Saturday, February 23, 2013

MACHUNGU YA TALAKA-PART-1

Asalaam Aleiykum,

Imekujia habari iumizayo Roho, Unalijua tendo lenye kuangamiza afya ya Mwanaadamu, basi kama huna habari hiyo sasa tega macho upate kufahamu vipi Talaka inavo kuangamiza baina ya muombaji na mtoaji wa hii tunayoita Talaka, Talaka inakuja kwa aina mbili ama kwa njia ya karatasi kama uthibitisho au maneno kuwa tamko, na haya yote yanakwenda (Deep)kwa mtoaji na anaepokea, kama zilivyo nguo au bendera zinavokwenda (Deep)kufahamisha huyu Mwanamme na huyu Mwanamke au bendera hii ya nchi fulani na ile ya nchi fulani.
Sasa hatuwezi kuizungumza Talaka ikiwa kwanza hatujaizungumza Ndoa, Nini Ndoa?(Harusi)Ndoa ni mvutano wa Roho mbili ziloamrishwa na Mollah wao kujiunga kisheria na kuishi katika ada ya maamrisho kama Mke na Mume, Wapi unatokea mvutano huu, Mvutano huu unapatikana pale kwenye tafauti ya kijinsia yaani baina ya mwanamke na mwaname, ili tufahamu kwa njia ya mvutano basi acha niipe jina mwanamme nimwite(Positive)na mwanamke namuita(Nagative) ndio katika aya 14 ya sura ya Imran ambayo nimeizungumza kwa urefu katika mada zilopita ilitaja hivi"زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٲتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ"
"Watu wametiwa Upendo wa kupenda wanawake" na mambo mengine kama inavoendelea aya kueleza, imelazimishwa nafsi katika huo mvuto nilioutaja, wapi linatokea tukio hili, linatokea katika hii ita (Eyes)au (Magnet-field ya Mind)ya mapenzi au kwa jina lengine huu uwanja wa (Hubu-Haba)Ikisha tena mvutano huu unapambwa kwa maua ya shauku na miasumin ya matamanio, hapo tena huanza kutaarishwa njia za halali za kufunga ndoa, ikiwa ndoa hii safi ilobarikiwa na Mwenye-enzi-Mungu basi pale pale inapofungwa Mollah huteremsha mambo yote mawili (Mapenzi na Rehma zake)kwa kuwa tayari wawili nyie mpo kwenye uwanja wa (Hubu-Haba). Na kama kuna mushkeli umepita basi hapo (Mollah)Huteremsha (Rehma) akawa anawasubiri waja wake kama watakua safi katika Muungano huu ili awakamilishie na hiyo sehemu ya pili nayo ni hayo mapenzi.
Sasa kivumbi kinaanzia wapi? kinaanza mwanzo kabisa kwa ushaulivu wa wana ndoa hawa kama harusi ni Muungano na maana ya muungano (The Others to disappear)Mume anakuja na Mama yake kwapani, na Mke anakuja na Mashoga zake kichwani, inaanza  ndoa hii na kindumbwe ndumbwe tokea mwanzoni, Ndoa yenyewe ni mkutano wa (Nagative na Positive)ndio maana mkutano huu hayeshi mabishano na magonvi, sikuwa wanachukiana wawili hawa lakini wamekutana viumbe hawa wakiwa tafauti na lazima utegemee kupatikana mikwaruzano ndio maana ya (Positive na Nagative) na wange gundua wawili hawa kama wao wamo kwenye majaribio,  na huo upendo upo kwenye
hiyo (Mind-Akili)basi wangetunza na kusubiri upendo huo kuanguka kwenye Moyo, hapo wangepata zawadi kutoka kwa Mollah wao nao ni hayo (Mapenzi).Mollah wako hupeleka mapenzi kwenye Moyo ikapatikana hiyo(Communion) au (Falling in Love)au kwa maana nyengine kuanguka kwenye bonde la Moyo wa Mapenzi.
Ukipata japo tone moja la mapenzi husahau tena raha hizo, au ladha hiyo na ndio maana wazungu wakatoa usemi huu(In memory love live forever)Inaanzia hali hiyo kwenye akili, ikisha inadondoka moyoni na hapa moyoni kuna njia mbili za ku(Test)mapenzi hayo au kuya(Experience)moja ni ile ya mwanamke, yeye ana bahati kwa kuwa ni (Nagative)penzi linapokewa moja kwa moja, au linaanguka haraka moyoni na anakuwa wazi hana hofu kama watu watamjua au watamzungumza, kwa Mwanamme kwa kuwa yeye nini (Positive)anafunga moyo anakua anaonesha kwa hisia na matendo yake yanaonekana kama vile kwa njia za kutoa zawadi na kadhalika, lakini kimsingi yote ni mapenzi, ila wanaume wanaogopa kujulikana kama wanapenda, wana wasiwasi watu watasemaje(Mbona kawezekana,kadhibitiwa), itakua vipi nk,
Sasa wawili hawa wanaishi ndani ya hili penzi kwa siri na dhahiri wakiwa na furaha, vicheko, na kubarikiwa watoto, wakashibana kwa mambo yao kwa upenzi na undugu, Sasa tizama nini kinatokea mmoja wapo akaamua kudai au kutoa Talaka.
Ukitaka kujua mashaka na madhila yanotokea katika hiyo Talaka basi Endelea-Part-2

MACHUNGU YA TALAKA-PART-2

Asalaam Aleiykum

Binaadamu katika kadhia hii ya Talaka anakutana na fimbo mbili, Anachapwa viboko viwili pasi mwenyewe kujielewa kutokana na makosa ya kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenye-enzi-Mungu, Anasema Mwenye-enzi-Mungu katika sura ya (Talaq)aya ya kwanza kabisa anachanganywa na Bwana Mtume s.a.w,"
"ـٰٓأَيُّہَا ٱلنَّبِىُّ إِذَا طَلَّقۡتُمُ ٱلنِّسَآءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِہِنَّ وَأَحۡصُواْ ٱلۡعِدَّةَ‌ۖ وَٱتَّقُواْ ٱللَّهَ رَبَّڪُمۡ‌ۖ لَا تُخۡرِجُوهُنَّ مِنۢ بُيُوتِهِنَّ وَلَا يَخۡرُجۡنَ إِلَّآ أَن يَأۡتِينَ بِفَـٰحِشَةٍ۬ مُّبَيِّنَةٍ۬‌ۚ وَتِلۡكَ حُدُودُ ٱللَّهِ‌ۚ وَمَن يَتَعَدَّ حُدُودَ ٱللَّهِ فَقَدۡ ظَلَمَ نَفۡسَهُ ۥ‌ۚ لَا تَدۡرِى لَعَلَّ ٱللَّهَ يُحۡدِثُ بَعۡدَ ذَٲلِكَ أَمۡرً۬ا"
"Ewe Nabii, Mtakapo wapa talaka wanawake(wake zenu)basi wapeni talaka katika Eda zao, Na fanyeni hisabu za Eda, Mcheni Mwenye-enzi-Mungu, Mollah wenu mlezi, Msiwatoe(Wanawake)katika nyumba zao, wala (Wao)wasitoke wenyewe, ila(Kama)watafanya jambo la uchafu ulio wazi(Kama vile mtu kafumaniwa kitandani nk)Hivyo ndiyo mipaka ya Mwenye-enzi-Mungu, msiivuke, na mwenye kuivuka mipaka ya Mwenye-enzi-Mungu, basi amejidhulumu nafsi yake, (Huwezi kujua)Hujui, labda Mwenye-enzi-Mungu ataleta jambo jengine baada ya haya."
Kuna makosa matatu yanatokea katika kupeana Talaka kwa karne hii tulonayo na hilo ndio linalo tupelekea kupata hizo fimbo za Mollah wetu. Amri ya kwanza kabisa ambayo hatuitekelezi(1)Hakuna anojali kabisa habari hii ya eda, si anosali au Sheikh au Ustaadh, jambo la mwanzo wanakimbilia katamka, na ukitamka umeumia, ndio kutamka kupo, lakini jee mlikaa mkahesabu miezi mitatu?.
Kosa la Pili(2)Msiwatoe au wao kutoka katika majumba yao, jee nyinyi mlikaa miezi mitatu mfululizo katika nyumba yenu ya ndoa?
Na kosa la tatu(3)Na hili ndio la kusikitisha zaidi linapita tendo la ndoa eti na huku eda inaendelea, hapo tena mtu anakua hajijui anapotoka na anapokwenda, hivi ndivo tulivofikia. Na hapa UK tunaachwa wanaume (Kama alivosema Mollah nyumba zao)basi hapa tunakiona cha-mtemakuni, unaweza kushtukia umefungiwa fuko lako la rambo(Black-bin-Bag)halafu linarushwa kutokea ghorofa ya kwanza, na ndani pengine umetiliwa na viatu vyako, fuko lile likifika chini linachanika kwa aibu unafanya haraka kuokota ili majirani wasione ikisha huyo unakimbilia kwa rafiki, hiyo ndio hali tulofikia sisi tunojiita waumini.
Basi msivuke mipaka ya Mwenye-enzi-Mungu, hapo sisi mipaka yote tunavuka na tuko tayari kwa chochote, tumeadhimia kumtii bwana wetu Ibilis hatusikii wala kuona, na huku tunaambiwa yoyote yule atokwenda kinyume na hayo basi amejidhulumu nafsi yake. Kwanini anajidhulumu nafsi? Sababu Mollah kakupeni Hekima zake, anakujueni viumbe vyake, na sababu ni zile zile nilizo zitaja mwanzoni, nyie mna (Magnet)menasana baina yenu na mkitaka kuinasua kwa nguvu basi mtajidhulumu, basi kwa hiyo kaeni kwanza miezi mitatu, huku mnapishana bila ya kufanya tendo lolote, huyu anapita huku kanga zinamuanguka na yule anapita kule anapiga ujicho, ikiwa kweli nyie mtafikisha miezi mitatu hamjapatana au hamaki hazijaondoka au hamjavamiana basi hapo rejeaneni kwa wema au tokaneni kwa wema. Nyinyi sasa mshaweza kuachana, kweli itakua Ibilis kamudu kukaa na nyinyi kwa miezi mitatu, kavunja kazi zake zote ili kukushughulikieni nyinyi tu, lakini pia eleweni Ibilis hatupi muda wote huo kukusubirini nyinyi, ndio maana mkapewa miezi mitatu, Haiwezekani mkakaa miezi yote hiyo mna hasira, hiyo ni (Cooling-off-Period)ilotoka kwa Mollah wenu. Eda ina hekima zake msiifanye Talaka ya kiislamu kuwa rahisi hata kupita bei ya (Njugu)watu wengi wanatizama ugonvi kuliko zile sheria za Mwenye-enzi-Mungu wanojinasib wanazifata, sasa ikiwa mshakaa hiyo miezi mitatu mkafata amri ya Mwenye-enzi-Mungu, basi tafuteni mashahidi wawili wa kuaminika na muwaeleze sisi tunarejeana kwa wema au tunaachana kwa wema na hapo Mwenye-enzi-Mungu anakufanyia urahisi njia ya (Move-on)kutokea, kama alivyoitaja kwenye aya ya pili ya sura hiyo hiyo.
Sasa kama unaenda kinyume cha hayo nini kinatokezea, vipi unayapata machungu na hizo bakora? kutokana na talaka zetu za siku hizi. Endelea-Part-3


MACHUNGU YA TALAKA-PART-3

Asalaam Aleiykum,

Ilivokua ushapinga amri za Mollah wako muumba, na meachana kama wanyama, sasa nenda kakutane na kifo cha (Mapenzi)Nenda ukapate mongonyoko wa ardhi uliyoibeba. Yanatokea vipi Machungu haya? Wanatwambia Madaktari(Doctors)na wakufunzi wengine wa mambo ya taaluma ya akili kwamba asilimia 95% ya maradhi ya mwanaadamu yana sababishwa na akili(Mind)Naam kama utaamini umerogwa hata uambiwe uongo wewe hukubali, ikiwa utaamini kwenye nyumba kuna shetani basi utaanza kuona mpaka mabuibui yanapita kizani, Sasa nini shughuli ya hii Akili(Mind) iwe jambo limetokea kweli, jambo lenyewe liwe lile la kutengana na mwenzio, pengine mepata kizazi mna vitoto pamoja au kuna kumbukumbu za mambo mazuri mlokua mnafanya pamoja, pengine iwe furaha au visa vya kufurahisha au labda matunzo alokua anakupa na wewe ukimpa vyote hivyo vimesaki Akilini na leo wawili nyie mnaamua kutengana(Mnaibandua ile Magnet)kwa nguvu, toka na mwanamke au mwanamme huyo anatoka nini hapo kinafatia.
Kinachofatia hapo ni fimbo ya mwanzo ya Mwenye-enzi-Mungu kwa kuwa mevuka mipaka yake, hamkufata amri zake jambo la mwanzo anafunga Mlango wa mapenzi, na ukifungwa mlango wa mapenzi (Automatic)unafunguka mlango wa chuki na hii chuki ni bakora ya pili, Nini chuki? chuki ni mbolea ya maradhi yenye kurutubisha Akili(Mind). Na akili haipendi kifo cha haraka, inapenda kuteseka na kufa kidogo kidogo, Na hapo ndipo Machungu yanapoanza, na machungu yakianza yanafatiwa na visa, Utaliona Dume linamfata fata mwanamke nyuma nyuma bure ili ajue aendako, sasa wewe ushaamua kumuacha hizi shughuli zinakufikia nini, na hutokea vita vikubwa ikiwa atamkuta anazungumza na mwanamme mwengine, wanaweza kuchapana ngumi sokoni kutokana na hamaki zinazo patikana hapo.
Na mwanamke hali kadhalika analia kwa mashoga zake, anaungulika kwa tabu na mashaka makubwa yanayompata, halafu hatua nyengine inayofatia(Anakaa kati Ibilis)kuamrisha sasa zamu ya matusi, akiona hamtaki matusi mnaogopa kunywa sumu hii basi hapo anakupelekeni kwenye uwanja wa visa, utaona mume ghafla kaanza kulewa au kuvuta (Mihadarati)au hata sigara pia lete au anakula miraa na kucheza kamari au kuzini, eti kujaribu kumsahau yule alo muacha bila ya utaratibu wa sheria, na huku unakuta mke kapayuka, kashetupa hijab, yuko uwanjani anarusha roho, pengine maskini alikua hana tabia hiyo, Mume kwa tafrani za talaka alotoa mwenyewe anaanza kuzungumza saana, mambo yakizidi anazusha balaa jengine la kulipiza kisasi, eti anatafuta mke mwengine au mume mwengine.
Anachukua zile chuki na bakora zake alizochapwa huko atokeapo na kwenda kumpachika nazo mtu mwengine aso husika kabisa, Zinaendelea chuki hizi na sumu za talaka na kama hazina pakutokea inabidi sasa zishuke kwenye (Body)sababu (Akili-Mind)ni sehemu ya kiwiliwili, na ikishuka chini sumu hii inaanza kuangamiza viuongo, ndio utasikia mara sukari, mara kichwa, tumbo halishi, na (Ulcer)za kila leo, mara mapigo ya moyo yanakwenda haraka haraka, mara shingo imevimba, miguu haishiki, na ugonjwa wa wasiwasi unafatia juu yake, kumbe chanzo cha hayo yote ni Talaka, nyie yafanyieni uchunguzi mtayagundua hayo.
Ndio maana mkaambiwa Talaka ni ruhusa anayo ichukia Mollah wetu, na ajue yoyote yule afanyae kwa makusudi kuivunja ndoa kwa kutoa talaka au kudai talaka basi ajue fimbo ya Mollah wake inamsubiri na ni lazima adhibiwe. Na mnapofikia hali yakua sasa hamuwezi hata mkijaribu kuishi pamoja, basi fanyeni hima kuikumbuka aya hii ya mwanzo ya sura ya Talaq, mwanamke asitoke ndani ya nyumba abadan. Amwambie mumewe mimi naogopa kukutesa wewe na kujitesa na mimi kwa ajili ya kupinga amri ya Mwenye-enzi-Mungu, au kama huwezi basi muandikie barua yeye si anaandika talaka, wewe andika barua mwambie"Ewe mwenzangu katika Imani, kumbuka wema na ihsani tokea tulipo funga ndoa, kumbuka heshima tulopewa katika harusi yetu, na zawadi zilotoka kwa watu na Mollah wetu, za furaha na mazuri"kwa ajili hiyo mimi naogopa kumuasi Mollah wangu kwa amri zake alizozitaja katika sura ya Talaq aya ya kwanza na ya pili, na kama wewe mwenye kusisitiza ya kuwa nitoke, basi namueka Mollah wangu kuwa shahidi wa hayo, na mimi namuomba Mollah wangu adhabu zote za hii Talaq akushushie wewe kwa uweza wake. Ikiwa umeridhika na hilo mimi nitaondoka, ikiwa mwanamme au mwanamke hayo ndio yawe maneno yako.
Ndugu zangu Msifanye talaka kuwa jambo la mchezo, Talaka zina athari kubwa katika maisha ya Binaadamu, zinaleta uharibifu wa afya, ukosefu wa furaha, upotoshaji wa kizazi, pamoja na kuiharibu akili yako, kwa kujidhulumu na kujinyima raha na ladha ya Mapenzi inakatika kabisa, mpaka upate mtu mwenye taaluma kubwa ya mapenzi na utiifu kwa Mollah wake ndio aweze kuufungua tena huo mlango, na hilo ni vigumu kutokea kila wakati.
Basi kwa yoyote yule mwenye kudhamiria kudai au kutoa hiyo Talaka basi kwanza azingatie hayo niliyoeleza kabla hajafikia uamuzi wa kutenda jambo hilo.
Namuomba Mollah wangu utudumishe katika ndoa zetu mpaka tuhitimishane, Wenye magonvi wapatane, waloachana warejeane, wanochukiana Rabb wapendane, Akija Ibilis Mollah wajaalie kwa dalili wamuone, Na akitokea Jasusi la kuharibu ndoa Rabbana tujaalie tushikane. Amin

