Monday, October 8, 2012

UNATAKA KUJUA KWANINI KILA UKITUBU UNAFANYA TENA?-PART-2

Asalaam Aleiykum,

"نٓ‌ۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ"
"Naapa kwa(Akili)na kalamu na yale wayaandikayo"
Nini Nuun?zimeletwa tafsiri nyingi za neno hili, lakini iliyo muafaka na karibu zaidi ni kama hii ya kiapo cha utendaji wa kazi wa Akili, Ameitukuza Mwenye-enzi-Mungu akili, na sisi wanaadamu hatuna budi ila kukirejesha kiapo hicho kwake mwenyewe Mbora wa (Uumbaji).
Ndio maana utakuta katika aya ya pili ya sura hiyo hiyo anaambiwa Bwana Mtume s.a.w haikua "Neema hii ikawa wendawazimu" Neema hii alotupa Mollah wetu ni zawadi iso mfano kwa mwanaadamu, Na kutokana na zawadi hii ya Akili ndio yamekua mategemeo yetu yote ya kufanikiwa au kuharibikiwa yanatokana kwenye hii Akili, vipi utaitumia hii akili ndio mtihani ulopewa.
Unakuja katika Ulimwengu huu ukiwa mweupe, Safi huna doa, ndio maana watu huzungumza kitu akifanya mtoto, maskini hana Akili, Sasa nini kinafanyika?anaitaja tena Mwenye-enzi-Mungu katika sura ya (Alaq-aya-ya-4)"ٱلَّذِى عَلَّمَ بِٱلۡقَلَمِ""Aliyemfundisha mwanaadamu kutokana na kalamu" (hapa napenda nifahamishe usije ukadhani kalamu ya ofisini, kumbuka hivi sasa tunaandika kwa computer, kwa hiyo sio kalamu tena)Lakini kalamu ilokusudiwa hapo ni hiyo Akili, Ukenda kuwauliza wanasayansi watakwambia Akili ufanyaji wake wa kazi zake kama vile kalamu au (Computer)inaandika kile inacho ona na kusikia inaweka kwenye (Memory)yake, ndio maana utaona ukifundishwa kuogelea au Baskeli  au gari wakati ule unapojifundisha inakua jambo moja jipya lazima uliandike kwa uangalifu na uwe makini, lakini ukishajua unakua huna haja kushughulika zaidi, inakua kama alivosema Mollah wako "(Na yale wayaandikayo)"kwa hiyo likija jambo ambalo ulokua ushalijua (umeliandika)kwenye (Memory)unachofanya ni kwenda kwenye ile (process) na kulirejea tena, Na hiyo ndio akili, Kutokana na utaratibu huo ndio tukambiwa "Ewe Mwanaadamu usikaribie (Zinaa)"sababu ukishaigusa huwezi kuacha, tabu kuitoa kwenye Akili, jambo hilo zito sana na hivi ndio mambo yanavo tuzunguka tukawa hatuwezi kuacha.
Sasa nini kinatokezea hapo? Mfano ni ule ule wa mtoto ukimfundisha baskeli huwezi kurudi ukataka eti sasa uondoe mafunzo yako mtoto asijue tena Baskeli, huwezi kufanya hivo, na hivo ndio inavokua kwako wewe, ukisha onja tunda haliachiki, ndio maana ukaambiwa usikaribie, wewe dhaifu huwezi kuacha, na zaidi ya hilo unapata shabiki mwengine na ni huyu Ibilis (Shetani)anafanya nini? pata habari hii ili ujue vipi shetani anavo fanya kazi zake.Quraan(Aaraf-aya-ya-16)
"قَالَ فَبِمَآ أَغۡوَيۡتَنِى لَأَقۡعُدَنَّ لَهُمۡ صِرَٲطَكَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ"
"Akasema(Ibilis)Kuwa umenihukumia upotofu basi nitawakalia (Waja wako)katika njia yako ilonyooka,(Ili niwapoteze)"
Sasa ni njia gani hii? Na nini kinachokujulisha hii njia, Quraan(Dahr aya-ya-2)"  إِنَّا خَلَقۡنَا ٱلۡإِنسَـٰنَ مِن نُّطۡفَةٍ أَمۡشَاجٍ۬ نَّبۡتَلِيهِ فَجَعَلۡنَـٰهُ سَمِيعَۢا بَصِيرًا"
"Hakika tumemuumba mwanaadamu kutokana na mbegu (ya uhai)ilochanganyika ili tumfanyie mtihani,(kwa hiyo)tukamfanya(Kumjaalia)mwenye kuona na kusikia".
Wanasayansi wamegundua si zamani sana yakua Binaadamu ni (Both)umbile lako limechanganya nusu Mama yako na Nusu Baba yako, na unaweza kujifanyia mtihani wewe mwenyewe utaona kuna upande una nguvu nyingi na upande mwengine upo dhaifu(male)na(female)Na huko kuona na kusikia viwili hivyo kuna nyakati vinaondoshwa, kama pale ukilala huoni wala husikii.
Sasa tunaingia hiyo njia anayokaa (Ibilis)ni ipi?Endelea-Part-3



No comments:

Post a Comment