Friday, May 18, 2012

MADALALI WA IBLIS (SHETANI) PART 1

Asalaam Aleiykum.


"Nakuomba Mollah wangu Yasipite Makala haya isipokua yawe uzinduo japo kwa mmoja atakayesoma na ikiwa imepatikana faida kwake ya kuacha japo moja katika yaliyomo kwenye maudhui hii basi Yaa Rabbi usimpe yeye peke yake faraja yako ya kusamehe ila naomba namie nilomtumia niwemo"

Na nyenyekea katika enzi ya uwezo wako kuwaombea Rehma Maiti wote wa Kiislam,pia Waislam wanaume pamoja na wanawake kwa sote tuteremshie Rehma yako ulotupangia ya kutusamehe "Dhanbi zetu".Amin.

"Waliulizana Malaika inakuaje kiumbe huyu mwanaadamu fadhila zote na wema wote alotukuzwa na Mollah wao mpaka sisi Malaika tukaambia tumsujudie halafu yeye anakua asi wala si mwenye kuhofu uwezo wa Mollah wao"

Malaika wamejaa huzuni dhambi anazotenda mwanaadamu zimetawala katika mazungumzo yao. Alisikia Ibilis mjadala huu akasema, Mnataka nikufahamisheni inakuaje?Wakajibu Malaika tujulishe ewe Ibilis kwani wewe uko nao hawa kila wakati.

"Akasema Ibilis" Jambo la mwanzo kabisa ninalofanya kwanza Nawavua nguo zao mbili, Mimi nawavamia hawa halafu nachana kabisa ile nguo yao ilogandana na mwili ili asinipe tabu kumshawishi, nikimaliza kuwavua tu huanza hawa kutamaniana na mimi najua udhaifu wao uko wapi, Halafu naliandama guo lao la pili hili la Ucha Mungu nikisha wavua hili wamekwisha wanabakia kama wanyama wanakua hawana tafauti tena na simba ,chui, farasi wanavamiana tu.
Huyo ndio Ibilis hayo ndio maneno anoyasema"sasa ukiyapinga rejea "Quraan"

يَا بَنِي آدَمَ لاَ يَفْتِنَنَّكُمُ الشَّيْطَانُ كَمَا أَخْرَجَ أَبَوَيْكُم مِّنَ الْجَنَّةِ يَنزِعُ عَنْهُمَا لِبَاسَهُمَا لِيُرِيَهُمَا سَوْءَاتِهِمَا إِنَّهُ يَرَاكُمْ هُوَ وَقَبِيلُهُ مِنْ حَيْثُ لاَ تَرَوْنَهُمْ إِنَّا جَعَلْنَا الشَّيَاطِينَ أَوْلِيَاء لِلَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ

"Enyi wanaadamu asikuftini Shetan kama alivowafitini wazee wenu akawatoa katika Pepo,(alifanya nini?)

"Kwanza"aliwavua nguo ili kuwaonesha (Jinsia zao)Hakika huyu (Ibilis)Na kabila lake ni wenye kukuoneni pasi ya nyinyi kuwaona,Na sisi tukajaalia shetani kuwa marafiki wa wale wasooamini.

"Enhe Endelea Ibilis kutujulisha nini cha zaidi unawafanyia"

Akaendelea Ibilis mimi huwagawa hawa katika makundi mawili kundi la mwanzo nalichukulia dhamana la kuingia nalo motoni, Kundi hili la mwanzo linajiunga kabisa na kabila langu linakua sisi na wao hatuna tafauti, sote tunakuwa tushafukuzwa katika ufalme wa Mtukufu Mollah wetu.Basi huwabatiza wakawa hawasikii tena dua yoyote, na mkitaka kuwajua hawa waliomo katika kabila langu wa kwanza kabisa ni kiongozi (Dhalim) huyu hana shaka, halafu tena wanafatia walevi,wazinifu,washirikina,wachawi,wapiga ramli na wengi walojifunga na mijidhanbi mikubwa.Hawa nakuwa sina haja nao tena kwani hunifanyia kazi zangu (automatic)sina haja hata ya kuwashawishi.

Amma kuhusu hawa madalali wangu "

وَزَيَّنَ لَهُمُ الشَّيْطَانُ أَعْمَالَهُمْ فَصَدَّهُمْ عَنِ السَّبِيلِ فَهُمْ لَا يَهْتَدُونَ 

"Na shetani amewapambia vitendo vyao na akawazuilia njia (wakawa hawaoni)njia zote za kheri, kwa hiyo hawakuongoka".

Usikose kuwajua Madalali wa Ibilis katika makala inofatia.

Imetaarishwa na kuletwa kwenu na
A.Baja

No comments:

Post a Comment