Asalaam Aleiykum,
Aya ya 31 sura ya kahf "أُوْلَـٰٓٮِٕكَ لَهُمۡ جَنَّـٰتُ عَدۡنٍ۬ تَجۡرِى مِن تَحۡتِہِمُ ٱلۡأَنۡہَـٰرُ يُحَلَّوۡنَ فِيہَا مِنۡ أَسَاوِرَ مِن ذَهَبٍ۬ وَيَلۡبَسُونَ ثِيَابًا خُضۡرً۬ا مِّن سُندُسٍ۬ وَإِسۡتَبۡرَقٍ۬ مُّتَّكِـِٔينَ فِيہَا عَلَى ٱلۡأَرَآٮِٕكِۚ نِعۡمَ ٱلثَّوَابُ وَحَسُنَتۡ مُرۡتَفَقً۬"
"Hao watapata mabustani ya Milele yanayopita mito(Maji)mbele yake, humo watapambwa kwa mavazi ya mikononi ya dhahabu na WATAVAA NGUO ZA KIJANI ZA HARIRI LAINI na za hariri nzito, wanaegemea humo juu ya vitanda vilivyopambwa, ni malipo mazuri yalioje hayo, na mahali pazuri palipoje hapo(pa Kupumzika)"
Umepata kujiuliza kwa nini Bendera au (Symbol)ya Kiislam ikawa kijani? Kwanini Bwana Mtume s.a.w akatuchagulia kijani na nyeupe ndio kuwa alama yetu?
Sababu kubwa ya mwanzo kijani ni (Nature) ya Ulimwengu huu na ndani ya Quraan imetajwa mara nyingi mahusiano ya rangi ya kijani na Ulimwengu huu, na wewe mwenyewe ukizunguka kila pahala utaona vipi unaishi ndani ya mazingira ya rangi ya kijani, (Mfano)kama mimea, miti na kadhalika, Na la pili mpaka wewe mwenyewe kama utapigwa ngumi na damu ikivilia basi unageuka rangi ya kijani, Na jambo la tatu kijani ni rangi inochukua (Light)au Nuru kwa urahisi ndio maana zikachanganywa rangi mbili hizi za nyeupe(Nuru)na kijani ili zende sambamba katika dini hii ya haki ili iwe (Alama)ya kiislam.
Sasa nini Kijani? Kijani kwa maana ya (Deep)ndani kabisa ina sifa mbili kwanza kijani ni (Active)kama unavoona maumbile yalivo kama pepo likivuma miti na majani inavo peperuka kwa kasi kubwa, halafu tena sifa ya pili ni (Calm)kupatikana utulivu wakati hakuna upepo au mvua nk, hiyo ndio sifa ya (Nature) na hivyo ndio Bwana Mtume s.a.w akatuchagulia Rangi yetu iwe ya kijani, tuhusiane na Ulimwengu, tuwe (Active)tusikubali uzembe, tusikubali kuonewa, ikisha tuwe (Calm)pale mambo yanapokua mazuri yametulia, hakuna uonevu au msukosuko wowote tukae kama Ulimwengu ulivyo, unakwenda pasi na matatizo yoyote, ndio maana hata utaona ndugu zetu Wanawake wanapenda kuvaa rangi hii wakati wa sherehe zao za harusi, Na utaona vipi huyo wanomvika nguo hiyo anavo funguka kwenye(Light)kutokana na uwezo wa rangi hiyo kuimeza taa(Light).
Nini Rangi Nyeupe? Nyeupe ni (Light)Nuru, Na kwenye Nuru unapatikana Muangaza na kwenye muangaza watu wote wanaona na watu wakionana inapatikana salama, kwa hiyo nyeupe ni Rangi ya Salama, Nyeupe Rangi ya Amani, Nyeupe Rangi ya (Surrender)Nyeupe ni (Islam)ndani ya nyeupe kila mtu anavutika, kila mtu anatamani aje karibu na nyeupe na siri ya nyeupe yakwamba imekusanya rangi zote ndio ikawa nyeupe, nyeupe ndio Uislam ulokusanya kila rangi mtu awe mweusi,cholate,mweupe wote mko katika Rangi moja ya weupe ambayo ndio rangi ya Nuru, tunamuomba Mollah atuongoze kwenye Nuru yake. Kwa hiyo ukichanganya Rangi mbili hizo za Kijani na Nyeupe unapata mambo haya matatu (Active+Calm+Peace)hiyo ndio Bendera ya Kiislam, hizo ndio Rangi zako Bwana Mtume s.a.w alizo kuchagulia ushikamane nazo, lakini hatari kubwa inapatikana pale ukichanganya kijani na rangi nyengine, kama vile ukaja kuchanganya na rangi yenye kuashiria Maradhi yaani Rangi ya Manjano, utaona matatizo yanavopatikana kwenye mkusanyo wa Rangi mbili hizo, kwa hiyo ndugu zangu muwe makini sana katika uchaguzi wa rangi zenu, pateni maana za rangi mzijue ili yasikufikeni matatizo sababu ikawa uchaguzi mbovu wa Rangi, Nakuomba Mollah wangu tujulishe yenye manufaa na sisi japo kwa uchache: Amin.
No comments:
Post a Comment