Asalaam Aleiykum,
Maudhui yetu ya leo inagusa ndoa zetu za kiislam kwa wakati huu tunaoenda nao, kumekuweko na mlipuko wa (Talaka)mpaka imefikia jambo hili la ndoa ya kiislam kufanywa kitu cha upuuzi tu na ambacho hakina thamani, labda maudhui hii italeta mwanga japo kidogo ili watakao faidika na darsa hii watapata bahati za kuzithamini na kuzitunza ndoa zao kama walivofanya wazee wetu.
Naam, ukitizama maajabu ya ndoa ya kiislam utaona mpango alotupangia Mollah wetu una manufaa makubwa kwetu sisi waumin wa dini ya kiislam, Japokua kuna baadhi ya watu wenye imani nyengine wanatubeza na kutucheka na kutushangaa, Lakini mwenendo wetu una kheri katika mambo mengi ukiyatia katika Akili.
Tafauti yetu kubwa ya Mwanzo sisi (Waislam)hatu(Falling in love)kwanza tunaoana(1)halafu tunazoeana(2)tena tunakuwa marafiki(3)ikisha tunapendana(4)mwisho wake tunaoneana huruma(5)hapo tena tunakamilisha (Circle)nzima ya ndoa, unaweza kuita upendavyo, Mke na Mume, Chanda na Pete au hata (Soul-mate). Sababu gani zino tufanya tufunge ndoa?Quraan Rumi aya 21
"وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ"
Na katika ishara zake, Amekuumbieni wake zenu katika(kutokana na) jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, Akayajaalia mapenzi na huruma baina yenu, Bila ya shaka katika(hayo)zimo ishara kwa watu wanaofikiri.
Yatosha maneno haya ya Mollah wetu katika aya hii moja kukichambua chuo hichi cha ndoa katika maisha ya Mume na Mke mwanzo mpaka mwisho. Mwanzo kabisa aya imeanza katika ishara zake amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu, hapakutajwa wanawake, ingetajwa wanawake jambo hili la ndoa lingekua(accident)linatokea tu bila ya kupangwa, mnakutana kwenye disco, taarab na kwengineko mnafunga ndoa, lakini imeanza kwa ishara, halafu ikafatia wake zenu ikaja kusita katika jinsi zenu, sasa kwanini ikasemwa ishara?na kwanini ikatajwa wake zenu? na vipi imekua kutokana na jinsi zetu?(Japokua utapata jawabu mwisho wa Mada)lakini wacha nikuchukue katika safari hii ili upate ufahamu mwengine kabisa kuhusiana na huyo mwenzio unaye ishi naye, huyo unomwita mama watoto wangu, huyo unomwita mimi na yeye kama chanda na pete, ukasema hapa mimi nimekutana na (soul-mate) wangu. Anasema Mwenye-enzi-Mungu "katika ishara zake" jee wewe umeshawahi kuingia katika kuzitizama hizo ishara, Ushawahi kujiuliza kwanini ikawa huyu? jee haya makutano yetu ni bahati au jambo hili limepangwa kabla ya kutokea?umeshawahi kusafiri kiroho ukapata kumjua mwenzio unaye kaa naye? Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, sasa ingia katika hizo ishara uzipate japo kwa uchache ili upate kufahamu mambo yanavokua-endelea-Part-2
Monday, October 15, 2012
MAISHA YA MUME NA MKE MAPENZI MAJAALIWA-PART-2
Asalaam Aleiykum,
Kuanzia leo usimnyanyase mwenzio, usimdharau Mkeo au Mumeo kwani kwenye Mamlaka ya (Roho) nyinyi nyote sawa(Equal)Roho si mwanamke wala mwanaume lakini tafauti ipo hapo kwenye jinsia na kubwa zaidi katika hilo la kuzaa, mengine yote siku hizi wanasayansi wamegundua, wanakupa dawa kila kitu kinabadilika dume linaweza kugeuka jike na jike likageuka dume, hayo yanafanyika na wala si maajabu tena Quraan imesema zamani (Amekuumbieni wake zenu kutoka katika jinsi zenu)nyie nyote jinsi moja, ili mpate utulivu kwao, ingia tena kwenye ishara utazame vipi unapatikana utulivu huu. Utulivu ulotajwa hapo upo wa aina mbili wa ndani na nje, Ama huu wa hali ya ndani chukua mfano wa kijana baro baro likipewa mke ghafla linavotulia, kama lilikua jitu la fujo, mtaani mnapata nafuu sasa, kwa sababu ameanza kupata utulivu, Baada ya kugundulikana hali hii inofanya watu wawe watulivu sasa ikaamuliwa majeshi yakakae kambini, kwani akiwachwa nyumbani jeshi hapigani tena, hana haja ya kuua, keshapata utulivu, hata wake zao hawaruhusiwi kwa sababu ikiwa hawajapata utulivu ndio wanageuka kuwa makatili kutokana na mafunzo wanopewa na hasira za kukosa utulivu.
Nguvu za (kiume)zikitoka hakuna jeshi tena nani anataka kupigana wakati keshapata matulizo, lakini ole wako yakiachiwa machafuko ya nguvu hii ndani na mafunzo ya nje wanayopewa inachobaki balaa tupu, Inaendelea kutufahamisha ishara hii utulivu wake huu wa ndani kuwa wakitulia wawili hawa basi kinachofatia kizazi cha halali.
Ama kuhusu utulivu kwa njia ya nje, ni kupata heshima kwa jamii, kujifunga udugu na familia nyengine na kupendana nao, na huu utulivu wa nje unakukupelekea kuipata hiyo (Taqwa)na Ibadah zako kwa njia ya utulivu bila ya misukosuko yoyote. Na kama unabisha unataka kuipima ishara hii kuwa kweli au uongo, maneno matupu, hakuna chochote, basi watazame wale wanokwenda nje ya ndoa zao wanavo kosa utulivu huu, awe mwanamme au mwanamke mtizame akili zinavomruka, kwanza lazima awe bingwa wa udanganyifu, mateso yanamzidi katika kichwa chake, midamu umechafua njia ya Mwenye-enzi-Mungu na yeye anakuchafulia yako, unakua hamkani fulani keshajua au bado, unapita ukiwaza wakati wote sijui wanajua au hawajui, wameniona au hawajaniona na ukitahamaki utulivu umeondoka, ukisema uongo mmoja lazima ukinge kwa mengine kumi na moja, mwenyewe unajijua muongo, watu wanakujua mdanganyifu, na Mollah wako anakuzidishia maradhi unaanza kufilisika na mali inaanza kutoweka.
Ama kwa wanawake wao Mollah kawajaalia umbile(Nature)yao utulivu, ndio maana utaona mara chache sana kuona mwanamke kakimbia kizazi chake, kwa sababu yeye karidhia, kakubali utumwa wa Mollah wake, kila wakati yupo anaishi katika utulivu, huwezi kukuta jeshi la wanawake, na yote hayo yamo katika hizo ishara ambazo ni nyingi kuzitaja zote nafasi tulo nayo ni finyu.
"Enyi ndugu zangu msipite mkapeana talaka kwa mambo ya upuuzi na kirahisi, na wala msivunje amri ya Mollah wenu mkatoka kwenye majumba kabla ya Eda zenu kumalizika hicho ni kipimo maalumu alichokuwekeeni Mollah wenu kwa hekima zake" na tambueni hayo makutano yenu sio ya kiwiliwili tu bali pia ni ya Roho, halafu tena mnakutana ki Akili na bila kuyakumbuka mawili haya basi ndoa yenu haiwezi kudumu abadan. Sasa ni mapenzi?endelea-part-3.

MAISHA YA MUME NA MKE MAPENZI MAJAALIWA-PART-3
Asalaam Aleiykum,
Kumbuka tumo katika kuichambua aya moja na sasa tunaingia katika hayo mapenzi yalotajwa katika hiyo aya.
Mapenzi ni Bustani maalum ambayo wote tunapigana tuifikie, Bustani hii ipo kwenye bonde la (Moyo)kuna watu wakiigundua Bustani hii basi wao huchupa moja kwa moja hawasubiri chochote, hao ndio tunawaita wame (Fall in love)lakini kuna wengine wanatumia utaratibu ulopangwa na Mollah wao wa kushuka taratibu kama (Nilivotaja kwenye part 1). Natoa mfano huu ili kujulisha kiini cha mapenzi mwanzo wake yanatokea kwenye kichwa halafu ndio yanashukia moyoni hapo inapatikana salama, Lakini ole wako yakishuka moja kwa moja moyoni mbeleni kuna hatari.
Amesema Mwenye-enzi-Mungu,"Akajaalia Mapenzi na Rehma"limetumika neno la jaala kuonesha dalili za kuwa jambo hili lina athari zile zile za kama hizi," Tukajaalia kuona na kusikia"ukilala kuona na kusikia kunatoweka"tukajaalia usiku kama guo"unaingia na kutoka na mchana hali kadhalika"na ukitizama aya nyingi ziloanza na neno hili zina dasturi za kuja na kutoweka, mfano kama vile zina mzunguko fulani, basi ukisha elewa hivyo ujue na mapenzi ni hali hiyo hiyo hayadumu moja kwa moja kama bendera ya chama, yanakuja na kuondoka, kama ilivokua huwezi kukaa masaa ishirini na nne umehamaki na pia huwezi kukaa masaa kama hayo unapenda, kuna wakati unalala ya wapi mapenzi yako.
Sasa tuingie katika bahari ya mapenzi ili tuzitizame ndoa zetu inakuaje. Wengine wanaita (Falling in love)lakini waislam Mollah wetu hatuachi tuanguke, ila katuwekea mpango tunateremka taratibu kwa kutumia ngazi yake ya Rehma nayo ndio hii (Ndoa)."Ewe Adam .a.s kaa peponi pamoja na mkeo"(Aaraf-19), ndoa ya mwanzo imefungwa peponi, na mpaka leo zinaendelea kufungwa huko huko mbinguni, Hamkutani tu kwa bahati mbaya isipokua kwa matakwa ya Mwenye-enzi-Mungu, ndio maana ukaona tukio hili likawa ni la furaha, nini kinachokutana hapo ni Roho mbili zilofanya safari tafauti kutokea kwa Mollah wake mpaka leo ujanani zinakuja kuungana, haiwezekani tukio hili likawa kwa bahati, Kwa hiyo ndoa ni makutano ya Roho mbili na zikisha kutana kidogo kidogo, mguu kwa mguu huku zimeshikana mikono zinaanza kushuka kwenye Bonde la mapenzi, kwa kuwa Roho mbili hizi zimekutana katika mji wa kigeni, watu wawili hawa lazima zitokee tafauti,mabishano yatakuwepo,ngazi refu ya bondeni kunatakiwa ustahamilivu,masikilizano,subira ili mmoja wenu asije akadondoka au ukaja msukuma mwenzio kwa maudhi na kero, msije mkapita kugonmbana mbele za watu, msitoe siri zenu, mkiwa na tabia nzuri za kuridhiana wawili nyie basi Mwenye-enzi-Mungu ndio hukufunulia hilo pazia la mapenzi na hakuna raha inayopata Roho kama kuondoshwa pazia ukawa unapendana na mkeo au mumeo, nini kinatokea pazia likiondoshwa?endelea part-4

MAISHA YA MUME NA MKE MAPENZI MAJAALIWA-PART-4
Asalaam Aleiykum
Linapofunguka pazia la mapenzi, kila hatua ya ngazi mnayoshuka kabla hata ya kufika huko bondeni(moyoni)basi kwenu nyinyi inakua mapenzi, mwenzio akiwa kazini wewe umejaa mapenzi,ukimuona yana kumiminika machozi ya furaha, usione haya ndio mapenzi na mapenzi ni (Feeling)usiogope kuzionesha sasa mwenzio atajuaje, haziwi kumbukumbu zenu ila isipokua mambo ya kheri, mkikoseana jambo moja tu basi linafatiwa na machozi ya huruma.
Hapo tena utaanza kuona mauwa ya mapenzi yanachanua, utakua unahisi huruma kwa mwenzio zina zidi, utaanza kumsaidia mpaka kazi ndogo ndogo za nyumbani usione haya, ukiona unafanya hivo usijiulize nini hichi jua moja kwa moja ni mapenzi. Ukitenda hayo utaona mapenzi yenu yanakua kitu kimoja, sasa tena mnageuka kuwa marafiki na mkishafikia (stage)hiyo hakuna anoweza kuyakata mapenzi yenu na hapo ndio utakua umekutana na (Soul-mate)wako. Pia napenda mjue mwanamke njia yake ya kuonesha mapenzi ni ya hisia(Feeling)na mwanamme njia yake yeye ya(Action)matendo, hayo kwa uchache ni maua ya mapenzi, lakini hizo hisia na vipi unakhisi hiyo imo ndani ya huo (Moyo)na hakuna awezaye kuileza siri hiyo ispokua wewe mwenyewe ndie unayoijua.
Ikiwa ndoto yako huwezi kumualika hata mumeo akawa anaiona vipi leo utahadithia nini mapenzi weka siri hiyo (enjoy)wala huna haja ya kuitoa siri ya moyoni.
Naam Nini Rehma? rehma ni hicho kinachoweka (Balance)katika maisha yenu, wakati ule penzi linapo ondoka Rehma inashika nafasi yake, Rehma zipo za aina nyingi wala hazihesabiki, na daima kumbuka mapenzi yakipungua Rehma zinazidi, kama vile afya njema, watoto na Riziki zinaongezeka, kuoneana huruma kunazidi nk.
Baada ya kujua hayo wasia wangu msipite mkazifanyia mzaha talaka zenu, msije kuachana kwa vikosa vidogo vidogo, jifundisheni tabia njema za mmoja akimuona mwenzie kaja juu basi yeye arejee chini, mkumbushe mwenzio kila wakati kuwa yupo moyoni, kumbushaneni siku za mwanzo za ndoa yenu, ukiyafanya hayo utapata heshima kutoka kwa mwenzio na uaminifu, pendelea kuiweka siku ya kukutana na mwenzio kimwili ifanye kama siku ile ya harusi.Endelea-part-5

MAISHA YA MKE NA MUME MAPENZI MAJAALIWA-PART-5
Asalaam Aleiykum,
Fanyeni siku maalumu za kutoka pamoja, jaribu utakavoweza kumpunguzia mkeo shughuli za jikoni, ifanyeni nyumba yenu iwe kivutio cha Ibadah,jitahidini sana msiseme uongo, asije mmoja wenu akawashambulia wazee wa mwenzie, pia msitumie lugha ya hasira na ghadhabu baina yenu. Semeni maneno matamu, mwenzio akikuwekea chai usisahau ahsante, akikupa maji mtazame usoni umpe ahsante, akikupa chakula sema Bismillah kwa sauti, na ukimaliza sema Alhamdullillah kwa sauti ikisha mpe ahsante, mimina mapenzi kwa mkeo au mumeo hayo yatafanya ndoa yenu idumu maisha, jaribuni kuishi maisha ya kawaida wala msifanye kuyataka mambo makubwa msokua na uwezo nayo.
Someni Quraan pamoja, nyote wawili kila wakati muwe mumependeza ndani ya nyumba, usimseme mwenzio kwa marafiki zako, usimcheke mbele za watu au mbele za watoto.
Usimfanyie vitimbi mwenzio, akikosea jaribu kumfundisha mwenzio kwa ukimya na mapenzi, mpikie mwenzio vyakula vizuri, ukiona baada ya hayo yote mwenzio ana safari za nje za udanganyifu usimzonge kwa matusi, ukigundua labda ana mambo fulani huko nje basi jiepushe kukutana naye kimwili mpaka ajirekebishe, mimina mapenzi na huruma mpaka mwenzio ajute moyoni. Kila wakati omba Mollah wangu nidumishe mimi na mume wangu, Kiroho, Kimwili, na ki Akili, utudumishe katika ufalme wako. Napenda kukumbusha Mume au Mke asidanganyike na vivutio vya nje, kwani hivo unavoviona nje ni (Projection)yako una buni wewe mwenyewe kwenye akili yako, ndio maana unachoona wewe kizuri mwenzio anakipita bila hata ya kugeuza uso, ukimuona fulani mbaya mwenzio anamkamata mkono hadharani, basi elewa hayo yote unayo yaona nje yanatokana na Akili yako na hiyo (Shetani)rahisi kukuchezea, lakini jambo la Mke au Mume ni jambo la Rohoni ambalo linadumu daima na hususan mkizaa, mnaweza kutengana kimwili lakini kiroho daima mtakua ndugu au marafiki.
Hapo aya inamalizia "Bila ya shaka katika hayo zimo ishara kwa watu wenye kufikiri" Na wewe kuwa mmoja wao katika hao wenye kufikiri ukifanikiwa kuipata hiyo fikira nini kitatokezea?Quraan Zukhruuf-70"ٱدۡخُلُواْ ٱلۡجَنَّةَ أَنتُمۡ وَأَزۡوَٲجُكُمۡ تُحۡبَرُونَ"
"Ingieni Bustanini (Peponi)nyinyi na wake zenu, mtafurahishwa (Humo)" Hapo tena unarejea kule mwanzoni "Nimekuumbieni wake zenu kutokana na jinsi yenu""Ewe Nabii Adam a.s kaa wewe na Mkeo kwenye Bustani", na nyinyi sasa mnaambiwa ingieni kwenye hii pepo(Bustani) nini mtafanyiwa(Zukhruuf-71)
"يُطَافُ عَلَيۡہِم بِصِحَافٍ۬ مِّن ذَهَبٍ۬ وَأَكۡوَابٍ۬ۖ وَفِيهَا مَا تَشۡتَهِيهِ ٱلۡأَنفُسُ وَتَلَذُّ ٱلۡأَعۡيُنُۖ وَأَنتُمۡ فِيهَا خَـٰلِدُونَ"
"Watakuwa wanapitishiwa sahani za (Dhahabu)na vikombe vya (Dhahabu),na vitakuwamo ambavyo nafsi zinavipenda na macho yanavifurahia, na nyinyi mtakaa humo milele"
Fanya subira na mkeo au mumeo tulia ulee watoto wako, ewe ndugu yangu pata shida hapa duniani ili ukapate hivyo ambavyo nafsi inavipenda na macho inavifurahia, inayotakiwa hapo ni subira tu wala si chengine, usije ukakimbia familia yako na mkeo hapa duniani utakosa hapa ulimwenguni na kesho huko akhera, mwisho ukifanya kheri utalipwa kheri, na ukifanya shari utalipwa kwa shari yako.Mollah wetu zisitiri ndoa zetu na vizazi vyetu, wapatanishe walogombana,zisafishe nyoyo zetu uyajaze mapenzi yako, ikisha utukirimu sisi pepo yako ya milele.Amin
Abdulla Baja

Monday, October 8, 2012
UNATAKA KUJUA KWANINI KILA UKITUBU UNAFANYA TENA?-PART-1
Asalaam Aleiykum,
Limekuja swali nimeona nisifanye uchoyo ila nishirikiane na nyinyi wenzangu katika jawabu lake, Nimefanya hivi kwa sababu sote tunaishi katika hali hii iloulizwa. Ana uliza Muulizaji kila nikitubia najikuta nafanya tena, hata nikiweka nia ya sasa sitofanya tena basi moyo unashindwa, Kwanini hali kama hii imenizonga sana?.
Muulizaji kwa bahati kataja makosa mawili matatu lakini hili la uzinifu ndio hassa linalo msumbua, nikamfahamisha akasome (mada)ilopita ya dawa ya dhanbi, lakini akanijibu anachotaka yeye ni kuwacha kabisa hayo madhanbi ili apate (Tawbat-Nasuha).Kesha choka Mja kumuasi Mollah wake, anataka ajisafishe kwani kishamaliza kila mbinu hajafanikiwa.
Naam hiyo ndio kawaida yetu wanaadamu lakini leo pengine unaweza kuondoka na mbinu au (Trick)ukaweza kupata mafanikio ya toba ya kudumu, ukaweza kuacha moja baada ya jengine, Ikiwa imefanikiwa kwangu mimi dawa hii kwanini isifanikiwe kwako wewe, lakini yategemea na wewe jee uko tayari kuchukua dawa hii?, Zengine nyingi ushapewa kama vile, Mzalia nyuma, Mkaburi shams, Mvule, Mtambaa nyumba nk, watu wamemaliza dawa hizo zote na sasa hawana la kufanya, kama mke ndio anakutizama, wazee hawana hamu, na wewe unahisi sasa kwa Mollah wako hutakiwi tena, ndipo ikakujia akili ya kuuliza ufanye nini?, Basi namie nakwambia soma taratibu yaingie moyoni mwako ili uipate(Tawbat-Nasuha).Sasa tuingie kwenye Mada:
Anasema Ibn Arabi, "Katika kitabu chake cha (Shajarat Al-kawn)"
"Katika jinsia ya Mwanaadamu kuna mazuri na mabaya, Na ndani ya matendo yake huyo(Mwanaadamu)kuna yenye manufaa na yenye madhara, na katika Umri wao huenda wakachagua ama kurejea kwa Mollah wao au kuangamia moja kwa moja". "Lakini inapo tokezea wakachagua kuwa (Wacha-Mungu)basi wanakua ni wenye kudhibiti kiwili wili(Umbile)lao, Na mbele ya Mollah wao wanakuwa bora zaidi ya Malaika. Lakini ikiwa hicho kiwili wili(Umbile)kimetawala Roho, hapo tena Roho inasagwa na (Kuvurumishwa)na weusi mpaka taa za nafsi zao kuzimika, na hapo ndio hurejeshwa wakawa chini ya wanyama(mnyama anafadhali), na hupiga khatua moja kumpita shetani"(Mwisho wa kunukuu).
Itabidi maudhui hii iwe ndefu kidogo ili upate ufahamu wa ndani katika nafsi yako,ili uipate hiyo (Tawbat-Nasuha).Sasa tuikaribishe Quraan kutufungulia rasmi somo letu la leo, hebu twende kukutana na sura ya (Al-Qalami)aya ya kwanza inatwambia nini?-Endelea Part-2

UNATAKA KUJUA KWANINI KILA UKITUBU UNAFANYA TENA?-PART-2
Asalaam Aleiykum,
"نٓۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ"
"Naapa kwa(Akili)na kalamu na yale wayaandikayo"
Nini Nuun?zimeletwa tafsiri nyingi za neno hili, lakini iliyo muafaka na karibu zaidi ni kama hii ya kiapo cha utendaji wa kazi wa Akili, Ameitukuza Mwenye-enzi-Mungu akili, na sisi wanaadamu hatuna budi ila kukirejesha kiapo hicho kwake mwenyewe Mbora wa (Uumbaji).
Ndio maana utakuta katika aya ya pili ya sura hiyo hiyo anaambiwa Bwana Mtume s.a.w haikua "Neema hii ikawa wendawazimu" Neema hii alotupa Mollah wetu ni zawadi iso mfano kwa mwanaadamu, Na kutokana na zawadi hii ya Akili ndio yamekua mategemeo yetu yote ya kufanikiwa au kuharibikiwa yanatokana kwenye hii Akili, vipi utaitumia hii akili ndio mtihani ulopewa.
