Asalaam Aleiykum,
Sasa inakuaje haya mambo ya kufuli mwanzo wake unakua wapi? kinapatikana chanzo kikubwa cha kufuli hii pale Mtu anapotaka kuoa au kuolewa au hata baada ya ndoa, na chanzo chenyewe inakua pengine unakwenda kuposa Nyumba fulani, lakini unampenda mtu fulani mwengine kabisa asokua yule, au na yeye anapendana na mtu mwengine kabisa, wawili nyie mnakutana mwanzo wenu umeshakua na mashaka makubwa, Eleweni Mollah wenu ni mwenye kujua kila jambo na hilo pia analo taarifa nalo na pahala hapo katika nyoyo hizo mbili hapawezi kuteremka Mapenzi abadan, itakua mnakaa kutizamana kasoro, mmeshaingia nyinyi na dosari ya uzinifu ima iwe aliotaja Nabii Mussa a.s au Nabii Isa a.s moja wapo katika hizo mshazibeba mnaingia nazo katika ndoa na mnaishi nazo bila ya kutubu, Mtakuta ndani ya nyumba hamna furaha, hamna mapenzi, ndani ya nyumba kila mmoja sasa anaanza kunyanyua macho yake juu, hapo tena Mnaanza kumpinga Mtume Muhammad s.a.w, Mnazidisha kufuli, mpaka inafikia Mume katoka mke hana habari au mke karudi mume hayupo, inakua kama watu wawili walopanga nyumba pamoja.
Yanazidi mambo haya katika nyumba ya ndoa mpaka baada ya kuishi ndani ya nyumba watu wawili mke na mume sasa mnaishi watu wanne,(kama nyinyi vijana wa siku hizi)Mume anampenda(Actress)Priyanka, na Mke anampenda(Actor)Rishi Kroshan, au Kama watu wazima kama sisi tena ndio bado umezama kwa Dharmendra na Hema malini, inakua hata mkikutana nyinyi wenyewe inabidi mzime taa ili (Ma-Actor's)wapate kutawala,umemkamata mke lakini mawazo yote yapo kwa hao(Ma-Actor's) hiyo ndio hali iliyomo majumbani, vipi leo yataingia mapenzi wakati anaingia Mume katika Moyo umejaa vimada,wanawake wote wa mjini unatamani wewe, katika moyo zimejaa biashara na faida, vipi yataingia Mapenzi Mke kajaza Ma-handsome kichwani kwake,Wivu umo humo, magonvi yamo humo, wewe huna nafasi ya kumuachia Mwenye-enzi-Mungu kukumiminia mapenzi yake katika moyo wako, umeutia mwenyewe kufuli na hutaki kuufungua, huwezi kukaa hata dakika tano na mkeo ima utataka iwashwe TV au ujibabaishe kwa hichi na kile, na mwanamke hali kadhalika tena kama anazungumza na simu anamwambia shoga yake hilo linaingia tutazungumza baadae, vipi yatapatikana Mapenzi kwa hali hiyo.
Ndio maana utaona kutokana na mti huo wa chuki mlopanda mnashindwa hata kupenda watoto wakizaliwa, utaona mara mume huyo kakimbia hataki kusidia hata watoto, Na hii inatokana pengine na yeye hakutendewa hayo(Hili darsa yake nyengine)lakini alama zote zinaonekana mapema kama humpendi mumeo au mkeo taabu sana kuwapenda watoto, utaishi nao, ndio watoto wako lakini mapenzi hakuna, jiulize wewe mwenyewe unawapenda au mazoea tu, hivi ndivo wengi wetu tulivo, tunaishi bila ya mapenzi kutokana na makosa yetu wenyewe, tunaikosa zawadi hii ya Mollah wetu adhimu ambayo ukiipata umo furahani, na mfano wake kama Afya na Maradhi, unaona wakati ukipewa Maradhi unakua katika hali gani, na wakati utakapopewa mapenzi umpende mkeo au mumeo utakua na hali gani, ikiwa mtu anajenga jumba kwa mapenzi ya mwanamke wa nje, nini habari yako wewe ikiwa unatenda hivyo kwa njia ya halali ya kumjengea mkeo au mumeo, sasa ufanye nini kuufungua huu moyo kwa hiyo (Pin-Number) endelea Part-3
No comments:
Post a Comment