Thursday, May 10, 2012

DALILI ZA MCHA MUNGU PART 1

Asalaam-aleikum.


Nini Ucha Mungu?




Ni Mapenzi yalokamilika(kwa tafsiri Yangu mimi)


Nini mapenzi?
Mapenzi yapo ya aina mbili aina ya


kwanza:
Ni ile ya kujilazimisha baada ya kukipenda kitu aidha kikupende au ukipate, Hapo tena unakua umetosheka unaanza kutafuta au kusubiri chengine ili upate kuanza tena(naweza kuita aina hii ya mapenzi ni hamu)kwani
ukichunguza utaona huwezi kudumu katika hali moja ya kukipenda kitu kwa kuendelea,Mapenzi haya huwa ya muda na hayachelewi kuondoka,kumbuka ukilala ya wapi mapenzi yako?.(haya nayaita-Artificial)


Aina ya pili ya mapenzi:
Ni ile ambayo kila mwanaadamu huonjeshwa aidha wakati wa (kukua-Baleghe)au kwenye utu-uzima wako, unaonjeshwa kidogo ladha hii na ukionjeshwa utajiona vipi hali yako inavokua,


ndio maana wazungu wakaiita hali hii (Falling in love)shekhe anaweza akatupa majoho yote na vilemba,waziri akakubali kufukuzwa kazi au aache madaraka kwa sababu ya mapenzi. nini kimetokea? wapi imetokea hali kama hii, mbona nimevamiwa sijijui, kinachotokea hapo ndio kimetokea kwa mcha-Mungu hali kama hiyo lakini mara isizo na idadi,na wala usidhani mapenzi haya yanakuja kwa urahisi kama wanavodai wengine,ni kazi pevu lakini inawezekana.


Nani Mcha-Mungu?
Nilipokua mdogo nilikua na mchezo wa kukimbia chuoni na kwenda Skuli ya Tumekuja hapo nilikua nikishuhudia wakubwa zangu wakipanda juu ya mabati halafu wanapiga kachumbe maneno walokua wakisema wakati ule hayakua na maana kwangu mie,


lakini nilipofikia utu-uzima nikagundua walikua wanakusudia nini,kabla ya kuchupa mtu akisema sina baba wala mama ikisha huyo anajiachia,maana yake kumbe alikua akitoa shahada kitotokea chochote huko chini yeye atakikabili,


akizama au kuchuna uso yote sawa,hana baba wala mama,naam sadakta kumbuka umekuja kwenye ulimwengu huu kwa mama na baba umepitia tu, lakini marejeo yako kule kule ulipotokea.


Mcha-Mungu ni yule alorejea akaamua kuchupa kuelekea kwa Mollah wake akiwa yuhai.


Vipi utajua yakua unaanza kupata mapenzi ya Mollah wako, utajua pale ambapo kila ukikaa iwe barazani au msikitini iwe marikiti au ofisini au hata kwenye harusi watu wameshughulika kuandika (novel-mabuku)yao kwenye vichwa,wewe upo katika hali ya kumkumbuka Mollah wako mpenzi,ndipo pale Bwana Mtume s.a.w "alipomuuliza ewe Bilal"r.a mbona nasikia nyayo zako peponi unafanya amali gani hata mimi nasikia nyayo zako,akajibu haunitoki udhu ila sala baada ya sala.


Huyo ndie kipenzi cha Mollah wake,maana hiyo anamkumbuka Mollah wake wakati wote akiwa anasali au hasali fikira zipo kwa Mollah wake,udhu hautoki,na wewe jaribu kuuweka udhu kutwa nzima utaona vipi unamkumbuka Mollah wako.