Friday, February 15, 2013

SHUKURANI ZA UHAI-PART-1

Asalaam Aleiykum,

Namuomba Mollah wangu niepushe na kupenda ufakhari, Ama kujulikana au kujijulisha mimi yakua Mcha Mungu au Sheikh, Ninyime mimi nafasi ya kujulikana kuwa najua, halafu nifiche mimi katika lile kundi la wasofahamu, usinipe nafasi ya kuhifadhi Msahafu wote, au Hadith chungu nzima ikawa nimevaa joho la Uanazuoni wakati nikijua Bahari ya Ulimwengu huu ni kubwa namie sina uwezo wa kuikoga nikaimaliza, Nakuomba nipe japo aya moja, niifahamu kiundani maana iliyofichikana kwa wale wengi wasofanya jitihada za kukumbuka wewe na kuzijua Rehma zako. Haina haja mie kupiga kelele kuamsha wenzangu wakati mie nimelala fofoo, Naam anaishi Mwanaadamu mpaka anaondoka katika Ulimwengu huu hajapata kutoa Shukrani za dhati kwa Mollah wake.
Umetukuka Mollah wangu kwa kutujaalia hisia hizi za Uhai, kutupa Baraka hii ya Uhai na thamani yake, Ikisha ukawajaalia baadhi ya waja wako kufahamu haki hii walonayo ikawaingia khofu na utiifu pasi na kutishwa wakaamua kukuabudu na kufata amri zako, hao ndio Waumini wa kweli kama ulivo wataja mwanzoni mwa sura ya (Baqarah-aya-ya-3)"ٱلَّذِينَ يُؤۡمِنُونَ بِٱلۡغَيۡبِ وَيُقِيمُونَ ٱلصَّلَوٰةَ وَمِمَّا رَزَقۡنَـٰهُمۡ يُنفِقُونَ "
"Ambao wanaamini yasiyo onekana na wanasimamisha Sala na kutoa yale Tuliyowapa"
Hawa ndio waloamini pasi na uthibitisho wowote, kabla ya kupata ushahidi wao wame(Surrender to Islam)wamekua Waumini, Ikisha wakaingia katika kundi la wale ulo waruzuku wakawa wanatoa kwa Shukurani kubwa, wanaona furaha kuvitoa hivyo ulivowapa, Na huku wanashukuru kwa zawadi hii ya Uhai ulowapa, Sasa vipi utasema Ahsante ?, kila kiungo chako kina fursa ya kusema Ahsante(Kutoa shukurani kwa Uhai huu)Kulea yatima hiyo shukurani, kutizama wagonjwa hiyo shukurani, kutoa damu pia shukurani, kulisha maskini nayo pia shukurani, kumsomesha mtu pia shukurani, kujenga zahanati pia kutoa shukurani, kuangalia wajane pia ni shukurani kila jambo la kheri ulifanyalo ni shukurani, lakini sharti lake ni moja nalo usitake malipo au kushukuriwa na binaadamu wenzio, anasema Mollah wako wale wanotoa shukurani wamo katika aya hii ya 9 ya sura ya (Insaan)"إِنَّمَا نُطۡعِمُكُمۡ لِوَجۡهِ ٱللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمۡ جَزَآءً۬ وَلَا شُكُورًا"
"Ambao wanatoa kwa ajili ya Mollah wao, hawataki wao malipo wala kushukuriwa"
Wanayafanya hayo kwa kutambua thamani hii ya Uhai na hiyo ndio njia yao pekee ya kutoa shukurani kwa Mollah wao, huku wakiwa na uhakika wa jambo ulolisema katika aya ya 10 ya sura hiyo hiyo
"إِنَّا نَخَافُ مِن رَّبِّنَا يَوۡمًا عَبُوسً۬ا قَمۡطَرِيرً۬"
"Hakika sisi tunaiogopa (Kwa ajili)ya Mollah wetu hiyo siku yenye shida na Taabu"
Jee siku hii ipo, inakuja, itatokea, nitaijuaje? Itabidi uwe mstahamilivu nikuchukue katika Ngarawa ya Wacha Mungu, Panda na mimi katika Mashua ya Mawalii(Mystic) ili nikupeleke katika kisiwa cha Ajabu sana cha Taaluma ya Tawhid, ukakutane na mambo yatakayo kukujulisha kuwepo kwa siku hiyo, ukitaka kuyajua hayo Endelea-Part-2

SHUKURANI ZA UHAI-PART-2

Asalaam Aleiykum,

Mwanzo kabisa tunapokewa katika kisiwa hiki na maneno mazito yaliyomo katika sura ya (An-Naba)aya ya 6 " أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَـٰدً۬ا "
"Kwani hatukuifanya Ardhi kama tandiko"
Hebu tumtizame Mwenyewe (Muumba)wa huu Ulimwengu anatwambia nini kuhusiana na hii ardhi, Amesema Muumba wa Mbingu na Ardhi "tumeijaalia hii Ardhi kama Tandiko(Tambarare)(Tectonic-Plate) Ikisha 7 "وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادً۬ا"Na Milima kama vigingi, Mizani ya kuweka hiyo (Balance)Basi ikiwa imewezwa kutengenezwa kwa hali hiyo, na kubomolewa vile vile inawezekana, ndio maana zikitingishika kidogo hizo sahani Ulimwengu mzima unapata habari.
Hapa itabidi nitoe mfano wa (Tandiko)lenyewe lilivyo na hakuna mfano mzuri kama ile sehemu ninayo fahamu Zanzibar na Tanganyika ikiwa Maji ya Bahari yataondoshwa ghafla basi utaikuta Ardhi ni moja (Tambarare)Lakini kwa Hekima za Muumba kazitenganisha Nchi hizi Mbili kwa kupitisha Maji baina yake kwa hivyo haiwezekani kuwa nchi moja, labda yaondoke maji, kwa hiyo ukizungumzia Muungano wa Nchi hizi mbili yaani(Union)haiwezekani kwa sababu ndani ya nadharia ya wazawa wa nchi hizi mbili kuna kitu(Imprinted)cha tafauti ya kuwa hii ni Zanzibar na hii ni Tanganyika, lakini linalowezekana ni Muungo yaani (Unity)kama vile kwa usafiri wa Meli au lijengwe (Bridge).
Hiyo ni Ardhi sasa wacha tumguse yule aloumbwa kutokana na hiyo Ardhi.
Nimesema katika darsa za nyuma na leo nasema tena Jaala maana yake ni tendo lenye kawaida za athari ya mabadiliko, nimesema hivyo kuonesha aya hii ya 8 ya sura hiyo hiyo haikutiwa jaala ila imesemwa " وَخَلَقۡنَـٰكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا"
"Na tukakuumbeni wanaume na wanawake"
Haina haja tena ukafanya mageuzi au operesheni ili ujigeuze vengine, kama una hisia za kike na wewe ni mwanamme basi Shukuru Mollah wako ndio alokuumba na kataka uwe hivyo, basi kubali uridhie umbile lako wala huna haja ya kujificha, kama unakwenda ukatikisika mabega nenda huku umeridhika, kama una sauti nyembamba sawa ndio sauti yako hiyo na huwezi kuibadilisha, waeleze ndugu zako, marafiki zako mimi hivi ndivo nilivo nikipunga mkono msishangae ndio umbile langu Mollah alonijaalia siwezi kuwa vengine, ila ujue kinacho katazwa ni kutenda Maasi na kujishuhubisha kwa kusudi, ukawa kama mwanamke kwa mavazi au operesheni au kujipamba hilo ni kosa. Na wanawake hali kadhalika ikiwa una hisia za kiume sio kosa Mollah wako ndivo alivokuumba usipite ukajificha wajulishe wenzio ili wapate kukubali na kukuelewa ili wasije kupita wakasema hivi na vile pia tambua hilo ndilo umbo Mollah wako alotaka uwe na kakuumba wewe(Unique)hakuna kama wewe wala hatomuumba mwengine kama wewe, tambua Mollah wako kakuumba wewe(Perfect)huna makosa kabisa toa shukrani kwa Mollah wako kwa kukupa Uhai kwa mapenzi yake, Ikiwa mbaya shukuru, na ukiwa mzuri pia shukuru, elewa na wewe ni kiumbe chake anakupenda kama anavo wapenda viumbe vyengine. Endelea part 3 upate habari ya usingizi.

SHUKURANI ZA UHAI-PART-3

Asalaam Aleiykum,
tuitizame aya ya 9 ya sura ya Nabaa inasemaje kuhusu kadhia hii ya usingizi "وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتً۬ا "
"Na tukaufanya usingizi wenu kama kufa".
Tukaujaalia huu usingizi kama kufa, hapa Sheikh Ali Muhsin Al-Barwan, yeye kauzungumza usingizi kwa ufasaha katika Tarjma aliyoifanya ya kiswahili ya Quraan Tukufu, kaizungumza aya hii kwa njia ya sayansi, akaeleza vipi Mwili unavopumzika katika tendo hili la usingizi, vipi viungo vinatulia baada ya harakati za mchana kutwa, maelezo hayo yamekita katika Sayansi ya (Outer-Observation)leo mimi nataka nigusie (Inner-Observation)kwa njia ya ndani, sio uhadithiwe ila wewe mwenyewe uwe shahidi wa tukio hilo la usingizi, upate kujua nikifa itakua vipi, (kwa sababu imetajwa kama kufa) Lakini kabla ya kwenda huko nataka nitoe tahadhari asije mtu akataka kujaribu mafunzo haya wakati yuko peke yake bila ya kuwa na mtu anaefahamu taaluma hii.
Lazima upate mtu akuongoze ili likitokea tatizo aweze kukusaidia, usije kuvamia majaribio haya unaweza kupoteza uhai au kuharibika akili kutokana na mambo yenyewe yanavotisha.
Sasa vipi huo mfano wa usingizi unavokua kama kufa, siku zote tukilala usingizi unakuja kutukuta (Unconscious)hatuna fahamu, mara moja moja unapata bahati yakua (Conscious)lakini unakua unaogopa, na unadhani Majini au Shetani yanataka kukuvaa kumbe ni usingizi lakini kwa ile khofu unajitupa kwenye (Unconscious)na usingizi unafanya kazi zake, lakini nini kitatokea ikiwa utakua kidume cha kweli ukaweza kuwa (Conscious)wakati usingizi unakuvaa, basi hapo utaona mambo ya ajabu yanakutokezea, utaona mwili wako umelala na wewe una ushuhudia kama vile umuonavyo (Maiti) katika hali hiyo ya ushuhuda unaondoshewa uwezo hata wa kunyanyua kidole unakua(Umepooza)kikamilifu.
Hapo tena unajua tafauti ya kuwa (Hai) na (Kufa)inavokua, na kama utaweza kuendelea kuwa shujaa ukaendelea kukaa katika hali hiyo ya Ushuhuda mpaka ingiapo alfajiri, utaona umerejeshewa ile hali ya kujimudu unapata(ability)ya kunyanyua viungo na kuweza kunyanyuka, na hapo tena kila kilicholala kinakurupuka na wewe unakua ushapata kujua na kuuona usingizi na kadhia yake, kuanzia hapo tena kulala kwako kutakuwa tafauti mpaka siku yako utakayo fariki au kuaga dunia na hapo utakua umepata siri ya usingizi unajua kumbe usingizi unaonekana kama vile unavoonekana usiku na mchana, na unakua na yakini ya kusimama kiyama na kuanzia hapo kila jambo lako linakua la shukurani.huo ndio usingizi unavoweza kuonekana. 
Sasa ni Habari ya Usiku,
Usiku ni (Absence of Light) au Giza ni muondoko wa taa, kama utafunga macho yako sasa hivi, basi unaweza kuisali Sala ya Isha wakati wa Adhuhuri, aya ya 10 ya sura hii tulonayo inasema,
"وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسً۬ا"
"Tukaujaalia Usiku (Kuwa kama)Guo"

Inakuaje ikawa kama Guo, umetoka mfano huu ili upate kujua kuwa hili giza(Usiku)ni (Nature)ya huu Ulimwengu, Na sisi na hii dunia yetu tunapita(Tunavaa) kwa mzunguko wa hii dunia yetu, tunapita katika hilo Giza ikisha tunatoka ndio ikawa mfano wake kama tunalivaa na kulivua, Yamefanywa haya ili mpate kupumzika kama ilivyotajwa katika aya ya 61 sura ya(Muumin) Hakuna jitihada zenye malipo mazuri kama ukifanya juhudi ukaona vipi huu usiku unavo ingia na kutuvaa, na ikisha ukaamka mapema uka shuhudia tena Usiku unavo vuliwa. Ukiyaona hayo utaomba Mollah wangu nijaalie niwe katika kundi la wale watoao shukurani kila huu usiku unapoingia na kutoka. Kutaka kuujua Mchana Endelea part-4

SHUKURANI ZA UHAI-PART-4

Asalaam Aleiykum,

Aya ya 11 inasema " وَجَعَلۡنَا ٱلنَّہَارَ مَعَاشً۬ا"
"Na tukaujaalia Mchana kama kufufuka",
Ikiwa umesoma uzuri habari ya usingizi basi utayarejea yale maneno nilosema unakua huna(Control)Amri ya kufanya jambo lolote, mara ghafla kwa kuamka huku inakuja ile (Idhini)amri ya uhai na hapo kila kinacho ishi kina nyanyuka na viungo vyote kuanza kufanya kazi, na wale walohukumiwa Umauti uwafike ndio wanabakia katika hali ile ile kila ukiwaamsha hawakujibu na wao hapo wako wakisubiri Amri  nyengine za Mollah wao zifatie.
Na aogope mtu isije ikamkuta hali kama hii na yeye hajatoa shukrani kwa Mollah wake, ndio maana ukiamka unashughulika na kazi zako na unamsahau Muumba wako unakua huna nafasi hata dakika tano ya kumkumbuka.
Tahadhari sana ya kughafilika na yule alo kukirim Uhai huu, unaipitisha siku hata bila ya kusema(Alhamdulillah). Unatakiwa uwe mnyenyekevu shukurani yako lazima iwe ya dhati kwa kusema Mollah wangu umenipa Uhai huu nakushukuru Mollah wangu, Mimi naanguka katika Ufalme wako nikiridhia kwa Mapenzi yako Mollah wangu umenipa siku nyengine ili nipate kukushukuru wewe, wewe ndie ulonijaalia Afya Mollah wangu, basi hata ukiamua kunipa Maradhi mimi nitakua mwenye kuridhia, basi mie leo nachukua ahadi ya kuonesha shukurani zangu kwako kwa kujifunga na kujizuia na maasi yote kwa siku hii ya leo, kwa ajili ya zawadi hii ya Uhai nachukua Ahadi ya siku hii ya leo kufanya mema matupu, kutokana na Imani yangu kama ulivonipa Uhai huu, basi naamini kiyama kipo, na siku hiyo Mollah wangu nataraji Rehma zako zinilinde mimi na misukosuko ya siku hiyo.
Aya ya 12 inasema " وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعً۬ا شِدَادً۬ا "
"Tukajenga juu yenu (Mbingu)saba madhubuti"
Habari hii ya Mbingu saba utaipata wakati utakapokua Mja (Swalihina)utafunguliwa siri hizo za kuwapo kwa mbingu saba  wakati itakapo julikana kwa dhati kuwa umejitupa kwa Mollah wako na umefungamana na yeye, sio kwa sasa unakesha ili upate kujua siri ya mambo ikisha uwe Mganga, zipo mbingu saba kama zilivo ardhi zenye (Layers)saba, wanasema pia wana historia mpaka bahari zilikua saba.
Aya ya 13  inasema "وَجَعَلۡنَا سِرَاجً۬ا وَهَّاجً۬ا"
"Na Tukaijaalia taa inga'rayo na yenye joto kubwa"
Ikisha tukajaalia taa hii yenye kutoa muanga wa joto, imetajwa kwa dasturi ya jaala sababu usiku linakua haipo inaondoka, hata hivyo jua linachangia sehemu kubwa ya maisha katika dunia hii tunoishi, Jua linatupa hii nuru ya mchana, kama ilivyotajwa katika aya ya 61 ya sura ya (Muumin)jua linatupa (Special-Energy)maalumu ambayo  sisi wanaadamu hatuna uwezo wa kuipata moja kwa moja kutoka kwenye jua kwa hiyo inaingia kwenye majani na mimea na wanyama sisi tunaipata kutokea katika vitu hivyo.
Aya ya 14 inasema " وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٲتِ مَآءً۬ ثَجَّاجً۬ا"
"Na tukateremsha maji yaangukayo kwa kasi kutoka mawinguni"
Aya ya 15 inasema "لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبًّ۬ا وَنَبَاتً۬ا "
"Ili tupate tuoteshe chembe chembe na mimea"
Aya ya 16 inasema " وَجَنَّـٰتٍ أَلۡفَافًا"
"Na Mabustani yenye miti iliyosongana"
Naam Ametumiliki Mollah wetu kwa kila jambo, yeye ndie mwenye kutupa Uhai, akautunza na kuurutubisha Miili yetu kwa riziki anazo tutolea katika ardhi hii, akatupa afya kutokana na hiyo riziki, akatufanyia na ladha za kila aina kutokana na vyakula hivyo, iwapi leo shukurani yetu kwa Mollah alotupa huu Uhai, akatumiliki kwa kutupa pumzi zake, akatuenzi kwa kila jema katika Ulimwengu huu, ziko wapi shukurani zetu, wakati kuanzia usingizi, mpaka chakula chetu, kazi zetu, furaha zetu, zoote zinamtegemea yeye, Mara ngapi umekula ukasema (Bismillah)na kumbuka lini ulimaliza kula ukasema (Alhamdulillah) kumbuka yeye ndie alo kutolea hiyo Riziki kutoka katika hiyo Ardhi, kwa hiyo mpaka hicho chakula unokula ni Ibada. Mollah wetu tusamehe kwa sahau zetu na upungufu wa shukurani juu yako, tupe faraja yako ya kupata kivuli chako siku hiyo Adhimu tusoijua muda wake, ikisha tuepushe na adhabu zako kubwa na ndogo, na utupe makaazi katika ufalme wako wenye kumiliki Pepo. Amin


Friday, February 8, 2013

PIN-NUMBER YA MAPENZI-PART-1

Asalaam Aleiykum,
Inawezekana kuandikwa maelfu ya vitabu linapotajwa neno hili la mapenzi, Na tena watamiminika wasomaji kwa hamu ya kujua tafsiri au siri hii ya mapenzi, lakini yote hayo ni mazoezi ya uandishi ambayo mtu anaweza kuandika akiwa hajawahi kupenda au kupendwa, sasa inakuaje mtu kama huyo ataweza kuyaeleza mapenzi, hiyo ndio hali tulonayo ambayo sote inatutesa na kila mtu anataka kupenda na kupendwa lakini nyoyo zetu zimefungika, sasa cha ajabu kubwa funguo tunazo wenyewe lakini hakuna anaejua kutumia akafungua mlango wa (Moyo)kwa hiyo funguo yake alonayo.
Mimi leo nimejitosa katika bahari hii kuzungumzia japo (Ufukwe)mmoja wa hii Bahari ya mapenzi ili nipate kukupa (Pin-Number)au ufunguo ili na wewe upate kufungua Moyo wako ili upendwe au upende, Pia Napenda uelewe kinachotakiwa kwako ni kufungua Moyo tu, ama kuhusu mapenzi yenyewe huna amri nayo yanaweza kushuka yakaingia au yasiingie hilo linatokana na Mollah wako, ambaye anakujua unastahiki hii zawadi ya Mapenzi au hustahiki, na kumbuka huwezi kufanya Ulaghai kama ufanyao hivi sasa.
Nimesema Mapenzi ni Bahari kubwa na yapo ya aina nyingi, mimi hapa leo naya zungumzia ya (Mke)na(Mume)ili pengine atakaesoma inaweza kumsaidia kuifufua ndoa yake ikawa hai tena, Inasikitisha sana na pia kuleta wasiwasi mkubwa kuona leo idadi ya waislam inaongezeka kusheherekea sherehe maalumu ya mapenzi(Valantine)eti siku ya mapenzi Duniani, Napata habari wanagombana wana ndoa eti kama Mke hajatolewa (Out)au Mume hajaja na maua na kadi, vinakua vita vikubwa, akaambiwa hanipendi mume huyu kasahau (Valantine). Vipi nyinyi leo mapenzi yenu yawe ya siku maalumu, kwanini ikawa hivyo mpaka msubiri mwezi wa (February)ndio mpendane, miezi 11 yote ilopita nyinyi mnafanya nini, mmewahi kujiuliza kwanini hamna mapenzi baina yenu? imeshakujieni fikra yakua katika ndoa yetu kinacho tuweka ni kipande cha karatasi kilichfunganishwa na sheria, lakini baada ya hapo hakuna hisia zozote zinazo safiri baina yangu na ya mwenzangu. Sasa nini kilo sababisha hayo yote, ndio azimio la hii mada yetu ya leo, sasa kabla ya kuendelea mbele hebu tuzijue kufuli zenyewe halafu huko mbele ndio tutaukuta Ufunguo. Kufuli ya Mwanzo ni ipi?
"ٱلزَّانِى لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوۡ مُشۡرِكَةً۬ وَٱلزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَآ إِلَّا زَانٍ أَوۡ مُشۡرِكٌ۬‌ۚ وَحُرِّمَ ذَٲلِكَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ"
"Mwanaume mzinifu hafungamani ila na Mwanamke mzinifu au Mwanamke Mshirikina, na Mwanamke mzinifu hafungamani ila na Mwanamme mzinifu au Mshirikina, Na hayo yameharamishwa kwa Waumini(Waislam)"
Sisemi mimi kama mume zini kabla ya kuona au mumemshirikisha Mollah wenu na chochote, lakini nataka kukuonesheni kitu kilofunga Nyoyo zetu yakawa mapenzi hayaingii baada ya huko kufunga ndoa, sababu kubwa ni yale alo haramisha Mollah wako, ambayo sisi tuna yatenda, ikiwa hujapata kuyatenda wewe umeokoka, na kama umefanya basi sasa ushajua na unapata nafasi ya kutubu urejee kwa Mollah wako ili akusamehe apate akushushie hayo mapenzi urudi kama(Ujana)utoto upendane na mwenzio kama ilivokua zamani.
"Anasema Nabii Mussa a.s katika Taurati zinaa ni dhanbi kubwa kabisa, na mwenye kuzini anastahiki auwawe"
"Akasema Nabii Issa a.s katika Injili" Nabii Mussa a.s kakwambieni yoyote yule anofanya tendo la zinaa basi kafanya Dhanbi kubwa, mimi nakwambieni yoyote yule Mwenye kumtizama Mwanamke au Mwanamee kwa Matamanio basi kesha zini"
"Anathibistisha Nabii Muhammad s.a.w katika Quraan na hadith kwa kusema""Nyie waumini angusheni macho yenu chini" msitizame kabisa mmekatazwa.Hao ndio Wajumbe wa Mwenye-enzi-Mungu, wakwanza anasema atofanya(1)wapili kasema atotizama(2)Na kipenzi chetu watatu yeye kasema Msitizame kabisa(3) Sasa ikiwa hufanyi hayo basi wewe uko katika kundi la ngazi ya juu kabisa, lakini ikiwa unatenda hayo basi mimi na wewe hatuvuki katika hiyo aya niloitaja hapo juu na hiyo ndio imekua chanzo ya Mioyo yetu kupigwa kufuli, Vipi inakua nitaelezea kwa urefu-Part-2

PIN-NUMBER YA MAPENZI-PART-2

Asalaam Aleiykum,

Sasa inakuaje haya mambo ya kufuli mwanzo wake unakua wapi? kinapatikana chanzo kikubwa cha kufuli hii pale Mtu anapotaka kuoa au kuolewa au hata baada ya ndoa, na chanzo chenyewe inakua pengine unakwenda kuposa Nyumba fulani, lakini unampenda mtu fulani mwengine kabisa asokua yule, au na yeye anapendana na mtu mwengine kabisa, wawili nyie mnakutana mwanzo wenu umeshakua na mashaka makubwa, Eleweni Mollah wenu ni mwenye kujua kila jambo na hilo pia analo taarifa nalo na pahala hapo katika nyoyo hizo mbili hapawezi kuteremka Mapenzi abadan, itakua mnakaa kutizamana kasoro, mmeshaingia nyinyi na dosari ya uzinifu ima iwe aliotaja Nabii Mussa a.s au Nabii Isa a.s moja wapo katika hizo mshazibeba mnaingia nazo katika ndoa na mnaishi nazo bila ya kutubu, Mtakuta ndani ya nyumba hamna furaha, hamna mapenzi, ndani ya nyumba kila mmoja sasa anaanza kunyanyua macho yake juu, hapo tena Mnaanza kumpinga Mtume Muhammad s.a.w, Mnazidisha kufuli, mpaka inafikia Mume katoka mke hana habari au mke karudi mume hayupo, inakua kama watu wawili walopanga nyumba pamoja.
Yanazidi mambo haya katika nyumba ya ndoa mpaka baada ya kuishi ndani ya nyumba watu wawili mke na mume sasa mnaishi watu wanne,(kama nyinyi vijana wa siku hizi)Mume anampenda(Actress)Priyanka, na Mke anampenda(Actor)Rishi Kroshan, au Kama watu wazima kama sisi tena ndio bado umezama kwa Dharmendra na Hema malini, inakua hata mkikutana nyinyi wenyewe inabidi mzime taa ili (Ma-Actor's)wapate kutawala,umemkamata mke lakini mawazo yote yapo kwa hao(Ma-Actor's) hiyo ndio hali iliyomo majumbani, vipi leo yataingia  mapenzi wakati anaingia Mume katika Moyo umejaa vimada,wanawake wote wa mjini unatamani wewe, katika moyo zimejaa biashara na faida, vipi yataingia Mapenzi Mke kajaza Ma-handsome kichwani kwake,Wivu umo humo, magonvi yamo humo, wewe huna nafasi ya kumuachia Mwenye-enzi-Mungu kukumiminia mapenzi yake katika moyo wako, umeutia mwenyewe kufuli na hutaki kuufungua, huwezi kukaa hata dakika tano na mkeo ima utataka iwashwe TV au ujibabaishe kwa hichi na kile, na mwanamke hali kadhalika tena kama anazungumza na simu anamwambia shoga yake hilo linaingia tutazungumza baadae, vipi yatapatikana Mapenzi kwa hali hiyo.
Ndio maana utaona kutokana na mti huo wa chuki mlopanda mnashindwa hata kupenda watoto wakizaliwa, utaona mara mume huyo kakimbia hataki kusidia hata watoto, Na hii inatokana pengine na yeye hakutendewa hayo(Hili darsa yake nyengine)lakini alama zote zinaonekana mapema kama humpendi mumeo au mkeo taabu sana kuwapenda watoto, utaishi nao, ndio watoto wako lakini mapenzi hakuna, jiulize wewe mwenyewe unawapenda au mazoea tu, hivi ndivo wengi wetu tulivo, tunaishi bila ya mapenzi kutokana na makosa yetu wenyewe, tunaikosa zawadi hii ya Mollah wetu adhimu ambayo ukiipata umo furahani, na mfano wake kama Afya na Maradhi, unaona wakati ukipewa Maradhi unakua katika hali gani, na wakati utakapopewa mapenzi umpende mkeo au mumeo utakua na hali gani, ikiwa mtu anajenga jumba kwa mapenzi ya mwanamke wa nje, nini habari yako wewe ikiwa unatenda hivyo kwa njia ya halali ya kumjengea mkeo au mumeo, sasa ufanye nini kuufungua huu moyo kwa hiyo (Pin-Number) endelea Part-3

PIN-NUMBER YA MAPENZI-PART-3

Asalaam Aleiykum,

Sasa hivi bado mko katika misukosuko wengine ndoa zenu zinaninginia vidoleni, sasa yapo matumaini ikiwa mtabadilika kutoka katika kundi moja kwenda kundi jengine ili mpate hayo mapenzi yatokayo kwa Mollah wenu kama inavosema Quraan sura ya Noor aya ya 26,
"ٱلۡخَبِيثَـٰتُ لِلۡخَبِيثِينَ وَٱلۡخَبِيثُونَ لِلۡخَبِيثَـٰتِ‌ۖ وَٱلطَّيِّبَـٰتُ لِلطَّيِّبِينَ وَٱلطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَـٰتِ‌ۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ "مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ‌ۖ لَهُم مَّغۡفِرَةٌ۬ وَرِزۡقٌ۬ ڪَرِيمٌ۬ 
"Wanawake wabaya(ni kwa)wanaume wabaya, na Wanaume wabaya (ni kwa)Wanawake wabaya,(Na kwa)Wanawake wema (ni kwa)Wanaume wema, Na Wanaume wema(ni kwa)Wanawake wema, hao wameepushwa na hayo wanayoyasema, wao watapata misamaha na riziki iliyo  Njema".
Kwanini aya ikaanza kwa kuwataja Wanawake, sababu kubwa Mume ni mwenye kufata, ndio maana utaona matangazo yote yamejaa Wanawake, ikiwa Mke ataanza kubadilika basi Mume atafatia, kwa sababu Mke ni kishawishi kikubwa cha kuweza kumfanya Mume ale tunda la mapenzi, mwanzo kabisa mnatakiwa mubadilike kutoka katika huo ubaya mlokua nao hivi sasa muanze kuwa waja wema, nini kitatokezea juu yenu mkibadilika, inatakiwa kitu kimoja tu Kubadilika, Mwenye-enzi-Mungu anatoa ahadi kwanza ya kukusameheni yale yalopita mwanzoni, ikisha atakupeni Riziki iliyo njema, ndani ya riziki na Mapenzi pia yamo yanaingia katika kiwiliwili chako kama kinavo ingia chakula.
Sasa vipi mabadiliko haya yatokee, inabidi upate huo ufunguo au hiyo (Pin-Number)na hakuna ufunguo utaoupata ila kurudi katika nafsi yako, rejea ndani ukaanze kuchakua chakua uyatupe (Mafaili)ya zamani, Safisha kifua chako kwa kuanza kuona hakuna mwanamke mzuri kama Mke wangu au Mume wangu, ona vyote vya nje kama milango tu isokua na funguo, au makabati yalotupwa, anza mazoezi yakutilia Mti wako wa mapenzi mbolea, panda mbegu huku una subiri kwa kupalilia, basi anza kwa kuanza kuchukia vilo nje, kila ukitaka kushughulika na vilo nje kumbuka pesa zako, kumbuka masikini mke wangu yupo nyumbani anasubiri hana hata haja ya pesa au mali yangu, halafu tanabahi hawa wa nje jee nikiwa mgonjwa watanipigia hata simu hawa, geuza muelekeo wako nyumbani anza kufanya shughuli za nyumbani pamoja na mkeo, kama husimamishi Sala, basi mfanyie (Surprise)ya kutaka kumsalisha, msikae mkasubiri (Valantine)kwani ishara na mbolea za Mapenzi ni vitu vile mnavopandisha kila siku, huku mkisubiri (Mche)uchomoze, Na nakwambia kwa yakini (Mche)utachomoza haziwi ahadi za Mollah wako zikapita bila ya kutekelezwa.
Badilika wewe wala usione haya chukua watoto uwakogeshe kama mnao, na kama hakuna basi mwambie Mkeo leo Bibie nakukogesha mie, ikisha nitakukata kucha, halafu nitakuchana nywele tukimaliza..Alaa mfanye nini, mwambie avae nguo mwende kwenye ufukwe wa Bahari mkatizame Mbaa mwezi, hivyo ndio inavotakiwa   
kutendeana wana ndoa, Na mwanamke pia jaribu kubadilika, anza na jiko lako isiwe siku zote wali, akichelewa Mume jilize kikweli kweli umwambie umemiss, sio akigeuza kichwa unamzomea, huyo Mumeo na Mume kama (Mtoto-mdogo)anataka kudekezwa ndio maana wanaume wanapenda kutafuta Mke alofanana na Tabia za mamake, basi na wewe Mtoto wa kike zichunguze Tabia za mamake zikoje halafu anza kuziiga utaona hivi Mume anakupenda na Mama mkwe wote wanakupenda, lakini usifanye kwa uongo, itakua unajidanganya nafsi yako na ya mwenzio, na hapo utakua hujabadilika,Fanya kila siku mambo mepya mepya weka siku maalumu na umwambie Mumeo leo usitoke mume wangu siku ya kukata kucha, na ukiambiwa siku ya kukata kucha isiwe unatoka na shoka ili ummalize haraka, kinachotakiwa unakata kidole kimoja unakwenda kuleta mshikaki,unakata cha pili unaleta juice, unakata cha tatu unaleta kitu unacho kijua mwenyewe huku umevaa kengele(Mapambo yako)na utizame kama paka shume atatoka, mapenzi yanakuja kwa njia ya (Surprise)na wewe anza mazoezi ya kushitukiza.Endelea-Part-4

PIN-NUMBER YA MAPENZI-PART-4

Asalaam Aleiykum,

Najua hakuna jambo gumu kama kubadilika, ni shida kubwa wakati tulo nao kupalilia mti wetu wa mapenzi, Uzito huu unatokana na (Viburi)vilotawala nafsi zetu, basi ikiwa hilo ndio tatizo letu inapaswa mtu aangalie mambo haya nitakayoyataja kabla ya kuoa au ikiwa kashaolewa pia anaweza kuyaangalia mambo haya ili apate kujirekibisha nayo,(1)katika mambo ambayo pengine laweza kukuvunja moyo ukawa hutaki kutia mbolea labda(Physical attraction)Umbile,mwenzio kabadilika (Mahanjumati)yamnenepesha au humpi chakula kakonda sana, tizama pengine hilo ndio linalo kufanya kutwa ukimbilie nje(2)Au swala la mchanganyiko wa kidini hamkutani katika shughuli hizo, basi hapo panataka marekebisho,(3)Katika medani ya (Akili)labda hamko sawa katika daraja za hekima, hapo panatakiwa maelewano,(4)Mambo ya vivazi na tabia za maingiliano katika jamii, pengine mmoja kati yenu hakuridhishi lakini wewe umekaa kimya hutaki kumwambia,(5)Pengine mwenzio ni mwenye kupenda mambo ya kifahari na kujifagharisha, hayo yanatakiwa muyazungumze,(6)Huruma za kupenda watu na Familia zenu kwa jumla, hilo pia lataka kushughulikiwa,(7)Na makutano yenu (Kiroho)vipi mumekamatana katika nafsi, kwenye Roho jee mwenzio yumo Rohoni na alama ya mwanzo katika hili la Roho jee una muheshimu, ikiwa una muheshimu mwenzio ukamfanya Rafiki yako, mshauri wako wa mambo yako yote, basi hapo ushaanza kuufungua Moyo wako, ushaanza kuijua (Pin-Number).
Lazima Mke na Mume wawe na dhumuni moja kama vile misimamo ya kidini au kusomesha watoto au maisha yao kwa ujumla isiwe mmoja ana (Agenda)za siri, hapo Penzi haliwezi kuteremka.
Mke na Mume lazima waungane kikamilifu kiroho na asiingie yoyote akaja kukaa baina yao, vipi utafanya hivyo ni pale ambapo baada ya kujisafisha na kubadilika kabla ya mapenzi linateremka jambo la kukukurubisheni wawili nyie(Magnetism)na hili ni lile jambo linalotokea kabla ya kitendo kama vile ukitaka chai, hutoka uamuzi wa kuichemsha na kuitia kikombeni na kuanza kunywa, hicho ndio kivutio au hamu, na baina ya Mke na Mume pia inapatikana hali kama hiyo na unaweza kuijua ikiwa unatizama mambo kwa uangalifu, hebu ukikaa mwenzio hakutizami wewe mtizame kwa jicho la Mapenzi, anza zoezi hilo utaona mabadiliko yake, fanya japo kwa siku tupa dakika kumi za kumtizama tu mwenzio, basi kidogo kidogo utaona anaaza kukujaa moyoni, sio kama sasa hivi jiulize lini mara ya mwisho umemuangalia mwenzio, na nikisema muangalie ni tafauti na kumtizama, kumuangalia uwe huna fikra zozote ndani ya mawazo yako, iwe hususia unamtizama Mkeo au Mumeo pasi  na chochote kujipenyeza kupita kati, hapo utaona huna haja ya kusubiri (Valantine)kila siku kwako itakua siku ya mapenzi, kila ukiamka unatilia mbolea mpya mti wako wa moyoni, na ukitoa vitu vyote moyoni ukawacha mweupe haikai fisadi yoyote kwa mara ya mwanzo inakua ushafungua hiyo kufuli na  penzi litaanza kupenya, Na kwanini penzi lisipenye wakati nyie wenyewe mapenzi matupu, ndio maana kwa kitendo chenu cha Ndoa mkikutana kwa shauku na Mapenzi Mollah anakupeni zawadi ya Mtoto ikisha mnakua mnampenda mtoto wenu, basi kama inaweza kutokea hivyo kwanini isitokee kwa wawili nyie.
Na ikitokea hali ya Mapenzi hakuna atoweza kuhadithia, ukimpenda Mumeo au Mkeo unakua kama (Laila na Majnu)akitokea mwanamke yoyote unataka awe kama (Laila) na ukiwa mwanamke akitokea mwanamme unataka awe kama (Majnu)Na hapo tena inakua umeshaonja kitu kilotokea kwa Mollah wako hata kikiondoka midamu ushaonja ladha haikwishi daima, na inayobaki ni Rehma ambayo haiondoki Milele, Nakushauri onja japo kidogo ladha ya Mapenzi itokayo kwa Mollah wako, na wewe utakua mtu mwengine kabisa, utapenda watoto wako, utapenda familia yako, utapenda hata wapita njia kwa kuonja japo kidogo Mapenzi yalotoka kwa Mollah wako, lakini lazima upate ladha hiyo ya mapenzi ndio utaweza kujua nini Mapenzi, lakini kwa sasa hivi yatizame hayo unayoita mapenzi yana nia gani nyuma yake, ukimpa mtu zawadi unataka malipo, mpaka nyumbani ukijchekesha Mke anajua huyo anataka nini, mapenzi hayana (Motive)ukitoa hutaraji malipo, na mwenye mapenzi ya kweli hakumbuki hata kulipwa yeye kila akitoa anataka atoe zaidi, na kila ukifanya zaidi malipo yake yanaongezeka kutokana na sheria za Ulimwengu huu,"Enyi Wanaume"Kumbukeni yale maneno ya yule Mshairi  Maarufu wa(Kiarabu)""Aliposema""Nilipogundua mimi kwamba katika huu moyo wangu anaweza kukaa asiyekua wewe Mollah wangu""Nilifanya jitihada za kuujaza uongofu wako hata akawa hakai asiyekuwa wewe""Sasa na wewe anza kupunguza mambo yalojaa katika moyo wako""Anza kupunguza kupenda wanawake wa nje""Acha kutizama vifua vya watu ikawa vidani vyote unavijua wewe""Hii mpaka rangi za kucha wewe ndio (Expert)unajua mpaka (Style)za nyusi hayo yote hayafai na yanakuzuia kupata zawadi ya mapenzi kutoka kwa Mollah wako, safisha Moyo ili mapenzi yaingie.  Namalizia kwa hadith hii ili iwe fundisho kwa ndugu zetu wa kike wasione wanaonewa au hawatopata kitu katika malipo yatokayo kwa Mollah wao, nini watapata?
Anahadithia  (Bayhaqi katika Sha'b)"Sayyidah Asmah bint Yazid Ansariyyah r.anha""Alikwenda kwa Mtume s.a.w akiwa kakaa na masahaba zake"Akasema nimekuja kama Mjumbe wa wanawake wenzangu, ambao hakuna mwanamke wa mashariki wala magharibi anajua kuja kwangu hapa, na hakuna yoyote yule alosikia haya ninayotaka kukuuliza, lakini wote wana shauku  na maoni ya jambo hili, tumeamini ulokuja nayo Bwana Mtume s.a.w,"Sisi wanawake tumefungiwa majumbani kwetu, na tumo kuwatimizia wanaume haja zao, sisi tunachukua mimba na kuzaa kwa shida, wakati wanaume wao wamepewa zawadi ya kusali Sala ya Ijumaa, wanakwenda kuwatizama wagonjwa, wanahudhuria mazishi, wanakwenda Hijja watakavo, wanapigana Jihad, sisi tumebakia nyumbani tunalinda majumba yao huku tukilea watoto, vipi tutakuwa sawa katika mgawanyo wa hayo malipo kutoka kwa Mollah wetu""Bwana Mtume s.a.w akawageukia Masahaba na kuwaambia mesikia swali la mwanamke huyu, akasema hakuna swali zuri katika dini kama hili""Wakajibu masahaba hatujui kwamba wana habari kama hizi katika dini""Akasema Bwana Mtume s.a.w "" Nenda kawaambie wanawake wote, wenye kuwafanyia mazuri waume zao, wakawaweka katika hali ya furaha, na kuwaridhia, basi na wao(Malipo)yao yatakuwa sawa na yale yote wayafanyayo wanaume""Akaondoka yule Bibi na Takbir na Tahlil(Allahu Akbar)(Laa-Illah-Illah-Allah).
Nakutakieni Maisha ya kheri na Ukarim wa Mapenzi yatokayo kwa Mollah, Muishi katika ndoa zenu kwa mapenzi makubwa na kila mmoja amsamehe mwenzie atakapo mkosea, ikisha kwa pamoja mgeuke kuwa waja wema:Ogopeni kupigwa bakora ya Mollah wenu kwa kuzivunja ndoa zenu, na mkaja kuzeeka mpaka ikawa Mtu anaishi peke yake hata hapati mtu wa kumpa Maji, Mollah wetu tuepushe na hayo Amin.

Friday, February 1, 2013

BENDERA YA KIISLAM-NA-MAANA YAKE

Asalaam Aleiykum,

Aya ya 31 sura ya kahf "أُوْلَـٰٓٮِٕكَ لَهُمۡ جَنَّـٰتُ عَدۡنٍ۬ تَجۡرِى مِن تَحۡتِہِمُ ٱلۡأَنۡہَـٰرُ يُحَلَّوۡنَ فِيہَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ۬ وَيَلۡبَسُونَ ثِيَابًا خُضۡرً۬ا مِّن سُندُسٍ۬ وَإِسۡتَبۡرَقٍ۬ مُّتَّكِـِٔينَ فِيہَا عَلَى ٱلۡأَرَآٮِٕكِ‌ۚ نِعۡمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتۡ مُرۡتَفَقً۬"
"Hao watapata mabustani ya Milele yanayopita mito(Maji)mbele yake, humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu na WATAVAA NGUO ZA KIJANI ZA HARIRI LAINI na za hariri nzito, wanaegemea humo juu ya vitanda vilivyopambwa, ni malipo mazuri yalioje hayo, na mahali pazuri palipoje hapo(pa Kupumzika)"

Umepata kujiuliza kwa nini Bendera au (Symbol)ya Kiislam ikawa kijani? Kwanini Bwana Mtume s.a.w akatuchagulia kijani na nyeupe ndio kuwa alama yetu?
Sababu kubwa ya mwanzo kijani ni (Nature) ya Ulimwengu huu na ndani ya Quraan imetajwa mara nyingi mahusiano ya rangi ya kijani na Ulimwengu huu, na wewe mwenyewe ukizunguka kila pahala utaona vipi unaishi ndani ya mazingira ya rangi ya kijani, (Mfano)kama mimea, miti na kadhalika, Na la pili mpaka wewe mwenyewe kama utapigwa ngumi na damu ikivilia basi unageuka rangi ya kijani, Na jambo la tatu kijani ni rangi  inochukua (Light)au Nuru kwa urahisi ndio maana zikachanganywa rangi mbili hizi za nyeupe(Nuru)na kijani ili zende sambamba katika dini hii ya haki ili iwe (Alama)ya kiislam.
Sasa nini Kijani? Kijani kwa maana ya (Deep)ndani kabisa ina sifa mbili kwanza kijani ni (Active)kama unavoona maumbile yalivo kama pepo likivuma miti na majani inavo peperuka kwa kasi kubwa, halafu tena sifa ya pili ni (Calm)kupatikana utulivu wakati hakuna upepo au mvua nk, hiyo ndio sifa ya (Nature) na hivyo ndio Bwana Mtume s.a.w akatuchagulia Rangi yetu iwe ya kijani, tuhusiane na Ulimwengu, tuwe (Active)tusikubali uzembe, tusikubali kuonewa, ikisha tuwe (Calm)pale mambo yanapokua mazuri yametulia, hakuna uonevu au msukosuko wowote tukae kama Ulimwengu ulivyo, unakwenda pasi na matatizo yoyote, ndio maana hata utaona ndugu zetu Wanawake wanapenda kuvaa rangi hii wakati wa sherehe zao za harusi, Na utaona vipi huyo wanomvika nguo hiyo anavo funguka kwenye(Light)kutokana na uwezo wa rangi hiyo kuimeza taa(Light).
Nini Rangi Nyeupe? Nyeupe ni (Light)Nuru, Na kwenye Nuru unapatikana Muangaza na kwenye muangaza watu wote wanaona na watu wakionana inapatikana salama, kwa hiyo nyeupe ni Rangi ya Salama, Nyeupe Rangi ya Amani, Nyeupe Rangi ya (Surrender)Nyeupe ni (Islam)ndani ya nyeupe kila mtu anavutika, kila mtu anatamani aje karibu na nyeupe na siri ya nyeupe yakwamba imekusanya rangi zote ndio ikawa nyeupe, nyeupe ndio Uislam ulokusanya kila rangi mtu awe mweusi,cholate,mweupe wote mko katika Rangi moja ya weupe ambayo ndio rangi ya Nuru, tunamuomba Mollah atuongoze kwenye Nuru yake. Kwa hiyo ukichanganya Rangi mbili hizo za Kijani na Nyeupe unapata mambo haya matatu (Active+Calm+Peace)hiyo ndio Bendera ya Kiislam, hizo ndio Rangi zako Bwana Mtume s.a.w alizo kuchagulia ushikamane nazo, lakini hatari kubwa inapatikana pale ukichanganya kijani na rangi nyengine, kama vile ukaja kuchanganya na rangi yenye kuashiria Maradhi yaani Rangi ya Manjano, utaona matatizo yanavopatikana kwenye mkusanyo wa Rangi mbili hizo, kwa hiyo ndugu zangu muwe makini sana katika uchaguzi wa rangi zenu, pateni maana za rangi mzijue ili yasikufikeni matatizo sababu ikawa uchaguzi mbovu wa Rangi, Nakuomba Mollah wangu tujulishe yenye manufaa na sisi japo kwa uchache: Amin.