Sunday, June 15, 2014

ANOSIKIA AMWAMBIE MWENZIE PART 1

Asalaam Aleiykum

Anosikia amwambie mwenzie yakwamba mwezi wa Ramadhan umeshawasili na upo pembezoni mwa Shaban. Katika makundi ya watu utawakuta wana tabia tafauti jinsi ya kumkaribisha mgeni, kuna wengine wanajiandaa kwa kukoga wakajisafisha, wakapamba nyumba zao kwa kila aina ya mapambo sababu mgeni anakuja, Na kuna wengine wao mpaka wasikie mgeni yupo mlangoni ndio wanaanza kukurupuka na maandalizi, Na wengine wao hawajali ikiwa mgeni atawakuta wachafu au vyovyote vile hawana habari au hawataki kumfanyia mgeni (Takrima) yoyote ile.
Na Mgeni anapowasili jambo la mwanzo analotizama ni nyumba ya mwenyeji ikoje, jee anaweza kukaa? akiangalia ndani kwenye hiyo nyumba ambayo ni huo mwili wako anakuta uchafu mtupu, imejaa majani ya mirungi, kuna vikopo vya Bia, kuna mali za wizi na haramu, damu imechafuka kwa michirizi ya rushwa, mifupa yote mizito kwa vitendo vya dhuluma na balaa chungu nzima zimesaki kwenye Jumba la Roho yako, Ramadhan inahuzunika hivi mimi nimeletwa kwenye nyumba hii ili nilete zawadi ya mapenzi ya Ibada na Rehma za Mwili, halafu niwachukulie dhamana hawa ya kuepushwa na moto, lakini sina nilichokikuta ila hawa Viumbe kila nikikaribia wao ndio wanafanya mazoezi ya kuingia motoni.
Hakuna idadi yoyote ile isipokua wachache sana wao ndio wamenusurika, lakini wengi wao nimewakuta wana matatizo makubwa na wamo wanajificha kwenye karata, mabarazani, kwenye ngoma na kila aina ya fujo, mpaka wamesahau kwamba wewe Mollah wao upo na unapaswa kupendwa kama ulivo wapenda na kuwapa zawadi ya Uhai.
Kiumbe kwenye miezi 11 umeshughulika na mambo yako, huna nafasi ya kumpenda na kumuabudu Mollah wako kwa ajili ya mambo ulo nayo, huna kituo kabisa uko (Busy) sasa basi kakutengea hizi siku chache mpeni yeye kwa shukran na kumkumbuka kila saa na dakika, vipi utamkumbuka ndio umepewa hii Ramadhan(Condition) Ufunge, vipi kufunga kwenyewe, shuruti lake hassa nini? (Bakara aya ya 183)
يَـٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ كُتِبَ عَلَيۡڪُمُ ٱلصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى ٱلَّذِينَ مِن قَبۡلِڪُمۡ لَعَلَّكُمۡ تَتَّقُونَ 
Enyi mloamini melazimishwa kufunga kama walivyo lazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu.
Haijambo inatia moyo watu wote wanao ukaribisha mwezi wa Ramadhan wanakutana katika jambo moja nalo la kukaa na njaa, lakini Ramadhan kusudio lake sio mkae na njaa, kusudio lake mpate mapenzi ya kumpenda Mollah wenu kwa (Devotion) na shukuran.
Endelea part 2

No comments:

Post a Comment