Asalaam Aleiykum
Na mfano huu si lazima uwe wa Mashamba inaweza kuwa kitu chochote, labda umepewa (Permit) Ya ukaazi kuishi nchi fulani daima, au umepewa (Igama) au (Green Card) ikisha ukapata na kazi nzuri ya kuendesha maisha yako, Na kama haijatosha unabadilisha na Uraia unakuwa Raia wa Nchi nyengine, Basi kama unakijua nini Kiburi kitizame kiburi chako unaposhuka hapo (Airport)mambo yanaanzia hapo.
"كِلۡتَا ٱلۡجَنَّتَيۡنِ ءَاتَتۡ أُكُلَهَا وَلَمۡ تَظۡلِم مِّنۡهُ شَيۡـًٔ۬اۚ وَفَجَّرۡنَا خِلَـٰلَهُمَا نَہَرً۬ا"
Mabustani mawili yote yalijaa matunda yake (Na)wala hayakupunguza chochote(Katika musimu wake)Na ndani yake tukapitisha mito.
Katika kupewa na Mwenye enzi mungu neema zake zinakuwepo nyingi sana, Na wala hakudhulumu Mollah wako katika hilo, isipokua wewe ndio unamkufuru eti kama hajakupa utajiri, na akikupa vile vile ndio unazidisha kufuru, Na inakua hakuna mwenye hasira kama kwa kunyimwa kama mfano wako, unafikia kuumwa hata kuabudu hutaki tena, na unahisi umeonewa.
Sasa kuutilia mkazo mfano huu jitizame na wewe unapewa kwa njia hiyo hiyo ila kwa mfano mwengine, Na wewe pia unapewa Nyumba mbili ndani yake zina (Swimming Pool), kama hujapewa mashamba unapewa mapesa yalojaa kwenye (Account)Bank, haupigwi mfano na Mwenye enzi Mungu ukawa mfano huo umekwisha au kukatika bali unaendelea.
"وَكَانَ لَهُ ۥ ثَمَرٌ۬ فَقَالَ لِصَـٰحِبِهِۦ وَهُوَ يُحَاوِرُهُ ۥۤ أَنَا۟ أَكۡثَرُ مِنكَ مَالاً۬ وَأَعَزُّ نَفَرً۬ا "
Na akawa na mali nyengine, akamwambia mwenzake(Rafiki yake)na hali ya kuwa akibishana naye, Mimi nina mali nyingi kuliko wewe na (Nina)nguvu zaidi kwa ajili ya wafuasi (watu wengi nilo nao).
Naam mali ikizidi au ukipanda cheo lazima na jeuri iongezeke na kiburi kitokeze, Ima kitatokeza kwa maneno utakitoa kwa siri, na kama Muislam hutotaka waumini wenzio wa msikitini wakajua, na lazima kawaida ya Kiburi uanze kwa majisifu, Na huwezi kwenda kwa walokuzidi au ulokuwa nao sawa, unamtafuta yule wachini yako pengine mtu hana elimu au maskini au yupo Africa anahangaika na maisha hapo ndio unapoanzia mazoezi , Na huyo mtu katika huo mfano kaanza kwa kusema "Mimi nina mali nyingi""Na wewe unasema labda nishaukata, sasa nina (Green Card)au nina hichi na kile, Na popote penye pesa au mali lazima walala hoi wakusanyike kama wanavokusanyika kwa Shekhe au kwa mwanasiasa, hakuna tafauti, wafuasi ni wale wale na wapo tayari kukupigia makofi kwa ajili ya kiburi chako.
"وَدَخَلَ جَنَّتَهُ ۥ وَهُوَ ظَالِمٌ۬ لِّنَفۡسِهِۦ قَالَ مَآ أَظُنُّ أَن تَبِيدَ هَـٰذِهِۦۤ أَبَدً۬ا"
Na akaingia katika Bustani(Shamba lake)yake na hali ya kuwa anajidhulumu nafsi yake"Akasema"sidhani abadan kuwa (Shamba)hili litaharibika.
Na hivi ndivo ilivyo tukiingia majumbani mwetu tunaambukiza sumu hii ya viburi mpaka kwa vizazi vyetu, tunadhulumu nafsi zetu kwa kitu ambacho hakina faida na sisi, Mwenye enzi Mungu alituambia tuhadithie neema zake sio tujivunie na kutakabar, nini kuhadithia? kuhadithia ni ku (Share) iwe hadith, neema, mapenzi au ujuzi, nini kujisifia? kujisifia ni Kiburi , maradhi, (Ubinafsi)kuzuia neema na kujitenga na kawaida ya Ulimwengu huu, Na sasa hivi kama utakua mjuzi wa kukaa kutizama nani na nani ana kiburi utagundua nyumba nzima imeambukizwa na kama hajatokea mtu kuwakumbusha basi inapatikana hasara kubwa kutokana na kawaida hii ya kuvifuga Viburi. Inshaa Allah itaendelea wiki ijayo.
No comments:
Post a Comment