Monday, October 15, 2012

MAISHA YA MUME NA MKE MAPENZI MAJAALIWA-PART-2

Asalaam Aleiykum,

Kuanzia leo usimnyanyase mwenzio, usimdharau Mkeo au Mumeo kwani kwenye Mamlaka ya (Roho) nyinyi nyote sawa(Equal)Roho si mwanamke wala mwanaume lakini tafauti ipo hapo kwenye jinsia na kubwa zaidi katika hilo  la kuzaa, mengine yote siku hizi wanasayansi wamegundua, wanakupa dawa kila kitu kinabadilika dume linaweza kugeuka jike na jike likageuka dume, hayo yanafanyika na wala si maajabu tena Quraan imesema zamani (Amekuumbieni wake zenu kutoka katika jinsi zenu)nyie nyote jinsi moja, ili mpate utulivu kwao, ingia tena kwenye ishara utazame vipi unapatikana utulivu huu. Utulivu ulotajwa hapo upo wa aina mbili wa ndani na nje, Ama huu wa hali ya ndani chukua mfano wa kijana baro baro likipewa mke ghafla linavotulia, kama lilikua jitu la fujo, mtaani mnapata nafuu sasa, kwa sababu ameanza kupata utulivu, Baada ya kugundulikana hali hii inofanya watu wawe watulivu sasa ikaamuliwa majeshi yakakae kambini, kwani akiwachwa nyumbani jeshi hapigani tena, hana haja ya kuua, keshapata utulivu, hata wake zao hawaruhusiwi kwa sababu ikiwa hawajapata utulivu ndio wanageuka kuwa makatili kutokana na mafunzo wanopewa na hasira za kukosa utulivu.
Nguvu za (kiume)zikitoka hakuna jeshi tena nani anataka kupigana wakati keshapata matulizo, lakini ole wako yakiachiwa machafuko ya nguvu hii ndani na mafunzo ya nje wanayopewa inachobaki balaa tupu, Inaendelea kutufahamisha ishara hii utulivu wake huu wa ndani kuwa wakitulia wawili hawa basi kinachofatia kizazi cha halali.
Ama kuhusu utulivu kwa njia ya nje, ni kupata heshima kwa jamii, kujifunga udugu na familia nyengine na kupendana nao, na huu utulivu wa nje unakukupelekea kuipata hiyo (Taqwa)na Ibadah zako kwa njia ya utulivu bila ya misukosuko yoyote. Na kama unabisha unataka kuipima ishara hii kuwa kweli au uongo, maneno matupu, hakuna chochote, basi watazame wale wanokwenda nje ya ndoa zao wanavo kosa utulivu huu, awe mwanamme au mwanamke mtizame akili zinavomruka, kwanza lazima awe bingwa wa udanganyifu, mateso yanamzidi katika kichwa chake, midamu umechafua njia ya Mwenye-enzi-Mungu na yeye anakuchafulia yako, unakua hamkani fulani keshajua au bado, unapita ukiwaza wakati wote sijui wanajua au hawajui, wameniona au hawajaniona na ukitahamaki utulivu umeondoka, ukisema uongo mmoja lazima ukinge kwa mengine kumi na moja, mwenyewe unajijua muongo, watu wanakujua mdanganyifu, na Mollah wako anakuzidishia maradhi unaanza kufilisika na  mali inaanza kutoweka.
Ama kwa wanawake wao Mollah kawajaalia umbile(Nature)yao utulivu, ndio maana utaona mara chache sana kuona mwanamke kakimbia kizazi chake, kwa sababu yeye karidhia, kakubali utumwa wa Mollah wake, kila wakati yupo anaishi katika utulivu, huwezi kukuta jeshi la wanawake, na yote hayo yamo katika hizo ishara ambazo ni nyingi kuzitaja zote nafasi tulo nayo ni finyu.
"Enyi ndugu zangu msipite mkapeana talaka kwa mambo ya upuuzi na kirahisi, na wala msivunje amri ya Mollah wenu mkatoka kwenye majumba kabla ya Eda zenu kumalizika hicho ni kipimo maalumu alichokuwekeeni Mollah wenu kwa hekima zake" na tambueni hayo makutano yenu sio ya kiwiliwili tu bali pia ni ya Roho, halafu tena mnakutana ki Akili na bila kuyakumbuka mawili haya basi ndoa yenu haiwezi kudumu abadan. Sasa ni mapenzi?endelea-part-3.


No comments:

Post a Comment