Tuesday, May 15, 2012

NINI IBADA? (NA MAANA YAKE) PART 1

Asalaam-Aleiykum.

Kabla ya kuanza Maudhui hii wacha nikupe faida ya kufahamu.



Nini kufahamu? 
Kufahamu ni kujenga daraja baina ya mimi muandikaji na wewe msomaji tukawa tunapita unakuja kwangu namie nakwenda kwako, ukipata jambo hilo ndio inapatikana (Fahamu)vipi napenda ufahamu hivi: 
Kusema na kuandika ni jambo moja lenye ncha mbili, kama ilivo kusoma na kusikia, Tafauti inapatikana kwamba kusema natumia sauti na kuandika natumia ukimya wa sauti, hapa nakuomba wewe msomaji ujenge hilo daraja la kupokea huu usikivu wa sauti ya ukimya, ukimaliza iwe kama wewe ndie uloandika na hapo itakua umepata kitu kinachoitwa(Kufahamu) na hakipatikani kitu hicho mpaka uhudhurie kwa (macho na masikio).

NINI IBADA?

Nitaeleza neno hili kiasi cha upeo wa ujuzi wangu, kwanza kabisa likitajwa neno hili wengi wetu moja kwa moja tunalipeleka katika kusimamisha (Sala) na hiyo sala ikimalizika na ibada imekwisha, sasa hapo ndio maana utaona (Shetani) anaanza kutawala, kutuingia na kutuchezea atakavyo.

Ukiichukua Ibada kwa jumla ni ngumu huiwezi kabisa bado hujafikia, ndio maana wanazuoni wakajaribu kuigawa kwa mafungu, kuna dua ya chakula, kuna dua ya kulala, dua ya hivi na vile nk, zote hizo ni sehemu katika ibada lakini zimeletwa vipande vipande ili uweze kuzitenda. Lakini tukija kuijibu nini maana ya Ibada ni hivi, Ibada ni mwenendo wa ukamilifu wa maisha yako mazima katika kurejea kwa Mollah wako.


Hebu tutupie macho mzizi wa chimbuko la hii Ibada lilianzia wapi. Tujikumbushe aya katika Quraan sura ya (Baqara-aya-ya-30)


وَإِذۡ قَالَ رَبُّكَ لِلۡمَلَـٰٓٮِٕكَةِ إِنِّى جَاعِلٌ۬ فِى ٱلۡأَرۡضِ خَلِيفَةً۬‌ۖ قَالُوٓاْ أَتَجۡعَلُ فِيہَا مَن يُفۡسِدُ فِيہَا وَيَسۡفِكُ ٱلدِّمَآءَ وَنَحۡنُ نُسَبِّحُ بِحَمۡدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ‌ۖ قَالَ إِنِّىٓ أَعۡلَمُ مَا لَا تَعۡلَمُو نَ

"Aliposema Mollah wako mlezi kuwaambia Malaika, 

Mimi Najaalia katika ardhi khalifa,Wakasema(Malaika)Unajaalia humo atakaye fanya uharibifu na kumwaga damu, hali yakua sisi tunakutukuza kwa sifa (Zako)na tunakutaja kwa utakatifu wako,

Akasema (Mollah)Hakika mimi nayajua msiyoyajua.


Alipokwisha Muumba mwanaadamu Mweny-enzi-Mungu akatueleza katika sura ya (Ai-Insaan-aya-ya-3) إِنَّا هَدَيۡنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرً۬ا وَإِمَّا كَفُورًا (٣)



"Tumemuonesha njia (tumempa fahamu)ima ashukuru au akufuru". 


Hapo ni khiari yako Mwanaadamu una uamuzi wako huingiliwi(umeachiwa free)umejengewa daraja la (Kufahamu)ukirejea kwa Mollah wako hiyo ndio Ibada na ukichagua kwenda upande wa pili wa hilo daraja yatokufika huko huna wa kumlaumu, ila jambo moja lina uhakika ujijue utakufa na huko kufa ni kurejea kwa Mollah wako sasa uamuzi ni wako urejee kabla hujafa upo safi, au baada ya kufa na makapu ya uchafu.

Ndugu yangu Muislamu Ibada ni marejeo ya ukamilifu kwa Mollah wako kwa vitendo na tabia elewa kila kitu kimezungukwa na Ibada na kama hiyo aya inavosema hapo juu (Ima ashukuru au akufuru) 



Hapa sasa inabidi tuutafute ufunguo wa Ibada na huupati ufunguo huu ila katika (sala)


"Ewe Mwanaadamu jaribu na ujitahidi sana katika kusimamisha sala pengine labda hatimaye unaweza kupeleka hizo shukuran kwa Mollah wako.

Mollah wako kawapa (Ahlil-kitab)wote funguo hii japo kwa njia tafauti ndio maana sote utaona tukimaliza tunaitikia Amin.


Funguo yenyewe ipi inayotupeleka kwenye hii Ibada ya Sala na jee?unafungua sala yako kwa unyenyekevu, unapata utulivu katika hiyo ibada yako ya sala, jawabu la hilo unalo mwenyewe soma ukurasa wa pili ili upate kubadilisha sala iwe unakwenda vyengine kabisa katika ibada zako.


Endelea Part 2:



Mollah wangu anajua zaidi.

A.Baja

No comments:

Post a Comment