Monday, October 8, 2012

UNATAKA KUJUA KWANINI KILA UKITUBU UNAFANYA TENA?-PART-4

Asalaam Aleiykum,

Napenda niongeze hili la kuona na kusikia ili nipate kuamsha kitu ndani ya fahamu yako, yatizame mambo haya mawili vizuri na utagundua vipi hiyo nyumba yako niloitaja ya fahamu inavo tawaliwa na mambo haya mawili, jitizame ukitizama mchezo kwenye TV au senema unasahau kila kitu chengine, au ukisikiliza muziki chochote kengine hakiingi na hiyo ndio fahamu ambayo ni zawadi na neema alotupa Mollah wetu. Nini dhumuni langu kukutajia kuona na kusikia, nia yangu ni kukufahamisha vipi fahamu inavotekwa na mambo mawili haya, na kwa mfano huo huo basi na maasi pia yanaiteka akili yako kama inavofanya tv na muziki, na inakua rahisi Ibilis kufanya kazi zake, na hiyo ndio maana ya kukukalia katika  hiyo njia.
Sasa ufanye nini na kila njia imeshindikana, napenda uelewe Dini zote za haki zimesisitiza au kuja na jawabu na huipati jawabu isipokua katika neno la (Dhikr)kukumbuka, Nini kukumbuka?ni (Awareness)au(Dhahir)au(Alertness)ndio ukaambiwa simamisha Sala,kumbuka, kufunga kukumbuka, kukaa na udhu kukumbuka na mengi mengineyo, nimeitaja hiyo fahamu na kutilia mkazo kwa kuwa ukiteleza kidogo ukawa hukumbuki hapo ndipo katika (gap) hiyo (Shetani)au wewe mwenyewe unapotenda kosa.
Sasa ufanye nini?jichunguze lipi kosa lako kubwa linalo kutesa huwezi kuliacha, tuseme mfano uzinifu (si huwezi kuacha)basi fanya kitu kimoja tu, vengine ndio vishashindwa, sasa ukiwa unakwenda katika hayo madhanbi (maasi)basi kumbuka kila tendo, kama sasa nakwenda, nimeshafika, jaribu usikumbuke chochote kumbuka ndio nakwenda kuzini, nimeshafika, nimekaa kitu kadhaa kinafanyika kumbuka kuanzia mwanzo mpaka mwisho usifikiri chengine chochote, au unakwenda kuiba kumbuka mwanzo mpaka mwisho, au unapokea rushwa kumbuka mwanzo mpaka mwisho wa hili tendo, unasengenya mtu endelea kumsengenya lakini kumbuka tu namsengenya fulani mwanzo mpaka mwisho, kila kile unachoona kigumu kuacha basi kifanye huku unakikumbuka mwanzo mpaka mwisho, hee hata ulevi, Naam mpaka pombe tokea unamimina mpaka unakunywa wewe kumbuka mpaka inaanza kukulevya wewe endelea kukumbuka tu na ukifanya kwa muda wa mara saba lakini kwa uyakinifu sio unazungumza halafu unakumbuka hapo itakua usha haribu, inatakiwa isipatikane (Gap)basi ikiwa utaweza kutenda tena mara ya nane hali yakua unakumbuka mwanzo mpaka mwisho basi wewe huna dawa,(Elewa booking yako ya motoni ishakua confirm)huwezekani tena.
Ikiwa mbinu hii imefanya kazi kwa watu wengi kwanini isifanye kazi kwako, Sasa nini kinatokezea hapo ukifanya mara mbili tatu, (Siri)yake unakua (Full-Alert)na hatendi mja kosa akiwa yupo hadhir, mwizi haingii katika nyumba wenyewe wakiwemo tena wamacho, itakufungukia fahamu kuwa hilo tendo lako ni la kipumbavu na kipuuzi, na halina maana, utaanza kulichukia moja kwa moja hakuna mwanaadamu mwenye kupenda dhiki, na hapo utaliacha mara moja na hiyo ndio (Tawbat-Nasuha)ndio maana ukaambiwa kwenye Quraan:Ankaboot.
"إِنَّ ٱلصَّلَوٰةَ تَنۡهَىٰ عَنِ ٱلۡفَحۡشَآءِ وَٱلۡمُنكَرِ‌ۗ وَلَذِكۡرُ ٱللَّهِ أَڪۡبَرُ‌ۗ "
"Hakika sala ni yenye kukuepusha na madhanbi(makubwa)na mambo ya munkar, na umkumbuke Mollah wako aliye Mkubwa"
Ukimkumbuka Mollah wako nyakati zote huwezi kutenda kosa na hiyo ndio maana ya (awareness)ndio maana ya kusimamisha sala, sio ile sala unayosimama huku unakumbuka biashara, au unakumbuka miadi, au harusi ya leo itakuaje. Sala ilokusudiwa hapa ni kuendelea bila kusita kumkumbuka Mollah wako, na hekima hapa ukimkumbuka Mollah wako inakuepusha na maasi, na ukikumbuka kosa lako vile vile linakurejesha kwa Mollah wako, hiyo ndio maana ya kujuta,na huko kujuta vile vile kuna kurejesha kwa Mollah wako (Njia moja)ilonyooka ukipita kokote unatokezea hapo hapo kwa Mollah wako nayo ni hiyo"ٱهۡدِنَا ٱلصِّرَٲطَ ٱلۡمُسۡتَقِيمَ"Na ukifika katika hiyo njia basi wewe unakua sawa sawa na Walii au Mcha Mungu, tafauti yenu ni Mcha Mungu anagonga mlango, na wewe umesimama hugongi hiyo ndio tafauti yenu, sasa anza na wewe kugonga hujui nani atafunguliwa mwanzo.Mwisho namalizia kwa kukwambia ichunguze sana tabia yako ina kawaida ya kurejea rejea mambo ndio maana kila ukitubu unafanya tena. Mollah wetu tujaalie nguvu ili tuweze kuipata toba ya moja kwa moja(Tawbat-nasuha)Mollah wangu ndie ajuae zaidi.
Abdulla Baja

No comments:

Post a Comment