Asalaam Aleiykum
Ukiwa Bingwa wa Lugha utauliza mbona kichwa cha darsa ya leo kimeanza hivi(Mwanzo wa furaha kuridhika)kwanini kisiwe kuridhika ndio mwanzo wa furaha, hivyo ndio daima wafanyavyo wachambuzi wa Lugha, wanaishi kwenye maneno na wanasahau kiini cha neno, au kitendo husika kilokusudiwa ambacho kimebeba hilo neno.
Sasa nini kilicho beba hilo neno, ni kitendo cha furaha ndio ambacho kimeanzia mwanzo kwenye Maumbile ya Mwanaadamu, Furaha ndio (Nature)Umbile lako, hiyo Roho yako daima ipo kwenye furaha, Na sisi kutaka kulijua hilo itabidi tutafute mfano ili tupate kuelewa kipindi gani tulikuwa na hiyo Furaha ya (Natural)vipi Roho ilikuwa katika kawaida ya umbile lake la kufurahi ikisha mara Furaha hiyoo ikatoweka, lini imetoweka, imekuaje mpaka ikatoweka, kwani kweli kuna nyakati mimi nilikua furahani, na sasa hivi nina furaha au ninaanza kuridhika tu.
Jee upo uwezekano wa kuzipata tena furaha hizo? Jawaabu naam inawezekana, lakini jee Wewe unaweza, shujaa kikweli kweli kuchupa kwenye bahari ya Furaha, Kumbuka wewe ulikuwamo kwenye Bahari hiyo na wimbi tu ndilo lilokurusha nchi kavu na sasa unataka urejee tena, uwezekano wa kurejea upo iwapo utataka.
Wewe Furaha ni (Nature)yako, kumbuka ulivokua mdogo, bado hujawa na kiburi, huna majifta yoyote kwenye nafsi yako, huna dhamana, hujali chochote, huogopi kufa wala kupona, bado hujapata mazingatio hayo jikumbuke ulivokua, unakwenda baharini kukoga bila ya kufundishwa, unayakabili mambo ya hatari bila ya woga, ulikua huru kama ndege unaingia msitu huu mara unapanda mti ule, kila ukifanyacho unakifanya kwa furaha huna wasi wasi hata wa kupata chakula chako, sasa jiulize nini kilichobadilika?.
Kilichobadilika sio wewe ni mazingira yalo lazimishwa kwako kutokana na mahitajio na mabadiliko yako ya kila siku, Na kwa ushahidi wa hilo wale walioko Ulaya na walioko Africa kama watazungumza watatambua hilo, Na mfano wenyewe (Mtizame kijana wa Miaka 25 anaeishi Ulaya na yule anoishi Africa, wa Ulaya bado ana mambo ya sherehe sherehe za Utoto, lakini wa Africa keshakua mtu mzima na kahitimu mambo yote hiyo ndio tafauti, ukiweza kuliona hilo utapata kutambua chembe ya furaha).
Sasa nani khasa wanoanza kuiondosha Furaha hiyo, utashangaa nikikwambia Wazee, najua mtaruka kwenye viti vya (Computer) lakini endelea part 2 nipate kukufahamisha kwa uzuri.
No comments:
Post a Comment