Sunday, May 25, 2014

MWANZO WA FURAHA KURIDHIKA PART 1

Asalaam Aleiykum

Ukiwa Bingwa wa Lugha utauliza mbona kichwa cha darsa ya leo kimeanza hivi(Mwanzo wa furaha kuridhika)kwanini kisiwe kuridhika ndio mwanzo wa furaha, hivyo ndio daima wafanyavyo wachambuzi wa Lugha, wanaishi kwenye maneno na wanasahau kiini cha neno, au kitendo husika kilokusudiwa ambacho kimebeba hilo neno.
Sasa nini kilicho beba hilo neno, ni kitendo cha furaha ndio ambacho kimeanzia mwanzo kwenye Maumbile ya Mwanaadamu, Furaha ndio (Nature)Umbile lako, hiyo Roho yako daima ipo kwenye furaha, Na sisi kutaka kulijua hilo itabidi tutafute mfano ili tupate kuelewa kipindi gani tulikuwa na hiyo Furaha ya (Natural)vipi Roho ilikuwa katika kawaida ya umbile lake la kufurahi ikisha mara Furaha hiyoo ikatoweka, lini imetoweka, imekuaje mpaka ikatoweka, kwani kweli kuna nyakati mimi nilikua furahani, na sasa hivi nina furaha au ninaanza kuridhika tu.
Jee upo uwezekano wa kuzipata tena furaha hizo? Jawaabu naam inawezekana, lakini jee Wewe unaweza, shujaa kikweli kweli kuchupa kwenye bahari ya Furaha, Kumbuka wewe ulikuwamo kwenye Bahari hiyo na wimbi tu ndilo lilokurusha nchi kavu na sasa unataka urejee tena, uwezekano wa kurejea upo iwapo utataka.
Wewe Furaha ni (Nature)yako, kumbuka ulivokua mdogo, bado hujawa na kiburi, huna majifta yoyote kwenye nafsi yako, huna dhamana, hujali chochote, huogopi kufa wala kupona, bado hujapata mazingatio hayo jikumbuke ulivokua, unakwenda baharini kukoga bila ya kufundishwa, unayakabili mambo ya hatari bila ya woga, ulikua huru kama ndege unaingia msitu huu mara unapanda mti ule, kila ukifanyacho unakifanya kwa furaha huna wasi wasi hata wa kupata chakula chako, sasa jiulize nini kilichobadilika?.
Kilichobadilika sio wewe ni mazingira yalo lazimishwa kwako kutokana na mahitajio na mabadiliko yako ya kila siku, Na kwa ushahidi wa hilo wale walioko Ulaya na walioko Africa kama watazungumza watatambua hilo, Na mfano wenyewe (Mtizame kijana wa Miaka 25 anaeishi Ulaya na yule anoishi Africa, wa Ulaya bado ana mambo ya sherehe sherehe za Utoto, lakini wa Africa keshakua mtu mzima na kahitimu mambo yote hiyo ndio tafauti, ukiweza kuliona hilo utapata kutambua chembe ya furaha).
Sasa nani khasa wanoanza kuiondosha Furaha hiyo, utashangaa nikikwambia Wazee, najua mtaruka kwenye viti vya (Computer) lakini endelea part 2 nipate kukufahamisha kwa uzuri.

MWANZO WA FURAHA KURIDHIKA PART 2

Asalaam Aleiykum

Wazee wanapokupeleka School kukupatia elimu wanakua wanajitahidi sana ufanikiwe, lakini wanashindwa kugundua au kufahamu kitu kimoja muhimu sana na kama wewe una watoto wako kiangalie sana kitu hicho utakacho kukigundua katika darsa hii pengine wewe kimekutokezea usikubali na watoto wako kiwatokezee, Anajitahidi Mzee na Walimu kuhangaika kwa jitihada zote wanasomesha lakini wewe kitu hakiingi kichwani, Wazazi wanakusukuma, walimu wanakusukuma, Jamii inakungoja umalize kusoma, wanakupeleka hivyo hivyo japo hufahamu pengine mpaka wanakufikisha (University) na kama tunavo fahamu huko (University) hakuna anofeli, kila mtu ana (Pass)kila mtu ana (Degree) mie naita (of Knowledge).
Mtu huyo anakuja kupewa Uongozi, tizama sasa uharibifu unaotokea hapo, au anapewa cheo chochote kile, kumbe huku Mollah wake kampangia awe Mkwezi au awe Mkulima, au awe fundi Seremala, Pengine kataka awe Daktari au uwe mfanya Biashara, Na hukuwa anavotaka Mollah wako, na wewe ndani ya Nafsi yako unajijua kama kwenye biashara mkono wangu mwepesi, kitu chochote nikiuza kinatoka, sasa umekua Daktari lakini nafsi ni ya mfanyabiashara, huna huruma visu vitupa, mtu anataka kukatwa ukucha unamkata na mguu ili upate pesa zaidi.
Au labda wewe Mwanasiasa unakuja kuwa Sheikh tizama vituko hapo, Unatakiwa uwe mkulima unakua Meneja, Hakuna hata (Inteligence) yoyote Kwenye kazi ulopangiwa, Umepewa Mwili wa kulima unakaa ofisini kwenye Feni lazima utasikia tafrani, kwa sababu huna Furaha, na unajijua ukiwa Shamba unakua umo furahani, ndio maana na wewe bila ya kujijua akija Mtu kwa hamaki zako za maisha unauliza nipe chochote, mie ntakula wapi? unaomba rushwa na kila ukipewa unakua ushatenda Dhanmbi, na malipo yake ni madhila na kunyimwa furaha kama unavowanyima wengine, kila wakihuzunika na wewe unahuzunika, na hayo ndio malipo ya Ulimwengu huu. Na hivyo ndivyo tunavoteseka kwa kuikosa Furaha, kila mmoja wetu hajaridhika elewa hapa siwazungumzii wale ambao kwa makusudi wamenyimwa fursa ya kutaka kuwa wanavotaka wenyewe ima kwa hila au kwa nguvu za kunyimwa haki hiyo, hao watakuwa wamedhulumiwa maisha yao.
Endelea part 3

MWANZO WA FURAHA KURIDHIKA PART 3

Asalaam Aleiykum

Na kaa ukijua Hakim wa haki analijua hilo na huwapa furaha kwa njia za maajabu wale walodhulumiwa. Sasa kwanini hatujaridhika?, Sababu kubwa hatuna Furaha, kwani lazima uwe na Furaha kwanza halafu ndio uridhike, kwanini ikawa hivyo hiyo ndio (Nature) kawaida ya maumbile, (Tizama wewe ukiwa mzima hupiti ukasema mie mzima, huna haja hiyo, lakini subiri ushikwe kidogo tu unavo tanganza naumwa mie, taabani ndio nakufa, unajua kwanini unasema hivyo kwa sababu furaha imeshaondoka, huridhiki tena mpaka upone).
Naam basi kwa kutaka ufahamu zaidi hekima ya Furaha na kuridhika tuhudhurie kisa hiki cha Mtoto na Baba yake kilosimuliwa na waja wenye hekima, "Baada ya kupita miaka mingi mtoto aliamua kurejea kwenda kuwasalimia wazee wake Kijijini kwao alipozaliwa, Ilipofika Magharibi wakakaa na Baba yake na kama kawaida Mzee akaanza kumuuliza Mwanawe vipi huko Mjini kuna Raha gani?, Mnatunyima nini watu wa mjini, Yule Mtoto akajibu ahh huko kuna vitu vya kila aina, Litizame swali la Mzee limeanza na nini? na Mtoto pia kaanza na nini? Mzee kaanza na Raha, na Mtoto kaanza na vitu, kumbuka vitu vinakaa nje, lakini Raha zinakaa ndani kwenye Jinsi yako.
Na hiyo ndio dasturi yetu viumbe sote, ila wachache tu waloigundua Raha wanajua haikai kwenye kitu, tuna tabia ya kuangalia kitu sana na ukiangalia kitu ina maana hujaridhika kwa sababu kitu hakileti Furaha, "Yule Mtoto akaendelea kusema Mjini kuna mataa na kuna meremeta sana kwa mataa hayo, Mjini kuna Magari mengi, Kuna Masenema, Kuna Mapesa, Kuna Watu, Kuna Mabiashara, Jee Baba Shamba kuna nini?.
Baba akajibu Mwanangu hapa kuna Raha, Kitu cha Mwanzo nasikia Furaha kuamshwa Kusali Alfajiri kwa Sauti ya kiumbe mwenzangu Jogoo, Nikimaliza Kusali Nasoma Quraan, Nikimaliza natulia kusikiliza Sauti za Ndege wanavo wasiliana kwa sauti zao nzuri, Ikisha Nakunywa Chai halafu huyo nashika njia kuelekea (Kondeni)Shamba huku nikimsabahi Mollah wangu, Ninapofika Shambani Nalima kwa Unyenyekevu huku nikimuomba Mollah wangu anipe alichonikadiria huku nikikumbuka maneno yaliyomo aya ya 7 sura ya (Talaq)
لِيُنفِقۡ ذُو سَعَةٍ۬ مِّن سَعَتِهِۦ‌ۖ وَمَن قُدِرَ عَلَيۡهِ رِزۡقُهُ ۥ فَلۡيُنفِقۡ مِمَّآ ءَاتَٮٰهُ ٱللَّهُ‌ۚ لَا يُكَلِّفُ ٱللَّهُ نَفۡسًا إِلَّا مَآ ءَاتَٮٰهَا‌ۚ سَيَجۡعَلُ ٱللَّهُ بَعۡدَ عُسۡرٍ۬ يُسۡرً۬ا 
Mwenye wasaa agharimu kadiri ya wasaa wake, Na yule ambaye amepungukiwa na Riziki yake, atoe katika kile alichopewa na Mwenye enzi Mungu, Mwenye enzi Mungu hamkalifishi Mtu yoyote ila kwa kadiri ya alichompa, Atajaalia Mwenye enzi Mungu baada ya Dhiki Faraji.
"Ewe Mwanangu zingatia sana maneno yaliyomo kwenye aya hiyo ukiyagundua maana yake utaingia ili uwemo kwenye Furaha" Baada ya kutoridhika utapata furaha, Ikisha huyo narudi nyumbani nikiwa na Furaha kumkuta Mke wangu keshapika, tunakaa wenyewe tunakula halafu tunapumzika, ikisha tena nyakati kama hizi za Usiku hapa hakuna Taa ila kuna Nuru ya Mwenye enzi Mungu ya Mbaa mwezi na Nyota ndiyo inayotumurika, baada ya hapo tunakwenda kulala salama usalimini hatuna fikra wala mawazo yoyote yanotupa wasiwasi au mashaka, Na wala hatukosi Rehma za Mollah wetu za usingizi.
Ila Mwanangu kuna kitu kimoja nataka kukujulisha ukifika usiku huja Simba akanguruma sana lakini usiogope, Hao wazee wakaaga kwenda kulala na yule Mtoto akaingia chumbani kwake lakini maskini hakuridhika kabisa akakaa macho anamsubiri Simba asikie Mngurumo wake, Na huku kashika panga labda simba atavunja Mlango, kitu cha ajabu chumba cha pili anasikia wazee wake wamelala wanakoroma, Na ndivo ilivo mpaka hivi sasa sote tupo tunasubiri Simba, Kila Mtu hajaridhika, kila mtu hana furaha, kila mtu hapati usingizi, na mifano tunaiona Mtu anajenga Jumba kubwa la Fahari ikisha analitia vyuma kwa kuogopa Simba, Na kama bado hajaridhika anaweka na walinzi, na ikiwa haijamridhisha anatia (Alarm) yote hayo yanafanywa kumsubiri Simba.
Na tumo hatujaridhika mpaka tusikie Ngurumo yake, Na kila tukipatacho haturidhiki, ukiwa Karani unautaka Umeneja, Ukiwa Mzuri huridhiki mpaka ujipambe zaidi, Ukiwa Tajiri huridhiki lazima uzidishe utajiri wako, ukiwa maskini ndio mama wee vita si vidogo, takriban maisha yetu yote tunoishi haturidhiki na wewe fanya uchunguzi uone umeridhika lini, na ikiwa hujaridhika basi huna Furaha, na kama huna Furaha unakosa jambo muhimu sana katika maisha haya, Na Mwisho nakukumbusha Ridhika na ukiridhika tu pale pale unaingia Furahani, na Furaha ndio maisha yenyewe usikae ukawa unaishi ndani ya Dhiki huku Faraja inakupita.


Sunday, May 18, 2014

UGUMU WA UCHA MUNGU PART 1

Asalaam Aleiykum,

Watu wengi wanaamini au wamefunikwa na dhana ya kuwa Ucha Mungu ni Jambo Rahisi unaloweza kulipata kwa njia ya (Cheap). Napenda kukujulisha ni vigumu sana kuwa Mcha Mungu, kwa sababu mtihani wa Ucha Mungu unatoka kwa yule alokuumba, Sasa baba au mama, au bosi wako unaweza kuwadanganya lakini vipi utaweza kumdanganya Mwenye kusikia,Kuona,kujua,asiyesahau au kupatwa na usingizi, vipi utamdanganya unaweza kudanganya viumbe vyake lakini sio Huyo Mwenye kutoa hiyo hadhi ya Ucha Mungu.
Sasa hebu jiangalie ikiwa Mitihani hii ya duniani lazima ukopie, ukitaka kutoa (Speech)Khutba lazima uandike, nini habari yako wewe na huo Mtihani wa Ucha Mungu, Mtihani ambao majaribio yake yanatoka kwa Mollah wako. Kutoka kwa Mollah wako unapewa karatasi nyeupe unaweza fanya mtihani wa Taqwa fanya, huwezi basi subiri Rehma za Mollah wako zikufikie, lakini usijinasibu hata kwa siri kuwa wewe Mcha Mungu.
Nimesikia Bwana Mmoja baada ya kusikia mawaidha makali yakamtoka machozi baada ya kujiona kafeli mitihani ya Mwenye enzi Mungu, ikisha akasema ingekua sio (Sex) sasa hivi namie  nakwenda peponi. Maneno mazuri sana katumia, kajielewa kwamba  yeye keshaingia kwenye gari la (motoni) ndio maana akasema ingekua sio (Sex) Na sio (Sex) pekee kuna mambo  mengi yanokuzuilia kuingia Peponi, mengi yanakuzuilia kuwa Mcha Mungu na usende peponi, Lakini hili la (Sex) ni (Nature) na kama jambo la (Nature) basi acha sasa nikupeleke  kwenye (Nature) yenyewe huko kwenye Mbuga za wanyama nikakuoneshe wanyama labda wanaweza kukutibu.
Wewe una kawaida ya kujiita Simba,(Kidume) Basi Simba yupo porini, sasa muangalie uone tafauti yako na yake, Simba akiwa na njaa anatafuta mawindo anakamata kinyama ikisha anakula akashiba, Basi utamuona Simba huyo hata ampitie kondoo mbele yake anakua hana haja, hatamani tena, lakini jitizame simba wewe, Nyumbani una Mke au Mume, unafurahishwa upendavo, basi ukimaliza tu uko kwenye simu unataarisha furaha nyengine za nje, Na hasara ilioje kwani nyumbani umefurahishwa wewe na kule nje unakwenda kumfurahisha mwengine, unayumba na makapu yako ya vitoweo, unapepesuka na doti za kanga, cheni za dhahabu na venginevyo, basi hiyo ndio tafauti yako wewe Simba wa mjini na yule wa porini, halafu tena unakaa kuomba Toba lazima useme ingekua si (Sex). endelea part 2

UGUMU WA UCHA MUNGU PART 2

Asalaam Aleiykum

Ingekua si (Sex) ningekwenda peponi, huwezi kwenda, na wala si rahisi kuwa Mcha Mungu kwa sababu zako za (Investment) za mambo mengi, na Ucha Mungu unatakiwa (Invest) ya kitu kimoja tu nacho ni kwa ajili ya Mollah wako, lakini wapi wewe ume (Invest) kwenye Biashara, Umetia hisa kwenye Siasa, Una (share) kwenye magonvi, kwenye husda, kwenye kusema watu, kwenye vikao vya mpira, na mabaraza ya karata na pombe, Na sasa umebakia kula faida ya Riba, kwa ajili ya Hisa zako zilivyozidi kwenye dunia ya ufisadi, jiangalie sana utayajua hayo hayafichiki, sasa vipi leo utaupata Ucha Mungu.
Ucha Mungu haupatikani kirahisi kwa njia ya mdomo na maonesho, Ucha Mungu lazima ujitolee hata kufa ili uupate Ucha Mungu, Utajiuliza Ufe vipi? Unatakiwa ufe (Painful Death) inakuaje hii (Painful Death) hapa ndio mwanzo wa Darsa yetu ya leo.
Itabidi tumsikilize kwa kituo msemezwa na Mwenye enzi Mungu Nabii Musa a.s anasemaje kuhusiana na kadhia hii ya Ucha Mungu, kwa kuwa kajua nyinyi mmekwisha (Invest) sana kwenye Ulimwengu huu, ili mpate kuupata huo Ucha Mungu Mjumbe wa Mwenye enzi Mungu anasema maneno haya:Quraan sura ya Saff aya ya 10 na 11.
"يَـٰٓأَيُّہَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ هَلۡ أَدُلُّكُمۡ عَلَىٰ تِجَـٰرَةٍ۬ تُنجِيكُم مِّنۡ عَذَابٍ أَلِيمٍ۬ "
Enyi Mlioamini je Nikujulisheni biashara itakayokuokoeni na adhabu iumizayo.
"تُؤۡمِنُونَ بِٱللَّهِ وَرَسُولِهِۦ وَتُجَـٰهِدُونَ فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ بِأَمۡوَٲلِكُمۡ وَأَنفُسِكُمۡ‌ۚ ذَٲلِكُمۡ خَيۡرٌ۬ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ "
(Basi)Muaminini Mwenye enzi Mungu na Mtume wake, na piganieni dini ya Mwenye enzi Mungu kwa mali zenu na nafsi zenu, haya ni bora kwenu ikiwa mnajua.
Inashangaza hapa maneno yameanzia kwa waloamini, utajiuliza vipi waloamini watapata adhabu ya Mwenye enzi Mungu, kwa ajili ya kuyachambua maneno haya itabidi nikujulishe (Level) mbili za Imani. Ama (Level) ya kwanza ya Imani yako imekaa kwenye Akili (Mind) ambayo inakua umekubali, umeambiwa au umesikia na wewe umekubali, hiyo ndio Imani yako, sasa Nabii Musa a.s alipokutaka uamini tena kakusudia uondoke kwenye (Level) ya kwanza na uende kwenye ya pili nayo ni Moyo (Falling in Love) si umejiona ukipenda unakuaje, uko tayari hata kufa kwa ajili ya mpenzi wako, uko tayari kufanya chochote ili mpenzi aridhike, na si unajijua hujali chochote kuyafanya hayo, sasa na huo Ucha Mungu unatakiwa uwe katika hali kama hiyo kwa ajili ya Mollah wako.
Na hilo anoweza kulifanya ni Mmoja tu naye ni (Mcha Mungu) mpenzi wa Mungu, na sisi Nabii Musa a.s katuona mapema kuwa wafanya Biashara, tushachuma Dhanmbi nyingi, hatuwezi kuwa wacha Mungu mpaka tujitolee (Muhanga) nayo ni hiyo (Painful Death)nayo ni Jihad, ndio neno la pili akatwambia nikujulisheni sasa Biashara, baada ya kuamini, na ukiamini tu uko tayari kwa lolote, ukiona unasita basi jijue Imani haijafika Moyoni, na kama imefika kweli jambo la mwanzo kupimwa kama kweli unautaka Ucha Mungu ni hiyo (Investment) ya Mali yako.
endelea part 3


UGUMU WA UCHA MUNGU PART 3

Asalaam Aleiykum

Unatizamwa Mali uliyonayo unaweza kuitoa kwa ajili ya (Allah) si unautaka Ucha Mungu, basi toa uonekane (Share) na wenzio igawe kama wewe kidume cha kweli, hiyo Mali itakufanya uepukane na adhabu za hapa Ulimwenguni na huko akhera uendako. Ndio maana nikakwambia vigumu sana kuwa Mcha Mungu, kwa sababu ndani ya Nafsi yako unaamini ukitoa utafilisika, na unasahau kujiuliza swali muhimu nani kakupa?. Basi hapo tena unaamua kubaki na Mali yako na uko Radhi adhabu za Mwenye enzi Mungu zikufike lakini hutoi chochote.
Basi hebu jiulize kama kweli uko tayari na hizo adhabu, wakati jino tu likikuuma au ukucha tu ukikatika Mtaa mzima wanajua leo fulani anaumwa, nini habari yako wewe kuhusiana na hizo adhabu za Mwenye enzi Mungu ambaye alokupa hilo jino(Hapo nakuachia mwenyewe utafakari) Na neno la tatu likawa hizo Nafsi zenu (Jihad ya Nafsi) mwanzo nilikupeleka Porini kuna kitu nimetia ndani ya nafsi yako, ndani ya Akili yako, kama utakua mwerevu basi yule Simba atakupa darsa kubwa, Na hili la Nafsi ndio zito zaidi, ikiwa unataka Ucha Mungu(Wakiristo wanasema Born again) mie nasema sio (Born again) sababu (Born again) unakua hujui mambo sasa hivi mambo unayajua mie naita (Painful Death) kifo cha machungu.
Uamuzi wa jambo hilo unalo wewe, na mimi kwanini nikaita hivyo kwa sababu ya (investment) zako, Ushazoea kusema uongo inabidi uache mpaka ukutoke uongo wote, vipi mpaka ule uongo wa mtu(Kapiga simu ishapokelewa unasema mwambie sipo)sasa useme ukweli mpaka watoto washangae, kwanini nikasema mpaka watoto washangae, sababu wewe umekulia katika mazingira ya kudanganywa na kudanganya kwa hiyo umerithisha na watoto, unamwambia mtoto nikirudi ntakuletea kitu fulani na ukirudi humletei, na unakua mkali, kwa hiyo mtoto anashangaa na sasa mfanye ashangae tena kwa kupona maradhi maradhi hayo, ndio maana nikaita (Painful death).
Uache kwenda Barazani wakati wewe ushazoea kwenda barazani, unadhani itakua rahisi,kuziacha karata, kuacha mipira, kuacha siasa, kuacha kusema watu, kuacha kusikiliza mambo ya kipuuzi,na kutizama (mambo machafu kwenye TV) ukiweza kuacha hayo yote basi moja kwa moja unakua Mcha Mungu, kwani ukiacha hayo yote, basi hiyo Nafsi moja kwa moja inajazwa na (Presence of God)Makumbuko ya Mwenye enzi Mungu, sasa kwanini haiwezekani na kwanini ikawa vigumu, haiwezekani kwa sababu ya Imani yako bado ndogo sana, na kutokana na hilo inakua vigumu kwa wewe kuwa Mcha Mungu, huwezi kuacha mambo yako, unayathamini sana, huwezi kuchagua baina ya mambo yako na Mollah wako, daima unachagua mambo yako na kwa hilo inakua vigumu kuupata Ucha Mungu.

Sunday, May 11, 2014

MADHARA YA MJA MWENYE KIBURI PART 4

Asalaam Aleiykum

Tunaendelea na darsa yetu ya kiburi tukiwemo tunaogelea katika aya ya 36 ya sura ya (Kahf)
"وَمَآ أَظُنُّ ٱلسَّاعَةَ قَآٮِٕمَةً۬ وَلَٮِٕن رُّدِدتُّ إِلَىٰ رَبِّى لَأَجِدَنَّ خَيۡرً۬ا مِّنۡهَا مُنقَلَبً۬ا "
Wala sidhani kama Kiama kitatokea, Na kama (Kikitokea)Nikarudishwa kwa Mollah wangu, bila shaka nitakuta(Kaniandalia)kikao chema kuliko hiki (alichonipa hapa Ulimwenguni).
Hicho ndio Kiburi kinatafauti ya kiasi tu, anasema huyo alopewa wala sidhani kama kiama kitasimama, hiyo ndio kufuru ilochanganyika na jeuri ikalelewa na Kiburi, Sasa njoo kwetu sisi ikisha ujichunguze upo unakula Raha za aina yoyote au upo kwenye Madaraka Fulani na wewe pia unatumia maneno hayo hayo , ila tafauti yake wewe umekua Bingwa wa kupindua lughaunabadilisha kidogo, unasema sidhani kama nitakufa sasa hivi, labda mpaka niwe Mzee, wacha nile Raha, Na hata kama nitakufa si ninazo Sala zangu tano nishatanguliza, Na pia siku fulani nilimsaidia fulani, basi namie nikirudi huko Akhera nitapewa hiyo pepo ya Jumba la ghorofa.
Hivyo ndivyo tulivyo na Viburi vyetu, vinatusahaulisha wazee wetu, ndugu zetu, marafiki zetu walo lala hoi maskini hawana hata cha kukila majumbani kwao na waislam wenzetu na walimwengu kwa jumla.
"قَالَ لَهُ ۥ صَاحِبُهُ ۥ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ ۥۤ أَكَفَرۡتَ بِٱلَّذِى خَلَقَكَ مِن تُرَابٍ۬ ثُمَّ مِن نُّطۡفَةٍ۬ ثُمَّ سَوَّٮٰكَ رَجُلاً۬ "
Mwenzake (Msokitu)akamwambia akiwa ana mjibu jee unamkufuru yule alokuumba kwa Udongo, ikisha kwa tone la manii, halafu akakufanya Mtu kamili.
Kumbuka Quraan ni mawaidha ya kukuzindua na kama bado umezama kwenye Kiburi huu ndio wakati muafaka wa kujiokoa, Na sisi tunakukumbusha jee umesahau kama wewe asili yako ni Udongo, jitizame vizuri ukitiwa (Vipodozi)ndipo dongo linavojitokeza, ikisha ukaumbwa kupitia mbegu ya uzazi, halafu tena ukafanywa Mtu mwengine kabisa uliye kamili, basi haya yote hayakukumbushi kitu ukajiona kumbe mimi ni dhaifu na wajibu wangu kuwa Mnyenyekevu, Na basi kama kweli ushakua Mtu kamili utaona unaanza kupata ishara za kuwacha Kiburi na unakuwa Binaadamu wa kawaida.
Na Kiburi kikiondoka unarejea kuwa Mtu kamili hutaki kufanya sura ya (Plastic) hutaki tena kucheka kwa kudanganya, humjali fulani atajua, fulani ataona, nani kasema  wewe unaamua kuwa Mtu (Natural)Mtu kamili, kinyume cha hivyo wewe (Feki)wewe ni Kiburi kitupu, na kaa ukijua Kiburi ni Maradhi.
"لَّـٰكِنَّا۟ هُوَ ٱللَّهُ رَبِّى وَلَآ أُشۡرِكُ بِرَبِّىٓ أَحَدً۬ا "
Lakini (Mimi Namuamini)Mwenye enzi Mungu wangu ndiye Mollah wangu  wala simshirikishi Mollah wangu na yoyote.
Mwanzo pametajwa maneno muhimu yanofaa kuzingatiwa kwa makini , Kasema Mnyenyekevu na hivi ndivo sote tunavotakiwa tuamini, kuwa Mwenye enzi Mungu kaumba kila kitu, Na vyote anavotupa vinatokana na yeye na pia kutokea kwake, Basi sio hilo tu hata mimi mwenyewe natokana na yeye Mollah wangu, kwa hiyo sina haja ya kumshirikisha na yoyote yule kwa sifa, kwa msaada wala kuogopa, kuanzia leo nawacha Kiburi changu, na najua chochote kinachotokea kwake hakuna mwengine mwenye uwezo wa kukizuia isipokua atake mwenyewe, na mimi sina jinsi ila kuwa mnyenyekevu kwake yeye Mollah wangu na viumbe vyake.
endelea part 5

MADHARA YA MJA MWENYE KIBURI PART 5

Asalaam Aleiykum

"وَلَوۡلَآ إِذۡ دَخَلۡتَ جَنَّتَكَ قُلۡتَ مَا شَآءَ ٱللَّهُ لَا قُوَّةَ إِلَّا بِٱللَّهِ‌ۚ إِن تَرَنِ أَنَا۟ أَقَلَّ مِنكَ مَالاً۬ وَوَلَدً۬ا "
Na Lau ulipoingia katika Bustani (Shamba)yako ungesema, Hivi nilivyo navyo amenitakia Mwenye enzi Mungu, (Na)Nguvu hazipatikani ila kwa (Kupewa na)Mwenye enzi Mungu, kama unaniona mimi nina mali kidogo na watoto wachache kuliko wewe.
Hayo ndio maneno unayotakiwa kusema wakati wowote unapopata mali au kitu chochote cha kheri, huko ndiko ku(Surrender)kujua kila kitu kumbe kinasababishwa na yeye, na mimi shukurani zangu ni kushirikiana na kila kiumbe kusheherekea Neema hii alonijaalia Mollah wangu.
Vipi utasheherekea? Huna haja ya kujisifu wala kufanya chochote cha majivuno, wewe unazijua nyumba za Maskini zipi, unawajua nani na nani wasio na uwezo, nini ufanye? toka bila ya vishindo nunua Chips kuku piga hodi kaa nao ule nao, au huwezi hivyo bado mawimbi ya Kiburi yanakuyumbisha, basi nunu gunia la Mchele wapelekee, na kama Mauti au chochote kitakukuta siku hiyo utakwenda huko Akhera ukakutane na Mlima wako wa (Thawabu). Lakini wapi ndio kwanza tumebaki kwenye fikra za kumzungumza fulani mpaka leo hana uwezo, hajamaliza kibanda chake, fulani anahangaika na maisha, yule mjinga sana atatupata wapi sie Familia yetu kubwa, tuko wengi, ikisha kabila letu tukufu, hicho ndio Kiburi.
"فَعَسَىٰ رَبِّىٓ أَن يُؤۡتِيَنِ خَيۡرً۬ا مِّن جَنَّتِكَ وَيُرۡسِلَ عَلَيۡہَا حُسۡبَانً۬ا مِّنَ ٱلسَّمَآءِ فَتُصۡبِحَ صَعِيدً۬ا زَلَقًا"
Basi huwenda Mollah wangu akanipa kilicho bora kuliko Bustani(Shamba)yako, Na kupelekea hiyo Bustani yako kwa mapigo ya Radi kutoka Mbinguni na ikawa ardhi tupu inayotelezesha.
Siku zote wanyenyekevu wanataraji kutoka kwa Mollah wao, akiwapa sawa, na asipowapa kwao sawa, wanajua Mollah wao ana sababu zake za kutokuwapa, Na hutaraji watakachopewa na Mollah wao kitakua daima kina kheri na chenye kuridhisha. Na angalia sana hususan Matajiri wangapi kwa viburi vyao wanavopigwa na Radi za Mwenye enzi Mungu wakafilisika, wanasiasa wangapi kwa Radi hizo wakashindwa kunyanyuka tena, ikawa kila Mtu unalolifanya haliwi, kila unalolitenda hufanikiwi, usisahau wakati huu ulopewa unafanya jeuri na Kiburi, basi na wewe ngojea wakati wako ukifika kila kitu kitabadilika utabaki na hadith nyingi nilikua hivi nikawa vile, unaishi kwa mawazo ya zamani ya kiburi, wakati huu unohadithia ndio (Nature)yako unayotakiwa uwe muda wote unaoishi katika Ulimwengu huu.
"أَوۡ يُصۡبِحَ مَآؤُهَا غَوۡرً۬ا فَلَن تَسۡتَطِيعَ لَهُ ۥ طَلَبً۬ا "
Au Maji yake yakawa yenye kuzama hata usiweze kuyapata(Mazao au mimea)
Kumbuka huo ni mfano, na wewe unaishi katika mifano kama hiyo, Na hivi ndivyo siku zote inavotokea, kama unaringia Mali, basi unaoneshwa vipi urahisi wake kuangamizwa mara moja, kama unaringia Majumba mafuriko au moto yanaweza kuyaangamiza mara moja, magari yanaweza kuungua moto au kupata ajali ukabaki huna hata moja, Dhahabu zinaweza kuibiwa zote ukawa huna kitu, na mambo haya usidhani yanafanyika kwa kutaka wewe, laa yanaweza kufanyika mara moja au yakafanyika kidogo kidogo ikawa kiburi chako kinakwenda arijojo kama kishada.

MADHARA YA MJA MWENYE KIBURI PART 6

Asalaam Aleiykum

وَأُحِيطَ بِثَمَرِهِۦ فَأَصۡبَحَ يُقَلِّبُ كَفَّيۡهِ عَلَىٰ مَآ أَنفَقَ فِيہَا وَهِىَ خَاوِيَةٌ عَلَىٰ عُرُوشِہَا وَيَقُولُ يَـٰلَيۡتَنِى لَمۡ أُشۡرِكۡ بِرَبِّىٓ أَحَدً۬ا 
Basi matunda (Mali yake)yakamungunyika(Kuharibika)na akawa anapindua viganja vyake(Kwa masikitiko)kwa ajili ya alichogharimia(Yale mashamba)ikawa miti yake imeanguka juu ya chanja zake, na akawa anasema, laiti nisinge mshirikisha Mollah wangu na yoyote.
Ukianza kufilisika jambo la mwanzo unaanza kufanya ishara za kushangaa, na kushangaa huku kunatokea ndani na kuko kwa aina mbili, Ima utashangaa kwa macho au kwa kutumia mikono, ukawa unauliza huku unapindua viganja vyako nini kimetokea, mbona sifahamu, Na ukifahamu tu, ndio vichekesho vinaanzia hapo, unajua unafanya nini? unaanza kuwa eti Mnyenyekevu, ghafla unageuka kuwa (Humble)unataka ufahamike sasa wewe mtu mzuri, kumbe vile kiburi kimeshakuacha mkono.
"وَلَمۡ تَكُن لَّهُ ۥ فِئَةٌ۬ يَنصُرُونَهُ ۥ مِن دُونِ ٱللَّهِ وَمَا كَانَ مُنتَصِرًا "
Wala hakua na Watu wa kumsaidia baada ya (Kumkosa)Mwenye enzi Mungu, wala mwenyewe kujisaidia.
Hivyo siku zote ndivyo inavotokea, Ukifilisika au ukianguka kivyovyote iwe kisiasa au kiofisi, watu wakishagundua sasa huna uwezo tena, huna cha kusomesha, kiburi kishakukimbia, utashitukia watu wote wametawanyika na umebaki peke yako, hakuna hata mtu mmoja atakae kupa msaada, hakuulizi mtu kitu, hata ukipita watu hawajui kapita nani, hapo tena unakua huna kiburi na wala huna kunyenyekevu.
Mwenye enzi Mungu kakutupa na sasa wewe mwenyewe huwezi kujisaidia, na hayo ndio malipo ya Kiburi katika Ulimwengu huu, ukiendekeza kiburi katika Ulimwengu huu na kuwanyanyasa wenzio, basi weka mbele kukutwa na mfano huu alokupigia Mwenye enzi Mungu.
"هُنَالِكَ ٱلۡوَلَـٰيَةُ لِلَّهِ ٱلۡحَقِّ‌ۚ هُوَ خَيۡرٌ۬ ثَوَابً۬ا وَخَيۡرٌ عُقۡبً۬ا "
Huko(Akhera na hapa Duniani)Ufalme ni wa Mwenye enzi Mungu(yeye)tu aliyoko daima, yeye ndio bora kwa malipo na (Ndiye)bora wa(kuleta)matokeo mazuri.
Napenda kukujulisha Ndugu yangu Mwenye enzi Mungu ndiye mtoaji hapa Ulimwenguni na huko Akhera, huna haja ya kufanya Kiburi, hukupata kwa uwezo wako, huna haja ya kujisifu, Na ukijitupa kwa Mollah wako basi utapata mazuri hapa Ulimwenguni na kesho Akhera. Mollah  tujaalie tukishinde Kiburi ili tuwe Wanyenyekevu, kwani Mwenye Kiburi hawezi kuipata Pepo ya Mwenye Enzi Mungu. Amin.

Sunday, May 4, 2014

MADHARA YA MJA MWENYE KIBURI PART 1

Asalaam Aleiykum

Napenda uelewe hakuna kitu chenye uharibifu na sumu kubwa ilofatana na Madhara kama kitu Kiitwacho (Kiburi), Na kitu hichi Kiburi kinatawala kila sehemu ya maisha ya Mwanaadamu, Iwe kwenye Dini, Siasa au Elimu, Kwenye Utajiri na hata mpaka kwenye Umaskini sumu hii inafika na kumuangamiza Mja.
Na hichi Kiburi ni nyenzo yenye nguvu ambayo inamfanya mpaka Mja aikose Pepo aliyoandaliwa na Mollah wake, Kwani kutokana na Kiburi (Ego)huwezi kabisa kuwa (Humble)Mnyenyekevu. Na kutokana na hicho Kiburi yanapatikana hayo madhara makubwa, Nini Madhara? Neno hili madhara lina mahusiano ya karibu na neno Maradhi, utaona yamepishana kwa herufi moja tu, na Kiburi kinaishi kwenye herufi mbili hizo, Vipi? Mwenye Kiburi kwa Watu anapeleka Madhara, na kwake Mwenyewe anajipa Maradhi.
Kabla ya kuingia katika Darsa yetu ya leo wacha tujitizame japo kidogo jee tunavyo Viburi au tumeepukana nacho, Alama ya mwanzo ya kukujulisha wewe umeepukana na Kiburi ni (Unyenyekevu). Na ukijijua kwamba wewe ni Mnyenyekevu basi ujue Kiburi kishapenya kwa siri kwenye unyenyekevu wako, Kinachokufahamisha kwa yakini kuwa wewe huna Kiburi ni Unyenyekevu ambao unakuja (Automatic)vitu viwili hivi havikutani kabisa Ima una unyenyekevu au una kiburi, huwezi ukawa na vyote viwili, Na hiyo ndio sheria ya Ulimwengu huu ikiwa utatizama Miti, Majabali na Milima, Mbingu na Nyota zake, Wanyama vyote vina nyenyekea isipokua Mwanaadamu.
Sasa tuviangalie Viburi vyetu vya kila siku na bora tuanze kwa wale walopewa Elimu iwe ya Dini au Dunia, na hapa nitawachagua watu wawili kuwaangalia, (Doctor na Sheikh)wawili hawa wana Mahusiano ya karibu na viumbe wenzao. Sasa muhudhurie  Daktari wakati yupo na Mgonjwa upate kuona Kiburi kinavo chukua (centre stage) unaweza kuingia ofisini kwake hata asikutizame usoni, wewe unamuhadithia maradhi yako makubwa umeshughulika unataka japo anyanyue uso, japo aone imani kwa hili kiumbe mwenzangu karibu atakufa, wacha nimtizame kwa jicho la huruma pengine kwa kufanya hivyo mie ntapata matumaini, (kwa sababu chunguza hata ukenda kutizama wagonjwa hhospital hali yako inavokua ukiingia ndani unakua na wewe tafrani unajua kwanini kwa sababu wagonjwa wanamuhitajia mzima ili wapate kunyonya nguvu za afya, ndio maana na wewe unajiona kama hujisikii sikii, wewe chunguza hilo mara nyengine ukenda kwenye chumba cha wagonjwa, na hiyo ndio inayomfanya Daktari wakati wote kanuna, kumbuka kununa sio Kiburi, na hivyo ndivyo watu wazamani walipokua wanasema usisimame unatunyonya Damu ikiwa wao wamekaa, ni kweli sababu (Energy)ya Mwanaadamu inamazoea ya (Levitation) kwa hiyo kama watu wamekaa na wewe umesimama unapata zaidi hiyo (Energy)ambayo inaoneka mpaka kwenye hizo Camera wanazoziita (Heating seeking Camera)na hizo ndio nguvu nilizokusudia).
Naam Basi Daktari wetu akiamua kukutizama basi huku anatafuna kalamu (Pen) Maskini Daktari anakosa bahati ya kupata (Transformation) na yeye akawa (Humble)mnyeyekevu na kugundua zawadi aliyoletewa na mgonjwa huyo. Na kuhusu wapili wetu huyu Shekhe, Endelea Part 2

MADHARA YA MJA MWENYE KIBURI PART 2

Asalaam Aleiykum

Sasa wacha Tumgeukie Sheikh tumuangalie na Majuba yake vipi kiburi kinavo muhangaisha, Mkono wa kulia kashika Funguo zimeandikwa(Peponi) Mkono wa kushoto kakamata (Raba) ya kufutia Madhanmbi, hapo tena hana shaka ya kudhulumu wala kusema uongo, haogopi kula haramu wala kutoa Fatwa za uongo, na kibaya zaidi anauza na Dua, Dua Elfu kumi, au Yasini Pound ishirini hivi ndivo tulivyo sisi tunao vaa vilemba vya Ushekhe, Viburi vimetutawala tunasahau kuwa tunawatumikia Binaadamu wenzetu kwa ajili ya Mwenye Enzi Mungu.
Na Wafuasi wanaendelea kukipalilia Kiburi hicho kwa kumwagia Shekehe huyo sifa kemkem kwa dua zake na kazi zake zisizo mfano, Na wawili wengine Mwanasiasa na Tajiri hawa hawana hata dawa, sina haja hata ya kuwazungumza, Mnajua vipi Viburi vyao vinavyo mwagiwa maji  na kupaliliwa, Na mambo hayo yote yanaletwa na watu wa nje, bila ya watu wa nje Kiburi kinakufa moja kwa moja, hakiwezi kusimama.
Tujitizame na maneno yetu unavoambiwa, "Eti watu watasemaje""Watu watakuonaje"Shughuli zote unajipamba wewe lakini kwa ajili ya kufurahisha Watu, Mwenye hufurahi na kama unataka kujijua kwanini ufurahi wacha aje mtu akwambie shati au kanzu yako ina doa au imechanika mbele ya halaiki ujione unavokua, hapo ndio utajua unafanya kila kitu kwa ajili ya watu, na kama watu hawajakusifu unaumia sana. Inafikia wakati mpaka kwenda msikitini inategemea watu watasemaje  kama hawajaniona, kutokana na hali hiyo sote tumegeuka kuoneana chuki, kufanyiana uadui, kuoneana husda yote sababu ya Kiburi.
Na kawaida ya Kiburi ukiwa nacho kwa siri au dhahiri basi unaelekea kwenye njia ya kumkufuru na kumshirikisha Mollah wako bila hata ya wasiwasi. 
Sasa leo tunaingia katika Darsa yetu ya Kiburi kwa aya zilizomo kwenye Sura ya (Al-Kahf-aya ya 32 mpaka 44)
"وَٱضۡرِبۡ لَهُم مَّثَلاً۬ رَّجُلَيۡنِ جَعَلۡنَا لِأَحَدِهِمَا جَنَّتَيۡنِ مِنۡ أَعۡنَـٰبٍ۬ وَحَفَفۡنَـٰهُمَا بِنَخۡلٍ۬ وَجَعَلۡنَا بَيۡنَہُمَا زَرۡعً۬ا "
"Na Wapigie mfano wa (Watu)waja  wawili, Mmoja wao tulimjaalia(Kumpa)Mabustani mawili(Mashamba)ya mizabibu, Na tukaizungushia mitende, Na pia katikati yake tukatia miti ya Nafaka(Ya kila aina)."
Mfano ndio mfano, unaweza kuwa wa aina yoyote, lakini cha muhumu ndani ya mfano huo kuna mafundisho, unaweza kuwa mfano huo wako wewe uko Dubai na mwenzio yuko pemba, au ukawepo England na mwenzio yuko yupo Unguja, ama wewe upo Oman na Rafiki yako yupo Tabora, la Muhimu ni mfano ulotolewa na Mwenye enzi Mungu na unaendelea kutokea mpaka hii leo kwako na kwangu, kumbuka ukipewa na Mollah wako hakuna kupingwa na mtu yoyote, Baraka zake zinaendelea kukushukia.
Na pia napenda utambue huu ni mfano wa waja wawili waliopo kwenye Mji fulani.
Endelea kukifatilia kisa hiki kwenye part 3 mpaka 6 itakayomalizikia wiki ijayo.

MADHARA YA MJA MWENYE KIBURI PART 3

Asalaam Aleiykum

Na mfano huu si lazima uwe wa Mashamba inaweza kuwa kitu chochote, labda umepewa (Permit) Ya ukaazi kuishi nchi fulani daima, au umepewa (Igama) au (Green Card) ikisha ukapata na kazi nzuri ya kuendesha maisha yako, Na kama haijatosha unabadilisha na Uraia unakuwa Raia wa Nchi nyengine, Basi kama unakijua nini Kiburi kitizame kiburi chako unaposhuka hapo (Airport)mambo yanaanzia hapo.
"كِلۡتَا ٱلۡجَنَّتَيۡنِ ءَاتَتۡ أُكُلَهَا وَلَمۡ تَظۡلِم مِّنۡهُ شَيۡـًٔ۬ا‌ۚ وَفَجَّرۡنَا خِلَـٰلَهُمَا نَہَرً۬ا"
Mabustani mawili yote yalijaa matunda yake (Na)wala hayakupunguza chochote(Katika musimu wake)Na ndani yake tukapitisha mito.
Katika kupewa na Mwenye enzi mungu neema zake zinakuwepo nyingi sana, Na wala hakudhulumu Mollah wako katika hilo, isipokua wewe ndio unamkufuru eti kama hajakupa utajiri, na akikupa vile vile ndio unazidisha kufuru, Na inakua hakuna mwenye hasira kama kwa kunyimwa kama mfano wako, unafikia kuumwa hata kuabudu hutaki tena, na unahisi umeonewa.
Sasa kuutilia mkazo mfano huu jitizame na wewe unapewa kwa njia hiyo hiyo ila kwa mfano mwengine, Na wewe pia unapewa Nyumba mbili ndani yake zina (Swimming Pool), kama hujapewa mashamba unapewa mapesa yalojaa kwenye (Account)Bank, haupigwi mfano na Mwenye enzi Mungu ukawa mfano huo umekwisha au kukatika bali unaendelea.
"وَكَانَ لَهُ ۥ ثَمَرٌ۬ فَقَالَ لِصَـٰحِبِهِۦ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ ۥۤ أَنَا۟ أَكۡثَرُ مِنكَ مَالاً۬ وَأَعَزُّ نَفَرً۬ا "
Na akawa na mali nyengine, akamwambia mwenzake(Rafiki yake)na hali ya kuwa akibishana naye, Mimi nina mali nyingi kuliko wewe na (Nina)nguvu zaidi kwa ajili ya wafuasi (watu wengi nilo nao).
Naam mali ikizidi au ukipanda cheo lazima na jeuri iongezeke na kiburi kitokeze, Ima kitatokeza kwa maneno utakitoa kwa siri, na kama Muislam hutotaka waumini wenzio wa msikitini wakajua, na lazima kawaida ya Kiburi uanze kwa majisifu, Na huwezi kwenda kwa walokuzidi au ulokuwa nao sawa, unamtafuta yule wachini yako pengine mtu hana elimu au maskini au yupo Africa anahangaika na maisha hapo ndio unapoanzia mazoezi , Na huyo mtu katika huo mfano kaanza kwa kusema "Mimi nina mali nyingi""Na wewe unasema labda nishaukata, sasa nina (Green Card)au nina hichi na kile, Na popote penye pesa au mali lazima walala hoi wakusanyike kama wanavokusanyika kwa Shekhe au kwa mwanasiasa, hakuna tafauti, wafuasi ni wale wale na wapo tayari kukupigia makofi kwa ajili ya kiburi chako.
"وَدَخَلَ جَنَّتَهُ ۥ وَهُوَ ظَالِمٌ۬ لِّنَفۡسِهِۦ قَالَ مَآ أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَـٰذِهِۦۤ أَبَدً۬ا"
Na akaingia katika Bustani(Shamba lake)yake na hali ya kuwa anajidhulumu nafsi yake"Akasema"sidhani abadan kuwa (Shamba)hili litaharibika.
Na hivi ndivo ilivyo tukiingia majumbani mwetu tunaambukiza sumu hii ya viburi mpaka kwa vizazi vyetu, tunadhulumu nafsi zetu kwa kitu ambacho hakina faida na sisi, Mwenye enzi Mungu alituambia tuhadithie neema zake sio tujivunie na kutakabar, nini kuhadithia? kuhadithia ni ku (Share) iwe hadith, neema, mapenzi au ujuzi, nini kujisifia? kujisifia ni Kiburi , maradhi, (Ubinafsi)kuzuia neema na kujitenga na kawaida ya Ulimwengu huu, Na sasa hivi kama utakua mjuzi wa kukaa kutizama nani na nani ana kiburi utagundua nyumba nzima imeambukizwa na kama hajatokea mtu kuwakumbusha basi inapatikana hasara kubwa kutokana na kawaida hii ya kuvifuga Viburi. Inshaa Allah itaendelea wiki ijayo.