Asalaam Aleiykum,
Jee unataka kujua vipi umezongwa na dunia? kwanini unachukia mambo ya darsa?, basi jitizame namna gani unavokimbia mawaidha na ukumbusho wa hicho unachokiamini na kukitegemea hata yakikujia mafundisho kama haya ya Tawhid ya kumjua Mollah wako, basi unakua kusoma kwako ni kwa kupita pita tu na wala si yenye kuzama ndani ya moyo mwako. Imekua hasara kubwa kwako wewe mwanaadamu kuikosa faida itakayo kukusaidia hapa Ulimwenguni na huko akhera uendako, kwa kuwa na sisi wajibu wetu kuufikisha ujumbe huu au dawa hii ya Roho basi tutaendelea kukupa na wewe una hiari yako kumeza(Kufikiri)au kutupa(kupuuza), Tunafanya hivi kama wafanyavo madaktari wanokupa dawa zako za mwili, ulipokua kijana ulikua mara chache sana kwenda kwa Doctor, lakini sasa Umuri usha sogea, uzee unapiga hodi, kifo hakipo mbali, sasa unahitaji vidonge huendi lazima upewe cha pressure au cha sukari n.k, hivi vya hospital unakula haraka haraka lakini hichi cha Roho hutaki kukiona au kukisikia unaona mambo gani, mara hii kasema nini, hebu tizama anatisha safari hii, unasahau hichi cha Roho ndio Muhimu sana kadir ya Umri unavo kwenda mbele.
Leo hii tunaendelea na somo letu la Tawhid ambalo pengine ulikua huna ujuzi nalo au umeghafilika, basi soma kwa utulivu uchukue faida hii kubwa iwe ufunuo kwako na umfahamishe mwenzio unaye mtakia kheri ili naye apate faida hii adhimu, na wala usijali inatoka kwa nani, wewe chukua faida yake na kuanzia leo utakua mtu mwengine kabisa wakati unapo kwenda kulala, utakua hujitupi tu kipuuzi, utakwenda kulala ukiwa na fahamu nzuri ya kiroho.
Vipi unashuhudiwa na Quraan? na ina umuhimu gani kushuhudiwa huku?na nini kinatokea wakati inapopatikana shahada yenyewe?na Kwanini hassa ikawa Alfajiri?(Qur'aan-Israa-78)
"أَقِمِ ٱلصَّلَوٰةَ لِدُلُوكِ ٱلشَّمۡسِ إِلَىٰ غَسَقِ ٱلَّيۡلِ وَقُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِۖ إِنَّ قُرۡءَانَ ٱلۡفَجۡرِ كَانَ مَشۡہُودً۬ا"
"Simamisha Sala, Jua linapopinduka, Mpaka(liingiapo)giza la usiku,Na Quraan ya Alfajiri, hakika Quraan ya Alfajiri Inashuhudiwa"
Inatosha Mwanaadamu aya hii moja kukufunga na Mollah wako ukawa huna haja na kitu chengine chochote, Kwanini ikawa hivyo?, imekua hivyo kama wewe ni mcha Mungu basi aya hii inakua Rafiki yako kipenzi, inakua ufungua wako, inakua ukumbusho wako, sababu kubwa ni kule kukupa ukamilifu wa Ibada.
"Ewe mwanaadamu simamisha Sala pale jua linapoanguka limeshauvuka utosi"Sasa sahau yote uanze safari ya kurejea nyumbani, Wapi? kwa uchambuzi zaidi itabidi kwanza tuhame kwenye aya hii ili tukachume kwenye bustani kubwa ya Quraan ili ipate kutupa maana halisi ya kushuhudiwa kwa kusoma Quraan nyakati za Alfajiri. Endelea Part-2
No comments:
Post a Comment