Monday, May 28, 2012
UMUHIMU WA KAZI KATIKA DINI
Asalaam-Aleiykum.
"Ametukuka Mollah wetu alieumba Ulimwengu huu na sisi wanaadamu ikisha akatuwekea njia tatu za lazima tuzipitie nazo ni Jitihada, Matatizo,na Kipato ili apate kututizama katika Ulimwengu wa akhera nani alofanikiwa katika hizo jitihada, Nani aloshindana na matatizo yake kimaisha akafaulu na yupi yule alopata kipato kizuri akakitumia kwa mambo ya kheri.
Kipato kwa mwanaadamu sio hasa kusudio la maisha ya kiumbe bali ni njia yakumuezesha kuishi katika ulimwengu huu kwa njia ya halali na kwa ajili ya kufanya ibada za kumuabudu Mollah wake na kupata radhi na Taqwa za ukamilifu kwa ajili ya kumkurubia Mollah wake,Ndio maana Bwana Mtume s.a.w akahimiza sana Umma wake watu watafute na wafanye kazi za halali pamoja na biashara akasema "Enyi Umma wangu jizuieni na kuomba,fanyeni jitihada kuzitizama familia zenu, pia kuweni na huruma kwa ajili ya majirani zenu,na yoyote yule ambaye atatafuta riziki yake kwa njia ya halali atakutana na Mollah wake uso wake unangara kama vile mbaa Mwezi ingaravo".
Siku moja Bwana Mtume s.a.w alikua amekaa na Masahaba akapita kijana anakwenda mbio dukani wakasema Masahaba lau mbio za kijana yule angekua anakimbilia mambo ya dini yake basi angepata kheri kubwa,"Akasema Bwana Mtume s.a.w" Msiseme maneno hayo lau ikiwa anakimbia kijana yule kujiepusha na kuomba au kutegemea watu wengine au akajikinga na jambo la kuomba au ikawa anawatizama wazee wake au watoto wake, basi yeye yumo katika Jihad kwa ajili ya Mollah wake. Akaendelea kusema Bwana Mtume s.a.w "Mollah anampenda yule ambaye anajitolea kufanya kazi ili asitegemee watu wengine". Akamalizia Bwana Mtume s.a.w na Kusema muogopeni Mollah wenu kwa kutafuta riziki ya halali.
Nabii Isa a.s Alimuuliza kijana Mmoja akamuuliza unafanya kazi gani katika maisha yako, yule kijana akajibu kazi yangu mimi ni kumuabudu Mollah,"akamuuliza nani anakupa chakula, yule kijana akajibu kaka yangu, Nabii Isa a.s akamwambia kaka yako anafanya ibada zaidi ya kumuabudu Mollah wake kuliko wewe.
Akasema Bwana Mtume s.a.w Bora uwe Mchukuzi wa mizigo kuliko ukapita ukawa unaomba, Yule Mpewa hekima na Mollah wake Luqman alimuusia mwanawe na kumwambia ewe Mwanangu ufunge mlango wa umaskini kwa kutafuta riziki ya halali, kwani yule asopenda kazi yanamkuta mambo matatu, la kwanza Dini haingii sawa sawa katika moyo wake, pili hapati elimu yoyote katika hekima zake,na la mwisho anapoteza utu wake.Amesema Bwana Mtume s.a.w "Ni sheria ya wajibu kwa kila Muislam kutafuta riziki ya halali, yoyote yule mwenye kujitahidi kutafuta riziki ya halali basi daraja yake ni sawa na yule ambaye amepigana jihad kwa ajili ya dini yake, akaendelea bwana Mtume s.a.w yoyote yule katika Muislam alokula riziki ya halali kwa muda wa siku arobaini basi Mollah wake atuungarisha moyo wake, atatia hekima katika akili yake na ulimi wake, basi ndugu zangu tujitahidini sana kutafuta kazi za halali na kuacha kula haramu.Tuombe Mollah atusaidie kwa hili.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment