Friday, February 8, 2013

PIN-NUMBER YA MAPENZI-PART-1

Asalaam Aleiykum,
Inawezekana kuandikwa maelfu ya vitabu linapotajwa neno hili la mapenzi, Na tena watamiminika wasomaji kwa hamu ya kujua tafsiri au siri hii ya mapenzi, lakini yote hayo ni mazoezi ya uandishi ambayo mtu anaweza kuandika akiwa hajawahi kupenda au kupendwa, sasa inakuaje mtu kama huyo ataweza kuyaeleza mapenzi, hiyo ndio hali tulonayo ambayo sote inatutesa na kila mtu anataka kupenda na kupendwa lakini nyoyo zetu zimefungika, sasa cha ajabu kubwa funguo tunazo wenyewe lakini hakuna anaejua kutumia akafungua mlango wa (Moyo)kwa hiyo funguo yake alonayo.
Mimi leo nimejitosa katika bahari hii kuzungumzia japo (Ufukwe)mmoja wa hii Bahari ya mapenzi ili nipate kukupa (Pin-Number)au ufunguo ili na wewe upate kufungua Moyo wako ili upendwe au upende, Pia Napenda uelewe kinachotakiwa kwako ni kufungua Moyo tu, ama kuhusu mapenzi yenyewe huna amri nayo yanaweza kushuka yakaingia au yasiingie hilo linatokana na Mollah wako, ambaye anakujua unastahiki hii zawadi ya Mapenzi au hustahiki, na kumbuka huwezi kufanya Ulaghai kama ufanyao hivi sasa.
Nimesema Mapenzi ni Bahari kubwa na yapo ya aina nyingi, mimi hapa leo naya zungumzia ya (Mke)na(Mume)ili pengine atakaesoma inaweza kumsaidia kuifufua ndoa yake ikawa hai tena, Inasikitisha sana na pia kuleta wasiwasi mkubwa kuona leo idadi ya waislam inaongezeka kusheherekea sherehe maalumu ya mapenzi(Valantine)eti siku ya mapenzi Duniani, Napata habari wanagombana wana ndoa eti kama Mke hajatolewa (Out)au Mume hajaja na maua na kadi, vinakua vita vikubwa, akaambiwa hanipendi mume huyu kasahau (Valantine). Vipi nyinyi leo mapenzi yenu yawe ya siku maalumu, kwanini ikawa hivyo mpaka msubiri mwezi wa (February)ndio mpendane, miezi 11 yote ilopita nyinyi mnafanya nini, mmewahi kujiuliza kwanini hamna mapenzi baina yenu? imeshakujieni fikra yakua katika ndoa yetu kinacho tuweka ni kipande cha karatasi kilichfunganishwa na sheria, lakini baada ya hapo hakuna hisia zozote zinazo safiri baina yangu na ya mwenzangu. Sasa nini kilo sababisha hayo yote, ndio azimio la hii mada yetu ya leo, sasa kabla ya kuendelea mbele hebu tuzijue kufuli zenyewe halafu huko mbele ndio tutaukuta Ufunguo. Kufuli ya Mwanzo ni ipi?
"ٱلزَّانِى لَا يَنكِحُ إِلَّا زَانِيَةً أَوۡ مُشۡرِكَةً۬ وَٱلزَّانِيَةُ لَا يَنكِحُهَآ إِلَّا زَانٍ أَوۡ مُشۡرِكٌ۬‌ۚ وَحُرِّمَ ذَٲلِكَ عَلَى ٱلۡمُؤۡمِنِينَ"
"Mwanaume mzinifu hafungamani ila na Mwanamke mzinifu au Mwanamke Mshirikina, na Mwanamke mzinifu hafungamani ila na Mwanamme mzinifu au Mshirikina, Na hayo yameharamishwa kwa Waumini(Waislam)"
Sisemi mimi kama mume zini kabla ya kuona au mumemshirikisha Mollah wenu na chochote, lakini nataka kukuonesheni kitu kilofunga Nyoyo zetu yakawa mapenzi hayaingii baada ya huko kufunga ndoa, sababu kubwa ni yale alo haramisha Mollah wako, ambayo sisi tuna yatenda, ikiwa hujapata kuyatenda wewe umeokoka, na kama umefanya basi sasa ushajua na unapata nafasi ya kutubu urejee kwa Mollah wako ili akusamehe apate akushushie hayo mapenzi urudi kama(Ujana)utoto upendane na mwenzio kama ilivokua zamani.
"Anasema Nabii Mussa a.s katika Taurati zinaa ni dhanbi kubwa kabisa, na mwenye kuzini anastahiki auwawe"
"Akasema Nabii Issa a.s katika Injili" Nabii Mussa a.s kakwambieni yoyote yule anofanya tendo la zinaa basi kafanya Dhanbi kubwa, mimi nakwambieni yoyote yule Mwenye kumtizama Mwanamke au Mwanamee kwa Matamanio basi kesha zini"
"Anathibistisha Nabii Muhammad s.a.w katika Quraan na hadith kwa kusema""Nyie waumini angusheni macho yenu chini" msitizame kabisa mmekatazwa.Hao ndio Wajumbe wa Mwenye-enzi-Mungu, wakwanza anasema atofanya(1)wapili kasema atotizama(2)Na kipenzi chetu watatu yeye kasema Msitizame kabisa(3) Sasa ikiwa hufanyi hayo basi wewe uko katika kundi la ngazi ya juu kabisa, lakini ikiwa unatenda hayo basi mimi na wewe hatuvuki katika hiyo aya niloitaja hapo juu na hiyo ndio imekua chanzo ya Mioyo yetu kupigwa kufuli, Vipi inakua nitaelezea kwa urefu-Part-2

No comments:

Post a Comment