Pia napenda uelewe Mapenzi ya Mollah wako yakikuzidi katika moyo wako ikawa huwezi kumsahau hata kwa nusu saa basi elewa na Mollah anakupenda na yakikumiminikia mapenzi ya Mollah wako basi unakua si mtu wa dunia hii tena ikiwa mtu wa hamaki,hamaki zote zinapotea,ikiwa ulikuwa na chuki zinapotea,ukiwa ulikua tajiri basi utakua utajiri upo lakini weye hujali tena aidha ukifilisika au ukiongezeka,


ukiwa maskini ndio zawadi kubwa kwako kwa ile hali ya kuridhika kwako, wala hukereki ukaona fulani kapata mimi sikupewa,ukiona hunazo hali kama hizo basi wewe bado fanya kazi ya ziada,ukiona unachukia watu bure basi jitilie shaka lazima una maradhi au kuna kitu kinakusumbua pahala fulani wewe jichungue siri unaijua mwenyewe,


wala isikuingie choyo wapo matajiri wacha Mungu na wanatoa sadaka mie sitoi,pengine wanazotoa sio sadaka huwezi kuibia maskini halafu ukarudi ukawapa kidogo kidogo ukaita sadaka hayo ni maonesho tu.


Nani Mcha-Mungu.?
Wanaadamu wanapenda au niseme wana maradhi ya kujitia katika makundi kwani kwa kufanya hivo kunawapa matumaini fulani kua mimi nipo katika kundi la haki,watu hawa wanaonesha hata maana ya neno haki hawaitambui,


Nini haki?
Ni ufupisho wa neno hakika na hakika unaipata kwenye mifano hii nina hakika ule mwezi, ile nyota ule mti vipi leo utakua una hakika yakua wewe mcha Mungu? usidhani kuweka madevu,au kuvaa malemba ni ucha-Mungu au kujifunika gubi-gubi na mabuibui huo ni ucha Mungu, utakua mashakani ukiwa na dhana hiyo,wewe ukitaka bakia kwenye kundi lako na shekhe atakupigia muziki mzuri wakukulaza ili usishtuke usingizini kwani kwa kufanya hivo yeye anapata natija zake na wewe unapata blanket lako ndoto zinaendelea uzuri.


England walifanya (Research)walichukuliwa watoto wadogo wenye fahamu zao walikua hawajui nini kinachoendelea wakapewa majina ya ,makundi moja likaitwa Abc na la pili likaitwa xyz, basi kila mmoja akaambiwa wewe uko kwenye kundi la abc na wewe umo kwenye kundi la xyz basi wakawa wako tayari kufanya chochote kulitetea kundi lake mpaka wamekua watu wazima bado wanaendelea kutambuana kwa label za makundi wewe abc na yule xyz na ukichungua mpaka hivi leo kama vile vilabu vya mpira mpaka unakufa wewe Malindi,Jamhuri, n.k hata timu yako ikifa bado unai-support na hivi ndio hata kwenye dini unaendelea ujihusisha mie kundi hili na lile, toka upesi kwenye hayo makundi ili upate kuwa Mcha-Mungu kwani ucha Mungu ni safari ya peke yako haitaki shekhe wala mwalimu ili akuone upate kuridhika, amka uwache kuyumbishwa elewa kwenye kundi nyote mnaridhishana tu, mtu wa msimamo ameshika dini lakini ndani ya moyo huna kitu mweupe na wewe unajua,unapita unasema muziki haramu, kutwa unaendelea kuimba kwenye kichwa chako, unasema TV haramu watu wakikupa mgongo unaitizama, tafadhali acha kujidanganya jionee huruma usijidanganye mwenyewe inatosha kudanganya watu basi hata mwenyewe.


Nani Mcha-Mungu?
Ikiwa bado kiburi kimekukamata unajihisi utapinga, hebu zifanyie kazi takwimu hizi halafu ujitizame wewe Mcha-Mungu kweli.


Umri wako unaoishi umepata sana miaka sitini(60)basi Thalathini(30) katika hiyo unatumia kwa kulala, sasa igawe thalathini ilobaki(30)kutafuta mali,au kwenda kazini,senema,harusini,karata,mazungumzo,marafiki,vilabuni ukitahamaki umri wako wote hujapata hata nusu siku katika kufanya ibada umeishi miaka sitini unapata nusu siku tu ya ibada, halafu unajiita mcha Mungu, haliwezekani kabisa jambo hilo kila kitu kina daraja zake na ucha-Mungu pia una daraja zake,usije ukafanya masikhara na mambo ya dini ikiwa huelewi bora nyamaza kimya,elewa huko kunyamza kwako kimya ushaanza hatua za kuelekea kwenye ucha Mungu.


Endelea part-2


Nani Mcha-Mungu? 


Abdallah Baja

No comments:

Post a Comment