Friday, May 18, 2012

ADHABU YA KABURI

Asalaam-Aleiykum

Katika Buku la Pope Gregory la Dilogue lilotungwa 6 century kuna habari ya Askari mmoja alokumbwa na maradhi ya (Plague) akadhaniwa amekufa kalala mwili hauna uhai kabisa.


"Anasimulia askari huyu Mara nikaona nimetoka kwenye mwili wangu nimekwenda mpaka karibu ya daraja nikaona daraja hilo chini yake linapita tope mfano wake kama tope za volcano zikikugusa umeumia upande wa pili wa hilo daraja nikaona kuna watu wamevaa vivazi vizuri na bustani za maua yanonukia sijapata kuona uzuri wa harufu yake na hao watu kila mtu ana sehemu yake ya kupumzikia wanatembea huku na kule kwa furaha na huku wakiwa wameridhika.

Juu ya lile Daraja nikaona kuna watu wengi wanafanyiwa mtihani wakupita lakini wengi wao wanaanguka na kila wakianguka anatangaza mtu hawa ndio walokua wakifanya mabaya ulimwenguni masikini wale watu wakianguka tu mara ngozi zina wavuka kwa moto mkali uliopo hapo chini ya hilo daraja, Huku nikawaona wengine wanapita bila ya wasi wasi na wanavuka kwa salama kwenda ule upande wa pili. 

Nikamuona mfanyabiashara Mmoja nnaye mjua anayeitwa Stephen naye anajaribu kuvuka mara akateleza mguu akawa ananinginia(hanging)akatokea kiumbe cha kutisha chini ya lile daraja na kuanza kumvuta mara huku juu akatokea kiumbe mzuri kavaa guo jeupe akawa anamvuta kwa juu.

Wakati kinyanganyiro hicho kinaendelea huyu anoshuhudia mambo hayo akarejea kwenye mwili wake na hakujua matokeo yale ya vuta nikuvute:

Naam hiyo ndio habari ya huyo Askari alo (survive plague)na kuhadithia hayo aloyaona-wakaiita hali kama hii kwa lugha ya kiengereza (OBE)out of body experience: 

Alisimama yule Sahaba mkubwa wa kiislamu,Anokesha usiku kusoma Quraa'n kipenzi cha Mwenye-enzi-Mungu Syd na Othman bin Affan r.a kasimama analia kwenye kaburi alipoulizwa unalilia nini? akasema silii kwa kukumbuka Pepo au Moto ila nalia kwa kukumbuka makaazi ya kaburini sehemu ya upweke hukutani na chochote isipokua adhabu na mateso au raha na ahadi njema, akaendelea kusema nimemsikia Bw Mtume s.a.w anasema,

 "hakika ya kaburi ni utambulisho wa Nyumba utakayokaa huko akhera mfano wa Peponi au Motoni:

Enyi wanaadamu ukishakufukiwa kaburi husema katika watu waloingia, leo umekuja leo weye na jeuri zako, hapa huna tena kiburi chako,hapa huna tena ule uwezo ulokutia jeuri huko ulimwenguni,mimi ni jumba la upweke,mimi ni jumba la wadudu leo humu uko peke yako na kabla hajakufaidi yoyote wacha nikuanze mimi hapo tena mtu muovu hubanwa mpaka mbavu zikakutana.

Enyi Wanaadamu tahadharini kuja huku na uovo wenu kwani mimi nimepewa amri nifanye nini?kwanza nilivunje vunje jeneza lake au kibox chake unozikiwa, Ikisha niichane sanda yako nianze kunywa damu na nyama yake, Hapo ndipo Hadrat "Abdul Aziz" r.a akasema 

"Enyi binaadamu Tahadharini sana na kuipenda dunia hii kwani ukiwa tajiri hapa huko kesho utakua muombaji, ukiwa kijana basi uzee unakusubiri, na Wako wapi walotawala miji,wakajenga majumba,wakadhulumu wenzao,mnajua nini kinawafika chini ya Ardhi? 

Isikudanganyeni dunia kwani tajiri na maskini wote wanalala chini ya Ardhi basi fanya mema ili tandiko lako liwe zuri.
Akitiwa mtu kaburini Ardhi ina nadi wacha leo ulipwe kama ulivokua unafanya duniani"

Alikuja kijana mmoja kwa Abdul Malik ana huzuni kubwa akamuuliza yule kijana nini umefanya yule kijana machozi yakawa yanamtoka hajibu kitu akamuuliza tena umefanya dhambi kubwa iso samahani yule kijana akasema naam mimi kazi yangu ilikua naiba sanda wakifukiwa maiti mimi nishafika nawavua nakwenda kuuza, siku hiyo nikachimba kaburi nikakuta maiti uso umevurugika kutaka kuondoka nikasikia sauti inanambia usiondoke unajua huyo maiti kwanini yuko hali hiyo nikasema sijui:

nikaambiwa huyo alikua akipuuza sala hataki jambo la kusali kabisa, nikaambiwa nenda kafukue Kaburi la pili: 

Baada ya kufukua nikaona mtu ana alama za kuteswa lakini ana uso wa nguruwe nikaambiwa huyo alikua mlevi na mpaka anaondoka ulimwenguni kashindwa kuuwacha mvino:nikaamrishwa nikafukue kaburi la tatu:

Na hapo nikakuta domo la maiti limevimba na ulimi umevutwa umechomwa moto,nikaambiwa huyo alikua kazi yake kusema watu na kufitinisha:

Nikapewa amri tena nifukue kaburi la nne 

Hapo nikaona maiti imepigiliwa na misumari sitini mkononi nikaambiwa huyu alikua akiwapa mikono wake za watu.

Halafu nikaambiwa kila anoingia huku na dhambi zake basi tumshghulikia mpaka iifike siku ya Kiama na akioza anarejeshwa tena huku hakuna mauti.

Yule kijana akachukua ahadi ya kuwacha na kuanza kuwa mtu mwema mpaka mwisho wa maisha yake:

Adhabu zipo nyingi sana itachukua bahari nzima kuziandika zote, Basi ikiwa wewe bado unapinga habari hii kwani hukumbuki sisi ndio tulokuwa tunakuangalia ule wakati wa miezi tisa tumboni?basi ikiwa unaamini makaazi yale yapo basi kuwa na hakika na huku vile vile yapo tafauti lile tumbo la mzazi wako na hili ulotiwa sasa hivi ni tumbo la Ardhi huku hakuna mtetezi isipokua amali zako njema: 

Inshaalah Mollah atuepushe na adhabu za kaburi sote jamii ya kiislamu.

Imetaarishwa na kuletwa kwenu na
A Baja

No comments:

Post a Comment