Sunday, June 1, 2014

UFUNGUO WA TOBA PART 1

Asalaam Aleiykum

Kila kiumbe anahitaji Toba ndio maana utaona Mtu anatafuta awe kwenye Dini ili apate kuwa karibu ya kutubu, kila mmoja wetu anajiuliza lini nitaacha? mbona nimezama? jee kweli haya nilo nayo yanaachika? nifanye nini nipate kuacha, hususan natia nia kila Ramadhan ikija nitaacha lakini nashindwa kuacha, na inapokwisha tu Ramadhan naanza tena nini kimenisibu?, mbona nateseka na mashaka haya.
Ama Mja kujiona na makosa peke yake ni maradhi, Halafu unaendelea kujiongezea maradhi kwa kutenda Dhanmbi zaidi, lini utapona na sasa uko hoi, Jee kweli wasemavo kuna hiyo Raba au Ufunguo nipate kuingia mimi kwenye hicho chumba cha Toba. Unajibiwa Naam Funguo ipo na leo ndio siku ya kukabidhiwa huo Ufunguo ukiwa unajitaarisha kuingia kwenye Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Sasa ukitaka kuipokea Funguo hii itabidi unyanyue mikono yako juu kama vile unapoitikia Aamin, kwa sababu kila wakati unapoitikia Aamin wewe huikamata Funguo hii au huwa inakuparaza vidoleni, lakini kwa kuwa Aamin yako sio (Deep)unaitikia kwa mazoea basi hukuponyoka Funguo hii. Kwanza kabisa wacha nikujulishe Funguo Yenyewe ili nipate kukufahamisha vipi utaitumia, kwa ajili hiyo inatubidi tuhudhurie sura ya (Qalam)aya ya mwanzo.
نٓ‌ۚ وَٱلۡقَلَمِ وَمَا يَسۡطُرُونَ 
"Nuun.(Naapa kwa) kalamu na yale wayaandikayo(Kwa kalamu hizo)".
Anaapa Mwenye Enzi Mungu kwa Akili na kile kiandikacho Akili hiyo. Na akasema katika aya ya mbele yake, haikua neema hiyo ni wenda wazimu, Akili iko katika mizani nyepesi sana ukiifanyia mchezo kidogo tu unaupata huo Wazimu, Na kama unataka kuijua mizani yenyewe, au kama yangu iko sahihi jiangalie unapo hamaki unakuaje?, Dakika moja tulikuwa na wewe mzima, Mtu kamili nini sasa hivi kimekutokezea, umegeuka si Mtu mzuri tena, nini kimekusibu, mbona umegeuka na kua (Monster).
Hamaki sio wazimu, hamaki ni (Energy) katika mwili wako, ikipanda (Energy)hiyo kwenye Akili inageuza akili hiyo kuwa wazimu, na kama unaweza kui (Transform) inakua (Compassion) baina ya ncha hizo mbili wazimu unakaa kati kati, ukiirudisha moyoni ni (Huruma) ukiipandisha juu (Hamaki)"Ndio Maana Bwana Mtume saw" akatumia Hekima kukwambia ukihamaki (chutama) kufanya hivyo unarejesha (Energy) hii moyoni, unajiepusha na wazimu, na unaweza kusamehe.
Sasa unatakiwa Akili yako uitumie kwa njia za Neema kama alivohimiza Mwenye enzi Mungu, Lakini wewe unaanza kuharibikiwa wapi?, unaharibikiwa pale unapoanza kuitumia Akili hiyo ulonayo kwa njia ya Ufisadi, matatizo yanaanzia hapo, lakini kama utakumbuka Neema hiyo alokupa Mollah wako ndio ilo vumbua Madege, na Meli, ikavumbua Ujenzi na kila kitu uanacho leo hii haya ma(Computer)na mengineyo, ikisha ukagundua kwanini mimi namkera alonipa Neema hii mpaka nikapoteza Funguo hii ya Toba, basi utakua umeshaanza kuutafuta huo ufunguo kwa kukumbuka hilo tu.
Nini kimekufanya baada ya kufungua chumba cha (Thawabu) umekwenda kufungua chumba cha (Dhanmbi) Nani alokupa Funguo hiyo? Sasa tega Macho vizuri, Nyoosha mikono yako huenda labda ukadondoshewa hilo (Funguo) katika Darsa hii ya Ufunguo wa Toba ili na wewe upate kufuta machozi, nakuona unalia siku nyingi, sasa nyamaza tukupe Funguo asaa unaweza kufungua chumba cha hazina ambacho kipo mbele yako, lakini umo kizani unaendelea kupapasa vyumba vya Dhanmbi.
Endelea part 2 ukachukue funguo yako.



No comments:

Post a Comment