera nani alofanikiwa katika hizo jitihada, Nani aloshindana na matatizo yake kimaisha akafaulu na yupi yule alopata kipato kizuri akakitumia kwa mambo ya kheri. Kipato kwa mwanaadamu sio hasa kusudio la maisha ya kiumbe bali ni njia yakumuezesha kuishi katika ulimwengu huu kwa njia ya halali na kwa ajili ya kufanya ibada za kumuabudu Mollah wake na kupata radhi na Taqwa za ukamilifu kwa ajili ya kumkurubia Mollah wake,Ndio maana Bwana Mtume s.a.w akahimiza sana Umma wake watu watafute na wafanye kazi za halali pamoja na biashara akasema "Enyi Umma wangu jizuieni na kuomba,fanyeni jitihada kuzitizama familia zenu, pia kuweni na huruma kwa ajili ya majirani zenu,na yoyote yule ambaye atatafuta riziki yake kwa njia ya halali atakutana na Mollah wake uso wake unangara kama vile mbaa Mwezi ingaravo". Siku moja Bwana Mtume s.a.w alikua amekaa na Masahaba akapita kijana anakwenda mbio dukani wakasema Masahaba lau mbio za kijana yule angekua anakimbilia mambo ya dini yake basi angepata kheri kubwa,"Akasema Bwana Mtume s.a.w" Msiseme maneno hayo lau ikiwa anakimbia kijana yule kujiepusha na kuomba au kutegemea watu wengine au akajikinga na jambo la kuomba au ikawa anawatizama wazee wake au watoto wake, basi yeye yumo katika Jihad kwa ajili ya Mollah wake. Akaendelea kusema Bwana Mtume s.a.w "Mollah anampenda yule ambaye anajitolea kufanya kazi ili asitegemee watu wengine". Akamalizia Bwana Mtume s.a.w na Kusema muogopeni Mollah wenu kwa kutafuta riziki ya halali. Nabii Isa a.s Alimuuliza kijana Mmoja akamuuliza unafanya kazi gani katika maisha yako, yule kijana akajibu kazi yangu mimi ni kumuabudu Mollah,"akamuuliza nani anakupa chakula, yule kijana akajibu kaka yangu, Nabii Isa a.s akamwambia kaka yako anafanya ibada zaidi ya kumuabudu Mollah wake kuliko wewe. Akasema Bwana Mtume s.a.w Bora uwe Mchukuzi wa mizigo kuliko ukapita ukawa unaomba, Yule Mpewa hekima na Mollah wake Luqman alimuusia mwanawe na kumwambia ewe Mwanangu ufunge mlango wa umaskini kwa kutafuta riziki ya halali, kwani yule asopenda kazi yanamkuta mambo matatu, la kwanza Dini haingii sawa sawa katika moyo wake, pili hapati elimu yoyote katika hekima zake,na la mwisho anapoteza utu wake.Amesema Bwana Mtume s.a.w "Ni sheria ya wajibu kwa kila Muislam kutafuta riziki ya halali, yoyote yule mwenye kujitahidi kutafuta riziki ya halali basi daraja yake ni sawa na yule ambaye amepigana jihad kwa ajili ya dini yake, akaendelea bwana Mtume s.a.w yoyote yule katika Muislam alokula riziki ya halali kwa muda wa siku arobaini basi Mollah wake atuungarisha moyo wake, atatia hekima katika akili yake na ulimi wake, basi ndugu zangu tujitahidini sana kutafuta kazi za halali na kuacha kula haramu.Tuombe Mollah atusaidie kwa hili.

Friday, May 18, 2012

ZAWADI YA RAMADHANI (TAQWA NA MAPENZI YA ALLAH) PART 2

Asalaam Aleiykum

"Ewe Jumba la milango Tisa"


Ukitaka kufunga na saum yako ipate Rehma za Mollah wako basi kwanza funga mlango wako wa kwanza yaani (macho)acha kutizama wanawake usirandishe macho yako katika kutizama mambo ya maasi jitahidi sana hata ukiweza kuondoka mjini chukua likizo kazini si unataka funga yako ikubalike jitenge na mji usitazame mambo ya maasi yasikushughlishe kabisa wakati huu wa mwezi mmoja mambo ya kidunia.

"Naam ikisha funga mlango wako wa pili Yaani (Mashikio)acha kusikiliza mambo machafu,fitna,na uongo jishughulishe na kusikiza maneno ya kuilea roho katika njia ya taqwa.

Ama mlango wa tatu ni pua zuia kunusa nusa manukato,harufu watu wamepika nini na n.k.

Na huu mlango wa nne ni katika kusema watu,kula haramu,kufanya masighara ya upuuzi katika mwezi huu mtukufu.

Na milango yako miwili ya mwisho ni kujizulia mambo ya (Sex)au kujamiana kwa njia za haramu, ukiweza kufanikiwa bara bara kujizuia na mambo yote yanotendwa na hiyo milango tisa kwa ukamilifu basi likitima kumi la mwanzo unakua umeshakamilishiwa Rehma yako utajiona mtu ulobadilika na Rehma za Mollah wako zinafanya kazi kwa siri na dhahiri pengine ulikua na maradhi yanataka kuja juu yanaponeshwa, unakamilika rasmi na matendo hayo yakikamilika hasa utaona mku wa jumba(Akili) anavotulia mustaqim katika mambo ya ibada na mapenzi juu ya Mollah wako na ukitimiza hayo unakua umekamilishan taqwa katika mezi huu.

"Amesema"Umar bin Abdul-aziz r.a"

"Sio kumcha Mollah kwa kufunga mchana au kusali usiku au yaliyomo baina yake"

Bali hiyo taqwa ni kuacha aloharamisha Mollah wako"ama hayo ya Ibada ni mapenzi kwa Mollah ndio unafanya kutukuza na kumuomba uwe karibu yake.

Akahadithia "Abuu Darda r.a "Taqwa ya kweli ni ile inayomfanya mja hata cha halali akawa anahofia kisije kuwa cha haramu" hivi ndio tunatakiwa tufunge ndio tukaitwa sote katika siku hizi chache tutende hayo si kujizuia kula ndio tukaaona tumefunga,ikisha tukaamrishwa ondokeni jitengeni mwezi huu nendeni kajificheni (miskitini)fanyeni itikaf mumkumbuke Mollah wenu wenzetu wanaita (meditation)unavotaka kuita lakini umeamrishwa ukajitenge ili upate kumkumbuka Mollah wako,usije ukasema aah imesemwa kwenye aya (Ankiffu fil masjid)ardhi yoyote ilo tohara basi hapo ndio masjid kwani neno masjid limetokana na sehemu wanayosujudu kwa hiyo popote unapoweza kusujudu hapo ndio msikiti wako.

Basi hilo ndilo kumi la mwanzo ukiliweza unapokewa katika kumi la pili la maghfira inshaalah kwenye maudhui ijayo tutalizungumza hilo.

Mollah ndie ajuae sisi ni wenye kujitahidi penye kosa nisahihisheni


A.Baja

ZAWADI YA RAMADHANI (TAQWA NA MAPENZI YA ALLAH) PART 1

Asalaam Aleiykum.

Ndugu zangu katika Uislam umetukaribia Mwezi mtukufu wa Ramadhan wenye mambo mawili makubwa yatokayo kwa Mollah wetu yaani Rehma na Baraka, ambayo unayo hakika kuyapata katika mwezi huu kuliko miezi mengine yoyote ilopita.

Kuyapata mambo hayo mawili unatakiwa kutimiza masharti yake ambayo ndio dhamira yangu ya maudhui hii, wengi wetu tunafata mwenendo tu yakua watu wameeacha kula mchana na sisi hatuli tunangoja magharibi jua likizama ili nasi tupate kula, basi nakujulisha kuwa hakushindwa Mollah wetu kutuambia 

"Enyi mloamini acheni kula mchana ili mle usiku"

Lakini katutakia kheri na rehma zake akatutengea mwezi wetu huu maalum kwa kutuamrisha 

"Enyi Mloamini nimekuamrisheni kufunga kama nilivowaamrisha walopita kabla yenu ili mpate kumcha Mollah".

Nini kufunga?
Iibada hii nyinyi mmekusanywa pamoja umma wote wa kiislamu haki sawa hakuna sheikh wala sharif hakuna yoyote isipokua yule atofunga inavotakiwa ndio atopata malipo yake, Ndani ya Mwezi huu kama ulivogawika mafungu matatu yaani la mwanzo Rehma, la pili Maghfira(kusamehewa)na la tatu Dhamana ya kutoingia motoni sasa mambo haya matatu yanapatikana vipi? 

Ama kuhusu hilo la Rehma ni kumi la mwanzo.

"Ewe jumba la milango tisa funga milango yako usiku na mchana katika mwezi huu upate kurehemewa" 

Na kama huijui hiyo Rehma basi jikumbushe kidogo sura ya "Maryam"na kisa cha Nabii Zakariyya a.s

"2(Wakumbushe)ukumbusho wa Rehma ya Mollah wako alipomrehemu mja wake Zakariyya" alifanya nini Zakariyya? 

"3(Alipomuomba)alipomlingania Mollah wake kwa siri". 

"4(Akasema Mollah wangu,mifupa yangu imekua dhaifu)(nimezeeka mimi)na kichwa changu kimeshakua kinang'ara kwa(Mvi)wala sikua mwenye bahati mbaya (au kuhasirika)katika kukuomba wewe.

"5(Na hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu(kuharibu dini) Na mke wangu ni tasa)(Hazai kabisa)basi naomba nipe mrithi (anijie)kutoka kwako.

"7(Ewe zakariyya tunakupa habari njema ya kuwa (utapata mtoto) Jina lake ni Yahya, hatujafanya kabla yake mwenye jina kama hilo).

Hiyo ndio Rehma ya Mollah wako huyo ni Nabii keshakua mtu mzima na mkewe Tasa kamlingania Mollah wake kwa siri akapewa Rehma kwa kupewa mtoto mambo yamegeuzwa kwa ajili ya maombi ya siri sasa nini habari yetu mimi na wewe tunofunga kwa siri? vipi tutapata Rehma tulopangiwa.

soma jumba la milango tisa katika ukurasa wa pili.

A.Baja

MADALALI WA IBLIS (SHETANI) PART 2

Asalaam Aleiykum.

"Naam Amma kuhusu Madalali kidogo hunifika kazi ya kuwabatiza, sababu wanashituka shituka kwa chembe za hofu zilobaki kwenye mioyo, basi hufanya nini?

Nitakujulisheni kujua dalili zao ni kama hivi:

" Humuingia dalali wa kike nikamshughulisha sana katika kivazi chake hatoki mwanamke huyu mpaka awe na hakika nyama zake zimeikamata sawa sawa na ile nguo, huyu ananifanyia kazi kwa kunipatia wateja kwa makundi kwani kila anayemtizama kaumia, basi hupita mwanamke huyu akiasi njia nzima pamoja na wanomtamani hakuna yoyote mwenye kutafakari kwamba hilo ni kosa.Humzidishia vituko huyu ikawa kila nguo anoivaa ni kubwa watu watasemaje ndio amezeeka basi hutoka yeye huku manyama yakimtetemeka na huwa shari tupu mpaka akirudi nyumbani.

Amma Dalali wangu mwengine yule mwenye kupita kutafuta habari za watu na kuzitangaza, Mimi humuandama huyu akawa kama mgonjwa lazima apate habari za fulani ikisha humshawishi aziongeze chumvi na hapo wengine wakizipokea na wao huzisambaza.Wote hao hunifanyia kazi yangu kwa kujitolea.

"Humtia dhiki mimi dalali wangu mwenye kufanya kazi sehemu za dhamana huyu humfanyia wasiwasi akajiona ni maskini huanza kuchukua mali ya watu kidogo kidogo akawa hana hofu kwa matendo hayo na huku akipita anatingisha ufunguo yakua sasa keshatajirika kwa pesa za haramu.

Ikisha humfanya mwengine kuwa Dalali kwa kupita kusema uongo na ukitaka kumjua, angalieni mkikutana naye basi huanza fulani hivi fulani hivi . 

Pia huwajulisha dalali wangu pale ukiona kundi la wanawake limevaa hijab na mmoja wao hakuvaa basi jueni huyo ni dalali wangu ,pia huwaingia mie matajiri na maskini katika kila nyanja ya maisha yao.

 قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ

"Naapa kwa haki ya Utukufu wako,Nitawapoteza wote(katika njia yako)"

Basi utawaona madalali zangu kwenye ngoma, huku wamejipanga kwa makundi wanamuasi Mollah wao, hawa kwenye maasi wao wanakua mwanzo, wakikaa hawana amali ili kuzungumza maasi na ufisadi,kila wakikaa wawili anoanza mazungumzo hamtaji Mollah wake kabisa. 

Msishtuke kuwaona wanadanganya danganya kuingia miskitini na kusoma Qur'aan hao hawana kitu kabisa, huwafata mimi ndani ya hiyo misikiti nikamfanya mmoja wao ndio awe anaona yeye amehitimu,sasa ndio anatoa fatwa za kuzua zua, na mtamuona ana kiburi yeye anajipeleka peponi wenzie wote anawatia motoni.

Kumbe maskini yeye mwenyewe hamjui hata Mollah wake, humtia nguvu huyu za kuupenda Uimamu akaupigania kwa nguvu zote ili afanye fisadi ndani ya Dini, jueni yakua huyo pia dalali wangu.

Bbasi huwaingia mie nikawatia matajiri wasi wasi mkubwa nikawafanya wao pia kuwa Madalali wangu kwa vipi, wako tayari kuchangia mambo ya ufuska kuliko kulisha yatima, zakka huisahau kabisa. Na huzipamba nyimbo na ngoma ili kuwasahaulisha kabisa kama Mollah anawaangalia.

"Wakasema Malaika" zaidi ya hayo yote Mollah wao kawachukulia dhamana kwa kuwashushia aya inosema "

وَمَا كَانَ اللّهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ وَمَا كَانَ اللّهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ 

"Na hakuwa Mollah wako mwenye kuwaadhibu hali uko nao, na hakua mwenye kuwaadhibu hali yakua wanaomba msamaha".

"Akasema Ibilis"Hawa ntawafanyia vitimbi hakuna hata mmoja atokumbuka huko kutubu, nitawakusanya hawa na watoto wao niwashushie kioo changu nini hicho kioo? 

Watakaa hawa kwenye TV wasikumbuke kabisa kumdhukuru Mollah na wakishamaliza basi nitawachunga chunga mpaka kitandani na kuhakikisha hakuna hata mmoja anomshukuru Mollah wake na wakiamka pia hawatomtaja. Wataendelea kusengenya watu,kudhulumu,kula rushwa watadumu hawa kwenye maasi mpaka siku wanokutana na Mollah wao na hata wasijijue kwanini hawa kutubu.

Kwa hiyo ndugu zangu kila mmoja akae na kutafakari vipi atapigana (Jihad)hii ili asiwe Dalali wa Ibilis.

Imetaarishwa na kuletwa kwenu na
A.Baja

MADALALI WA IBLIS (SHETANI) PART 1

Asalaam Aleiykum.


"Nakuomba Mollah wangu Yasipite Makala haya isipokua yawe uzinduo japo kwa mmoja atakayesoma na ikiwa imepatikana faida kwake ya kuacha japo moja katika yaliyomo kwenye maudhui hii basi Yaa Rabbi usimpe yeye peke yake faraja yako ya kusamehe ila naomba namie nilomtumia niwemo"

Na nyenyekea katika enzi ya uwezo wako kuwaombea Rehma Maiti wote wa Kiislam,pia Waislam wanaume pamoja na wanawake kwa sote tuteremshie Rehma yako ulotupangia ya kutusamehe "Dhanbi zetu".Amin.

"Waliulizana Malaika inakuaje kiumbe huyu mwanaadamu fadhila zote na wema wote alotukuzwa na Mollah wao mpaka sisi Malaika tukaambia tumsujudie halafu yeye anakua asi wala si mwenye kuhofu uwezo wa Mollah wao"

Malaika wamejaa huzuni dhambi anazotenda mwanaadamu zimetawala katika mazungumzo yao. Alisikia Ibilis mjadala huu akasema, Mnataka nikufahamisheni inakuaje?Wakajibu Malaika tujulishe ewe Ibilis kwani wewe uko nao hawa kila wakati.

"Akasema Ibilis" Jambo la mwanzo kabisa ninalofanya kwanza Nawavua nguo zao mbili, Mimi nawavamia hawa halafu nachana kabisa ile nguo yao ilogandana na mwili ili asinipe tabu kumshawishi, nikimaliza kuwavua tu huanza hawa kutamaniana na mimi najua udhaifu wao uko wapi, Halafu naliandama guo lao la pili hili la Ucha Mungu nikisha wavua hili wamekwisha wanabakia kama wanyama wanakua hawana tafauti tena na simba ,chui, farasi wanavamiana tu.
Huyo ndio Ibilis hayo ndio maneno anoyasema"sasa ukiyapinga rejea "Quraan"

يَا بَنِي آدَمَ لاَ يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْءَاتِهِمَا إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لاَ تَرَوْنَهُمْ إِنَّا جَعَلْنَا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاء لِلَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ

"Enyi wanaadamu asikuftini Shetan kama alivowafitini wazee wenu akawatoa katika Pepo,(alifanya nini?)

"Kwanza"aliwavua nguo ili kuwaonesha (Jinsia zao)Hakika huyu (Ibilis)Na kabila lake ni wenye kukuoneni pasi ya nyinyi kuwaona,Na sisi tukajaalia shetani kuwa marafiki wa wale wasooamini.

"Enhe Endelea Ibilis kutujulisha nini cha zaidi unawafanyia"

Akaendelea Ibilis mimi huwagawa hawa katika makundi mawili kundi la mwanzo nalichukulia dhamana la kuingia nalo motoni, Kundi hili la mwanzo linajiunga kabisa na kabila langu linakua sisi na wao hatuna tafauti, sote tunakuwa tushafukuzwa katika ufalme wa Mtukufu Mollah wetu.Basi huwabatiza wakawa hawasikii tena dua yoyote, na mkitaka kuwajua hawa waliomo katika kabila langu wa kwanza kabisa ni kiongozi (Dhalim) huyu hana shaka, halafu tena wanafatia walevi,wazinifu,washirikina,wachawi,wapiga ramli na wengi walojifunga na mijidhanbi mikubwa.Hawa nakuwa sina haja nao tena kwani hunifanyia kazi zangu (automatic)sina haja hata ya kuwashawishi.

Amma kuhusu hawa madalali wangu "

وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ فَهُمْ لَا يَهْتَدُونَ 

"Na shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia (wakawa hawaoni)njia zote za kheri, kwa hiyo hawakuongoka".

Usikose kuwajua Madalali wa Ibilis katika makala inofatia.

Imetaarishwa na kuletwa kwenu na
A.Baja

ADHABU YA KABURI

Asalaam-Aleiykum

Katika Buku la Pope Gregory la Dilogue lilotungwa 6 century kuna habari ya Askari mmoja alokumbwa na maradhi ya (Plague) akadhaniwa amekufa kalala mwili hauna uhai kabisa.


"Anasimulia askari huyu Mara nikaona nimetoka kwenye mwili wangu nimekwenda mpaka karibu ya daraja nikaona daraja hilo chini yake linapita tope mfano wake kama tope za volcano zikikugusa umeumia upande wa pili wa hilo daraja nikaona kuna watu wamevaa vivazi vizuri na bustani za maua yanonukia sijapata kuona uzuri wa harufu yake na hao watu kila mtu ana sehemu yake ya kupumzikia wanatembea huku na kule kwa furaha na huku wakiwa wameridhika.

Juu ya lile Daraja nikaona kuna watu wengi wanafanyiwa mtihani wakupita lakini wengi wao wanaanguka na kila wakianguka anatangaza mtu hawa ndio walokua wakifanya mabaya ulimwenguni masikini wale watu wakianguka tu mara ngozi zina wavuka kwa moto mkali uliopo hapo chini ya hilo daraja, Huku nikawaona wengine wanapita bila ya wasi wasi na wanavuka kwa salama kwenda ule upande wa pili. 

Nikamuona mfanyabiashara Mmoja nnaye mjua anayeitwa Stephen naye anajaribu kuvuka mara akateleza mguu akawa ananinginia(hanging)akatokea kiumbe cha kutisha chini ya lile daraja na kuanza kumvuta mara huku juu akatokea kiumbe mzuri kavaa guo jeupe akawa anamvuta kwa juu.

Wakati kinyanganyiro hicho kinaendelea huyu anoshuhudia mambo hayo akarejea kwenye mwili wake na hakujua matokeo yale ya vuta nikuvute:

Naam hiyo ndio habari ya huyo Askari alo (survive plague)na kuhadithia hayo aloyaona-wakaiita hali kama hii kwa lugha ya kiengereza (OBE)out of body experience: 

Alisimama yule Sahaba mkubwa wa kiislamu,Anokesha usiku kusoma Quraa'n kipenzi cha Mwenye-enzi-Mungu Syd na Othman bin Affan r.a kasimama analia kwenye kaburi alipoulizwa unalilia nini? akasema silii kwa kukumbuka Pepo au Moto ila nalia kwa kukumbuka makaazi ya kaburini sehemu ya upweke hukutani na chochote isipokua adhabu na mateso au raha na ahadi njema, akaendelea kusema nimemsikia Bw Mtume s.a.w anasema,

 "hakika ya kaburi ni utambulisho wa Nyumba utakayokaa huko akhera mfano wa Peponi au Motoni:

Enyi wanaadamu ukishakufukiwa kaburi husema katika watu waloingia, leo umekuja leo weye na jeuri zako, hapa huna tena kiburi chako,hapa huna tena ule uwezo ulokutia jeuri huko ulimwenguni,mimi ni jumba la upweke,mimi ni jumba la wadudu leo humu uko peke yako na kabla hajakufaidi yoyote wacha nikuanze mimi hapo tena mtu muovu hubanwa mpaka mbavu zikakutana.

Enyi Wanaadamu tahadharini kuja huku na uovo wenu kwani mimi nimepewa amri nifanye nini?kwanza nilivunje vunje jeneza lake au kibox chake unozikiwa, Ikisha niichane sanda yako nianze kunywa damu na nyama yake, Hapo ndipo Hadrat "Abdul Aziz" r.a akasema 

"Enyi binaadamu Tahadharini sana na kuipenda dunia hii kwani ukiwa tajiri hapa huko kesho utakua muombaji, ukiwa kijana basi uzee unakusubiri, na Wako wapi walotawala miji,wakajenga majumba,wakadhulumu wenzao,mnajua nini kinawafika chini ya Ardhi? 

Isikudanganyeni dunia kwani tajiri na maskini wote wanalala chini ya Ardhi basi fanya mema ili tandiko lako liwe zuri.
Akitiwa mtu kaburini Ardhi ina nadi wacha leo ulipwe kama ulivokua unafanya duniani"

Alikuja kijana mmoja kwa Abdul Malik ana huzuni kubwa akamuuliza yule kijana nini umefanya yule kijana machozi yakawa yanamtoka hajibu kitu akamuuliza tena umefanya dhambi kubwa iso samahani yule kijana akasema naam mimi kazi yangu ilikua naiba sanda wakifukiwa maiti mimi nishafika nawavua nakwenda kuuza, siku hiyo nikachimba kaburi nikakuta maiti uso umevurugika kutaka kuondoka nikasikia sauti inanambia usiondoke unajua huyo maiti kwanini yuko hali hiyo nikasema sijui:

nikaambiwa huyo alikua akipuuza sala hataki jambo la kusali kabisa, nikaambiwa nenda kafukue Kaburi la pili: 

Baada ya kufukua nikaona mtu ana alama za kuteswa lakini ana uso wa nguruwe nikaambiwa huyo alikua mlevi na mpaka anaondoka ulimwenguni kashindwa kuuwacha mvino:nikaamrishwa nikafukue kaburi la tatu:

Na hapo nikakuta domo la maiti limevimba na ulimi umevutwa umechomwa moto,nikaambiwa huyo alikua kazi yake kusema watu na kufitinisha:

Nikapewa amri tena nifukue kaburi la nne 

Hapo nikaona maiti imepigiliwa na misumari sitini mkononi nikaambiwa huyu alikua akiwapa mikono wake za watu.

Halafu nikaambiwa kila anoingia huku na dhambi zake basi tumshghulikia mpaka iifike siku ya Kiama na akioza anarejeshwa tena huku hakuna mauti.

Yule kijana akachukua ahadi ya kuwacha na kuanza kuwa mtu mwema mpaka mwisho wa maisha yake:

Adhabu zipo nyingi sana itachukua bahari nzima kuziandika zote, Basi ikiwa wewe bado unapinga habari hii kwani hukumbuki sisi ndio tulokuwa tunakuangalia ule wakati wa miezi tisa tumboni?basi ikiwa unaamini makaazi yale yapo basi kuwa na hakika na huku vile vile yapo tafauti lile tumbo la mzazi wako na hili ulotiwa sasa hivi ni tumbo la Ardhi huku hakuna mtetezi isipokua amali zako njema: 

Inshaalah Mollah atuepushe na adhabu za kaburi sote jamii ya kiislamu.

Imetaarishwa na kuletwa kwenu na
A Baja

Tuesday, May 15, 2012

NINI IBADA? (NA MAANA YAKE) PART 1

Asalaam-Aleiykum.

Kabla ya kuanza Maudhui hii wacha nikupe faida ya kufahamu.



Nini kufahamu? 
Kufahamu ni kujenga daraja baina ya mimi muandikaji na wewe msomaji tukawa tunapita unakuja kwangu namie nakwenda kwako, ukipata jambo hilo ndio inapatikana (Fahamu)vipi napenda ufahamu hivi: 
Kusema na kuandika ni jambo moja lenye ncha mbili, kama ilivo kusoma na kusikia, Tafauti inapatikana kwamba kusema natumia sauti na kuandika natumia ukimya wa sauti, hapa nakuomba wewe msomaji ujenge hilo daraja la kupokea huu usikivu wa sauti ya ukimya, ukimaliza iwe kama wewe ndie uloandika na hapo itakua umepata kitu kinachoitwa(Kufahamu) na hakipatikani kitu hicho mpaka uhudhurie kwa (macho na masikio).

NINI IBADA?

Nitaeleza neno hili kiasi cha upeo wa ujuzi wangu, kwanza kabisa likitajwa neno hili wengi wetu moja kwa moja tunalipeleka katika kusimamisha (Sala) na hiyo sala ikimalizika na ibada imekwisha, sasa hapo ndio maana utaona (Shetani) anaanza kutawala, kutuingia na kutuchezea atakavyo.

Ukiichukua Ibada kwa jumla ni ngumu huiwezi kabisa bado hujafikia, ndio maana wanazuoni wakajaribu kuigawa kwa mafungu, kuna dua ya chakula, kuna dua ya kulala, dua ya hivi na vile nk, zote hizo ni sehemu katika ibada lakini zimeletwa vipande vipande ili uweze kuzitenda. Lakini tukija kuijibu nini maana ya Ibada ni hivi, Ibada ni mwenendo wa ukamilifu wa maisha yako mazima katika kurejea kwa Mollah wako.


Hebu tutupie macho mzizi wa chimbuko la hii Ibada lilianzia wapi. Tujikumbushe aya katika Quraan sura ya (Baqara-aya-ya-30)


وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ إِنِّى جَاعِلٌ۬ فِى ٱلۡأَرۡضِ خَلِيفَةً۬‌ۖ قَالُوٓاْ أَتَجۡعَلُ فِيہَا مَن يُفۡسِدُ فِيہَا وَيَسۡفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحۡنُ نُسَبِّحُ بِحَمۡدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ‌ۖ قَالَ إِنِّىٓ أَعۡلَمُ مَا لَا تَعۡلَمُو نَ

"Aliposema Mollah wako mlezi kuwaambia Malaika, 

Mimi Najaalia katika ardhi khalifa,Wakasema(Malaika)Unajaalia humo atakaye fanya uharibifu na kumwaga damu, hali yakua sisi tunakutukuza kwa sifa (Zako)na tunakutaja kwa utakatifu wako,

Akasema (Mollah)Hakika mimi nayajua msiyoyajua.


Alipokwisha Muumba mwanaadamu Mweny-enzi-Mungu akatueleza katika sura ya (Ai-Insaan-aya-ya-3) إِنَّا هَدَيۡنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرً۬ا وَإِمَّا كَفُورًا (٣)



"Tumemuonesha njia (tumempa fahamu)ima ashukuru au akufuru". 


Hapo ni khiari yako Mwanaadamu una uamuzi wako huingiliwi(umeachiwa free)umejengewa daraja la (Kufahamu)ukirejea kwa Mollah wako hiyo ndio Ibada na ukichagua kwenda upande wa pili wa hilo daraja yatokufika huko huna wa kumlaumu, ila jambo moja lina uhakika ujijue utakufa na huko kufa ni kurejea kwa Mollah wako sasa uamuzi ni wako urejee kabla hujafa upo safi, au baada ya kufa na makapu ya uchafu.

Ndugu yangu Muislamu Ibada ni marejeo ya ukamilifu kwa Mollah wako kwa vitendo na tabia elewa kila kitu kimezungukwa na Ibada na kama hiyo aya inavosema hapo juu (Ima ashukuru au akufuru) 



Hapa sasa inabidi tuutafute ufunguo wa Ibada na huupati ufunguo huu ila katika (sala)


"Ewe Mwanaadamu jaribu na ujitahidi sana katika kusimamisha sala pengine labda hatimaye unaweza kupeleka hizo shukuran kwa Mollah wako.

Mollah wako kawapa (Ahlil-kitab)wote funguo hii japo kwa njia tafauti ndio maana sote utaona tukimaliza tunaitikia Amin.


Funguo yenyewe ipi inayotupeleka kwenye hii Ibada ya Sala na jee?unafungua sala yako kwa unyenyekevu, unapata utulivu katika hiyo ibada yako ya sala, jawabu la hilo unalo mwenyewe soma ukurasa wa pili ili upate kubadilisha sala iwe unakwenda vyengine kabisa katika ibada zako.


Endelea Part 2:



Mollah wangu anajua zaidi.

A.Baja

Saturday, May 12, 2012

LAAILLAH-ILLA-ALLAH (SHAHADA NA MAANA YAKE) PART 2

بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Asalaam-aleikum


الَّذِينَ يَذْكُرُونَ اللَّهَ قِيَامًا وَقُعُودًا وَعَلَىٰ جُنُوبِهِمْ وَيَتَفَكَّرُونَ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ رَبَّنَا مَا خَلَقْتَ هَٰذَا بَاطِلًا سُبْحَانَكَ فَقِنَا عَذَابَ النَّارِ


(Ambao wanamkumbuka Mollah wao wakiwa wamesimama,wamekaa, na wakiwa wamelala, na wakafikiri katika kuumbwa mbingu na ardhi;wakasema Mollah wetu hukuviumba hivi bure,basi subhannaka tuepushe na adhabu ya moto).