Unakuja katika Ulimwengu huu ukiwa mweupe, Safi huna doa, ndio maana watu huzungumza kitu akifanya mtoto, maskini hana Akili, Sasa nini kinafanyika?anaitaja tena Mwenye-enzi-Mungu katika sura ya (Alaq-aya-ya-4)"ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ""Aliyemfundisha mwanaadamu kutokana na kalamu" (hapa napenda nifahamishe usije ukadhani kalamu ya ofisini, kumbuka hivi sasa tunaandika kwa computer, kwa hiyo sio kalamu tena)Lakini kalamu ilokusudiwa hapo ni hiyo Akili, Ukenda kuwauliza wanasayansi watakwambia Akili ufanyaji wake wa kazi zake kama vile kalamu au (Computer)inaandika kile inacho ona na kusikia inaweka kwenye (Memory)yake, ndio maana utaona ukifundishwa kuogelea au Baskeli au gari wakati ule unapojifundisha inakua jambo moja jipya lazima uliandike kwa uangalifu na uwe makini, lakini ukishajua unakua huna haja kushughulika zaidi, inakua kama alivosema Mollah wako "(Na yale wayaandikayo)"kwa hiyo likija jambo ambalo ulokua ushalijua (umeliandika)kwenye (Memory)unachofanya ni kwenda kwenye ile (process) na kulirejea tena, Na hiyo ndio akili, Kutokana na utaratibu huo ndio tukambiwa "Ewe Mwanaadamu usikaribie (Zinaa)"sababu ukishaigusa huwezi kuacha, tabu kuitoa kwenye Akili, jambo hilo zito sana na hivi ndio mambo yanavo tuzunguka tukawa hatuwezi kuacha.
Sasa nini kinatokezea hapo? Mfano ni ule ule wa mtoto ukimfundisha baskeli huwezi kurudi ukataka eti sasa uondoe mafunzo yako mtoto asijue tena Baskeli, huwezi kufanya hivo, na hivo ndio inavokua kwako wewe, ukisha onja tunda haliachiki, ndio maana ukaambiwa usikaribie, wewe dhaifu huwezi kuacha, na zaidi ya hilo unapata shabiki mwengine na ni huyu Ibilis (Shetani)anafanya nini? pata habari hii ili ujue vipi shetani anavo fanya kazi zake.Quraan(Aaraf-aya-ya-16)
"قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِى لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٲطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ"
"Akasema(Ibilis)Kuwa umenihukumia upotofu basi nitawakalia (Waja wako)katika njia yako ilonyooka,(Ili niwapoteze)"
Sasa ni njia gani hii? Na nini kinachokujulisha hii njia, Quraan(Dahr aya-ya-2)" إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٍ۬ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَـٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا"
"Hakika tumemuumba mwanaadamu kutokana na mbegu (ya uhai)ilochanganyika ili tumfanyie mtihani,(kwa hiyo)tukamfanya(Kumjaalia)mwenye kuona na kusikia".
Wanasayansi wamegundua si zamani sana yakua Binaadamu ni (Both)umbile lako limechanganya nusu Mama yako na Nusu Baba yako, na unaweza kujifanyia mtihani wewe mwenyewe utaona kuna upande una nguvu nyingi na upande mwengine upo dhaifu(male)na(female)Na huko kuona na kusikia viwili hivyo kuna nyakati vinaondoshwa, kama pale ukilala huoni wala husikii.
Sasa tunaingia hiyo njia anayokaa (Ibilis)ni ipi?Endelea-Part-3

UNATAKA KUJUA KWANINI KILA UKITUBU UNAFANYA TENA?-PART-3
Asalaam Aleiykum,
"إِنَّا هَدَيۡنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرً۬ا وَإِمَّا كَفُورًا"
"Hakika sisi tumemuongoza(Tumemuonesha) njia (akitaka)atakua mwenye kushukuru au mwenye kukufuru (kupotea)"
Iliposemwa njia wenye kufahamu mambo wakaona haijambo kidogo tumepata nafuu, kumbe Ibilis (Shetani)hawezi kukaa kwenye nyumba, anaishia njiani tu, ujanja wake wote hawezi kukaa wala kuingia katika nyumba yangu anaishia mlangoni, kumbe naweza kubadilisha njia nikapita pembezoni, sasa hii njia ni ipi alopewa mwanaadamu hata (Ibilis)akawa anaiandama? Hapo inatajwa Akili lakini kwa methali nyengine kabisa.
Njia yenyewe ni hii alopewa mwanaadamu huku kufahamu,(Fahamu)(Hekima)(Busara)ikisha akapewa uhuru akitaka afate au apotee, Hapa ndipo aliposema Ibilis (Shetani)nitawakalia katika njia yako, si ushawafundisha mengi ya uongofu, sasa mie nakwenda kukaa njiani, vipi nitakaa(Quraan-Aaraf-17)
"ثُمَّ لَأَتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِہِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَييۡمَـٰنِہِمۡ وَعَن شَمَآٮِٕلِهِمۡۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَـٰكِرِينَ "Ikisha nitawafikia kwa mbele yao na nyuma yao,na kuumeni kwao na kushotoni kwao, wengi katika wao hutawakuta ni wenye kushukuru"
Naomba pita katika aya hii na fahamu nzuri, ukipafahamu hapa itakua rahisi kwako kuwafahamu (Mashetani)na utakua unakaribia kuipata hiyo (Tawbat-Nasuha). Hapa Ibilis anaingia katika (Nature)ya Akili(Brain)ukiitizama Akili utaona ina mambo mawili na (wewe mwenyewe jitizame)Nilipoanza mwanzoni nilitaja aya inayosema"Naapa kwa Akili na yale waandikayo", Ukichunguza utakuta Akili inaandika (Past)yalopita yaani (Memory)kumbukumbu, na (Future)yajayo bado hayajakua, Akili ina safiri katika viwili hivyo future na past ama utafikiri mambo yalopita au yajayo lakini taabu sana kufikiri wakati ulo nao wa hivi sasa, Sasa Ibilis kwa kujua (Nature)ya Akili akasema nitawafikia mbeleni kwao kwenye (Future)watasahau wakati huu wa sasa (Hivi)au nitakwenda nyuma kwao(Memory)na mfano kama vile ukiona (Figure)ya Mwaname au Mwanamke, unaanza kupanga ntampataje, itakuaje, na kama mshafanya maasi zinamiminika zile kumbukumbu ilikua hivi ikawa vile nk, hapo unarejea kwenye (memory)unachambua na ukitahamaki unapanga mikakati vipi au lini mtakutana usha safiri baina ya future na past na hapo shetani anachofanya nikuja kukumbusha tu, sababu tayari imo kwenye (memory)yako. Anakwenda Shetani huyu kwa mwanamke anamnogoneza (Figure)hiyo lazima uioneshe, bana zaidi nguo yako, halafu anarudi kwa mwanamme kesha ibana kama jana na ukitizama umeumia, hivi ndivo akili inavofanya kazi zake hapo ulipo ukitaka kurudi utotoni kwenye Akili yako ukifunga macho tu unarejea moja kwa moja utotoni, sasa ukigundua hivo basi unaweza kutafautisha, umeshaweza kuweka tafauti na ukigundua tafauti hiyo basi jiulize nani huyu ano kumbuka?huyo alokumbuka sasa hivi, huyo ndio asoweza kuingiwa na shetani, hapo shetani haingii, hiyo ndio nyumba ambayo shetani hafiki anabakia njiani kwenye akili, na hizo ndio hizo kumbukumbu (memory)nilizozitaja na mpaka hapa utakua ushaanza kujua kumbe wewe na akili ni vitu viwili tafauti, na vile vile ushagundua kumbe inayosahaulishwa ni akili yangu, kumbe nikiwa (hadhir)siwezi kutenda kosa.
