Sunday, June 29, 2014

RAHA YA RAMADHAN PART 1

Asalaam Aleiykum

Kitendo cha kufunga lazima kiwe na mahusiano na uwepo wa tendo la Uwazi, ndio kunapatikana kufunga, hakuna shaka kabisa kuwa tunaishi katika huo uwazi, na katika maisha yetu uwazi huu ni mpana sana(Vast)tunayafanya tunayo yaweza na kuyapa jina matendo hayo la (Freedom) huo ndio uwazi wenyewe, katika miezi 11 yote Mtu anacheza sakata analo lijua, unatenda utendavyo katika uhuru huo hata bila ya kuwa na wasiwasi wowote, baada ya hiyo miezi 11 Mollah wako anajua kwenye Uhuru huo wewe umefanya mengi, una magunia kwa magunia ya Madhanmbi, Na sheria ya Ulimwengu huu na kwa masharti yalowekwa ikiwa mnataka Uhuru basi kila Dhanmbi, kila kosa ni Deni na lazima deni hilo lilipwe.
Mnajulikana wazi hamuwezi kuyalipa madeni yenu, Madeni ni mengi mno, Pengine umemcheka Mtu, labda umemsengenya huyu, Umemdhulumu yule, na mengine unayafanya bila kujua, umekikanyaga kinyama na kukiua, umemzulia fulani mambo ya uwongo, una Dhanmbi za macho hazina idadi, za masikio hazisemeki, takriban katika huo uhuru wako umefanya ya kufanya halafu ukaja tenda ile Dhanmbi kubwa ya kumsahau Mollah wako, basi ili usizidi kuangamia, usije kuharibikiwa kwenye uhuru huu, ndio Mollah wako kakuita kwenye mwezi huu, njoo kidogo tukufunge ili upate Rehma ya kupunguza hayo mambo, tupate kukumbusha kuwa upo upande wa pili na unaweza ukapiga jicho ukaona japo ishara kwa kufunga hii Ramadhan.
Na Waumini wanapewa nafasi ya kuangalia upande wa pili lakini sote tunaitupa nafasi hii na badala ya kumkumbuka Mollah jiangalie kwenye mwezi huu unakumbuka Nini?, Huna unacho kumbuka ila vyakula, Makaimati, masambusa, madizi mabivu, Njugu mawe, tena njaa ikikutafuna zaidi utaona unakimbilia jikoni kuagiza ziongezwe sukari, tunakosa nafasi adhimu ya funga yenyewe,  Unaitupa kabisa raha ya Ramadhan ambayo ni ya kumkumbuka Mollah wako mwanzo wake mpaka mwisho wake.
Basi kama ulikua huijui hii Ramadhan ni nyenzo(Tools) ya (Awareness), sasa mwaka huu kuwa (Hadhir) (Alert)shindana na njaa yako, ili uipate Saum na Raha yake, ukikumbuka Katlesi, jilazimishe uone ndio unakumbushwa sala ya Sunna, Ukikumbuka mpira elewa ndio wakati wa darsa ushawasili, ukikumbuka TV kumbuka muda wa kusoma Quraan huo umefika kila ukikumbuka mambo yote yaliyomo ndani ya ile miezi 11 ilopita jitahidi ukumbuke ya huu mwezi mmoja nao ni huu wa Ramadhan.
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment