Monday, October 1, 2012

VIPI UNASHUHUDIWA KWA QURAAN YA ALFAJIRI-PART-2

Asalaam Aleiykum,

Imekufikia habari, au ushawahi kuuliza au kujiuliza mtu anae kunywa mvinyo(Ulevi)au mcheza taarab usiku kucha au Dance au mkesha wa chakacha usiku kucha  kwanini wakiamka wanakua wamechoka, au vichwa vina wauma?, Na Umemuuliza Mcha Mungu au anaye simamisha Sala mbona wao wakiamka wako(Fresh)mbichi, nguvu mpya, tayari kwa siku ianze apate kushughulika na maisha?jee unayo majawabu ya maswali haya, na kama huna safiri na mimi ili nipate kukupa siri ya mambo yanavokua upate kuwa muangalifu kuanzia leo hata huko kulala kwako kuwe Ibada, upate kujiepusha na mambo fulani fulani wakati unapo kwenda kulala utakua daima na wewe unaamka (fresh)msafi huna doa na unashuhudiwa kwa matendo yako yote, hapana pengine pakuuliza isipokua Quraan-sura ya Zumar aya ya 42.
"ٱللَّهُ يَتَوَفَّى ٱلۡأَنفُسَ حِينَ مَوۡتِهَا وَٱلَّتِى لَمۡ تَمُتۡ فِى مَنَامِهَا‌ۖ فَيُمۡسِكُ ٱلَّتِى قَضَىٰ عَلَيۡہَا ٱلۡمَوۡتَ وَيُرۡسِلُ ٱلۡأُخۡرَىٰٓ إِلَىٰٓ أَجَلٍ۬ مُّسَمًّى‌ۚ إِنَّ فِى ذَٲلِكَ لَأَيَـٰتٍ۬ لِّقَوۡمٍ۬ يَتَفَكَّرُونَ "
"Mwenye-enzi-Mungu huzipokea Roho wakati wa Mauti, Na zile zisizokufa pia(Mwenye-enzi-Mungu) huzitakabadhi katika (usingizi)kulala kwake, Na huzizuia zile zilo hukumiwa kufa, huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa(pangiwa)Hakika katika hayo mna mazingatio kwa watu wanao fikiri"
Siku zote natilia mkazo tuwe waja wenye kufikiri, tunahimizwa tufikiri na leo hapa hebu tulitupie macho tukio hili la usingizi tulifikiri kwa pamoja, Utagundua katika umri wako kila usiku wewe unarejea nyumbani kwa Mollah wako, hujawahi kuwa mbali na Mollah wako, kuna nyakati za usiku unaondoka katika huo mwili unaoringia unarejea kule ulipotokea, unakwenda kuchukua nguvu mpya, Unarejea kupewa Rehma mpya, unarejea tena Ulimwenguni ukiwa msafi, kumbuka tukio hili unalitenda kila pale unapokwenda kulala lazima urejee, Ukiwa Umelewa au mzima, ukiwa unaumwa mgonjwa au una afya yako marejeo ni lazima, ndio maana utaona madaktari wanahimiza mgonjwa lazima apumzike alale apate kwenda kwa Mollah wake kutibiwa, huko ndiko kunako toka tiba zote, Sasa nini habari yako wewe unarejea kila siku Umelewa, au umedhulumu watu, au umefitini watu au umevuta (Mihadarati)au umezini unarejea kwa Mollah wako na machafu haya, jiangalie mwenyewe kiafya na kia Akili una hali gani?.
"Enyi ndugu zangu tujihadhari sana kila siku kurejea tukiwa na hali kama hizo tunarejea kwa Mollah wetu na Mzigo wa madhanbi"shukuru sana unarejea kwa Mollah wako hali ya kuwa huna fahamu, lau ungepaona pahala unapowekwa kwenye hayo masaa yako manne au sita unayolala basi usingetenda dhanbi tena.Laiti ungetambua kiasi gani unakera kwenye Ufalme wa Mwenye-enzi-Mungu basi ungekaa mbali na maovu. 
Sasa nini kinatokea ikiwa  usiku umerejea kwa Mollah wako na Moyo wa Salama, Umerejea na huku umefunikwa na Taqwa, uko msafi, basi dalili zake ni zile za  wewe pale unapoamka uko msafi, Roho yako ina Tohara tupu, mweupe huna doa, Roho haijafikwa na madhila yoyote, Akili nyeupe haijaingia uongo wala mambo ya kidunia hujayaona, wala matamanio hayajafika moyoni, wala picha za maasi hujafungua, bado hujenda kwenye Face book, hujafungua Computer na kuona matangazo yoyote, hujenda barazani au kuanza kuzungumza chochote, hapo ndipo unapoambiwa kitu cha mwanzo Roho imetokea kwa Mollah wako kinachofatia soma Quraan,(Ndio maana school zikawa asubuhi ingekua usiku nani angefahamu)kitu cha mwanzo yajaze maneno yetu Rohoni ungali safi, kabla hazijaingia biashara kichwani na mambo mengine ya kipuuzi, ukifanya hivo inakua maneno ya mwanzo yanaingia kitabu cha Mwenye-enzi-Mungu na ukiwa na Tabia hii basi mpaka maisha yako yatabadilika utaishi kwa mwenendo wa Quraan, na hapo ndipo (Malaika)watashuhudia matendo yako, Quraan ndio inakua dira yako, mpaka wanaadamu wataanza kukushuhudia yanakua Maisha yako toka ukiamka una shika Ibada mpaka kulala kwako wewe unakuwa umo ndani ya Ibada na hapo tena unaingia kwenye fungu la wale walotajwa katika sura ya Saffat aya ya 3.
"فَٱلتَّـٰلِيَـٰتِ ذِكۡرًا"
"(Na)Kwa wale wasomao ukumbusho(mawaidha)ya (Mollah)wao"
Kila alfajiri wewe umepata (ukumbusho)basi kutwa nzima unakua  ni mwenye kukumbuka na ukikumbuka unasimamisha sala na siku nzima unakua tajiri mwenye kumkumbuka Mollah wako, na ukiendelea na kawaida hii kwa muda wa miezi mitatu mfululizo Mollah wako hukuteremshia Nuru mpaka wanaadamu wenzio watakua wanaanza kuiona, lakini wale wenye macho.
Na huko ndiko kushuhudiwa kwenyewe na yoyote mwenye kutaka kuhifadhi Quraan au hata masomo mengine ajaribu kuamka nyakati hizi za Alfajiri na ataona mafanikio yake. Namuomba Mollah atujaalie tuwe wenye kushuhudiwa kwa matendo haya ya kheri. atujaalie tuishi kwa mujibu wa mawaidha yake na uongofu wake.Amin
Abdulla Baja




No comments:

Post a Comment