Akaendelea kusema Ibilis nitawakalia kuumeni kwao na kushotoni, Naam aya imetaja wewe una mbegu mbili zilochanganyika, una jinsia mbili (Mke na Mume)katika umbile lako ndio maana mara nyengine unakua mpole na maridhia kama mwanamke na mara nyengine unakua mkali hushikiki kama vile mwanamme. Wanasayansi wameita (Akili ya upande wa kushoto na upande wa kulia)Alipogundua Ibilis utendaji wake wa kazi ndio akasema nitawakalia katika jinsia zao zote mbili, kuumeni kwo na kushotoni kwao, kwani viwili hivi kimoja kikipinga basi hakuna jambo linalofanyika, ndio maana saa nyengine unasema roho yangu nzito, Ibilis kakugundua inakua vigumu lazima azipate pande zote mbili. Sasa kabla yakutaja nini cha kufanya kuepuka hali hii ili usikubali tena upumbavu huu wakuteseka kwa madhanbi, basi tutupie macho kauli hii niloitaja kutoka kwenye aya za mwanzoni kuhusu kuona na kusikia.Endelea-4

UNATAKA KUJUA KWANINI KILA UKITUBU UNAFANYA TENA?-PART-4
Asalaam Aleiykum,
Napenda niongeze hili la kuona na kusikia ili nipate kuamsha kitu ndani ya fahamu yako, yatizame mambo haya mawili vizuri na utagundua vipi hiyo nyumba yako niloitaja ya fahamu inavo tawaliwa na mambo haya mawili, jitizame ukitizama mchezo kwenye TV au senema unasahau kila kitu chengine, au ukisikiliza muziki chochote kengine hakiingi na hiyo ndio fahamu ambayo ni zawadi na neema alotupa Mollah wetu. Nini dhumuni langu kukutajia kuona na kusikia, nia yangu ni kukufahamisha vipi fahamu inavotekwa na mambo mawili haya, na kwa mfano huo huo basi na maasi pia yanaiteka akili yako kama inavofanya tv na muziki, na inakua rahisi Ibilis kufanya kazi zake, na hiyo ndio maana ya kukukalia katika hiyo njia.
Sasa ufanye nini na kila njia imeshindikana, napenda uelewe Dini zote za haki zimesisitiza au kuja na jawabu na huipati jawabu isipokua katika neno la (Dhikr)kukumbuka, Nini kukumbuka?ni (Awareness)au(Dhahir)au(Alertness)ndio ukaambiwa simamisha Sala,kumbuka, kufunga kukumbuka, kukaa na udhu kukumbuka na mengi mengineyo, nimeitaja hiyo fahamu na kutilia mkazo kwa kuwa ukiteleza kidogo ukawa hukumbuki hapo ndipo katika (gap) hiyo (Shetani)au wewe mwenyewe unapotenda kosa.
Sasa ufanye nini?jichunguze lipi kosa lako kubwa linalo kutesa huwezi kuliacha, tuseme mfano uzinifu (si huwezi kuacha)basi fanya kitu kimoja tu, vengine ndio vishashindwa, sasa ukiwa unakwenda katika hayo madhanbi (maasi)basi kumbuka kila tendo, kama sasa nakwenda, nimeshafika, jaribu usikumbuke chochote kumbuka ndio nakwenda kuzini, nimeshafika, nimekaa kitu kadhaa kinafanyika kumbuka kuanzia mwanzo mpaka mwisho usifikiri chengine chochote, au unakwenda kuiba kumbuka mwanzo mpaka mwisho, au unapokea rushwa kumbuka mwanzo mpaka mwisho wa hili tendo, unasengenya mtu endelea kumsengenya lakini kumbuka tu namsengenya fulani mwanzo mpaka mwisho, kila kile unachoona kigumu kuacha basi kifanye huku unakikumbuka mwanzo mpaka mwisho, hee hata ulevi, Naam mpaka pombe tokea unamimina mpaka unakunywa wewe kumbuka mpaka inaanza kukulevya wewe endelea kukumbuka tu na ukifanya kwa muda wa mara saba lakini kwa uyakinifu sio unazungumza halafu unakumbuka hapo itakua usha haribu, inatakiwa isipatikane (Gap)basi ikiwa utaweza kutenda tena mara ya nane hali yakua unakumbuka mwanzo mpaka mwisho basi wewe huna dawa,(Elewa booking yako ya motoni ishakua confirm)huwezekani tena.
Ikiwa mbinu hii imefanya kazi kwa watu wengi kwanini isifanye kazi kwako, Sasa nini kinatokezea hapo ukifanya mara mbili tatu, (Siri)yake unakua (Full-Alert)na hatendi mja kosa akiwa yupo hadhir, mwizi haingii katika nyumba wenyewe wakiwemo tena wamacho, itakufungukia fahamu kuwa hilo tendo lako ni la kipumbavu na kipuuzi, na halina maana, utaanza kulichukia moja kwa moja hakuna mwanaadamu mwenye kupenda dhiki, na hapo utaliacha mara moja na hiyo ndio (Tawbat-Nasuha)ndio maana ukaambiwa kwenye Quraan:Ankaboot.
"إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِۗ وَلَذِكۡرُ ٱللَّهِ أَڪۡبَرُۗ "
"Hakika sala ni yenye kukuepusha na madhanbi(makubwa)na mambo ya munkar, na umkumbuke Mollah wako aliye Mkubwa"
Ukimkumbuka Mollah wako nyakati zote huwezi kutenda kosa na hiyo ndio maana ya (awareness)ndio maana ya kusimamisha sala, sio ile sala unayosimama huku unakumbuka biashara, au unakumbuka miadi, au harusi ya leo itakuaje. Sala ilokusudiwa hapa ni kuendelea bila kusita kumkumbuka Mollah wako, na hekima hapa ukimkumbuka Mollah wako inakuepusha na maasi, na ukikumbuka kosa lako vile vile linakurejesha kwa Mollah wako, hiyo ndio maana ya kujuta,na huko kujuta vile vile kuna kurejesha kwa Mollah wako (Njia moja)ilonyooka ukipita kokote unatokezea hapo hapo kwa Mollah wako nayo ni hiyo"ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٲطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ"Na ukifika katika hiyo njia basi wewe unakua sawa sawa na Walii au Mcha Mungu, tafauti yenu ni Mcha Mungu anagonga mlango, na wewe umesimama hugongi hiyo ndio tafauti yenu, sasa anza na wewe kugonga hujui nani atafunguliwa mwanzo.Mwisho namalizia kwa kukwambia ichunguze sana tabia yako ina kawaida ya kurejea rejea mambo ndio maana kila ukitubu unafanya tena. Mollah wetu tujaalie nguvu ili tuweze kuipata toba ya moja kwa moja(Tawbat-nasuha)Mollah wangu ndie ajuae zaidi.

Monday, October 1, 2012
VIPI UNASHUHUDIWA KWA QURAAN YA ALFAJIRI-PART-1
Asalaam Aleiykum,
Jee unataka kujua vipi umezongwa na dunia? kwanini unachukia mambo ya darsa?, basi jitizame namna gani unavokimbia mawaidha na ukumbusho wa hicho unachokiamini na kukitegemea hata yakikujia mafundisho kama haya ya Tawhid ya kumjua Mollah wako, basi unakua kusoma kwako ni kwa kupita pita tu na wala si yenye kuzama ndani ya moyo mwako. Imekua hasara kubwa kwako wewe mwanaadamu kuikosa faida itakayo kukusaidia hapa Ulimwenguni na huko akhera uendako, kwa kuwa na sisi wajibu wetu kuufikisha ujumbe huu au dawa hii ya Roho basi tutaendelea kukupa na wewe una hiari yako kumeza(Kufikiri)au kutupa(kupuuza), Tunafanya hivi kama wafanyavo madaktari wanokupa dawa zako za mwili, ulipokua kijana ulikua mara chache sana kwenda kwa Doctor, lakini sasa Umuri usha sogea, uzee unapiga hodi, kifo hakipo mbali, sasa unahitaji vidonge huendi lazima upewe cha pressure au cha sukari n.k, hivi vya hospital unakula haraka haraka lakini hichi cha Roho hutaki kukiona au kukisikia unaona mambo gani, mara hii kasema nini, hebu tizama anatisha safari hii, unasahau hichi cha Roho ndio Muhimu sana kadir ya Umri unavo kwenda mbele.
Leo hii tunaendelea na somo letu la Tawhid ambalo pengine ulikua huna ujuzi nalo au umeghafilika, basi soma kwa utulivu uchukue faida hii kubwa iwe ufunuo kwako na umfahamishe mwenzio unaye mtakia kheri ili naye apate faida hii adhimu, na wala usijali inatoka kwa nani, wewe chukua faida yake na kuanzia leo utakua mtu mwengine kabisa wakati unapo kwenda kulala, utakua hujitupi tu kipuuzi, utakwenda kulala ukiwa na fahamu nzuri ya kiroho.
Vipi unashuhudiwa na Quraan? na ina umuhimu gani kushuhudiwa huku?na nini kinatokea wakati inapopatikana shahada yenyewe?na Kwanini hassa ikawa Alfajiri?(Qur'aan-Israa-78)
"أَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِدُلُوكِ ٱلشَّمۡسِ إِلَىٰ غَسَقِ ٱلَّيۡلِ وَقُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِۖ إِنَّ قُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِ كَانَ مَشۡہُودً۬ا"
"Simamisha Sala, Jua linapopinduka, Mpaka(liingiapo)giza la usiku,Na Quraan ya Alfajiri, hakika Quraan ya Alfajiri Inashuhudiwa"
Inatosha Mwanaadamu aya hii moja kukufunga na Mollah wako ukawa huna haja na kitu chengine chochote, Kwanini ikawa hivyo?, imekua hivyo kama wewe ni mcha Mungu basi aya hii inakua Rafiki yako kipenzi, inakua ufungua wako, inakua ukumbusho wako, sababu kubwa ni kule kukupa ukamilifu wa Ibada.
"Ewe mwanaadamu simamisha Sala pale jua linapoanguka limeshauvuka utosi"Sasa sahau yote uanze safari ya kurejea nyumbani, Wapi? kwa uchambuzi zaidi itabidi kwanza tuhame kwenye aya hii ili tukachume kwenye bustani kubwa ya Quraan ili ipate kutupa maana halisi ya kushuhudiwa kwa kusoma Quraan nyakati za Alfajiri. Endelea Part-2

VIPI UNASHUHUDIWA KWA QURAAN YA ALFAJIRI-PART-2
Asalaam Aleiykum,
Imekufikia habari, au ushawahi kuuliza au kujiuliza mtu anae kunywa mvinyo(Ulevi)au mcheza taarab usiku kucha au Dance au mkesha wa chakacha usiku kucha kwanini wakiamka wanakua wamechoka, au vichwa vina wauma?, Na Umemuuliza Mcha Mungu au anaye simamisha Sala mbona wao wakiamka wako(Fresh)mbichi, nguvu mpya, tayari kwa siku ianze apate kushughulika na maisha?jee unayo majawabu ya maswali haya, na kama huna safiri na mimi ili nipate kukupa siri ya mambo yanavokua upate kuwa muangalifu kuanzia leo hata huko kulala kwako kuwe Ibada, upate kujiepusha na mambo fulani fulani wakati unapo kwenda kulala utakua daima na wewe unaamka (fresh)msafi huna doa na unashuhudiwa kwa matendo yako yote, hapana pengine pakuuliza isipokua Quraan-sura ya Zumar aya ya 42.
