Asalaam Aleiykum,
Maudhui yetu ya leo inagusa ndoa zetu za kiislam kwa wakati huu tunaoenda nao, kumekuweko na mlipuko wa (Talaka)mpaka imefikia jambo hili la ndoa ya kiislam kufanywa kitu cha upuuzi tu na ambacho hakina thamani, labda maudhui hii italeta mwanga japo kidogo ili watakao faidika na darsa hii watapata bahati za kuzithamini na kuzitunza ndoa zao kama walivofanya wazee wetu.
Naam, ukitizama maajabu ya ndoa ya kiislam utaona mpango alotupangia Mollah wetu una manufaa makubwa kwetu sisi waumin wa dini ya kiislam, Japokua kuna baadhi ya watu wenye imani nyengine wanatubeza na kutucheka na kutushangaa, Lakini mwenendo wetu una kheri katika mambo mengi ukiyatia katika Akili.
Tafauti yetu kubwa ya Mwanzo sisi (Waislam)hatu(Falling in love)kwanza tunaoana(1)halafu tunazoeana(2)tena tunakuwa marafiki(3)ikisha tunapendana(4)mwisho wake tunaoneana huruma(5)hapo tena tunakamilisha (Circle)nzima ya ndoa, unaweza kuita upendavyo, Mke na Mume, Chanda na Pete au hata (Soul-mate). Sababu gani zino tufanya tufunge ndoa?Quraan Rumi aya 21
"وَمِنۡ ءَايَـٰتِهِۦۤ أَنۡ خَلَقَ لَكُم مِّنۡ أَنفُسِكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا لِّتَسۡكُنُوٓاْ إِلَيۡهَا وَجَعَلَ بَيۡنَڪُم مَّوَدَّةً۬ وَرَحۡمَةًۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ"
Na katika ishara zake, Amekuumbieni wake zenu katika(kutokana na) jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, Akayajaalia mapenzi na huruma baina yenu, Bila ya shaka katika(hayo)zimo ishara kwa watu wanaofikiri.
Yatosha maneno haya ya Mollah wetu katika aya hii moja kukichambua chuo hichi cha ndoa katika maisha ya Mume na Mke mwanzo mpaka mwisho. Mwanzo kabisa aya imeanza katika ishara zake amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu, hapakutajwa wanawake, ingetajwa wanawake jambo hili la ndoa lingekua(accident)linatokea tu bila ya kupangwa, mnakutana kwenye disco, taarab na kwengineko mnafunga ndoa, lakini imeanza kwa ishara, halafu ikafatia wake zenu ikaja kusita katika jinsi zenu, sasa kwanini ikasemwa ishara?na kwanini ikatajwa wake zenu? na vipi imekua kutokana na jinsi zetu?(Japokua utapata jawabu mwisho wa Mada)lakini wacha nikuchukue katika safari hii ili upate ufahamu mwengine kabisa kuhusiana na huyo mwenzio unaye ishi naye, huyo unomwita mama watoto wangu, huyo unomwita mimi na yeye kama chanda na pete, ukasema hapa mimi nimekutana na (soul-mate) wangu. Anasema Mwenye-enzi-Mungu "katika ishara zake" jee wewe umeshawahi kuingia katika kuzitizama hizo ishara, Ushawahi kujiuliza kwanini ikawa huyu? jee haya makutano yetu ni bahati au jambo hili limepangwa kabla ya kutokea?umeshawahi kusafiri kiroho ukapata kumjua mwenzio unaye kaa naye? Amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mpate utulivu kwao, sasa ingia katika hizo ishara uzipate japo kwa uchache ili upate kufahamu mambo yanavokua-endelea-Part-2
No comments:
Post a Comment