Monday, October 15, 2012

MAISHA YA MUME NA MKE MAPENZI MAJAALIWA-PART-3

Asalaam Aleiykum,

Kumbuka tumo katika kuichambua aya moja na sasa tunaingia katika hayo mapenzi yalotajwa katika hiyo aya.
Mapenzi ni Bustani maalum ambayo wote tunapigana tuifikie, Bustani hii ipo kwenye bonde la (Moyo)kuna watu wakiigundua Bustani hii basi wao huchupa moja kwa moja hawasubiri chochote, hao ndio tunawaita wame (Fall in love)lakini kuna wengine wanatumia utaratibu ulopangwa na Mollah wao wa kushuka taratibu kama (Nilivotaja kwenye part 1). Natoa mfano huu ili kujulisha kiini cha mapenzi mwanzo wake yanatokea kwenye kichwa halafu ndio yanashukia moyoni hapo inapatikana salama, Lakini ole wako yakishuka moja kwa moja moyoni mbeleni kuna hatari.
Amesema Mwenye-enzi-Mungu,"Akajaalia Mapenzi na Rehma"limetumika neno la jaala kuonesha dalili za kuwa jambo hili lina athari zile zile za kama hizi," Tukajaalia kuona na kusikia"ukilala kuona na kusikia kunatoweka"tukajaalia usiku kama guo"unaingia na kutoka na mchana hali kadhalika"na ukitizama aya nyingi ziloanza na neno hili zina dasturi za kuja na kutoweka, mfano kama vile zina mzunguko fulani, basi ukisha elewa hivyo ujue na mapenzi ni hali hiyo hiyo hayadumu moja kwa moja kama bendera ya chama, yanakuja na kuondoka, kama ilivokua huwezi kukaa masaa ishirini na nne umehamaki na pia huwezi kukaa masaa kama hayo unapenda, kuna wakati unalala ya wapi mapenzi yako.
Sasa tuingie katika bahari ya mapenzi ili tuzitizame ndoa zetu inakuaje. Wengine wanaita (Falling in love)lakini waislam Mollah wetu hatuachi tuanguke, ila katuwekea mpango tunateremka taratibu kwa kutumia ngazi yake ya Rehma nayo ndio hii (Ndoa)."Ewe Adam .a.s kaa peponi pamoja na mkeo"(Aaraf-19), ndoa ya mwanzo imefungwa peponi, na mpaka leo zinaendelea kufungwa huko huko mbinguni, Hamkutani tu kwa bahati mbaya isipokua kwa matakwa ya Mwenye-enzi-Mungu, ndio maana ukaona tukio hili likawa ni la furaha, nini kinachokutana hapo ni Roho mbili zilofanya safari tafauti kutokea kwa Mollah wake mpaka leo ujanani zinakuja kuungana, haiwezekani tukio hili likawa kwa bahati, Kwa hiyo ndoa ni makutano ya Roho mbili na zikisha kutana kidogo kidogo, mguu kwa mguu huku zimeshikana mikono zinaanza kushuka kwenye Bonde la mapenzi, kwa kuwa Roho mbili hizi zimekutana katika mji wa kigeni, watu wawili hawa lazima zitokee tafauti,mabishano yatakuwepo,ngazi refu ya bondeni kunatakiwa ustahamilivu,masikilizano,subira ili mmoja wenu asije akadondoka au ukaja msukuma mwenzio kwa maudhi na kero, msije mkapita kugonmbana mbele za watu, msitoe siri zenu, mkiwa na tabia nzuri za kuridhiana wawili nyie basi Mwenye-enzi-Mungu ndio hukufunulia hilo pazia la mapenzi na hakuna raha inayopata Roho kama kuondoshwa pazia ukawa unapendana na mkeo au mumeo, nini kinatokea pazia likiondoshwa?endelea part-4

No comments:

Post a Comment