"ٱللَّهُ يَتَوَفَّى ٱلۡأَنفُسَ حِينَ مَوۡتِهَا وَٱلَّتِى لَمۡ تَمُتۡ فِى مَنَامِهَاۖ فَيُمۡسِكُ ٱلَّتِى قَضَىٰ عَلَيۡہَا ٱلۡمَوۡتَ وَيُرۡسِلُ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ إِلَىٰٓ أَجَلٍ۬ مُّسَمًّىۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ "
"Mwenye-enzi-Mungu huzipokea Roho wakati wa Mauti, Na zile zisizokufa pia(Mwenye-enzi-Mungu) huzitakabadhi katika (usingizi)kulala kwake, Na huzizuia zile zilo hukumiwa kufa, huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa(pangiwa)Hakika katika hayo mna mazingatio kwa watu wanao fikiri"
Siku zote natilia mkazo tuwe waja wenye kufikiri, tunahimizwa tufikiri na leo hapa hebu tulitupie macho tukio hili la usingizi tulifikiri kwa pamoja, Utagundua katika umri wako kila usiku wewe unarejea nyumbani kwa Mollah wako, hujawahi kuwa mbali na Mollah wako, kuna nyakati za usiku unaondoka katika huo mwili unaoringia unarejea kule ulipotokea, unakwenda kuchukua nguvu mpya, Unarejea kupewa Rehma mpya, unarejea tena Ulimwenguni ukiwa msafi, kumbuka tukio hili unalitenda kila pale unapokwenda kulala lazima urejee, Ukiwa Umelewa au mzima, ukiwa unaumwa mgonjwa au una afya yako marejeo ni lazima, ndio maana utaona madaktari wanahimiza mgonjwa lazima apumzike alale apate kwenda kwa Mollah wake kutibiwa, huko ndiko kunako toka tiba zote, Sasa nini habari yako wewe unarejea kila siku Umelewa, au umedhulumu watu, au umefitini watu au umevuta (Mihadarati)au umezini unarejea kwa Mollah wako na machafu haya, jiangalie mwenyewe kiafya na kia Akili una hali gani?.
"Enyi ndugu zangu tujihadhari sana kila siku kurejea tukiwa na hali kama hizo tunarejea kwa Mollah wetu na Mzigo wa madhanbi"shukuru sana unarejea kwa Mollah wako hali ya kuwa huna fahamu, lau ungepaona pahala unapowekwa kwenye hayo masaa yako manne au sita unayolala basi usingetenda dhanbi tena.Laiti ungetambua kiasi gani unakera kwenye Ufalme wa Mwenye-enzi-Mungu basi ungekaa mbali na maovu.
Sasa nini kinatokea ikiwa usiku umerejea kwa Mollah wako na Moyo wa Salama, Umerejea na huku umefunikwa na Taqwa, uko msafi, basi dalili zake ni zile za wewe pale unapoamka uko msafi, Roho yako ina Tohara tupu, mweupe huna doa, Roho haijafikwa na madhila yoyote, Akili nyeupe haijaingia uongo wala mambo ya kidunia hujayaona, wala matamanio hayajafika moyoni, wala picha za maasi hujafungua, bado hujenda kwenye Face book, hujafungua Computer na kuona matangazo yoyote, hujenda barazani au kuanza kuzungumza chochote, hapo ndipo unapoambiwa kitu cha mwanzo Roho imetokea kwa Mollah wako kinachofatia soma Quraan,(Ndio maana school zikawa asubuhi ingekua usiku nani angefahamu)kitu cha mwanzo yajaze maneno yetu Rohoni ungali safi, kabla hazijaingia biashara kichwani na mambo mengine ya kipuuzi, ukifanya hivo inakua maneno ya mwanzo yanaingia kitabu cha Mwenye-enzi-Mungu na ukiwa na Tabia hii basi mpaka maisha yako yatabadilika utaishi kwa mwenendo wa Quraan, na hapo ndipo (Malaika)watashuhudia matendo yako, Quraan ndio inakua dira yako, mpaka wanaadamu wataanza kukushuhudia yanakua Maisha yako toka ukiamka una shika Ibada mpaka kulala kwako wewe unakuwa umo ndani ya Ibada na hapo tena unaingia kwenye fungu la wale walotajwa katika sura ya Saffat aya ya 3.
"فَٱلتَّـٰلِيَـٰتِ ذِكۡرًا"
"(Na)Kwa wale wasomao ukumbusho(mawaidha)ya (Mollah)wao"
Kila alfajiri wewe umepata (ukumbusho)basi kutwa nzima unakua ni mwenye kukumbuka na ukikumbuka unasimamisha sala na siku nzima unakua tajiri mwenye kumkumbuka Mollah wako, na ukiendelea na kawaida hii kwa muda wa miezi mitatu mfululizo Mollah wako hukuteremshia Nuru mpaka wanaadamu wenzio watakua wanaanza kuiona, lakini wale wenye macho.
Na huko ndiko kushuhudiwa kwenyewe na yoyote mwenye kutaka kuhifadhi Quraan au hata masomo mengine ajaribu kuamka nyakati hizi za Alfajiri na ataona mafanikio yake. Namuomba Mollah atujaalie tuwe wenye kushuhudiwa kwa matendo haya ya kheri. atujaalie tuishi kwa mujibu wa mawaidha yake na uongofu wake.Amin

Subscribe to:
Posts (Atom)