Watu hawa ni wepi?, Jee na wewe umo katika watu hawa? (Laaillah-Illah-ALLAH).
Shahada ni jambo la kuendelea katika umri wako wote, sio jambo la mchezo ikawa umeona ikisha basi, laa ndio maana unatakiwa mpaka siku ya kufa kwako uwe unarudi kwa Mollah wako na neno hili(lakini muradi wake)ni kuthibitisha,kukubali (surrender) umekua muislam kamili (laaillah-illah-allah) ndio maana ikasisitizwa neno hili likuingie kwenye fahamu zako na haliwezi kukuingia ndio maana ukapewa (nyenzo) ikiwa unaweza kutumia njia ya moja kwa moja basi wewe umefaulu, lakini kwa kuwa njia ya moja kwa moja ni ngumu, ndio maana umepewa (kalimat-tawhid)I weze kukumbusha, na kama unapinga jaribu japo kwa masaa(12) kutamka neno hili kama utaweza, na ikiwa huwezi ndio maana ikawa njia ya shahada moja kwa moja ni vigumu.


Naam sasa watu gani hawa wenye kumkumbuka Mollah wao, hao ni watu ambao wamepata hekima kutoka kwa Mollah wao, vipi wamepata hekima hiyo, kwa ajili ya kukumbuka kwao wamepindukia kutoka kwenye akili wameingia kwenye hekima, utaona aya ya mwanzo imewataja wenye akili, na hii ya pili imetaja wenye kufikiri, kwanini kwa sababu ukidumu na (laaillah-illah-allah) mawazo yanapotea na hapo inazaliwa fikira(hekima)na hiyo huipati ila kutokea kwa Mollah wako.


Mja anapofunguliwa hekima huanza kuiona dunia hii kwa mtizamo mpya kabisa lakini lazima lipatikane lile shuruti lake la (kumkumbuka Mollah)wako, ukiwa umesimama yaani kusudio lake katika matendo uyafanyayo, kama vile upo kazini au unatembea nk, au ukiwa umekaa pengine unacheza karata, au upo msikitini barazani watu wanazungumza siasa wewe unamkumbuka Mollah wako, au umelala umejinyoosha basi umo katika hali ya kumkumbuka Mollah wako, basi ujue hata ukikushika usingizi ndotoni utakua unamkumbuka Mollah wako, ndoto za kipuuzi zote zitaanza kupotea, hapo inajumuisha matendo yote utayofanya ukiwa katika hali hizo, uwe unamkumbuka Mollah wako, ukiwa umejizatiti sawa sawa basi jaribu kwa muda wa siku saba(24-7)kulizoea neno hili utaanza kuliona faida yake.fanya majaribio, utaona faida yake.


Hiyo ndio shahada tunayotakiwa waislamu tuwe nayo katika vifua vyetu, na wakati wa kutoka roho zetu. (pale inaposomwa ile aya inayosema) "nasisi tupo karibu nae zaidi-lakini hamtuoni" (84-85-surat-al-waaqiah) huku wewe unajibu (laaillah-illah-allah) mimi nimeshuhudia katika uhai wangu na sasa nashuhudia kurejea kwa Mollah wangu.


Katika maudhui ilopita niliitaja hadithi ya Sayyidna Bilal (r.a) alipokua anakaa na udhu, hiyo ni njia moja na nyengine ni hii ya kulikumbuka neno hili la (tawhid)linakupeleka kumkumbuka Mollah wako, tafauti yake hili la pili linakupeleka zaidi, unaipata shahada.(laaillah-illah-allah) kama nilivo eleza, huo ni upande wa kwanza wa shahada, ama upande wa pili Muhammad Rassullallah huo unafatia katika
(maana ya shahada part 3 na 4)




Mollah wangu anajua zaidi




Abdallah Baja

Thursday, May 10, 2012

LAAILLAH-ILLAH-ALLAH (SHAHADA NA MAANA YAKE) PART 1

.بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Asalaam-aleikum.


Nakuomba mollah wangu uniongoze kwenye nuru, uniepushe mimi na waislamu wenzangu katika kila jambo linalo tutenganisha sisi tusiwe karibu na wewe, hakuna hasara anayopata muumin kama kuwa mbali na wewe. 


Umetufahamisha mollah wetu yakwamba katika jumla ya watu (1000)basi ni mtu mmoja tu ambaye anakutafuta na kutaka kuwa karibu na wewe.


Baada ya dua na ukumbusho huo napenda uelewe wengi wetu tunazaliwa kwenye ulimwengu huu mpaka tunafikia kufariki hatujui faida na maana ya neno hili (laaillah-illah-allah) pindipo tungegundua japo chembeya siri ya neno hili thamani yake, basi tusingeliwacha hata dakika moja kulitamka katika ndimi zetu.


Tunakusahau mollah wetu na jeuri zimetushika ingekuaje lau ungelitupa jukumu tuweze kukumbuka huku (kuvuta pumzi) kuhema tu sisi tungefanyaje.


Lakini kwa kuwa unajua udhaifu wetu umetufanyia hisani za (rehma zako)tunapumua bila ya jitihada zetu (automatic) basi inatosha hilo kuwa ushahidi tosha wa (kalima hii ya tawhid)laaillah-illah-allah.


Nini shahada?
Ushuhuda unatokana na mambo matatu, lazima yapatikane matatu haya na yatumike ipasavyo ili ipatikane hiyo shahada, mambo yenyewe ni la 


Kwanza macho.
Pili masikio na la
Tatu akili.


Macho ni ya mwanzo kukupa yakini ya ulimwengu huu, yanakufunulia ukweli wa wazi kabisa, yanakupa ushaidi kamili yakuwa katika ulimwengu huu lazima yupo muumbaji(laaillah-illah-allah)ambaye haonekani na wala hajulikani na asie na mfano wa chochote. (lakini macho yenyewe ni ya aina gani?) fanya jitihada soma kwa utulivu upate kufahamu macho yanaokusudiwa.


Masikio yanathibitisha shuhuda inayopatikana(kupitia mawasiliano)au kwa njia ya sauti.
Halafu linafatia jambo la tatu nalo ni Akili na hili ndio la karibu zaidi kukupeleka katika hiyo shahada, sasa inakuwaje kuipata hii shahada? na hali yakuwa mimi nimezoea kuitaja katika ulimi pengine mara moja kwa mwaka au kwenye kila sala lakini siijui hasa maana yake, 


Naam maana ya shahada lazima ikotoe katika ulimi,kwani ulimi ni daraja la kukuvusha kukupeleka huko kwenye ushahidi ndio maana mollah wako akakwita uzingatie aya hii: (190-al-imran)


اإِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ




اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾


(Katika kuumbwa mbingu na ardhi,na katika kubadilika usiku na mchana kuna dalili kwa wenye akili)


Naam ni kweli huna haja ya kufundishwa chochote wewe mwenyewe ukikaa na kuzingatia ukavitizama kwa macho ya ushahidi sio kupita pita kwa macho ya mitaani huwezi kuona kitu hata chembe, lazima uyatulize macho yako kwa utulivu huku neno la (laaillah-illah-allah)limo kifuani kwako basi wallahi neno hili litakutupa katika hiyo shahada ilokusudiwa nayo ni sehemu ambayo utajikuta unafunuliwa na kuona kumbe mimi na ulimwengu huu hatuna tafauti, ile nyota ya mbinguni, ule mti ulo pembeni yangu, na vyote viliomo katika ulimwengu huu pia vimo katika mwili wangu.


(kwani hamsomi aya inosema kutokana na ardhi hii nyinyi tumekuumbeni-surat-taha-aya-55) ukishagundua kua huu mwili wangu umebeba pia vyote viliomo kwenye ulimwengu huu basi hapo ndio inakutoka (laaillah-illah-allah)ya kweli katika moyo wako, unatoa shahada ya kuthibitisha hakuna mollah yoyote isipokua(subhanna-allah)hapo unakua umeingia katika kundi lilotajwa hapo juu, unakua umeshapindukia kutoka katika


shahada ya ulimini umeanza kuingia katika shuhuda yakinifu yakuweza kugundua kilichomo baina ya kutoka usiku na kuingia mchana, hebu jaribu kupata japo siku moja kwenye umri wako kuipata (siku)vipi? Siku inazaliwa alfajiri imeeingia (shuhudia)siku ndio kwanza changa(utoto), siku imefikia mchana (ujanani)endelea kushudia, mpaka pale siku inaelekea kufariki(uzeeni)magharibi ishafika endelea kushudia hapo kidogo utakua unapata nini maana ya shahada, mambo mengine ni magumu basi japo hili weka nadhiri ulitimize, litakubadilisha mtizamo wako kuhusiana na shahada.lakini sio wote wenye kuupata ufunuo huu, mpaka kuna ada zake ufanye ndio unapata ladha ya ufunuo huu kama:tutavoziona kwenye (part 2)

mollah wangu anajua zaidi.


Abdallah Baja.

DALILI ZA MCHA-MUNGU PART 3

Asalaam-Aleikum.


Nani Mcha-Mungu?.
Naam itizame aya inofatia inasema nini na kwanini?mwanzo ilianza na mawalii wa Mwenye-enzi Mungu halafu hapa inataja hivi:
Ambao wameamini na wakafanya vitendo vya Taqwa:


Nini imani?
Kwa tulivo mimi na wewe imani ipo kwenye zile nguzo sita ndio maana utaona tumekubali tu lakini hatuijui nini Imani, kwa kuwa tupo kwenye nguzo, zikiyumba tunazini, zikitingishika tuna kula rushwa, tunasema uongo, tunadhulumu hizo ndizo nguzo zetu, na ukiulizwa unasema naamini vitabu vyake, naamini Mitume yake, naamini Malaika wake, lakini ni mdomo mtupu, hiyo si Imani ila huko ni kukubali kwa hiyo unakua huna mashiko yoyote, Jitizame mwenyewe usianze kubisha kabla ya kujitizama halafu ukigundua kama uko mweupe basi anza safari ya kujiunga na wacha Mungu kwa kuitafuta nini imani.


Sasa nini kafanya Mcha-Mungu hata akaitwa kaamini?
Mcha-Mungu kapiga kachumbe hakukubali kubakia na nguzo kenda (Deep) kwenye msingi, na nini kitokujulisha huo msingi wa Imani, hakuna chengine isipokua msingi wa hizo nguzo ni (Tawhid) hapo ndipo alipofika Mcha-Mungu na wewe unaitwa huko.


Qur'aan nzima inakuita katika msingi huo lakini kwa kuwa una pita juu juu hupati kitu unabakia kukusanya mahadithi wala hujui maana yake unakua (story teller) hebu jiulize umeshawahi wewe kuisoma Qur'aan ikakwambia (hakika katika kuutoa usiku na kuuwingiza mchana kuna dalili zetu) hebu pata japo siku moja upate kuuona usiku unavomalizika na asubuhi inapoingia tulia upate kujua nini kinatokea, au subiri uone magharibi ishaingia na mchana haujatoka vitu viwili hivo vimekutana ili upate kujua miujiza iliopo hapo.


Imani yako itageuka kabisa, au kama hayo makubwa japo pata kutawadha, maana yake sala ngumu, basi kutawadha hebu kamilisha udhu wako, hata udhu hupati , wazee wetu wakiibaadhi walikua wanatwambia udhu ni ibada unajua wana maana gani, waligundua kuwa maji yanafanyika kwa gas mbili yaani (Hydrogen na Oxygen) lakini hizi mbili zote zinapatikana hata hospital lakini kwanini haziwi maji, ni lazima kipatikane hichi cha tatu ukigundua nini hicho kitu cha tatu, basi udhu ukakamilika kikweli utajua kama udhu ni Ibada, au ni kutia maji tu kama unavofanya sasa hivi.


Basi kama umeshindwa na udhu jaribu kwenye chakula, hata kula umesahau jiulize una meno thalathini na nne (34), mbona unatafuna chakula mara tatu tu, hujiulizi kwanini.?


Mambo yako mengi sana yakukutupa katika msingi wa(Tauhid) na wala usione vibaya au ukawa na woga katika kujenga Imani yako hata Mitume waliomba wasukumwe katika msingi wa (Tauhid)wasukumwe vipi, "Anasema Nabii Ibrahim katika sura ya Baqara(aya-260) "Nioneshe vipi unavofufua wafu,Mollah wako akasema: kwani huamini, akasema nataka kuutosheleza moyo wangu,(nipate kuridhika)Akasema Mollah,chukua ndege wanne na wazoee(wahifadhi)ikisha uwachinje uwaweke kwenye juu ya kilima,kisha waite,watakujia mbio.


Huyo ndio Mtume na rafiki wa Mollah wake na yeye anataka kuuridhisha moyo na visa ni vingi kikumbuke pia kisa cha Nabii Musa a.s na wengine.


Sasa ikiwa wao wametaka matumaini ya msingi wa tauhid nini hali yako wewe wakati Quraan aya chungu nzima zina kwita ili zikuthibitishie imani yako, lakini umekua mkaidi hutaki kabisa kuchupa ukaanza safari ya ucha Mungu kwanini?.


Kwani hujaambiwa kwenye Quraan katika aya inosema na atazame mwanaadamu chakula chake, sisi ndio wenye kukisababisha,jee hivo ushapata kukila chakula hasa ikakujia fikira kama mimi nikikikosa kwa miezi mitatu chakula hichi nakufa, ushauliza swali hilo kwenye nafsi yako?


Lakini usende huko mbali wewe umesahau hata kula basi anza kwa kujiuliza kwanini umepewa meno 34 na unatafuna chakula mara tatu tu, sasa hayo meno 31 yako holiday,anza na mambo madogo madogo kama hayo ikisha makubwa yatafatia baadae.


Nakupa ahadi moja ukisha kuchupa msingini hutotaka kutoka tena. Ipitie aya ya (Fusilati 53)ukathibitishe maneno haya ninayo kwambia.


Neno la pili la aya hii linasema ikisha wakawa watu wa taqwa: Wafanyao vitendo vya Taqwa.


Nini Taqwa?
Taqwa ni vitendo vya mapenzi, unapoigusa imani basi tambua inakugeuza unakua mtu wa mapenzi,mtu wa hisia, kila kitendo chako kinakua cha mapenzi yaani (Taqwa)tupu, kama nini huwezi kabisa kuwaona jirani zako na watoto wake wanalala na njaa wewe huku umeshiba na ukisha unasali naye ubavuni, Mcha-Mungu hawezi kuchukua itamkera usiku kucha, inakuingia huruma, ikikuingia huruma unaona imani, ukiona imani unataka kusaidia ukisaidia unafanya kwa mapenzi,ndio maana nikaiita (Taqwa)ni mapenzi,unatizama mayatima kwa mapenzi moyoni mwako,unakwenda kutizama wagonjwa kwa ajili ya mapenzi moyoni mwako,unasaidia watu kwa njia ya mapenzi hutaki malipo wala sifa au watu wengine wajue.


Sio kama sisi watu wa kawaida hisia inakuja siku moja tu kwenye umri mzima eti labda ufiwe na mwanao au mkeo,au afe mume hapo utaona mtu vipi anovosawajika kwa hisia za uchungu, napenda kukujulisha hisia kama hizo zinaweza kukujia wakati unasali,au umekwenda kumtizama mtu mzima mgonjwa nk, ukiona hisia kama hizo zinakujia katika vitu vidogo vidogo kama hivo basi jijue upo ukingoni na wakati wowote unaweza kuchupa.


Katika ulimwengu huu tunokwenda nao hatuna imani wala hisia ndio maana utaona unadhulumu, unakula rushwa, na mengi tuyafanyayo sababu moyo ushakufa hamna imani (Taqwa)mapenzi yatatokea wapi, ndio maana hata mkeo au mumeo ukimwambia unampenda inatokea mdomoni tu haifiki moyoni, wallahi kama itakua inatokea moyoni kweli kweli basi katika nyumba yako hayatokei matatizo kabisa wewe jaribu na utanikumbuka itoe katika moyo uone mambo yanavobadilika.


Nakwambia hivo sababu imani na mapenzi ni kitu kimoja chenye pande mbili,kwa hiyo mtu wa (Taqwa)anageuka yeye mwenyewe kuwa mapenzi,na akisha kugeuka hivo utaona mpaka vinyama vinampenda,analisha sisimizi akiwapa sukari,akiona ndege anawapa mtama,akiona maskini yeye wa mwanzo kukaa nao,hampiti mzee ila hutaka kumsaidia,vitendo vyote huwa mapenzi matupu,Mcha Mungu hawezi kutenda kinyume cha mapenzi,akicheka penzi tupu,akisema maneno ni kheri ilo jaa mapenzi, tahadhari msomaji usije ukatafsiri mapenzi haya katika fikra zako zilojaa kichwani mwako(kumbuka hayo ni matamanio).


Hiyo ndio Taqwa ilokusudiwa na tafauti yako na Mcha Mungu inakua hivi yeye akiswali anafanya hivo kwa ajili ya mapenzi ya Mollah wake,sala yake imejaa shukura na furaha na unyenyekevu wakuona Mollah wake kamuumba ikisha kamleta kuwa karibu na sasa anazungumza na Mollah wake.


Jitizame wewe unahangaika kumjulisha malaika wa thawabu kuwa sasa una sali hasara kubwa ilioje ikiwa tutabaki katika daraja hii.


Na aya inamalizia kwa kusema:





Wao wanabashiriwa mambo katika hii dunia:usije ukadhani (bishara)yenyewe kama utabiri laa, wanabashiriwa kwa kuondolewa pazia katika hii dunia wakawa wanajua mambo,wakawa wanaona mambo,ndio maana utakuta Mcha-Mungu anaweza kukwambia fulani mie nimebakisha siku tatu ukiniacha London au ukinipeleka Zanzibar nina siku tatu.


Naam kweli baada ya siku tatu utaona huyo kajiondokea na kama utahudhuria katika sakarati mauti yake basi utakuta yumo furahani anakwenda kukutana na Mollah wake, Na uzuri zaidi na huko endapo pia keshajua mapokezi yake yatakuje na wape anaondoka bila ya khofu wala huzuni,anaondoka huku anaaga.


Na ikiwa una shaka kwani hujaisoma ile aya inosema (na sisi tuko nae karibu zaidi lakini hamtuoni),basi hayo ndio Mcha-Mungu anobashiriwa akiwa hai, Na huo ndio (mwenendo)ulokwisha kupangwa wala si wenye kubadilika na huko ni kufuzu kuliko kukubwa kuwa kipenzi cha Mollah wako,kupanda daraja kulikoje ambako hushuki tena ukawa mtu wa chini,hizo ndio fadhila za Mcha-Mungu.


Naomba kwa Mollah wangu atufikishe katika daraja hizo ile tuwe karibu yake tupate ladha na nuru ya wacha Mungu.


Na Mollah wangu ndie ajuae zaidi


Mwenzenu.
Abdulla Baja

DALILI ZA MCHA MUNGU PART 2

Asalaam-Aleikum


Nani Mcha-Mungu?
Kabla hatujaigusa aya ya ucha Mungu wacha tuendelee kumchambua Mcha Mungu ni mtu wa aina gani.


Mcha Mungu ni mja aliyekufa kwa mapenzi ya Mollah wake wakati akiwa hai, hataki yeye sifa, wala kufanya jambo kwa malipo yoyote halei yatima kwa kuhitaji malipo, halishi maskini kwa kuhitaji aongezewe utajiri.


Zitazame sala zetu zilivo husali ila ni mwenye kuhitaji pepo au utajiri au ufanikiwe hili na lile ukichunguza sala zako zote (full of Bussines)zimejaa biashara na kama sio biashara basi unasali kwa woga usitiwe motoni.


Imani yako (empty) ukiulizwa leo unaamini nini basi utarusha ngumi kwa sababu huna (Empty) utatumia maneno kujibia imani na hivo viwili ni vitu tafauti.


Maneno yanatoka kwenye ulimi, imani inatokea kwenye (Moyo-Heart)Feeling) umesali miaka yote hata siku moja yashakutoka machozi kwa ajili ya sala yako, haiwezekani kwa sababu huna feeling hujapata kumiminikiwa na Imani hujakutana nayo imani ana kwa ana kila kitu kimo ulimini (Ndio maana bwana Mtume s.a.w"akaonesha kifuani mara tatu kuashiria
moyo")


Jitizame unajiita Mcha-Mungu hata siku moja umepata sala, ukiwa dukani au kazini unawaza kwenda kusali ukifika msikitini unawaza kazini na dukani hivi ndivo sala zetu zilivo hivi ndio ucha Mungu wetu ulivo, hatusali ila kuonesha watu kila kitu maonesho matupu, ukikataa au ukipinga ukweli hivi ndivyo tutendavyo.


Nani Mcha-Mungu?
Mcha Mungu ni yule ambaye masaa(24)yupo anaishi na Mollah wake katawaliwa na Mollah wake akivuta pumzi anamkumbuka Mollah, akisimama anamkumbuka Mollah wake, akilala anamkumbuka Mollah wake.


Ukianza kuupata ucha Mungu kweli kweli basi (Automatic) unaanza kuihama dunia hutaki tena yanakukera mambo yake, sasa unakua unaona raha kila wakati unataka uwe na kipenzi chako, (na kama nani anotaka awe mbali na Mpenzi wake) kumbuka


Mcha Mungu hana khofu yoyote anaishi katika ulimwengu yupo na wenzie kila mtu rafiki yake lakini (inside)yupo na Mollah wake hasahau hata dakika moja kumdhukuru Mollah wake.


Sasa wacha tuitizame aya ya Mcha Mungu inasemaje,

Aya hiyo ya 62 inamtaja Mcha-Mungu kuwa mtu asie na khofu vipi?.


(Hakika ya wale mawalii wa kweli kweli wa Mwenye-enzi-Mungu wale vipenzi walojitupa kwa Mollah wao wakajiweka karibu kabisa na Mollah wao hakuna khofu juu yao kabisa)


Kwa nini ikawa hivyo?
Napenda uelewe nyuma ya khofu kuna matumaini, ndio maana wewe Muumin wa kawaida hujijui itakuwaje mwisho wako, lakini kwa Mcha-Mungu jambo hilo hakuna.


Kwake kuna nini?
Ipo yakinifu (Gurantee) ithbati ya njia ya Mollah wake kwa jambo lolote ulifanyalo unaridhia chochote kile unakua kama majani, Upepo ukija unayumba nao ukenda kusini unafata ukenda kaskazini unafata, huwi kama mti unabishana na upepo ndio maana kikija kimbunga kikali mti unakatika tena hapo hakuna kinachobaki ila hugeuzwa majina ikawa hii kuni, lile gogo na kadhalika.


Naam na wala hana khofu kesho atakula nini au atavaa nini, jumba lake atalimaliza lini, afya yake ikoje huwa na Imani ikiwa Mollah wangu anaweza kumponesha Ndege alo msituni, basi atashindwa na mie ninayeishi nyumbani, 


Mcha-Mungu anafunguliwa mambo na Mollah wake akajua nini afya, na hilo ni jambo kubwa kabisa ukiweza kungundua nini afya, hata madaktari wenye elimu za kupindukia hawezi kukwambia nini afya, atakutajia maradhi ya aina yote lakini hawezi kukutamkia nini afya, ndio maana ukenda kwa Mcha Mungu akizungumza na Mollah wake upesi upesi utaona mbona nimepona mara moja imekuaje hajafanya lolote? huyo ndio mcha Mungu.


Na hana kuhuzunika katika nafsi yake fulani mbona vile mie mbona hivi, mbona sasa umeniondoshea afya umenipa maradhi yote hayo kwake huwa maridhia akipewa anaona kajaribiwa na akinyimwa pia huona kanusuriwa, hayamtoki mdomoni kwake ila maneno ya shukura.


Endelea part 3


Abdulla Baja

DALILI ZA MCHA MUNGU PART 1

Asalaam-aleikum.


Nini Ucha Mungu?




