Asalaam Aleiykum
Nini Maana ya Toba.
Toba maana yake ni kurejea (Ujingani) lakini sasa ukiwa na fahamu, kumbuka kwanza ulikua ukijua, na sasa una fahamu (Vitu viwili tafauti) na nikisema ujinga nakusudia (Innocent) sasa imekuaje hata urejee, sote mfano wetu kama baba yetu Adam a.s , Haijambo yeye alitolewa Peponi sisi tukipata huko kujua tunakimbia wenyewe, tunakua werevu(Wajanja) tunaikimbia Bustani tunakimbilia Msituni.
Nini kinatokezea kwenye msitu huu wa Ulimwengu, wengine wanajeruhiwa na Simba, wengine wanatafunwa na Chui, Msitu mkubwa kuna wengine wanatafunwa na Nyoka, kuna na wengine wanachaniwa majuba na kanzu zao, kila mtu kabeba begi lake la mbao ndani kuna (Book) kubwa anapepesuka kutafuta njia ya kurudi lakini haijui, kashikwa na werevu wake hajui chochote anakua maskini wa kila kitu, na ukikimbia kutoka kwenye himaya ya Mwenye enzi Mungu na kupinga amri zake na Mollah wako na yeye anaondosha kidogo kidogo Neema yake ya mapenzi kwenye nafsi yako, ndio maana unajikuta huwezi kufanya (Taqwa) yanakutoka mapenzi yalojaa furaha, na kitu hicho kikiondoka ndio mnakua maadui nyinyi kwa nyinyi, Na mapenzi yakiondoka moyoni Roho inaingia mashakani kwa sababu Roho haiwezi kuishi bila ya Furaha, hapo ndio unaanza kuhangaika kutafuta chanzo, mpaka pale utakapo onewa huruma upewe(Maneno ya kutubu) muongozo wa Toba, hapo tena unaanza taratibu kurudi huko(Kwenye mlango wa peponi) ndio Toba yenyewe, na tafauti yako na Mcha Mungu mwenzio tayari keshafika Mlangoni na wewe unapiga hatua za (Mlevi) tatu mbele mbili nyuma, unatokea msituni na makovu chungu nzima huku umebeba (Skeleton)wako, na Toba unaambiwa huku hakutakiwi chochote, ukitaka kurudi uje mweupe, hatutaki hata hilo begi lako la mbao, hatutaki mali ya haramu, hatutaki hata vikosa vidogo vidogo, huko ndiko kutubu, na kama umetubu kweli basi huruhusiwi hata kugeuka nyuma.(Na hiyo ndio inaitwa Tawbat Nasuha),Mollah atujaalie tuipate kwa uweza wake.
No comments:
Post a Comment