Friday, February 8, 2013

PIN-NUMBER YA MAPENZI-PART-3

Asalaam Aleiykum,

Sasa hivi bado mko katika misukosuko wengine ndoa zenu zinaninginia vidoleni, sasa yapo matumaini ikiwa mtabadilika kutoka katika kundi moja kwenda kundi jengine ili mpate hayo mapenzi yatokayo kwa Mollah wenu kama inavosema Quraan sura ya Noor aya ya 26,
"ٱلۡخَبِيثَـٰتُ لِلۡخَبِيثِينَ وَٱلۡخَبِيثُونَ لِلۡخَبِيثَـٰتِ‌ۖ وَٱلطَّيِّبَـٰتُ لِلطَّيِّبِينَ وَٱلطَّيِّبُونَ لِلطَّيِّبَـٰتِ‌ۚ أُوْلَـٰٓٮِٕكَ "مُبَرَّءُونَ مِمَّا يَقُولُونَ‌ۖ لَهُم مَّغۡفِرَةٌ۬ وَرِزۡقٌ۬ ڪَرِيمٌ۬ 
"Wanawake wabaya(ni kwa)wanaume wabaya, na Wanaume wabaya (ni kwa)Wanawake wabaya,(Na kwa)Wanawake wema (ni kwa)Wanaume wema, Na Wanaume wema(ni kwa)Wanawake wema, hao wameepushwa na hayo wanayoyasema, wao watapata misamaha na riziki iliyo  Njema".
Kwanini aya ikaanza kwa kuwataja Wanawake, sababu kubwa Mume ni mwenye kufata, ndio maana utaona matangazo yote yamejaa Wanawake, ikiwa Mke ataanza kubadilika basi Mume atafatia, kwa sababu Mke ni kishawishi kikubwa cha kuweza kumfanya Mume ale tunda la mapenzi, mwanzo kabisa mnatakiwa mubadilike kutoka katika huo ubaya mlokua nao hivi sasa muanze kuwa waja wema, nini kitatokezea juu yenu mkibadilika, inatakiwa kitu kimoja tu Kubadilika, Mwenye-enzi-Mungu anatoa ahadi kwanza ya kukusameheni yale yalopita mwanzoni, ikisha atakupeni Riziki iliyo njema, ndani ya riziki na Mapenzi pia yamo yanaingia katika kiwiliwili chako kama kinavo ingia chakula.
Sasa vipi mabadiliko haya yatokee, inabidi upate huo ufunguo au hiyo (Pin-Number)na hakuna ufunguo utaoupata ila kurudi katika nafsi yako, rejea ndani ukaanze kuchakua chakua uyatupe (Mafaili)ya zamani, Safisha kifua chako kwa kuanza kuona hakuna mwanamke mzuri kama Mke wangu au Mume wangu, ona vyote vya nje kama milango tu isokua na funguo, au makabati yalotupwa, anza mazoezi yakutilia Mti wako wa mapenzi mbolea, panda mbegu huku una subiri kwa kupalilia, basi anza kwa kuanza kuchukia vilo nje, kila ukitaka kushughulika na vilo nje kumbuka pesa zako, kumbuka masikini mke wangu yupo nyumbani anasubiri hana hata haja ya pesa au mali yangu, halafu tanabahi hawa wa nje jee nikiwa mgonjwa watanipigia hata simu hawa, geuza muelekeo wako nyumbani anza kufanya shughuli za nyumbani pamoja na mkeo, kama husimamishi Sala, basi mfanyie (Surprise)ya kutaka kumsalisha, msikae mkasubiri (Valantine)kwani ishara na mbolea za Mapenzi ni vitu vile mnavopandisha kila siku, huku mkisubiri (Mche)uchomoze, Na nakwambia kwa yakini (Mche)utachomoza haziwi ahadi za Mollah wako zikapita bila ya kutekelezwa.
Badilika wewe wala usione haya chukua watoto uwakogeshe kama mnao, na kama hakuna basi mwambie Mkeo leo Bibie nakukogesha mie, ikisha nitakukata kucha, halafu nitakuchana nywele tukimaliza..Alaa mfanye nini, mwambie avae nguo mwende kwenye ufukwe wa Bahari mkatizame Mbaa mwezi, hivyo ndio inavotakiwa   
kutendeana wana ndoa, Na mwanamke pia jaribu kubadilika, anza na jiko lako isiwe siku zote wali, akichelewa Mume jilize kikweli kweli umwambie umemiss, sio akigeuza kichwa unamzomea, huyo Mumeo na Mume kama (Mtoto-mdogo)anataka kudekezwa ndio maana wanaume wanapenda kutafuta Mke alofanana na Tabia za mamake, basi na wewe Mtoto wa kike zichunguze Tabia za mamake zikoje halafu anza kuziiga utaona hivi Mume anakupenda na Mama mkwe wote wanakupenda, lakini usifanye kwa uongo, itakua unajidanganya nafsi yako na ya mwenzio, na hapo utakua hujabadilika,Fanya kila siku mambo mepya mepya weka siku maalumu na umwambie Mumeo leo usitoke mume wangu siku ya kukata kucha, na ukiambiwa siku ya kukata kucha isiwe unatoka na shoka ili ummalize haraka, kinachotakiwa unakata kidole kimoja unakwenda kuleta mshikaki,unakata cha pili unaleta juice, unakata cha tatu unaleta kitu unacho kijua mwenyewe huku umevaa kengele(Mapambo yako)na utizame kama paka shume atatoka, mapenzi yanakuja kwa njia ya (Surprise)na wewe anza mazoezi ya kushitukiza.Endelea-Part-4

No comments:

Post a Comment