Asalaam Aleiykum,
Imekujia habari iumizayo Roho, Unalijua tendo lenye kuangamiza afya ya Mwanaadamu, basi kama huna habari hiyo sasa tega macho upate kufahamu vipi Talaka inavo kuangamiza baina ya muombaji na mtoaji wa hii tunayoita Talaka, Talaka inakuja kwa aina mbili ama kwa njia ya karatasi kama uthibitisho au maneno kuwa tamko, na haya yote yanakwenda (Deep)kwa mtoaji na anaepokea, kama zilivyo nguo au bendera zinavokwenda (Deep)kufahamisha huyu Mwanamme na huyu Mwanamke au bendera hii ya nchi fulani na ile ya nchi fulani.
Sasa hatuwezi kuizungumza Talaka ikiwa kwanza hatujaizungumza Ndoa, Nini Ndoa?(Harusi)Ndoa ni mvutano wa Roho mbili ziloamrishwa na Mollah wao kujiunga kisheria na kuishi katika ada ya maamrisho kama Mke na Mume, Wapi unatokea mvutano huu, Mvutano huu unapatikana pale kwenye tafauti ya kijinsia yaani baina ya mwanamke na mwaname, ili tufahamu kwa njia ya mvutano basi acha niipe jina mwanamme nimwite(Positive)na mwanamke namuita(Nagative) ndio katika aya 14 ya sura ya Imran ambayo nimeizungumza kwa urefu katika mada zilopita ilitaja hivi"زُيِّنَ لِلنَّاسِ حُبُّ ٱلشَّهَوَٲتِ مِنَ ٱلنِّسَآءِ"
"Watu wametiwa Upendo wa kupenda wanawake" na mambo mengine kama inavoendelea aya kueleza, imelazimishwa nafsi katika huo mvuto nilioutaja, wapi linatokea tukio hili, linatokea katika hii ita (Eyes)au (Magnet-field ya Mind)ya mapenzi au kwa jina lengine huu uwanja wa (Hubu-Haba)Ikisha tena mvutano huu unapambwa kwa maua ya shauku na miasumin ya matamanio, hapo tena huanza kutaarishwa njia za halali za kufunga ndoa, ikiwa ndoa hii safi ilobarikiwa na Mwenye-enzi-Mungu basi pale pale inapofungwa Mollah huteremsha mambo yote mawili (Mapenzi na Rehma zake)kwa kuwa tayari wawili nyie mpo kwenye uwanja wa (Hubu-Haba). Na kama kuna mushkeli umepita basi hapo (Mollah)Huteremsha (Rehma) akawa anawasubiri waja wake kama watakua safi katika Muungano huu ili awakamilishie na hiyo sehemu ya pili nayo ni hayo mapenzi.
Sasa kivumbi kinaanzia wapi? kinaanza mwanzo kabisa kwa ushaulivu wa wana ndoa hawa kama harusi ni Muungano na maana ya muungano (The Others to disappear)Mume anakuja na Mama yake kwapani, na Mke anakuja na Mashoga zake kichwani, inaanza ndoa hii na kindumbwe ndumbwe tokea mwanzoni, Ndoa yenyewe ni mkutano wa (Nagative na Positive)ndio maana mkutano huu hayeshi mabishano na magonvi, sikuwa wanachukiana wawili hawa lakini wamekutana viumbe hawa wakiwa tafauti na lazima utegemee kupatikana mikwaruzano ndio maana ya (Positive na Nagative) na wange gundua wawili hawa kama wao wamo kwenye majaribio, na huo upendo upo kwenye
hiyo (Mind-Akili)basi wangetunza na kusubiri upendo huo kuanguka kwenye Moyo, hapo wangepata zawadi kutoka kwa Mollah wao nao ni hayo (Mapenzi).Mollah wako hupeleka mapenzi kwenye Moyo ikapatikana hiyo(Communion) au (Falling in Love)au kwa maana nyengine kuanguka kwenye bonde la Moyo wa Mapenzi.
Ukipata japo tone moja la mapenzi husahau tena raha hizo, au ladha hiyo na ndio maana wazungu wakatoa usemi huu(In memory love live forever)Inaanzia hali hiyo kwenye akili, ikisha inadondoka moyoni na hapa moyoni kuna njia mbili za ku(Test)mapenzi hayo au kuya(Experience)moja ni ile ya mwanamke, yeye ana bahati kwa kuwa ni (Nagative)penzi linapokewa moja kwa moja, au linaanguka haraka moyoni na anakuwa wazi hana hofu kama watu watamjua au watamzungumza, kwa Mwanamme kwa kuwa yeye nini (Positive)anafunga moyo anakua anaonesha kwa hisia na matendo yake yanaonekana kama vile kwa njia za kutoa zawadi na kadhalika, lakini kimsingi yote ni mapenzi, ila wanaume wanaogopa kujulikana kama wanapenda, wana wasiwasi watu watasemaje(Mbona kawezekana,kadhibitiwa), itakua vipi nk,
Sasa wawili hawa wanaishi ndani ya hili penzi kwa siri na dhahiri wakiwa na furaha, vicheko, na kubarikiwa watoto, wakashibana kwa mambo yao kwa upenzi na undugu, Sasa tizama nini kinatokea mmoja wapo akaamua kudai au kutoa Talaka.
Ukitaka kujua mashaka na madhila yanotokea katika hiyo Talaka basi Endelea-Part-2
No comments:
Post a Comment