Monday, October 8, 2012

UNATAKA KUJUA KWANINI KILA UKITUBU UNAFANYA TENA?-PART-3

Asalaam Aleiykum,

"إِنَّا هَدَيۡنَـٰهُ ٱلسَّبِيلَ إِمَّا شَاكِرً۬ا وَإِمَّا كَفُورًا"
"Hakika sisi tumemuongoza(Tumemuonesha) njia (akitaka)atakua mwenye kushukuru au mwenye kukufuru (kupotea)"
Iliposemwa njia wenye kufahamu mambo wakaona haijambo kidogo tumepata nafuu, kumbe Ibilis (Shetani)hawezi kukaa kwenye nyumba, anaishia njiani tu, ujanja wake wote hawezi kukaa wala kuingia katika nyumba yangu anaishia mlangoni, kumbe naweza kubadilisha njia nikapita pembezoni, sasa hii njia ni ipi alopewa mwanaadamu hata (Ibilis)akawa anaiandama? Hapo inatajwa Akili lakini kwa methali nyengine kabisa.
Njia yenyewe ni hii alopewa mwanaadamu huku kufahamu,(Fahamu)(Hekima)(Busara)ikisha akapewa uhuru akitaka afate au apotee, Hapa ndipo aliposema Ibilis (Shetani)nitawakalia katika njia yako, si ushawafundisha mengi ya uongofu, sasa mie nakwenda kukaa njiani, vipi nitakaa(Quraan-Aaraf-17)
"ثُمَّ لَأَتِيَنَّهُم مِّنۢ بَيۡنِ أَيۡدِہِمۡ وَمِنۡ خَلۡفِهِمۡ وَعَنۡ أَييۡمَـٰنِہِمۡ وَعَن شَمَآٮِٕلِهِمۡ‌ۖ وَلَا تَجِدُ أَكۡثَرَهُمۡ شَـٰكِرِينَ "Ikisha nitawafikia kwa mbele yao na nyuma yao,na kuumeni kwao na kushotoni kwao, wengi katika wao hutawakuta ni wenye kushukuru"
Naomba pita katika aya hii na fahamu nzuri, ukipafahamu hapa itakua rahisi kwako kuwafahamu (Mashetani)na utakua unakaribia kuipata hiyo (Tawbat-Nasuha). Hapa Ibilis anaingia katika (Nature)ya Akili(Brain)ukiitizama Akili utaona ina mambo mawili na (wewe mwenyewe jitizame)Nilipoanza mwanzoni nilitaja aya inayosema"Naapa kwa Akili na yale waandikayo", Ukichunguza utakuta Akili inaandika (Past)yalopita yaani (Memory)kumbukumbu, na (Future)yajayo bado hayajakua, Akili ina safiri katika viwili hivyo future na past ama utafikiri mambo yalopita au yajayo lakini taabu sana kufikiri wakati ulo nao wa hivi sasa, Sasa Ibilis kwa kujua (Nature)ya Akili akasema nitawafikia mbeleni kwao kwenye (Future)watasahau wakati huu wa sasa (Hivi)au nitakwenda nyuma kwao(Memory)na mfano kama vile ukiona (Figure)ya Mwaname au Mwanamke, unaanza kupanga ntampataje, itakuaje, na kama mshafanya maasi zinamiminika zile kumbukumbu ilikua hivi ikawa vile nk, hapo unarejea kwenye (memory)unachambua na ukitahamaki unapanga mikakati vipi au lini mtakutana usha safiri baina ya future na past na hapo shetani anachofanya nikuja kukumbusha tu, sababu  tayari imo kwenye (memory)yako. Anakwenda Shetani huyu kwa mwanamke anamnogoneza (Figure)hiyo lazima uioneshe, bana zaidi nguo yako, halafu anarudi kwa mwanamme kesha ibana kama jana na ukitizama umeumia, hivi ndivo akili inavofanya kazi zake hapo ulipo ukitaka kurudi utotoni kwenye Akili yako ukifunga macho tu unarejea moja kwa moja utotoni, sasa ukigundua hivo basi unaweza kutafautisha, umeshaweza kuweka tafauti na ukigundua tafauti hiyo basi jiulize nani huyu ano kumbuka?huyo alokumbuka sasa hivi, huyo ndio asoweza kuingiwa na shetani, hapo shetani haingii, hiyo ndio nyumba ambayo shetani hafiki anabakia njiani kwenye akili, na hizo ndio hizo kumbukumbu (memory)nilizozitaja na mpaka hapa utakua ushaanza kujua kumbe wewe na akili ni vitu viwili tafauti, na vile vile ushagundua kumbe inayosahaulishwa ni akili yangu, kumbe nikiwa (hadhir)siwezi kutenda kosa.
Akaendelea kusema Ibilis nitawakalia kuumeni kwao na kushotoni, Naam aya imetaja wewe una mbegu mbili zilochanganyika, una jinsia mbili (Mke na Mume)katika umbile lako ndio maana mara nyengine unakua mpole na maridhia kama mwanamke na mara nyengine unakua mkali hushikiki kama vile mwanamme. Wanasayansi wameita (Akili ya upande wa kushoto na upande wa kulia)Alipogundua Ibilis utendaji wake wa kazi ndio akasema nitawakalia katika jinsia zao zote mbili, kuumeni kwo na kushotoni kwao, kwani viwili hivi kimoja kikipinga basi hakuna jambo linalofanyika, ndio maana saa nyengine unasema roho yangu nzito, Ibilis kakugundua inakua vigumu lazima azipate pande zote mbili. Sasa kabla yakutaja nini cha kufanya kuepuka hali hii ili usikubali tena upumbavu huu wakuteseka kwa madhanbi, basi tutupie macho kauli hii niloitaja kutoka kwenye aya za mwanzoni kuhusu kuona na kusikia.Endelea-4

No comments:

Post a Comment