Asalaam Aleiykum,
Aya ya 11 inasema " وَجَعَلۡنَا ٱلنَّہَارَ مَعَاشً۬ا"
"Na tukaujaalia Mchana kama kufufuka",
Ikiwa umesoma uzuri habari ya usingizi basi utayarejea yale maneno nilosema unakua huna(Control)Amri ya kufanya jambo lolote, mara ghafla kwa kuamka huku inakuja ile (Idhini)amri ya uhai na hapo kila kinacho ishi kina nyanyuka na viungo vyote kuanza kufanya kazi, na wale walohukumiwa Umauti uwafike ndio wanabakia katika hali ile ile kila ukiwaamsha hawakujibu na wao hapo wako wakisubiri Amri nyengine za Mollah wao zifatie.
Na aogope mtu isije ikamkuta hali kama hii na yeye hajatoa shukrani kwa Mollah wake, ndio maana ukiamka unashughulika na kazi zako na unamsahau Muumba wako unakua huna nafasi hata dakika tano ya kumkumbuka.
Tahadhari sana ya kughafilika na yule alo kukirim Uhai huu, unaipitisha siku hata bila ya kusema(Alhamdulillah). Unatakiwa uwe mnyenyekevu shukurani yako lazima iwe ya dhati kwa kusema Mollah wangu umenipa Uhai huu nakushukuru Mollah wangu, Mimi naanguka katika Ufalme wako nikiridhia kwa Mapenzi yako Mollah wangu umenipa siku nyengine ili nipate kukushukuru wewe, wewe ndie ulonijaalia Afya Mollah wangu, basi hata ukiamua kunipa Maradhi mimi nitakua mwenye kuridhia, basi mie leo nachukua ahadi ya kuonesha shukurani zangu kwako kwa kujifunga na kujizuia na maasi yote kwa siku hii ya leo, kwa ajili ya zawadi hii ya Uhai nachukua Ahadi ya siku hii ya leo kufanya mema matupu, kutokana na Imani yangu kama ulivonipa Uhai huu, basi naamini kiyama kipo, na siku hiyo Mollah wangu nataraji Rehma zako zinilinde mimi na misukosuko ya siku hiyo.
Aya ya 12 inasema " وَبَنَيۡنَا فَوۡقَكُمۡ سَبۡعً۬ا شِدَادً۬ا "
"Tukajenga juu yenu (Mbingu)saba madhubuti"
Habari hii ya Mbingu saba utaipata wakati utakapokua Mja (Swalihina)utafunguliwa siri hizo za kuwapo kwa mbingu saba wakati itakapo julikana kwa dhati kuwa umejitupa kwa Mollah wako na umefungamana na yeye, sio kwa sasa unakesha ili upate kujua siri ya mambo ikisha uwe Mganga, zipo mbingu saba kama zilivo ardhi zenye (Layers)saba, wanasema pia wana historia mpaka bahari zilikua saba.
Aya ya 13 inasema "وَجَعَلۡنَا سِرَاجً۬ا وَهَّاجً۬ا"
"Na Tukaijaalia taa inga'rayo na yenye joto kubwa"
Ikisha tukajaalia taa hii yenye kutoa muanga wa joto, imetajwa kwa dasturi ya jaala sababu usiku linakua haipo inaondoka, hata hivyo jua linachangia sehemu kubwa ya maisha katika dunia hii tunoishi, Jua linatupa hii nuru ya mchana, kama ilivyotajwa katika aya ya 61 ya sura ya (Muumin)jua linatupa (Special-Energy)maalumu ambayo sisi wanaadamu hatuna uwezo wa kuipata moja kwa moja kutoka kwenye jua kwa hiyo inaingia kwenye majani na mimea na wanyama sisi tunaipata kutokea katika vitu hivyo.
Aya ya 14 inasema " وَأَنزَلۡنَا مِنَ ٱلۡمُعۡصِرَٲتِ مَآءً۬ ثَجَّاجً۬ا"
"Na tukateremsha maji yaangukayo kwa kasi kutoka mawinguni"
Aya ya 15 inasema "لِّنُخۡرِجَ بِهِۦ حَبًّ۬ا وَنَبَاتً۬ا "
"Ili tupate tuoteshe chembe chembe na mimea"
Aya ya 16 inasema " وَجَنَّـٰتٍ أَلۡفَافًا"
"Na Mabustani yenye miti iliyosongana"
Naam Ametumiliki Mollah wetu kwa kila jambo, yeye ndie mwenye kutupa Uhai, akautunza na kuurutubisha Miili yetu kwa riziki anazo tutolea katika ardhi hii, akatupa afya kutokana na hiyo riziki, akatufanyia na ladha za kila aina kutokana na vyakula hivyo, iwapi leo shukurani yetu kwa Mollah alotupa huu Uhai, akatumiliki kwa kutupa pumzi zake, akatuenzi kwa kila jema katika Ulimwengu huu, ziko wapi shukurani zetu, wakati kuanzia usingizi, mpaka chakula chetu, kazi zetu, furaha zetu, zoote zinamtegemea yeye, Mara ngapi umekula ukasema (Bismillah)na kumbuka lini ulimaliza kula ukasema (Alhamdulillah) kumbuka yeye ndie alo kutolea hiyo Riziki kutoka katika hiyo Ardhi, kwa hiyo mpaka hicho chakula unokula ni Ibada. Mollah wetu tusamehe kwa sahau zetu na upungufu wa shukurani juu yako, tupe faraja yako ya kupata kivuli chako siku hiyo Adhimu tusoijua muda wake, ikisha tuepushe na adhabu zako kubwa na ndogo, na utupe makaazi katika ufalme wako wenye kumiliki Pepo. Amin
No comments:
Post a Comment