Thursday, May 10, 2012

LAAILLAH-ILLAH-ALLAH (SHAHADA NA MAANA YAKE) PART 1

.بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَٰنِ الرَّحِيمِ
Asalaam-aleikum.


Nakuomba mollah wangu uniongoze kwenye nuru, uniepushe mimi na waislamu wenzangu katika kila jambo linalo tutenganisha sisi tusiwe karibu na wewe, hakuna hasara anayopata muumin kama kuwa mbali na wewe. 


Umetufahamisha mollah wetu yakwamba katika jumla ya watu (1000)basi ni mtu mmoja tu ambaye anakutafuta na kutaka kuwa karibu na wewe.


Baada ya dua na ukumbusho huo napenda uelewe wengi wetu tunazaliwa kwenye ulimwengu huu mpaka tunafikia kufariki hatujui faida na maana ya neno hili (laaillah-illah-allah) pindipo tungegundua japo chembeya siri ya neno hili thamani yake, basi tusingeliwacha hata dakika moja kulitamka katika ndimi zetu.


Tunakusahau mollah wetu na jeuri zimetushika ingekuaje lau ungelitupa jukumu tuweze kukumbuka huku (kuvuta pumzi) kuhema tu sisi tungefanyaje.


Lakini kwa kuwa unajua udhaifu wetu umetufanyia hisani za (rehma zako)tunapumua bila ya jitihada zetu (automatic) basi inatosha hilo kuwa ushahidi tosha wa (kalima hii ya tawhid)laaillah-illah-allah.


Nini shahada?
Ushuhuda unatokana na mambo matatu, lazima yapatikane matatu haya na yatumike ipasavyo ili ipatikane hiyo shahada, mambo yenyewe ni la 


Kwanza macho.
Pili masikio na la
Tatu akili.


Macho ni ya mwanzo kukupa yakini ya ulimwengu huu, yanakufunulia ukweli wa wazi kabisa, yanakupa ushaidi kamili yakuwa katika ulimwengu huu lazima yupo muumbaji(laaillah-illah-allah)ambaye haonekani na wala hajulikani na asie na mfano wa chochote. (lakini macho yenyewe ni ya aina gani?) fanya jitihada soma kwa utulivu upate kufahamu macho yanaokusudiwa.


Masikio yanathibitisha shuhuda inayopatikana(kupitia mawasiliano)au kwa njia ya sauti.
Halafu linafatia jambo la tatu nalo ni Akili na hili ndio la karibu zaidi kukupeleka katika hiyo shahada, sasa inakuwaje kuipata hii shahada? na hali yakuwa mimi nimezoea kuitaja katika ulimi pengine mara moja kwa mwaka au kwenye kila sala lakini siijui hasa maana yake, 


Naam maana ya shahada lazima ikotoe katika ulimi,kwani ulimi ni daraja la kukuvusha kukupeleka huko kwenye ushahidi ndio maana mollah wako akakwita uzingatie aya hii: (190-al-imran)


اإِنَّ فِي خَلْقِ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَاخْتِلَافِ




اللَّيْلِ وَالنَّهَارِ لَآيَاتٍ لِأُولِي الْأَلْبَابِ ﴿١٩٠﴾


(Katika kuumbwa mbingu na ardhi,na katika kubadilika usiku na mchana kuna dalili kwa wenye akili)


Naam ni kweli huna haja ya kufundishwa chochote wewe mwenyewe ukikaa na kuzingatia ukavitizama kwa macho ya ushahidi sio kupita pita kwa macho ya mitaani huwezi kuona kitu hata chembe, lazima uyatulize macho yako kwa utulivu huku neno la (laaillah-illah-allah)limo kifuani kwako basi wallahi neno hili litakutupa katika hiyo shahada ilokusudiwa nayo ni sehemu ambayo utajikuta unafunuliwa na kuona kumbe mimi na ulimwengu huu hatuna tafauti, ile nyota ya mbinguni, ule mti ulo pembeni yangu, na vyote viliomo katika ulimwengu huu pia vimo katika mwili wangu.


(kwani hamsomi aya inosema kutokana na ardhi hii nyinyi tumekuumbeni-surat-taha-aya-55) ukishagundua kua huu mwili wangu umebeba pia vyote viliomo kwenye ulimwengu huu basi hapo ndio inakutoka (laaillah-illah-allah)ya kweli katika moyo wako, unatoa shahada ya kuthibitisha hakuna mollah yoyote isipokua(subhanna-allah)hapo unakua umeingia katika kundi lilotajwa hapo juu, unakua umeshapindukia kutoka katika


shahada ya ulimini umeanza kuingia katika shuhuda yakinifu yakuweza kugundua kilichomo baina ya kutoka usiku na kuingia mchana, hebu jaribu kupata japo siku moja kwenye umri wako kuipata (siku)vipi? Siku inazaliwa alfajiri imeeingia (shuhudia)siku ndio kwanza changa(utoto), siku imefikia mchana (ujanani)endelea kushudia, mpaka pale siku inaelekea kufariki(uzeeni)magharibi ishafika endelea kushudia hapo kidogo utakua unapata nini maana ya shahada, mambo mengine ni magumu basi japo hili weka nadhiri ulitimize, litakubadilisha mtizamo wako kuhusiana na shahada.lakini sio wote wenye kuupata ufunuo huu, mpaka kuna ada zake ufanye ndio unapata ladha ya ufunuo huu kama:tutavoziona kwenye (part 2)

mollah wangu anajua zaidi.


Abdallah Baja.

No comments:

Post a Comment