Friday, May 18, 2012

ZAWADI YA RAMADHANI (TAQWA NA MAPENZI YA ALLAH) PART 2

Asalaam Aleiykum

"Ewe Jumba la milango Tisa"


Ukitaka kufunga na saum yako ipate Rehma za Mollah wako basi kwanza funga mlango wako wa kwanza yaani (macho)acha kutizama wanawake usirandishe macho yako katika kutizama mambo ya maasi jitahidi sana hata ukiweza kuondoka mjini chukua likizo kazini si unataka funga yako ikubalike jitenge na mji usitazame mambo ya maasi yasikushughlishe kabisa wakati huu wa mwezi mmoja mambo ya kidunia.

"Naam ikisha funga mlango wako wa pili Yaani (Mashikio)acha kusikiliza mambo machafu,fitna,na uongo jishughulishe na kusikiza maneno ya kuilea roho katika njia ya taqwa.

Ama mlango wa tatu ni pua zuia kunusa nusa manukato,harufu watu wamepika nini na n.k.

Na huu mlango wa nne ni katika kusema watu,kula haramu,kufanya masighara ya upuuzi katika mwezi huu mtukufu.

Na milango yako miwili ya mwisho ni kujizulia mambo ya (Sex)au kujamiana kwa njia za haramu, ukiweza kufanikiwa bara bara kujizuia na mambo yote yanotendwa na hiyo milango tisa kwa ukamilifu basi likitima kumi la mwanzo unakua umeshakamilishiwa Rehma yako utajiona mtu ulobadilika na Rehma za Mollah wako zinafanya kazi kwa siri na dhahiri pengine ulikua na maradhi yanataka kuja juu yanaponeshwa, unakamilika rasmi na matendo hayo yakikamilika hasa utaona mku wa jumba(Akili) anavotulia mustaqim katika mambo ya ibada na mapenzi juu ya Mollah wako na ukitimiza hayo unakua umekamilishan taqwa katika mezi huu.

"Amesema"Umar bin Abdul-aziz r.a"

"Sio kumcha Mollah kwa kufunga mchana au kusali usiku au yaliyomo baina yake"

Bali hiyo taqwa ni kuacha aloharamisha Mollah wako"ama hayo ya Ibada ni mapenzi kwa Mollah ndio unafanya kutukuza na kumuomba uwe karibu yake.

Akahadithia "Abuu Darda r.a "Taqwa ya kweli ni ile inayomfanya mja hata cha halali akawa anahofia kisije kuwa cha haramu" hivi ndio tunatakiwa tufunge ndio tukaitwa sote katika siku hizi chache tutende hayo si kujizuia kula ndio tukaaona tumefunga,ikisha tukaamrishwa ondokeni jitengeni mwezi huu nendeni kajificheni (miskitini)fanyeni itikaf mumkumbuke Mollah wenu wenzetu wanaita (meditation)unavotaka kuita lakini umeamrishwa ukajitenge ili upate kumkumbuka Mollah wako,usije ukasema aah imesemwa kwenye aya (Ankiffu fil masjid)ardhi yoyote ilo tohara basi hapo ndio masjid kwani neno masjid limetokana na sehemu wanayosujudu kwa hiyo popote unapoweza kusujudu hapo ndio msikiti wako.

Basi hilo ndilo kumi la mwanzo ukiliweza unapokewa katika kumi la pili la maghfira inshaalah kwenye maudhui ijayo tutalizungumza hilo.

Mollah ndie ajuae sisi ni wenye kujitahidi penye kosa nisahihisheni


A.Baja

No comments:

Post a Comment