Sunday, June 8, 2014

TOBA NA MAANA YAKE PART 1

Asalaam Aleiykum

Binaadamu rahisi sana kujificha kwenye kundi la Werevu, kila mtu mjuaji, ukileta somo lolote yeye kesha khitimu, kitu chochote yeye anakijua zaidi kuliko wewe mletaji, hakubali kabisa mwanaadamu huyu kukaa katika kundi la wajinga, japokua anajijua anateseka kwa kutokujua kitu, Na siku zote tizama (Mfano) huu baina ya Mjanja na Mwerevu, ikitokea Mjanja(Mwerevu) kuibiwa anakua na Hamaki sana, lakini Mjinga akiibiwa ima atakua hana habari au akijua anacheka baadae, unajua kwanini?.
Kwa sababu moja tu Mjinga hana Fikira za Mbeleni, Nikisema mjinga nina maanisha(Innocent one), Lakini Mjanja mambo yake yote ya mipango mipango, mbele itakuaje, wakati hakuna yoyote yule ajuae kesho kitatokea nini. Na hivi ndivo wengi wetu tunavoishi tukiendekeza tamaa mwanzo, mateso baadae, Sasa katika jambo la (Toba) Mjanja hujipa tamaa kuwa kesha samehewa yote ayafanyao, hali ya kuwa haijui  hata maana ya Toba.
Haijambo ukiwa Mjinga unakuwa unaishi kwenye maisha ya Khofu na Tamaa, kwa ajili ya khofu kwanza unatekeleza shuruti la Toba na kuacha yote ukisha kuyatambua kuwa haya ni makosa, halafu tamaa unafanya mema kwa kutaraji kusamehewa na Mollah wako, huyu kwenu nyinyi anaonekana Mjinga kwa ajili ya kuacha Raha zote za Kidunia, Lakini (Kwenye Jicho la Dini) Mtu huyu anathaminiwa sana katika kundi la Toba kutokana kwa hiyari yake kaacha (Disco) kwa Hiyari yake kaacha Ulevi, Kwa Hiyari yake kaacha Uzinifu, kwa hiyari yake kaingia kwenye Jihadi ya kuacha Rushwa, Kaacha Dhuluma, na mambo mengi ya kupigiwa mfano, huku nyinyi Mashabiki wa Ulimwengu mnamwita Mjinga, Huyu ndie aliyejua maana ya Kutubu na masharti yake, Na hapa ndio tunaingia kwenye Darsa yetu ya leo tupate kuifahamu maana halisi ya Toba.
Toba au Kusamehewa kuna pande mbili , Upande wa kwanza ni kwa yale ulomkosea Mwenye enzi Mungu kwa kupinga amri zake, Na upande wa pili kwa ajili ya makosa ulowafanyia Binaadamu wenzako, Halafu katika hiyo Samahani pia ipo ya aina mbili, yenye kuonekana na isoonekana, Ili kusamehewa unatakiwa uiyone dalili ya hii yenye kuonekana, ndio tena utakua na tamaa pengine asaa Mollah wangu atanisamehe na hayo mengine siku ya siku.
Kwanini sasa Tunaomba Msamaha? Kwanini tuna Tubu? kuyapata majibu hayo inatupasa tukumbuke kitu cha mwanzo kwamba Makosa ni Mtihani, Na mpaka Ukatubu ina maana Umefeli, na Kutubu unapewa (Chance) Nyengine ili ufanye tena, unaomba utizamwe vipi utajirekebisha kwenye hayo Makosa.
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment