Asalaam Aleiykum
Sura ya Muzammil aya ya Mwanzo kuna baadhi ya watu wanashikilia kuwa kakusudiwa Mtume pekee, sio hivyo Quraan imekuja kwa ajili ya Viumbe na mafundisho yote yanatuhusu na sisi.
"ـٰٓأَيُّہَا ٱلۡمُزَّمِّلُ""Ewe Uliyejifunika maguo"
Hapa imekua uzuri hakutajwa mtu kwa jina ingekua aya hii imefungika kabisa, na kama imewachwa wazi basi sote tunaingia kwa kuwa tuna tabia ya kujifunika maguo tunapolala, kama hujapata shuka japo kanga na hata kama kuna joto, sasa unaambiwa
قُمِ ٱلَّيۡلَ إِلَّا قَلِيلاً۬""Simama usiku (Kucha kufanya Ibada)ila muda mdogo(Tu ndio Ulale)
Kwanini ikawa hivyo, kwanza kabisa kuambiwa usimame usiku ni tendo la kuifanyia (Shock your system)wewe umezoea kulala, ukianza kusimama ina maana unabadilisha Tabia, na usingizi ni Tabia,(Hapa nataka uwe makini na utambue kuwa nazungumzia kiwiliwili) umeonekana kama ukiachiwa utaendelea kulala zaidi, ukiachiwa hivyo hivyo utaendelea kusahau lazima upewe nyezo ya kukuwezesha kubadilika, sasa ufanye nini acha kulala amka usiku usimamishe Sala, Sababu mchana kutwa umo katika tabia ya kusahau, sasa unaamrishwa (Disturb the System)na kama utaweza kwa muda mrefu, fanya hivyo usiku mzima, ukiendelea na Ibada hii unaizuilia (Mind)kulimbikiza ndoto na matatizo yote ya mchana kutwa, unainyima fursa ya ku (Deposit)matatizo na magonvi fikra na mbinu za kila aina kwenye (Memory)yako.
"نِّصۡفَهُ ۥۤ أَوِ ٱنقُصۡ مِنۡهُ قَلِيلاً""Nusu yake au ipunguze kidogo"
Hapa unapewa(Choice)kama huwezi fanya nusu au ipunguze kidogo, kuwa na taratibu hii isikutoke kama huwezi yote fanya nusu, huwezi nusu umeambiwa fanya japo kidogo, amua mwenyewe hicho kiasi cha udogo wenyewe.
"أَوۡ زِدۡ عَلَيۡهِ وَرَتِّلِ ٱلۡقُرۡءَانَ تَرۡتِيلاً ""Au izidishe na soma Quraan kwa (Ufasaha)ilivyo".
Ukiweza zidisha ndio uzuri zaidi, halafu isome Quraan kwa ufasaha na umakini mkubwa kwa nyakati hizi za usiku iwe unafanya vilivyo vipi, yaani wakati unasoma na uwe wakati huo huo unaisikia, kitu kizuri sana kitakutokezea ikiwa utaweza kusoma na huku unasikia kile unacho soma, utafikia kwenye sehemu ambayo (peace)inakushukia na kitu kizuri kabisa kinateremka katika kifua chako naita hiyo (Secret Energy).
"إِنَّا سَنُلۡقِى عَلَيۡكَ قَوۡلاً۬ ثَقِيلاً ""Hakika sisi tutakuteremshia kauli nzito"
Bwana Mtume s.a.w kateremshiwa Quraan, ndio hii watu wengine waloipinga wakakataa kuiamini, maneno mazito sana kifua cha mwanaadamu hakiwezi kuchukua ndio unaona mpaka leo hata mimi na wewe kuna mengine yanatuumbisha kwa uzito wake. Sasa na wewe ukidumu katika Ibada hii nini kitakuremkia, hakuna chengine isipokua hiyo hekima, na wewe ushauri wako, muongozo wako utakua mzito kila mtu atataka kukufata ili aupate, kauli zako zitakua si za ulimwengu huu bali zinatokea kwa mwenyewe Muumba Mbingu na Ardhi.
" إِنَّ نَاشِئَةَ ٱلَّيۡلِ هِىَ أَشَدُّ وَطۡـًٔ۬ا وَأَقۡوَمُ قِيلاً ""Hakika kuamka usiku(Na kufanya Ibada)Kunawafikiana zaidi na Moyo, Na maneno (yake)Yanatua zaidi"
Hapo ndio inapotajwa faida kubwa ya kunyanyuka kwako usiku, unaelezwa kuwa ukinyanyuka usiku ukadumu katika Ibada hii unapata kitu kinachoitwa (Awakening) Nini hii (Awakening)?Mwanaadamu una aina mbili unazopita katika uhai wako moja ni ya kulala ambayo ni usiku, na ya pili ni ya kuamka ambayo ni mchana, lakini kwa wakati huu wewe unaishi katika moja tu ambayo ni ya kulala usiku na mchana, hii ya kuamka huijui kabisa, mpaka uambiwe, na mimi leo nachukua hii dhamana ya kukwambia kuwa ukiwa macho unakua huzioni ndoto zako, sio kua hazipo bali unapuuza kuziangalia vipi?
Tatizo kubwa la Mwanaadamu unatumia uhai wako wote katika kulala, Wanasayansi wanasema unatumia nusu ya Umuri wako katika usingizi, Wacha Mungu wao wanajua unatumia Asilimia 90 ya Uhai wako ukiwa Umelala, Inakuaje hali hii?
Endelea part 4
No comments:
Post a Comment