Ni Mapenzi yalokamilika(kwa tafsiri Yangu mimi)


Nini mapenzi?
Mapenzi yapo ya aina mbili aina ya


kwanza:
Ni ile ya kujilazimisha baada ya kukipenda kitu aidha kikupende au ukipate, Hapo tena unakua umetosheka unaanza kutafuta au kusubiri chengine ili upate kuanza tena(naweza kuita aina hii ya mapenzi ni hamu)kwani
ukichunguza utaona huwezi kudumu katika hali moja ya kukipenda kitu kwa kuendelea,Mapenzi haya huwa ya muda na hayachelewi kuondoka,kumbuka ukilala ya wapi mapenzi yako?.(haya nayaita-Artificial)


Aina ya pili ya mapenzi:
Ni ile ambayo kila mwanaadamu huonjeshwa aidha wakati wa (kukua-Baleghe)au kwenye utu-uzima wako, unaonjeshwa kidogo ladha hii na ukionjeshwa utajiona vipi hali yako inavokua,


ndio maana wazungu wakaiita hali hii (Falling in love)shekhe anaweza akatupa majoho yote na vilemba,waziri akakubali kufukuzwa kazi au aache madaraka kwa sababu ya mapenzi. nini kimetokea? wapi imetokea hali kama hii, mbona nimevamiwa sijijui, kinachotokea hapo ndio kimetokea kwa mcha-Mungu hali kama hiyo lakini mara isizo na idadi,na wala usidhani mapenzi haya yanakuja kwa urahisi kama wanavodai wengine,ni kazi pevu lakini inawezekana.


Nani Mcha-Mungu?
Nilipokua mdogo nilikua na mchezo wa kukimbia chuoni na kwenda Skuli ya Tumekuja hapo nilikua nikishuhudia wakubwa zangu wakipanda juu ya mabati halafu wanapiga kachumbe maneno walokua wakisema wakati ule hayakua na maana kwangu mie,


lakini nilipofikia utu-uzima nikagundua walikua wanakusudia nini,kabla ya kuchupa mtu akisema sina baba wala mama ikisha huyo anajiachia,maana yake kumbe alikua akitoa shahada kitotokea chochote huko chini yeye atakikabili,


akizama au kuchuna uso yote sawa,hana baba wala mama,naam sadakta kumbuka umekuja kwenye ulimwengu huu kwa mama na baba umepitia tu, lakini marejeo yako kule kule ulipotokea.


Mcha-Mungu ni yule alorejea akaamua kuchupa kuelekea kwa Mollah wake akiwa yuhai.


Vipi utajua yakua unaanza kupata mapenzi ya Mollah wako, utajua pale ambapo kila ukikaa iwe barazani au msikitini iwe marikiti au ofisini au hata kwenye harusi watu wameshughulika kuandika (novel-mabuku)yao kwenye vichwa,wewe upo katika hali ya kumkumbuka Mollah wako mpenzi,ndipo pale Bwana Mtume s.a.w "alipomuuliza ewe Bilal"r.a mbona nasikia nyayo zako peponi unafanya amali gani hata mimi nasikia nyayo zako,akajibu haunitoki udhu ila sala baada ya sala.


Huyo ndie kipenzi cha Mollah wake,maana hiyo anamkumbuka Mollah wake wakati wote akiwa anasali au hasali fikira zipo kwa Mollah wake,udhu hautoki,na wewe jaribu kuuweka udhu kutwa nzima utaona vipi unamkumbuka Mollah wako.


Pia napenda uelewe Mapenzi ya Mollah wako yakikuzidi katika moyo wako ikawa huwezi kumsahau hata kwa nusu saa basi elewa na Mollah anakupenda na yakikumiminikia mapenzi ya Mollah wako basi unakua si mtu wa dunia hii tena ikiwa mtu wa hamaki,hamaki zote zinapotea,ikiwa ulikuwa na chuki zinapotea,ukiwa ulikua tajiri basi utakua utajiri upo lakini weye hujali tena aidha ukifilisika au ukiongezeka,


ukiwa maskini ndio zawadi kubwa kwako kwa ile hali ya kuridhika kwako, wala hukereki ukaona fulani kapata mimi sikupewa,ukiona hunazo hali kama hizo basi wewe bado fanya kazi ya ziada,ukiona unachukia watu bure basi jitilie shaka lazima una maradhi au kuna kitu kinakusumbua pahala fulani wewe jichungue siri unaijua mwenyewe,


wala isikuingie choyo wapo matajiri wacha Mungu na wanatoa sadaka mie sitoi,pengine wanazotoa sio sadaka huwezi kuibia maskini halafu ukarudi ukawapa kidogo kidogo ukaita sadaka hayo ni maonesho tu.


Nani Mcha-Mungu.?
Wanaadamu wanapenda au niseme wana maradhi ya kujitia katika makundi kwani kwa kufanya hivo kunawapa matumaini fulani kua mimi nipo katika kundi la haki,watu hawa wanaonesha hata maana ya neno haki hawaitambui,


Nini haki?
Ni ufupisho wa neno hakika na hakika unaipata kwenye mifano hii nina hakika ule mwezi, ile nyota ule mti vipi leo utakua una hakika yakua wewe mcha Mungu? usidhani kuweka madevu,au kuvaa malemba ni ucha-Mungu au kujifunika gubi-gubi na mabuibui huo ni ucha Mungu, utakua mashakani ukiwa na dhana hiyo,wewe ukitaka bakia kwenye kundi lako na shekhe atakupigia muziki mzuri wakukulaza ili usishtuke usingizini kwani kwa kufanya hivo yeye anapata natija zake na wewe unapata blanket lako ndoto zinaendelea uzuri.


England walifanya (Research)walichukuliwa watoto wadogo wenye fahamu zao walikua hawajui nini kinachoendelea wakapewa majina ya ,makundi moja likaitwa Abc na la pili likaitwa xyz, basi kila mmoja akaambiwa wewe uko kwenye kundi la abc na wewe umo kwenye kundi la xyz basi wakawa wako tayari kufanya chochote kulitetea kundi lake mpaka wamekua watu wazima bado wanaendelea kutambuana kwa label za makundi wewe abc na yule xyz na ukichungua mpaka hivi leo kama vile vilabu vya mpira mpaka unakufa wewe Malindi,Jamhuri, n.k hata timu yako ikifa bado unai-support na hivi ndio hata kwenye dini unaendelea ujihusisha mie kundi hili na lile, toka upesi kwenye hayo makundi ili upate kuwa Mcha-Mungu kwani ucha Mungu ni safari ya peke yako haitaki shekhe wala mwalimu ili akuone upate kuridhika, amka uwache kuyumbishwa elewa kwenye kundi nyote mnaridhishana tu, mtu wa msimamo ameshika dini lakini ndani ya moyo huna kitu mweupe na wewe unajua,unapita unasema muziki haramu, kutwa unaendelea kuimba kwenye kichwa chako, unasema TV haramu watu wakikupa mgongo unaitizama, tafadhali acha kujidanganya jionee huruma usijidanganye mwenyewe inatosha kudanganya watu basi hata mwenyewe.


Nani Mcha-Mungu?
Ikiwa bado kiburi kimekukamata unajihisi utapinga, hebu zifanyie kazi takwimu hizi halafu ujitizame wewe Mcha-Mungu kweli.


Umri wako unaoishi umepata sana miaka sitini(60)basi Thalathini(30) katika hiyo unatumia kwa kulala, sasa igawe thalathini ilobaki(30)kutafuta mali,au kwenda kazini,senema,harusini,karata,mazungumzo,marafiki,vilabuni ukitahamaki umri wako wote hujapata hata nusu siku katika kufanya ibada umeishi miaka sitini unapata nusu siku tu ya ibada, halafu unajiita mcha Mungu, haliwezekani kabisa jambo hilo kila kitu kina daraja zake na ucha-Mungu pia una daraja zake,usije ukafanya masikhara na mambo ya dini ikiwa huelewi bora nyamaza kimya,elewa huko kunyamza kwako kimya ushaanza hatua za kuelekea kwenye ucha Mungu.


Endelea part-2


Nani Mcha-Mungu? 


Abdallah Baja