Friday, February 8, 2013

PIN-NUMBER YA MAPENZI-PART-4

Asalaam Aleiykum,

Najua hakuna jambo gumu kama kubadilika, ni shida kubwa wakati tulo nao kupalilia mti wetu wa mapenzi, Uzito huu unatokana na (Viburi)vilotawala nafsi zetu, basi ikiwa hilo ndio tatizo letu inapaswa mtu aangalie mambo haya nitakayoyataja kabla ya kuoa au ikiwa kashaolewa pia anaweza kuyaangalia mambo haya ili apate kujirekibisha nayo,(1)katika mambo ambayo pengine laweza kukuvunja moyo ukawa hutaki kutia mbolea labda(Physical attraction)Umbile,mwenzio kabadilika (Mahanjumati)yamnenepesha au humpi chakula kakonda sana, tizama pengine hilo ndio linalo kufanya kutwa ukimbilie nje(2)Au swala la mchanganyiko wa kidini hamkutani katika shughuli hizo, basi hapo panataka marekebisho,(3)Katika medani ya (Akili)labda hamko sawa katika daraja za hekima, hapo panatakiwa maelewano,(4)Mambo ya vivazi na tabia za maingiliano katika jamii, pengine mmoja kati yenu hakuridhishi lakini wewe umekaa kimya hutaki kumwambia,(5)Pengine mwenzio ni mwenye kupenda mambo ya kifahari na kujifagharisha, hayo yanatakiwa muyazungumze,(6)Huruma za kupenda watu na Familia zenu kwa jumla, hilo pia lataka kushughulikiwa,(7)Na makutano yenu (Kiroho)vipi mumekamatana katika nafsi, kwenye Roho jee mwenzio yumo Rohoni na alama ya mwanzo katika hili la Roho jee una muheshimu, ikiwa una muheshimu mwenzio ukamfanya Rafiki yako, mshauri wako wa mambo yako yote, basi hapo ushaanza kuufungua Moyo wako, ushaanza kuijua (Pin-Number).
Lazima Mke na Mume wawe na dhumuni moja kama vile misimamo ya kidini au kusomesha watoto au maisha yao kwa ujumla isiwe mmoja ana (Agenda)za siri, hapo Penzi haliwezi kuteremka.
Mke na Mume lazima waungane kikamilifu kiroho na asiingie yoyote akaja kukaa baina yao, vipi utafanya hivyo ni pale ambapo baada ya kujisafisha na kubadilika kabla ya mapenzi linateremka jambo la kukukurubisheni wawili nyie(Magnetism)na hili ni lile jambo linalotokea kabla ya kitendo kama vile ukitaka chai, hutoka uamuzi wa kuichemsha na kuitia kikombeni na kuanza kunywa, hicho ndio kivutio au hamu, na baina ya Mke na Mume pia inapatikana hali kama hiyo na unaweza kuijua ikiwa unatizama mambo kwa uangalifu, hebu ukikaa mwenzio hakutizami wewe mtizame kwa jicho la Mapenzi, anza zoezi hilo utaona mabadiliko yake, fanya japo kwa siku tupa dakika kumi za kumtizama tu mwenzio, basi kidogo kidogo utaona anaaza kukujaa moyoni, sio kama sasa hivi jiulize lini mara ya mwisho umemuangalia mwenzio, na nikisema muangalie ni tafauti na kumtizama, kumuangalia uwe huna fikra zozote ndani ya mawazo yako, iwe hususia unamtizama Mkeo au Mumeo pasi  na chochote kujipenyeza kupita kati, hapo utaona huna haja ya kusubiri (Valantine)kila siku kwako itakua siku ya mapenzi, kila ukiamka unatilia mbolea mpya mti wako wa moyoni, na ukitoa vitu vyote moyoni ukawacha mweupe haikai fisadi yoyote kwa mara ya mwanzo inakua ushafungua hiyo kufuli na  penzi litaanza kupenya, Na kwanini penzi lisipenye wakati nyie wenyewe mapenzi matupu, ndio maana kwa kitendo chenu cha Ndoa mkikutana kwa shauku na Mapenzi Mollah anakupeni zawadi ya Mtoto ikisha mnakua mnampenda mtoto wenu, basi kama inaweza kutokea hivyo kwanini isitokee kwa wawili nyie.
