Sunday, June 1, 2014

UFUNGUO WA TOBA PART 3

Asalaam Aleiykum

Sasa nini ufanye ili upate huo Ufunguo, ili usiendelee kujidanganya, ukawa unapanda ile pembea ya (Merry go Round) ya kutubu na kufanya tena, kuepukana na hilo itabidi ukabidhiwe funguo ili upate Toba ya kweli (Tawbat Nasuha), Na Toba hii haipatikani mpaka pale utakapokata shauri la kumsikiliza huyo ano Kusamehe yeye kasema nini?
Kwanza kakwambia Jiepushe kwenye vikao vya kipuuzi, halafu na la pili kakwambia ukitembea angusha macho yako, (wacha hapa nikupe faida ndogo ya kuangusha macho yako)ukitembea ukawa unatizama macho chini jua una (Preserve) nguvu zako za mwili huchoki haraka, nguvu hazipotei, lakini ukiweka macho juu ukawa unataka uone kila kitu, elewa kila kitu ukitizama una (Realese)nguvu unazitoa kwenda nje, kwa hiyo ni faida ya kwanza ya kuangusha macho yako.Na faida ya pili Ukiweza kufanya hayo utakua ushaanza kutubu, ushakamata Funguo mkononi, halafu jambo la tatu kwa lugha nyepesi inaitwa kufuta, Sasa chukua na (Raba) kamata vitu hivi, vipi?(Furqan 70).

"إِلَّا مَن تَابَ وَءَامَنَ وَعَمِلَ عَمَلاً۬ صَـٰلِحً۬ا فَأُوْلَـٰٓٮِٕكَ يُبَدِّلُ ٱللَّهُ سَيِّـَٔاتِهِمۡ حَسَنَـٰتٍ۬‌ۗ وَكَانَ ٱللَّهُ غَفُورً۬ا رَّحِيمً۬ا"
Ila yule atakaetubia na kuamini na kufanya  vitendo vizuri, basi hao ndio Mwenye enzi Mungu atawabadilishia maovu yako kuwa mema, Na Mwenye enzi Mungu ni mwingi wa kusamehe (Na) Mwingi wa Kurehemu.
Kwanza Tubu, acha yote, geuza Akili yako kwenye mambo ya Neema, ikisha jitahidi kuamini, tafuta mambo yatokufanya uamini, basi hata (Mauti)hayakufanyi ukaamini?, halafu tenda vitendo vizuri(Tumia Raba) Mollah wako sio atavifuta vitendo vyako viovu bali atavibadilisha kuwa wema,(kwa kufanya yale mabaya yako yasahauliwe) na yeye Mollah wako ni Mwenye kusamehe na Kukurehemu mja wake kwa kukujulisha hiyo njia ya Ufunguo wa Toba.
Sasa vipi utatubu wakati ushasahau matendo yako maovu, Dhanmbi zako umesahau umefanya nini?. Kuhusu hayo mengine Mollah wako atakusaidia lakini hili la kwenye Akili yako itabidi ufanye Mwenyewe na hapo ndio inabidi ufanye kitu kiitwacho (Regress) uhudhurie tena yale makosa yako, na kila ukiyahudhuria na kuyakumbuka kama kweli unataka kutubia basi utajuta, na ukijuta tu ushalifuta hilo kwenye Akili yako. Lakini hivi sasa unakua umesahau unakumbushwa na Akili yako unarejea kufanya tena, lakini ukikumbuka mwenyewe unakua umekamilisha (Process) kumbuka kila kitu kina sehemu mbili, wewe umefanya sehemu moja tu ya kuandika lakini hujafuta, kamilisha (Full Circle)na hiyo ndio Raba.
Huo ndio Ufunguo wa (Mind) yako itakapokua (Empty) haijaandika mambo ya (Munkarat) machafu, hapo utakua ushafungua Mlango wa Toba, usharudi kwa Mollah wako, na kwa Mollah kama umetubu unaambiwa hivi (Hud 3)
وَأَنِ ٱسۡتَغۡفِرُواْ رَبَّكُمۡ ثُمَّ تُوبُوٓاْ إِلَيۡهِ يُمَتِّعۡكُم مَّتَـٰعًا حَسَنًا إِلَىٰٓ أَجَلٍ۬ مُّسَمًّ۬ى وَيُؤۡتِ كُلَّ ذِى فَضۡلٍ۬ فَضۡلَهُ
Na ili Muombe msamaha kwa Mollah wenu, ikishi Mtubie kwake, atakustarehesheni kwa starehe nzuri mpaka muda maalumu,(Wa kuondoka Ulimwenguni)Na atampa (Akhera) kila mwenye fadhila, fadhila yake, (Mpaka mwisho wa aya).
hayo ndio uyapatayo ukianza kushika ufunguo wa Toba, Dhanmbi zina hama kwenye akili na Toba inatawala, mawazo yako yanakua ya vitendo vya Thawabu, Na Mollah wako anakufanyia kila zito kuwa wepesi, unaongezewa riziki, unakingwa na maradhi na kuepushwa na ajali, na hakuna wakati mzuri wa kuchukua funguo hii kama wakati huu wa kuukaribisha mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Inshaa Allah Mwenye Enzi Mungu atujaalie Tawbat Nasuha kwa sote. Aamin.


No comments:

Post a Comment