Asalaam Aleiykum,
tuitizame aya ya 9 ya sura ya Nabaa inasemaje kuhusu kadhia hii ya usingizi "وَجَعَلۡنَا نَوۡمَكُمۡ سُبَاتً۬ا "
"Na tukaufanya usingizi wenu kama kufa".
Tukaujaalia huu usingizi kama kufa, hapa Sheikh Ali Muhsin Al-Barwan, yeye kauzungumza usingizi kwa ufasaha katika Tarjma aliyoifanya ya kiswahili ya Quraan Tukufu, kaizungumza aya hii kwa njia ya sayansi, akaeleza vipi Mwili unavopumzika katika tendo hili la usingizi, vipi viungo vinatulia baada ya harakati za mchana kutwa, maelezo hayo yamekita katika Sayansi ya (Outer-Observation)leo mimi nataka nigusie (Inner-Observation)kwa njia ya ndani, sio uhadithiwe ila wewe mwenyewe uwe shahidi wa tukio hilo la usingizi, upate kujua nikifa itakua vipi, (kwa sababu imetajwa kama kufa) Lakini kabla ya kwenda huko nataka nitoe tahadhari asije mtu akataka kujaribu mafunzo haya wakati yuko peke yake bila ya kuwa na mtu anaefahamu taaluma hii.
Lazima upate mtu akuongoze ili likitokea tatizo aweze kukusaidia, usije kuvamia majaribio haya unaweza kupoteza uhai au kuharibika akili kutokana na mambo yenyewe yanavotisha.
Sasa vipi huo mfano wa usingizi unavokua kama kufa, siku zote tukilala usingizi unakuja kutukuta (Unconscious)hatuna fahamu, mara moja moja unapata bahati yakua (Conscious)lakini unakua unaogopa, na unadhani Majini au Shetani yanataka kukuvaa kumbe ni usingizi lakini kwa ile khofu unajitupa kwenye (Unconscious)na usingizi unafanya kazi zake, lakini nini kitatokea ikiwa utakua kidume cha kweli ukaweza kuwa (Conscious)wakati usingizi unakuvaa, basi hapo utaona mambo ya ajabu yanakutokezea, utaona mwili wako umelala na wewe una ushuhudia kama vile umuonavyo (Maiti) katika hali hiyo ya ushuhuda unaondoshewa uwezo hata wa kunyanyua kidole unakua(Umepooza)kikamilifu.
Hapo tena unajua tafauti ya kuwa (Hai) na (Kufa)inavokua, na kama utaweza kuendelea kuwa shujaa ukaendelea kukaa katika hali hiyo ya Ushuhuda mpaka ingiapo alfajiri, utaona umerejeshewa ile hali ya kujimudu unapata(ability)ya kunyanyua viungo na kuweza kunyanyuka, na hapo tena kila kilicholala kinakurupuka na wewe unakua ushapata kujua na kuuona usingizi na kadhia yake, kuanzia hapo tena kulala kwako kutakuwa tafauti mpaka siku yako utakayo fariki au kuaga dunia na hapo utakua umepata siri ya usingizi unajua kumbe usingizi unaonekana kama vile unavoonekana usiku na mchana, na unakua na yakini ya kusimama kiyama na kuanzia hapo kila jambo lako linakua la shukurani.huo ndio usingizi unavoweza kuonekana.
Sasa ni Habari ya Usiku,
Usiku ni (Absence of Light) au Giza ni muondoko wa taa, kama utafunga macho yako sasa hivi, basi unaweza kuisali Sala ya Isha wakati wa Adhuhuri, aya ya 10 ya sura hii tulonayo inasema,
"وَجَعَلۡنَا ٱلَّيۡلَ لِبَاسً۬ا"
"Tukaujaalia Usiku (Kuwa kama)Guo"
Inakuaje ikawa kama Guo, umetoka mfano huu ili upate kujua kuwa hili giza(Usiku)ni (Nature)ya huu Ulimwengu, Na sisi na hii dunia yetu tunapita(Tunavaa) kwa mzunguko wa hii dunia yetu, tunapita katika hilo Giza ikisha tunatoka ndio ikawa mfano wake kama tunalivaa na kulivua, Yamefanywa haya ili mpate kupumzika kama ilivyotajwa katika aya ya 61 sura ya(Muumin) Hakuna jitihada zenye malipo mazuri kama ukifanya juhudi ukaona vipi huu usiku unavo ingia na kutuvaa, na ikisha ukaamka mapema uka shuhudia tena Usiku unavo vuliwa. Ukiyaona hayo utaomba Mollah wangu nijaalie niwe katika kundi la wale watoao shukurani kila huu usiku unapoingia na kutoka. Kutaka kuujua Mchana Endelea part-4
No comments:
Post a Comment