Na ikitokea hali ya Mapenzi hakuna atoweza kuhadithia, ukimpenda Mumeo au Mkeo unakua kama (Laila na Majnu)akitokea mwanamke yoyote unataka awe kama (Laila) na ukiwa mwanamke akitokea mwanamme unataka awe kama (Majnu)Na hapo tena inakua umeshaonja kitu kilotokea kwa Mollah wako hata kikiondoka midamu ushaonja ladha haikwishi daima, na inayobaki ni Rehma ambayo haiondoki Milele, Nakushauri onja japo kidogo ladha ya Mapenzi itokayo kwa Mollah wako, na wewe utakua mtu mwengine kabisa, utapenda watoto wako, utapenda familia yako, utapenda hata wapita njia kwa kuonja japo kidogo Mapenzi yalotoka kwa Mollah wako, lakini lazima upate ladha hiyo ya mapenzi ndio utaweza kujua nini Mapenzi, lakini kwa sasa hivi yatizame hayo unayoita mapenzi yana nia gani nyuma yake, ukimpa mtu zawadi unataka malipo, mpaka nyumbani ukijchekesha Mke anajua huyo anataka nini, mapenzi hayana (Motive)ukitoa hutaraji malipo, na mwenye mapenzi ya kweli hakumbuki hata kulipwa yeye kila akitoa anataka atoe zaidi, na kila ukifanya zaidi malipo yake yanaongezeka kutokana na sheria za Ulimwengu huu,"Enyi Wanaume"Kumbukeni yale maneno ya yule Mshairi  Maarufu wa(Kiarabu)""Aliposema""Nilipogundua mimi kwamba katika huu moyo wangu anaweza kukaa asiyekua wewe Mollah wangu""Nilifanya jitihada za kuujaza uongofu wako hata akawa hakai asiyekuwa wewe""Sasa na wewe anza kupunguza mambo yalojaa katika moyo wako""Anza kupunguza kupenda wanawake wa nje""Acha kutizama vifua vya watu ikawa vidani vyote unavijua wewe""Hii mpaka rangi za kucha wewe ndio (Expert)unajua mpaka (Style)za nyusi hayo yote hayafai na yanakuzuia kupata zawadi ya mapenzi kutoka kwa Mollah wako, safisha Moyo ili mapenzi yaingie.  Namalizia kwa hadith hii ili iwe fundisho kwa ndugu zetu wa kike wasione wanaonewa au hawatopata kitu katika malipo yatokayo kwa Mollah wao, nini watapata?
Anahadithia  (Bayhaqi katika Sha'b)"Sayyidah Asmah bint Yazid Ansariyyah r.anha""Alikwenda kwa Mtume s.a.w akiwa kakaa na masahaba zake"Akasema nimekuja kama Mjumbe wa wanawake wenzangu, ambao hakuna mwanamke wa mashariki wala magharibi anajua kuja kwangu hapa, na hakuna yoyote yule alosikia haya ninayotaka kukuuliza, lakini wote wana shauku  na maoni ya jambo hili, tumeamini ulokuja nayo Bwana Mtume s.a.w,"Sisi wanawake tumefungiwa majumbani kwetu, na tumo kuwatimizia wanaume haja zao, sisi tunachukua mimba na kuzaa kwa shida, wakati wanaume wao wamepewa zawadi ya kusali Sala ya Ijumaa, wanakwenda kuwatizama wagonjwa, wanahudhuria mazishi, wanakwenda Hijja watakavo, wanapigana Jihad, sisi tumebakia nyumbani tunalinda majumba yao huku tukilea watoto, vipi tutakuwa sawa katika mgawanyo wa hayo malipo kutoka kwa Mollah wetu""Bwana Mtume s.a.w akawageukia Masahaba na kuwaambia mesikia swali la mwanamke huyu, akasema hakuna swali zuri katika dini kama hili""Wakajibu masahaba hatujui kwamba wana habari kama hizi katika dini""Akasema Bwana Mtume s.a.w "" Nenda kawaambie wanawake wote, wenye kuwafanyia mazuri waume zao, wakawaweka katika hali ya furaha, na kuwaridhia, basi na wao(Malipo)yao yatakuwa sawa na yale yote wayafanyayo wanaume""Akaondoka yule Bibi na Takbir na Tahlil(Allahu Akbar)(Laa-Illah-Illah-Allah).
Nakutakieni Maisha ya kheri na Ukarim wa Mapenzi yatokayo kwa Mollah, Muishi katika ndoa zenu kwa mapenzi makubwa na kila mmoja amsamehe mwenzie atakapo mkosea, ikisha kwa pamoja mgeuke kuwa waja wema:Ogopeni kupigwa bakora ya Mollah wenu kwa kuzivunja ndoa zenu, na mkaja kuzeeka mpaka ikawa Mtu anaishi peke yake hata hapati mtu wa kumpa Maji, Mollah wetu tuepushe na hayo Amin.

No comments:

Post a Comment