Asalaam Aleiykum
Ili kuyapata hayo mapenzi itakubidi ujitoe (muhanga) ufunge kila kitu, una mambo mengi wewe unafanya katika mwaka mzima, sasa ukitaka uipate (Saum) itakubidi uyafunge kama unavo ifunga milango ili mwizi asiingie, mambo yepi? una vikao vya Mpira, vikundi vya mazoezi, una biashara zisizo za muhimu, mikutano ya harusi, mkesha wa jumapili, Baraza ya usiku, jioni ya kutizama mandhar, vipindi vya TV, Kibaraza mawazo, kusoma vitabu vya hadith, takriban acha acha mambo ya kilimwengu katika mwezi huu kwa jumla, (hata ukiweza kujiepusha na kitanda kama utaweza kwa hiyari yako basi fanya, usione nimekwambia lala chini, laa kama utaweza kujiepusha na Mume au Mke fanya, Ramadhan mwanzo mpaka hayo yalipigwa marufuku mpaka watu yalipowashinda ndio wakapewa unafuu)sasa ukiacha hayo yote halafu ufanye nini? unaambiwa usifanye chochote nenda kakae Msikitini (Itikaf) وَلَا تُبَـٰشِرُوهُنَّ وَأَنتُمۡ عَـٰكِفُونَ فِى ٱلۡمَسَـٰجِدِۗ
Wala msichanganyike nao na hali mnakaa Itikaf msikitini.
Sasa kwanini ukae msikitini? kwa sababu ndani ya Msikiti kuna salio la (Energy) za Ibada za Waumin wanazofanya siku zote, miaka yote wanamsabahi Mollah wao wanaitikia Amin, Na Msikitini hakipotei kitu, hata zile Nguvu za walokufa miaka ya nyuma bado zimo na zitaendelea kuwamo, sasa wewe ukenda ukafanya hilo tendo la kukaa Itikaf, ukakaa Kimya na Saum yako unakua kivutio cha nguvu hizo kuja kwako, na zikiungana na wewe nguvu hizo unapata (Separation) na mambo yote ya kidunia kwanza yanakujia moja baada ya moja yakimalizika (Mpito wa Separation) ghafla utaona mapenzi yana miminika, utaanza kupenda Ibada, utapenda Binaadamu wenzio, kama una pesa unaanza kuzitoa, hufutari tena peke yako, unasaidia maskini na wagonjwa, Na unatamani kila wakati kufanya Ibada, na ukijiona katika hali hiyo basi ushayapata mapenzi ushaupata Ucha Mungu, ushaipata Saum na huko ndiko kufuzu katika dini, na hili anosikia amwambie mwenzie.
No comments:
Post a Comment