Asalaam Aleiykum,
Mwanzo kabisa tunapokewa katika kisiwa hiki na maneno mazito yaliyomo katika sura ya (An-Naba)aya ya 6 " أَلَمۡ نَجۡعَلِ ٱلۡأَرۡضَ مِهَـٰدً۬ا "
"Kwani hatukuifanya Ardhi kama tandiko"
Hebu tumtizame Mwenyewe (Muumba)wa huu Ulimwengu anatwambia nini kuhusiana na hii ardhi, Amesema Muumba wa Mbingu na Ardhi "tumeijaalia hii Ardhi kama Tandiko(Tambarare)(Tectonic-Plate) Ikisha 7 "وَٱلۡجِبَالَ أَوۡتَادً۬ا"Na Milima kama vigingi, Mizani ya kuweka hiyo (Balance)Basi ikiwa imewezwa kutengenezwa kwa hali hiyo, na kubomolewa vile vile inawezekana, ndio maana zikitingishika kidogo hizo sahani Ulimwengu mzima unapata habari.
Hapa itabidi nitoe mfano wa (Tandiko)lenyewe lilivyo na hakuna mfano mzuri kama ile sehemu ninayo fahamu Zanzibar na Tanganyika ikiwa Maji ya Bahari yataondoshwa ghafla basi utaikuta Ardhi ni moja (Tambarare)Lakini kwa Hekima za Muumba kazitenganisha Nchi hizi Mbili kwa kupitisha Maji baina yake kwa hivyo haiwezekani kuwa nchi moja, labda yaondoke maji, kwa hiyo ukizungumzia Muungano wa Nchi hizi mbili yaani(Union)haiwezekani kwa sababu ndani ya nadharia ya wazawa wa nchi hizi mbili kuna kitu(Imprinted)cha tafauti ya kuwa hii ni Zanzibar na hii ni Tanganyika, lakini linalowezekana ni Muungo yaani (Unity)kama vile kwa usafiri wa Meli au lijengwe (Bridge).
Hiyo ni Ardhi sasa wacha tumguse yule aloumbwa kutokana na hiyo Ardhi.
Nimesema katika darsa za nyuma na leo nasema tena Jaala maana yake ni tendo lenye kawaida za athari ya mabadiliko, nimesema hivyo kuonesha aya hii ya 8 ya sura hiyo hiyo haikutiwa jaala ila imesemwa " وَخَلَقۡنَـٰكُمۡ أَزۡوَٲجً۬ا"
"Na tukakuumbeni wanaume na wanawake"
Haina haja tena ukafanya mageuzi au operesheni ili ujigeuze vengine, kama una hisia za kike na wewe ni mwanamme basi Shukuru Mollah wako ndio alokuumba na kataka uwe hivyo, basi kubali uridhie umbile lako wala huna haja ya kujificha, kama unakwenda ukatikisika mabega nenda huku umeridhika, kama una sauti nyembamba sawa ndio sauti yako hiyo na huwezi kuibadilisha, waeleze ndugu zako, marafiki zako mimi hivi ndivo nilivo nikipunga mkono msishangae ndio umbile langu Mollah alonijaalia siwezi kuwa vengine, ila ujue kinacho katazwa ni kutenda Maasi na kujishuhubisha kwa kusudi, ukawa kama mwanamke kwa mavazi au operesheni au kujipamba hilo ni kosa. Na wanawake hali kadhalika ikiwa una hisia za kiume sio kosa Mollah wako ndivo alivokuumba usipite ukajificha wajulishe wenzio ili wapate kukubali na kukuelewa ili wasije kupita wakasema hivi na vile pia tambua hilo ndilo umbo Mollah wako alotaka uwe na kakuumba wewe(Unique)hakuna kama wewe wala hatomuumba mwengine kama wewe, tambua Mollah wako kakuumba wewe(Perfect)huna makosa kabisa toa shukrani kwa Mollah wako kwa kukupa Uhai kwa mapenzi yake, Ikiwa mbaya shukuru, na ukiwa mzuri pia shukuru, elewa na wewe ni kiumbe chake anakupenda kama anavo wapenda viumbe vyengine. Endelea part 3 upate habari ya usingizi.
No comments:
Post a Comment