Friday, May 18, 2012

ZAWADI YA RAMADHANI (TAQWA NA MAPENZI YA ALLAH) PART 1

Asalaam Aleiykum.

Ndugu zangu katika Uislam umetukaribia Mwezi mtukufu wa Ramadhan wenye mambo mawili makubwa yatokayo kwa Mollah wetu yaani Rehma na Baraka, ambayo unayo hakika kuyapata katika mwezi huu kuliko miezi mengine yoyote ilopita.

Kuyapata mambo hayo mawili unatakiwa kutimiza masharti yake ambayo ndio dhamira yangu ya maudhui hii, wengi wetu tunafata mwenendo tu yakua watu wameeacha kula mchana na sisi hatuli tunangoja magharibi jua likizama ili nasi tupate kula, basi nakujulisha kuwa hakushindwa Mollah wetu kutuambia 

"Enyi mloamini acheni kula mchana ili mle usiku"

Lakini katutakia kheri na rehma zake akatutengea mwezi wetu huu maalum kwa kutuamrisha 

"Enyi Mloamini nimekuamrisheni kufunga kama nilivowaamrisha walopita kabla yenu ili mpate kumcha Mollah".

Nini kufunga?
Iibada hii nyinyi mmekusanywa pamoja umma wote wa kiislamu haki sawa hakuna sheikh wala sharif hakuna yoyote isipokua yule atofunga inavotakiwa ndio atopata malipo yake, Ndani ya Mwezi huu kama ulivogawika mafungu matatu yaani la mwanzo Rehma, la pili Maghfira(kusamehewa)na la tatu Dhamana ya kutoingia motoni sasa mambo haya matatu yanapatikana vipi? 

Ama kuhusu hilo la Rehma ni kumi la mwanzo.

"Ewe jumba la milango tisa funga milango yako usiku na mchana katika mwezi huu upate kurehemewa" 

Na kama huijui hiyo Rehma basi jikumbushe kidogo sura ya "Maryam"na kisa cha Nabii Zakariyya a.s

"2(Wakumbushe)ukumbusho wa Rehma ya Mollah wako alipomrehemu mja wake Zakariyya" alifanya nini Zakariyya? 

"3(Alipomuomba)alipomlingania Mollah wake kwa siri". 

"4(Akasema Mollah wangu,mifupa yangu imekua dhaifu)(nimezeeka mimi)na kichwa changu kimeshakua kinang'ara kwa(Mvi)wala sikua mwenye bahati mbaya (au kuhasirika)katika kukuomba wewe.

"5(Na hakika mimi nawahofia jamaa zangu baada yangu(kuharibu dini) Na mke wangu ni tasa)(Hazai kabisa)basi naomba nipe mrithi (anijie)kutoka kwako.

"7(Ewe zakariyya tunakupa habari njema ya kuwa (utapata mtoto) Jina lake ni Yahya, hatujafanya kabla yake mwenye jina kama hilo).

Hiyo ndio Rehma ya Mollah wako huyo ni Nabii keshakua mtu mzima na mkewe Tasa kamlingania Mollah wake kwa siri akapewa Rehma kwa kupewa mtoto mambo yamegeuzwa kwa ajili ya maombi ya siri sasa nini habari yetu mimi na wewe tunofunga kwa siri? vipi tutapata Rehma tulopangiwa.

soma jumba la milango tisa katika ukurasa wa pili.

A.Baja

No comments:

Post a Comment