Sunday, June 22, 2014

MTUKUFU RAMADHAN PART 1

Asalaam Aleiykum

Watu wanakua na Furaha pale wanapoandaa harusi ya Mtoto, Kuandaa mikutano na Sherehe nyengine, lakini akipewa habari ya kujiandaa na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan hapo hapo anabadilika uso, utaona rangi inabadilika hata kama anajificha, moyoni anasema "Mama wee"Kiama hicho.
Sisi wa Ulaya ukitajiwa tu unaanza kukiona kimbunga cha masaa 18 hayoo, Bali kila mmoja wetu ana sababu za kuuwekea alama ya kuuliza mwezi huu wa Ramadhan, hapo tena utaona wenye Maradhi yanakuja juu ghafla, na kwa kuwa hayajatajwa Maradhi gani basi hata ukucha unatosha kumpa mtu sababu ya kutokufunga, Lakini wale Wenye kumpenda Mollah na Maamrisho yake huwa wanausubiri kwa hamu zawadi hii ili wapate kujikurubisha zaidi kwa Mollah wao, wapate kuonesha mapenzi kwa ajili ya Ibada.
Na ikiwa wewe humo katika kundi hilo anza kupata wasiwasi, Wenye penzi la (Taqwa)wanajua yaliyomo kwenye mwezi huu, ndio maana wakafurahi kuwasili kwake.
Na wewe kama hujui kilichomo ndani ya Mwezi huu basi tega sikio, dondosha jicho upate kufaidika na maudhui hii ambayo kwa leo tunaanza kuchuma tunda la aya ya 185 iliyomo kwenye sura ya (Baqarah)"شَہۡرُ رَمَضَانَ ٱلَّذِىٓ أُنزِلَ فِيهِ ٱلۡقُرۡءَانُ هُدً۬ى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَـٰتٍ۬ مِّنَ ٱلۡهُدَىٰ وَٱلۡفُرۡقَانِ‌ۚ "(Mpaka mwisho wa aya)
"Mwezi huu wa Ramadhan (Ndio)ambao imetermshwa hii Quraan, Uwe Uongozi (Kwa) Watu, Na hoja zilizo wazi na upambanuzi".
 فَمَن شَہِدَ مِنكُمُ ٱلشَّہۡرَ فَلۡيَصُمۡهُ‌ۖ وَمَن ڪَانَ مَرِيضًا أَوۡ عَلَىٰ سَفَرٍ۬ فَعِدَّةٌ۬ مِّنۡ أَيَّامٍ أُخَرَ‌ۗ يُرِيدُ ٱللَّهُ بِڪُمُ ٱلۡيُسۡرَ وَلَا يُرِيدُ بِڪُمُ ٱلۡعُسۡرَ وَلِتُڪۡمِلُواْ ٱلۡعِدَّةَ وَلِتُڪَبِّرُواْ ٱللَّهَ عَلَىٰ مَا هَدَٮٰكُمۡ وَلَعَلَّڪُمۡ تَشۡكُرُونَ 
"Basi atakae kuwa katika Mji katika Mwezi huu (Na) afunge, Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizowacha) katika siku nyengine, Mwenye enzi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, Na pia mtimize hisabu hiyo, Na kumtukuza Mwenye enzi Mungu kwa kuwa kakuongozeni, ili mpate kushukuru"
Basi leo tutazunguka kwenye Bustani ya aya hii ili tupate kuchuma matunda  yake asaa unaweza kupata Vitamin ya Muongozo
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment