Asalaam Aleiykum
Linapofunguka pazia la mapenzi, kila hatua ya ngazi mnayoshuka kabla hata ya kufika huko bondeni(moyoni)basi kwenu nyinyi inakua mapenzi, mwenzio akiwa kazini wewe umejaa mapenzi,ukimuona yana kumiminika machozi ya furaha, usione haya ndio mapenzi na mapenzi ni (Feeling)usiogope kuzionesha sasa mwenzio atajuaje, haziwi kumbukumbu zenu ila isipokua mambo ya kheri, mkikoseana jambo moja tu basi linafatiwa na machozi ya huruma.
Hapo tena utaanza kuona mauwa ya mapenzi yanachanua, utakua unahisi huruma kwa mwenzio zina zidi, utaanza kumsaidia mpaka kazi ndogo ndogo za nyumbani usione haya, ukiona unafanya hivo usijiulize nini hichi jua moja kwa moja ni mapenzi. Ukitenda hayo utaona mapenzi yenu yanakua kitu kimoja, sasa tena mnageuka kuwa marafiki na mkishafikia (stage)hiyo hakuna anoweza kuyakata mapenzi yenu na hapo ndio utakua umekutana na (Soul-mate)wako. Pia napenda mjue mwanamke njia yake ya kuonesha mapenzi ni ya hisia(Feeling)na mwanamme njia yake yeye ya(Action)matendo, hayo kwa uchache ni maua ya mapenzi, lakini hizo hisia na vipi unakhisi hiyo imo ndani ya huo (Moyo)na hakuna awezaye kuileza siri hiyo ispokua wewe mwenyewe ndie unayoijua.
Ikiwa ndoto yako huwezi kumualika hata mumeo akawa anaiona vipi leo utahadithia nini mapenzi weka siri hiyo (enjoy)wala huna haja ya kuitoa siri ya moyoni.
Naam Nini Rehma? rehma ni hicho kinachoweka (Balance)katika maisha yenu, wakati ule penzi linapo ondoka Rehma inashika nafasi yake, Rehma zipo za aina nyingi wala hazihesabiki, na daima kumbuka mapenzi yakipungua Rehma zinazidi, kama vile afya njema, watoto na Riziki zinaongezeka, kuoneana huruma kunazidi nk.
Baada ya kujua hayo wasia wangu msipite mkazifanyia mzaha talaka zenu, msije kuachana kwa vikosa vidogo vidogo, jifundisheni tabia njema za mmoja akimuona mwenzie kaja juu basi yeye arejee chini, mkumbushe mwenzio kila wakati kuwa yupo moyoni, kumbushaneni siku za mwanzo za ndoa yenu, ukiyafanya hayo utapata heshima kutoka kwa mwenzio na uaminifu, pendelea kuiweka siku ya kukutana na mwenzio kimwili ifanye kama siku ile ya harusi.Endelea-part-5
No comments:
Post a Comment