Monday, October 8, 2012

UNATAKA KUJUA KWANINI KILA UKITUBU UNAFANYA TENA?-PART-1

Asalaam Aleiykum,

Limekuja swali nimeona nisifanye uchoyo ila nishirikiane na nyinyi wenzangu katika jawabu lake, Nimefanya hivi kwa sababu sote tunaishi katika hali hii iloulizwa. Ana uliza Muulizaji kila nikitubia najikuta nafanya tena, hata nikiweka nia ya sasa sitofanya tena basi moyo unashindwa, Kwanini hali kama hii imenizonga sana?.
Muulizaji kwa bahati kataja makosa mawili matatu lakini hili la uzinifu ndio hassa linalo msumbua, nikamfahamisha akasome (mada)ilopita ya dawa ya dhanbi, lakini akanijibu anachotaka yeye ni kuwacha kabisa hayo madhanbi ili apate (Tawbat-Nasuha).Kesha choka Mja kumuasi Mollah wake, anataka ajisafishe kwani kishamaliza kila mbinu hajafanikiwa.
Naam hiyo ndio kawaida yetu wanaadamu lakini leo pengine unaweza kuondoka na mbinu au (Trick)ukaweza kupata mafanikio ya toba ya kudumu, ukaweza kuacha moja baada ya jengine, Ikiwa imefanikiwa kwangu mimi dawa hii kwanini isifanikiwe kwako wewe, lakini yategemea na wewe jee uko tayari kuchukua dawa hii?, Zengine nyingi ushapewa kama vile, Mzalia nyuma, Mkaburi shams, Mvule, Mtambaa nyumba nk, watu wamemaliza dawa hizo zote na sasa hawana la kufanya, kama mke ndio anakutizama, wazee hawana hamu, na wewe unahisi sasa kwa Mollah wako hutakiwi tena, ndipo ikakujia akili ya kuuliza ufanye nini?, Basi namie nakwambia soma taratibu yaingie moyoni mwako ili uipate(Tawbat-Nasuha).Sasa tuingie kwenye Mada:
Anasema Ibn Arabi, "Katika kitabu chake cha (Shajarat Al-kawn)"
"Katika jinsia ya Mwanaadamu kuna mazuri na mabaya, Na ndani ya matendo yake huyo(Mwanaadamu)kuna yenye manufaa na yenye madhara, na katika Umri wao huenda wakachagua ama kurejea kwa Mollah wao au kuangamia moja kwa moja". "Lakini inapo tokezea wakachagua kuwa (Wacha-Mungu)basi wanakua ni wenye kudhibiti kiwili wili(Umbile)lao, Na mbele ya Mollah wao wanakuwa bora zaidi ya Malaika. Lakini ikiwa hicho kiwili wili(Umbile)kimetawala Roho, hapo tena Roho inasagwa na (Kuvurumishwa)na weusi mpaka taa za nafsi zao kuzimika, na hapo ndio hurejeshwa wakawa chini ya wanyama(mnyama anafadhali), na hupiga khatua moja kumpita shetani"(Mwisho wa kunukuu).
Itabidi maudhui hii iwe ndefu kidogo ili upate ufahamu wa ndani katika nafsi yako,ili uipate hiyo (Tawbat-Nasuha).Sasa tuikaribishe Quraan kutufungulia rasmi somo letu la leo, hebu twende kukutana na sura ya (Al-Qalami)aya ya kwanza inatwambia nini?-Endelea Part-2

No comments:

Post a Comment