Friday, May 18, 2012

MADALALI WA IBLIS (SHETANI) PART 2

Asalaam Aleiykum.

"Naam Amma kuhusu Madalali kidogo hunifika kazi ya kuwabatiza, sababu wanashituka shituka kwa chembe za hofu zilobaki kwenye mioyo, basi hufanya nini?

Nitakujulisheni kujua dalili zao ni kama hivi:

" Humuingia dalali wa kike nikamshughulisha sana katika kivazi chake hatoki mwanamke huyu mpaka awe na hakika nyama zake zimeikamata sawa sawa na ile nguo, huyu ananifanyia kazi kwa kunipatia wateja kwa makundi kwani kila anayemtizama kaumia, basi hupita mwanamke huyu akiasi njia nzima pamoja na wanomtamani hakuna yoyote mwenye kutafakari kwamba hilo ni kosa.Humzidishia vituko huyu ikawa kila nguo anoivaa ni kubwa watu watasemaje ndio amezeeka basi hutoka yeye huku manyama yakimtetemeka na huwa shari tupu mpaka akirudi nyumbani.

Amma Dalali wangu mwengine yule mwenye kupita kutafuta habari za watu na kuzitangaza, Mimi humuandama huyu akawa kama mgonjwa lazima apate habari za fulani ikisha humshawishi aziongeze chumvi na hapo wengine wakizipokea na wao huzisambaza.Wote hao hunifanyia kazi yangu kwa kujitolea.

"Humtia dhiki mimi dalali wangu mwenye kufanya kazi sehemu za dhamana huyu humfanyia wasiwasi akajiona ni maskini huanza kuchukua mali ya watu kidogo kidogo akawa hana hofu kwa matendo hayo na huku akipita anatingisha ufunguo yakua sasa keshatajirika kwa pesa za haramu.

Ikisha humfanya mwengine kuwa Dalali kwa kupita kusema uongo na ukitaka kumjua, angalieni mkikutana naye basi huanza fulani hivi fulani hivi . 

Pia huwajulisha dalali wangu pale ukiona kundi la wanawake limevaa hijab na mmoja wao hakuvaa basi jueni huyo ni dalali wangu ,pia huwaingia mie matajiri na maskini katika kila nyanja ya maisha yao.

 قَالَ فَبِعِزَّتِكَ لَأُغْوِيَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ

"Naapa kwa haki ya Utukufu wako,Nitawapoteza wote(katika njia yako)"

Basi utawaona madalali zangu kwenye ngoma, huku wamejipanga kwa makundi wanamuasi Mollah wao, hawa kwenye maasi wao wanakua mwanzo, wakikaa hawana amali ili kuzungumza maasi na ufisadi,kila wakikaa wawili anoanza mazungumzo hamtaji Mollah wake kabisa. 

Msishtuke kuwaona wanadanganya danganya kuingia miskitini na kusoma Qur'aan hao hawana kitu kabisa, huwafata mimi ndani ya hiyo misikiti nikamfanya mmoja wao ndio awe anaona yeye amehitimu,sasa ndio anatoa fatwa za kuzua zua, na mtamuona ana kiburi yeye anajipeleka peponi wenzie wote anawatia motoni.

Kumbe maskini yeye mwenyewe hamjui hata Mollah wake, humtia nguvu huyu za kuupenda Uimamu akaupigania kwa nguvu zote ili afanye fisadi ndani ya Dini, jueni yakua huyo pia dalali wangu.

Bbasi huwaingia mie nikawatia matajiri wasi wasi mkubwa nikawafanya wao pia kuwa Madalali wangu kwa vipi, wako tayari kuchangia mambo ya ufuska kuliko kulisha yatima, zakka huisahau kabisa. Na huzipamba nyimbo na ngoma ili kuwasahaulisha kabisa kama Mollah anawaangalia.

"Wakasema Malaika" zaidi ya hayo yote Mollah wao kawachukulia dhamana kwa kuwashushia aya inosema "

وَمَا كَانَ اللّهُ لِيُعَذِّبَهُمْ وَأَنتَ فِيهِمْ وَمَا كَانَ اللّهُ مُعَذِّبَهُمْ وَهُمْ يَسْتَغْفِرُونَ 

"Na hakuwa Mollah wako mwenye kuwaadhibu hali uko nao, na hakua mwenye kuwaadhibu hali yakua wanaomba msamaha".

"Akasema Ibilis"Hawa ntawafanyia vitimbi hakuna hata mmoja atokumbuka huko kutubu, nitawakusanya hawa na watoto wao niwashushie kioo changu nini hicho kioo? 

Watakaa hawa kwenye TV wasikumbuke kabisa kumdhukuru Mollah na wakishamaliza basi nitawachunga chunga mpaka kitandani na kuhakikisha hakuna hata mmoja anomshukuru Mollah wake na wakiamka pia hawatomtaja. Wataendelea kusengenya watu,kudhulumu,kula rushwa watadumu hawa kwenye maasi mpaka siku wanokutana na Mollah wao na hata wasijijue kwanini hawa kutubu.

Kwa hiyo ndugu zangu kila mmoja akae na kutafakari vipi atapigana (Jihad)hii ili asiwe Dalali wa Ibilis.

Imetaarishwa na kuletwa kwenu na
A.Baja

No comments:

Post a Comment